BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI WAANDAMANA October, 28, 2008

Filed under: Watu na Matukio — bongocelebrity @ 5:57 AM

Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wameandamana leo asubuhi jijini Dar es salaam,maandamano hayo yalianzia mtaa wa Lugoda na kuelekea wizara ya habari utamaduni na michezo,ambako walikabidhi barua kwa Waziri wa wizara hiyo Mh George Mkuchika,aidha madhumuni ya maandamano hayo yalikuwa ni kupinga kufungiwa kwa gazeti la mwanahalisi na serikali kwa muda wa miezi 3 na pia kuishinikiza serikali ifanye marekebisho ya sheria ya uhuru wa vyombo vya habari ya mwaka 1976

Advertisements
 

41 Responses to “WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI WAANDAMANA”

 1. Edwin Ndaki Says:

  Serikali nataka kuwakumbusha maneno yalisemwa miaka mingi iliyopita kwenye vitabu vitakatifi..

  Wasiposema hawa..mawe yatasema….

  Ndio yaliyotokea mbeya(ingawa siungi mkono violence)..mh wakamnaniihii kwa mawe.

  News paper Act 1976 hakika inamapungufu mengi.Ila miaka nenda rudi wasomi wanasema inamapungufu lakini SIRIKALI kwa kulinda maslai yake ndio maana hawataki kuibadilisha.

  Mfano kuna kipengelee kimoja kinampa nguvu hata mlinda amani wa wilaya mfano mkuu wa wilaya kumuweka kizuizini mwandishi kwa masaa na kumuhoji bila kumfikisha popote..

  Tuna hitaji uhuru wa kweli wa vyombo vya habari kupata taarifa.

  Ila naona safari inaenda vema tutafika tu.

  BC naomba ingawa ni katikati ya juma..Hebu tutafutie kibao kikali za enziiiii hizoooooo kiwe sehemu ya kupunguza machungu baada ya kukosa burudani kwa wiki endi kadhaa…aaa

  Watu wangu tutafika tu..Matty,Any,Chris,Kekue,Gervas,Majita,Binti mzuri,BLACKMANMEN,mama wa kichaga,Hombiz,Angel,Dinah,Mswahilina,Dunga na wadau woooote ambao kamuda hakajaniruhusu kuwataja..

  Nawamiss sana watu wangu..naamini BC imerudi kwa nguvu zote

 2. abel Says:

  Napenda niwashukuru sana wahariri wa vyombo vya habari kuionesha serikali hususani huyu Dikteta Mkuchika kwa kulifungia MwanaHalisi,amini utumiaji wa udicteta dhidi ya vyombo vya habari ambavyo kucha kutwa ndio vinawasaidia wanasiasa kupanda chati ni unafiki,uzandiki na ukiritimba kama sio urapurapu na ufinyufinyu wa mawazo na mgando wa akili zenye fikra zenye ukakasi na utapiamlo.Hakika Watanzania tunabidi tujiulize tunakoelekea,maana viongozi wetu wanajitenga na Ukweli na Wananchi wao.TUNAKWENDA MBELE,TUNARUDI NYUMA AU TUNAPIGA MARK TIME?
  TUAMKE WATANZANIA.

 3. halima Says:

  kudadadeki!!!!!!!!!!! hiyo style ya miplasta mdomoni ni noma no kuchema na ukichema tu utafungiwa hahahaahha bongo tambarareeee kila mtu na mnyonge wake.

 4. majita Says:

  Hiyo picha moja imeongea maneno mengi sana.
  Mimi sina la kuongeza kwa sababu nina hasira hadi nabonyeza hii keyboard kwa nguvu utafikiri sijui nini tu.Ngoja nitoke nisije kuiharibu bure.
  Ndaki asante kwa kunikumbuka

 5. majita Says:

  Inatia huuruma na kuamsha ari furani ya ukombozi.Am down
  Ndaki asante kwa kunikumbuka mkuu

 6. sellanda Says:

  kuna mmoja hapo sidhani hata kama anapumua maana plasta yake mpaka kwenye pua kwikwikwi

 7. SHUBI Says:

  JAMANI NIKWELI DIKTETA HUYU SIYO VIZURI KULIFUNGIA GAZETI LA WATU KAMA MWANAHALISI,ILA VYOMBO VYA HABARI MMEFANYA SAFI KUONYESHA MSHIKAMANO WENU

 8. Mutwiba Says:

  Nimesema haya kabla sijayaona. Niliposikia habari za kufungiwa kwa mwanahalisi nikajiuliza kama kuna msanii angefanya aliyofanya Pink kwenye huu wimbo kwa Bush (bofya http://www.youtube.com/watch?v=mQYHKILXD4k) sijui ingekuwaje? Maana yeye kaeleza ukweli bila kuficha na wala hayuko ndani.
  Angekuwa “kwetu” angekiona.
  Wakiamia na kunuia watasaidia maana yaonesha serikali inataka ku-control habari kwa remote.
  Blessings

 9. Matty Says:

  Edo tutafika lakini kwa kuchoka!

 10. mtz Says:

  Mwanahalisi JELA; mafisadi HURU??? I like that msg.

 11. kahindi Says:

  HIZO PLASTA MIDOMONI ZINAMAANANISHA….NO COMMENT….

 12. hombiz Says:

  Sheria ya Magazeti (The Newspaper Act 1976) inampa mamlaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuzuia chapisho lolote linalotengenezwa hapa nchini ama kuingizwa kutoka nje ya nchi ambalo linaweza kuhatarisha matakwa ya nchi. Sheria hii vilevile inampa mamlaka Waziri anayeshughulikia mambo ya habari kuzuia kuchapishwa kwa toleo lolote la gazeti, na kwamba itakuwa ni kosa kwa mtu yeyote atakayechapisha, kuuza ama kusambaza gazeti hilo baada ya amri ya Waziri kutolewa.

  Watanzania wenzangu! Hivi hiyo hapo juu ni sheria inayotoa uhuru kwa vyombo vya habari kweli? Kwangu mimi naona hiki ni kichekesho cha serikali cha kumtazama chura kwakuwa hana masikio wala mkia. Matakwa ya nchi wanayoyaongelea kwenye sheria yao mbaya (kwa sasa) ni ufisadi wa viongozi ambao wako madarakani. Wanataka wafanye ufisadi, waibe weeeeee! Ila magazeti yasiseme. Mala EPA, mala RICHMOND, mala MEREMETA, mala KIWILA,..yote hayo wanataka waandishi wa habari wayafumbie macho ili kusudi wananchi tusijue uozo wao hawa mafisadi wa kutupa. That is not gonna work! They need to quit! Hiyo sheria ni lazima ifanyiwe marekebisho na vyombo vya habari viwe huru ktk utendaji wa kazi zao kama ilivyo kwa vyombo vya habari vya Marekani kaskazini. Bila vyombo vya habari kuwa huru, mapambano dhidi ya tabia chafu za viongozi kama rushwa, ufisadi haviwezi kupungua na hatimaye kutokomezwa kabisa. Tuwaunge mkono waandishi wa habari ili wapewe uhuru wa kweli na si wa bendera.
  Edwin Ndaki, asante kwa kunikumbuka
  Stay focused everybody!

 13. EDWIN NDAKI Says:

  aaaa..aaaa BC nimependa sana kasi mliyorudi nao naona sasa mwendo mdundo..tulifikiri na wewe wamekuMWANAHALISI.kwiiii kwiii tteeee teeeee aaaa haaaaaa

  Matty ..umenichekesha kwamba tutafika lakini tumechoka..aaa aaa

 14. hilly Says:

  Mh kwa kweli wanahaki ya kuandamana,maana nchi yetu huwa haipendi kutoa uhuru kwenye vyombo vya habari.Halafu hii nchi yetu bwana.,hilo gazeti wanalotaka kulifungia ndilo lenye habari nzito kuhusu mambo yanavyoendelea huko serikalini.Msikate tamaa waandishi songa mbele…..

 15. binti-mzuri Says:

  hhahaha nimechekaa! plasta mdomoni! i hope ujumbe wenu utafika!

 16. BLACKMANNEN Says:

  Waandishi wa habari, waalimu na wengine wote wanaotumia taaluma zao kuihujumu serikali yao, kwa kuandika uchochezi na kutumia haki ya kugoma pasipokuangalia athari za matendo hayo nchini Tanzania. Mimi siwaungi mkono kabisa.

  Kupigana mawe mikutanoni, na kuushambulia msafara wa Rais, ni vitendo vya kihalifu, na uhaini, wenye nia ya kumwondoa kwa nguvu madarakani Kiongozi wa nchi aliyechaguliwa na Watanzania wote. Mimi siwaungi mkono, na ninaomba serikali iwachukulie hatua kali, kufuatana na uzito wa makosa yao.

  Baada ya kuayaona matukio haya yote, Watanzania wote tujiulize…….!!!! Je, ni kwanini yanatokea sasa mambo haya Tanzania???? Je, ni mkono wa watu wachache, wanaohofia hatima zao, kutokana na kashifa zao, ambazo serikali na hasa Kiongozi wa nchi (Rais), aliyeamua kufungia kibwebwe sakata lao??? Je, ni wanasiasa wachache walioamua kuidhoofisha serikali iliyomo madarakani kwa kuwarubuni wananchi kwa maneno ya uchochezi, na kupandikiza chuki kati wananchi na serikali iliyomo madarakani, katika kuainishwa na sakata la UFISADI, likiwa kama chambo????

  Mbona matatizo ya walimu yalikuwapo hata huko nyuma, lakini walimu hawakufikia hatua ya kufanya migomo kama leo hii????? Mbona sheria ya magazeti ilikuwapo tangu 1976, waandishi hawakuivalia njuga sheria hiyo isipokuwa iwe sasa???????????

  Ndugu zangu, Watanzania wenzangu, NJAA zetu hizi zitatupeleka pabaya. Tuwe wavumilivu, na tusubiri ahadi za viongozi wetu kutimizwa, na kama hazitatimizwa rungu lipo mikononi mwetu, mwaka 2010.

  Ahsante sana Edwin Ndaki kwa salaamu zako kwangu. Matty, tutafika tu, bila ya kuchoka.

  This Is Black=Blackmannen

 17. majita Says:

  Rafiki yangu Blackmannen,
  Nafurahi kwa chapisho lako.Lakini nafurahi zaidi kwani unajijibu mwenyewe.Mimi nilifikiri ungejiuliza hivi,”KWA NINI HAYA YOTE YANATOKEA SASA NA ISIWE ZAMANI?” Hata hivyo ningekujibu kuwa “DUNIA YA SASA SIYO YA LEO.INGEKUWA JANA NI LEO BASI KUNA UWEZEKANO MKUBWA WEWE SASA HIVI UNGEKUWA BADO NI NYANI”.

 18. Mama wa Kichagga Says:

  Mmmmmm,

  Moja kwa moja kutoka eneo la tukio! Demokrasia yakua ghafla na kusababisha watu kutembea kwa pamoja tehetehe tehe.

  Sasa wafuatao watakuwa watoto wa chekechea , sijui itakuwaje Mungu wangu teheteheteteeeeee.

  Ndaki asante ndugu yangu na wengine wote karibuni tuifurahie BC yetu kwani ilianguka ikasinzia hapo kidoooogo tu halafu imekuja kwa kasi mpya haaaaaaaaaaaaa.

  NB:
  La muhimu hapa wakuu watumie akili zaidi kuliko kutumia nguvu maana woga wote Nyerere aliondoka nao na sasa ni kizazi kipya tena tofauti kifikra na kiutendaji. Wasipofanya homework yao vizuri michemsho itakuwa mingi halafu hapatatosha.

  Mungu ibariki na kuilinda TZ

 19. Chris Says:

  LMAO at those plasters! Lkn interpretation ya hizo plasters ni nini? Kwamba wanafungwa katika kutoa kile wajuacho na kitokeacho au? Lakini wana rungu la pen na karatasi! Je, wanafungwa au wanajifunga wenyewe?

  Mimi si mtaalamu sana wa habari lkn nafikiri chochote kiandikwacho na mwandishi kinatakiwa kuwa na proof especially ktk ulimwengu huu wa teknolojia ya juu ya mawasiliano, otherwise you you’ll be misleading and possibly reporting unfounded and baseless info.

  Kubenea ni one of my fave journalists ktk Tanzania. Nafikiri ni vizuri pia kwa MwanaHalisi na Said Kubenea kutoa proof ya hiyo habari ambayo binafsi naamini atakua nayo! Maana si haiwezekani kuandika habari kama hiyo bila kuwa na vithibitisho!

  Mwisho kasi ya BC nimeipenda, maana duuuuuh, nimekuta postings nyingi na nzuri. Head up Jeff!

 20. john Says:

  jamani hii yote ina zihirisha kwamba rais jakaya kikwete inabidi aojiwe juu ya uwezo wake wa kuongoza nchi.

  nafikiri tuna fanya masihara lakini salim mohamed salim ndie aliyekuwa ana paswa kuwa kiongozi wa nchi hii.

 21. hombiz Says:

  BLACKMANNEN sikubaliani na wewe katika swala hili kabisa. I think you need to go sit down somewhere.
  Kwanza kabisa napenda ufahamu Raisi Kikwete hakuchaguliwa na wananchi wote. Isipokuwa, alichaguliwa na asilimia kubwa ya watanzania.
  Pili, ni lazima ufahamu siku zote binadamu ana kiwango cha kuvumilia mateso, manyanyaso na matatizo. Ila akishachoka kuvumilia na kusema “enough is enough” hapo sasa huchukua hatua anazoona ni muafaka kwake. Hiyo inaitwa ni hatua ya liwalo na liwe!. Hii ni kama vile watani wangu wa kihehe wanaposema swela! Hapo panakuwa hapatoshi.

  Kuhusu swala la vyombo vya habari kufungiwa, mimi sikubaliani na swala hilo, “as long as”, vinasema ukweli. Tatizo hapa ni nini? Kama vimeandika habari isiyo sahihi, kwanini visiombwe kuthibitisha mbele ya mahakama? Wanakimbilia kuvifungia ili iweje?. Huu ni mpango wa kuficha maovu yao vigogo(MAFISADI) They need to STOP this unacceptable behaviour. Let the media inform subjects what is going on in BONGO politics and the whole World at large.

  Blackmannen, walimu wanashahili kufanya walichokifanya. Hii tabia ya kuwataka watanzania wawe wapole na kusifia eti Tanzania ni nchi yenye amani na utulivui, imepitwa na wakati. Viongozi wa Tanzania(ambao wengi ni mafisadi) wamekuwa wakitumia kigezo cha utulivu upole na amani, kulihujumu taifa huku wakitaka watanzania tuwe wapole tukishuhudia ubabeli wao. Hawa mafisadi ni kama panya ambaye anatafuni miguu ya mtanzania aliyelala. Na pili mtanzania akitaka kuamka usingizini, basi huyu panya anapuliza unyayo wa mtanzania ili asikie raha na badala yake asiamke ila aendelee kulala! Watanzania wenzangu, sote tunapaswa kuamka!. We need to kick the rat off our feet.
  Big up Mama wa kichaga na Majita
  Stay focused y`all

 22. trii Says:

  mi si semi kitu hadi 2010.

 23. BLACKMANNEN Says:

  Kwako Hombiz,

  Watanzania usiwafanye hawajui wanachokifanya katika maisha yao ya kila siku, maana wewe unajiona ndiye mwerevu kuliko hata wao waliokulea na kukusomesha hadi kwenda nchi za nje, na kufikia hapo ulipo, eti unasema wamelala unataka waamke.

  Rais Kikwete unayemlinganisha na chura asiyekuwa na masikio wala mkia, wamemchagua wao wenyewe ikiwa ni pamoja na ndugu zako uliowaacha Tanzania wameshiriki kumchagua Kikwete kuwa Kiongozi wao Tanzania, kwa kipindi cha miaka mitano. Kama watanzania, wataona Kikwete hafai, watachagua mtu mwingine hapo mwaka 2010, wakati huo, wewe utatakiwa kukaa pembeni na kukubaliana na uchaguzi wa Watanzania hawa, kama ambavyo unatakiwa ukae sasa hivi, huko uliko bila kuwaletea za kuleta.

  Werevu wako waonyeshe hao waliokupokea huko Marekani kwa kuishi maisha yanayojulikana na wewe pekee yako.

  Watu msiwe “malimbukeni” mnapokwenda nje ya nchi zenu. Watanzania ni watu wastaarabu sana. Wamempokea vizuri sana, na kwa ukarimu mkubwa Rais wa nchi unayokaa wewe “Hombiz”. Hawakumtukana wala kumtupia mawe, ingawaje ni mtu anayechukiwa na kila mtu mpenda amani na utulivu duniani, ikiwa ni pamoja na wananchi wa Marekani anaowaongoza huko unakoishi wewe.

  Wamarekani wako tayari kumchagua hata “Mbwa”, ili awe Rais wao, kuliko kumrudisha madarakani Rais Joji Pori, lakini wewe mwenzangu na mie, unamwona ni mali sana, kuliko Rais wa Tanzania. Katika kila comments zako ni kumtukana Rais wetu wa Tanzania, sijui ni kwanini?

  Ikiwa kama ni kweli kama ulivyoandika katika comment yako nr.21″…. viongozi wa Tanzania (ambao wengi ni mafisadi) wamekuwa wakitumia kigezo cha utulivu upole na amani, kulihujumu taifa…”. Mimi nakuona unajichanganya na huelewi unachoongea na badala yake, “chuki” yako kwao inajionyesha wazi.

  Amani na Utulivu haviimbwi kama nyimbo, bali ni hali halisi ambayo ipo, na kama kungekuwa na hali nyingine mbaya, inayowakera Watanzania, amani na utulivu huo vingepotea mara moja. Tungekuwa tumeanza vita tayari.

  Kuhusu matatizo ya hapa na pale yanayotokea Tanzania, ni hali ya kawaida katika nchi inayofuata sheria na demokrasia ya juu kwa wananchi wake, katika kujieleza hisia zao walizonazo kwa viongozi. Lakini serikali nayo haitakubali watu kujieleza hisia zao kuvuka mipaka yake.

  Ndugu yangu “Homboz” kwako ni kwako hata kama ni kubaya, usijione umefika kuishi Marekani. Watu walidhani kuwa Afrika Kusini ni nyumbani, lakini yaliyowapata hivi karibuni, hawana hamu na nchi hiyo tena, wanahamu ya kurudi makwao wanaoweza kufanya hivyo. Lakini watu wa Congo, Somalia, Sudan, hawana pa kwenda. Wewe unayo Tanzania.

  It’s Great To Be Black=Blackmannen

 24. XXX Says:

  ahh wabongo nao kwa kuiga hio styl ya ma plasta mdomoni wameiga kwenye ile video ya …ahhh sijui anajiitaje ni black amrican anaimba hip hop wimbo unaitwa g rod anthem pia wameiga kwenye video ya sema nami ya lady b na noninini!ebu acheni kuiga iga ovyo!

 25. halima Says:

  mmmh isha kuwa soo

 26. Gervas Says:

  Blackmannen, Tatizo ni hiyo sheria ya magazeti, mpango wa kuirekebisha(amend/repeal) upo kwa muda sasa, ila serikali inachelewesha kwa sababu kama hizi, kuhalalisha ubabe wake. Nafikiri unaelewa kuwa jamii inavobadilika, sheria nazo zapaswa kubadilika. Wakati inatungwa mwaka 1976 mambo hayakuwa kama yalivo kwa sasa. Kwa kifupi nataka kusema hivi, Pamoja nakuufahamu uzee wa sheria hii serikali, serkali haikupaswa kuitumia sheria hii katika swala la mwanahalisi( for public interest), na badala yake wangetumia mahakama, Kama mwanahalisi waliandika habari za uongo mahakama ndo ingeamua. Hata hivo kwa upande mwingine, wahariri wanapaswa waichallenge sheria hii mahakamani kusudi mahakama iipige chini. JK anasisitiza kuwepo kwa uhuru wa vyombo vya habari majukwaani lakini sheria ya magazeti inauchukua uhuru huo…

 27. hombiz Says:

  BLACKMANNEN, Watanzania tumeamka na ndio maana waandishi wa habari, na walimu wanaandamana. Kumbuka huko nyuma na wanafunzi wa shule ya msingi, waliandamana pia.
  BLACKMANNEN, Unaposoma comments zangu, inabidi uzielewe kwanza kabla ya kuchukua maamuzi ya kujibu. Ni sehemu gani ya mfano wa ngu imemlinganisha Raisi Kikwete na chura?. Kama umeweza kukosoa kiswahili changu cha o-level, basi inawezekana wewe ni mtaalamu wa kukosoa. How did you miss my frog example then!?
  Naurudia mfano huo tena labda safari hii utauelewa vizuri. Kwenye mfano wangu wa chura, niliandika kama ifuatavyo: ” Kwangu mimi naona hiki ni kichekesho cha serikali cha kumtazama chura kwakuwa hana masikio wala mkia”. Sasa, je mfano huu kweli umemfananisha Rais Kikwete na Chura!? Do you real get what i say BLACKMANNEN?
  BLACKMANNEN, acha ulimbukeni wa kuandika mambo bila ya kuwa na uthibitisho nayo. Hakuna sehemu hata moja niliyosema mimi nakubaliana na raisi Bushi na sera zake. Mimi kama HOMBIZ, napenda wewe ufahamu rasmi kuwa sikubaliani na sera nyingi za raisi Bush. Ila nampa credid kwa baadhi ya sera zake kama ile ya uhamiaji.
  Kwa mtazamo wangu mimi, naamini wapiga kura walio wengi nchini Tanzania, wako vijijini. Na huko vijijini, asilimia kubwa ya wanavijiji bado hawana elimu ya kutosha kuwafanya wawe na uelewa wa kutosha kuchambua vizuri mambo ya kisiasa. Ndio maana inakuwa vigumu kwa sasa vyama vya upinzani kushinda. Usishangae kuwa mpaka leo ukienda vijijini ndani, kuna baadhi ya wana vijiji bado wanafikili Nyerere ndio raisi wa Nchi. Na chama wanachokijua zaidi ni CCM, CCM, CCM!. Hivyo kubadili fikra za wanavijiji hawa na kuwaamsha ili waone kweli CCM ni chama chenye bla bla!, itachukua muda. Lakini naamini kabisa kwakuwa “at least” sasa hivi elimu imeanza kupewa kipaumbele, basi bila shaka miaka ijayo wasomi watakuwa ni wengi na popote mtu atakapojitokeza kugombea nafasi yoyote ya uongozi, itamlazimu awe na nguvu za hoja na sio hoja za nguvu.
  Vile vile uozo wa rushwa uliopo serikalini hivi sasa, ni moja ya mambo yanayorudisha demokrasia nyuma. Kila siku tunasikia takrima,takrima, takrima kwenye chaguzi mbali mbali. Hizi Takrima sio kitu kingine bali ni rushwa. Viongozi wanatumia rushwa ili kuingia madarakani. Wakishaingia madarakani, wanatumia vyeo vyao kulinda maslahi na biashara zao pamoja na kulipa fadhira kwa wafadhili wao. Mambo kama hayo ndiyo yanayopelekea wao kwa wao kulindana pale ufisadi unapotendeka. Rushwa hiyo hiyo (inayoanzia ngazi za juu serikalini) ndio inayoshuka na kuenea mpaka ngazi ya chini kwa mtanzania wa kawaida. Na isipokemewa vya kutosha, rushwa hii itakuwa kama ugonjwa wa kansa isiyotibika na inayosambaa kwa kasi mwilini. Every Tanzanian, including you BLACKMANNEN, needs to do something about this so that we can put this dirty culture to rest.
  Nalisikitishwa sana na mambo ya kibaguzi yaliyowakuwa watanzania waishi S. Afrika kama ulivyosema hama awali blackmannen. Lakini hiyo nadhani ilisababishwa na uelewa mdogo wa watu waliosababisha unyama ule. Wanacholalamika wao ni kuwa waafrika toka nje ya nchi yao wanakwenda S. Afrika na kuchukua kazi zao. Km hao wageni ndio wenye elimuna ujuzi wa kufanya kazi husika ubaya uko wapi? Wao( South Africans wengi-weusi) walikuwa kwenye vita dhidi ya ubaguzi wa rangi kwa muda mrefundio maana hawakuweza kupata muda mwingi wa kujiendeleza kielemu. However, it will take sometime, but they will finally get there. Once they they are educated enough, all the hatred will diminish.
  BLACKMANNEN! I am running out of time. However, my closing opinion is, I, HOMBIZ, don’t need to be out of Tanzania to have the opinions that I post on BC Blog.
  Sio lazima “mimi km mtanzania”, niwe na mtazamo wako ili utanzania wangu ukubalike. Vigezo ulivyovitumia kunifanya mimi kama mtanzania niliyejifunga minyororo ya utumwa dhidi ya nchi yangu mwenyewe, havina mantiki yoyote. Mimi ni mtanzania alisi kama alivyosema Profesa Jay, nna alama ya ndui na sio tattoo! Pia nna machungu na nchi yangu. Siku zote naona fahari kuwatetea walalahoi wenzangu dhidi ya MAFISADI walioko madarakani. Na wala sitaacha kufanya hivyo, no matter what! Mwendo mdundo, hadi kieleweke!.

 28. hombiz Says:

  BLACKMANNEN i forgot this!, hakuna taifa lolote duniani( ikiwa ni pamoja na marekani) ambalo liko tayari kumchagua mbwa kuwa kiongozi wao wa nchi. Likitokea taifa ambalo liko tayari kuongozwa na mbwa, mimi nitapendekeza likuchukue wewe uwe kiongozi wao!

 29. binti-mzuri Says:

  eh! kazi kweli kweli!

 30. Mama wa Kichagga Says:

  Hombiz,

  Unakosea sana kumuita kiumbe wa Mungu Mbwa! Ilhali ukijua fika yeye siyo mbwa!

  Nafikiri next time chunga hasira na mdomo wako maana nakuona hujatulia kabisa. Kwani ukiwakilisha hoja yako bila tusi haitaeleweka!

  Huu ni ukosefu wa busara na kamwe hauna nafasi katika karne hii ya utandawazi.

  Hivi nikuuliza:
  Umekwenda kukata majani na panga/shami lako ghafla unasikia joto kali na mbele yako kuna mto. Mara unaamua kuvua na kuoga maana unajihisi uko pekeyako. Wakati unaoga anatokea mtu ambaye watu wanamtambua kuwa ni kichaa anaanza kukufukuza. Mara moja akili yako inakutuma uwahi silaha yako ukimbie ili asije akaiwahi akakudhuru na kwa kufanya hivyo yeye anakaribia (bido uko utupu) unaamua tutimua mbio uchi chiiiiiiiiiiiiiiiiiiiziiiiiiii chiziiiiiiiiiiiiiiii. Yeye kavaa nguo wewe uko uchi na silaha mkononi! Kati yenu nani tutamuita chizi? Kwa vyovyote wewe uliye mtupu na silaha!

  “MIND YOUR LANGUAGE & WORK OUT YOUR ANGER” USIFIKIRI NI SIFA KUTUKANA NA KUONYESHA UBABE MTANDAONI. ELIMIKA!!!!

 31. hombiz Says:

  Your mfano is out dated Mama wa Kichaga!
  Nikuulize wewe swali yeye alipatia aliposema Marekani wako tayari kumchagua mbwa awaongoze kuliko kuongozwa na raisi anayemaliza muda wake George Bush!.
  Get the…….out of here zxsxd

 32. mss Says:

  duuuh kudadadeki aithee thatha wajameni mbona tena naona kama panakuwa hapatoshi

 33. BLACKMANNEN Says:

  Ahsante sana “Mama wa Kichagga” kwa kumpasha huyu ndugu yetu, maana hata mie nimemwambia amtake radhi ndugu yetu “Aligator”, aliyemwambia kuwa hatashangaa (Hombiz) kumwona (Aligator) akiwa amevaa suruali inayoonyesha makalio yake. Hayakuwa maneno mazuri – Mimi sikuyapenda!

  Pia, kila mara amekuwa akimfananisha Rais wetu wa Tanzania, kama “chura asie na masikio wala mkia”. Sisi wote ni ndugu (Watanzania), mfano wa “Mbwa” haukutolewa kwa Mtanzania, lakini mfano huo, umemkasirisha kupita kipimo Hombiz, sawa na msemo usemao, “Mkuki kwa Nguruwe, Kwa Binadamu….Unauma sana”. Asitufanye Watanzania “Nguruwe”.

  Ni kweli “mss”, hapa hapatatosha kama (Hombiz) ataendelea kututukania Rais wetu wa Tanzania. Hoja Ndiyo Hiyo!

  This Is Black=Blackmannen

 34. Mama wa Kichagga Says:

  Mwenye akili timamu atulie mpumbavu aendelee kuleta za kuleta sisi tuangalie linalofaa na tusonge mbele.

  NB: Hapa nina wasiwasi unaweza kuondoka na mtu kwa kupambana ukijua mpo pamoja kumbe hamnazo.

  Got me? Tusongage mbele.

 35. Hombiz Says:

  BLACKMANNEN you never get my points, i think something is wrong with you. You will never get no points by trying to twists my words. People who understand the language i

 36. Hombiz Says:

  BLACKMANNEN People, who understand the language I speak, already got my points. But you who don’t even know what the heck you are talking about, you’ll never understand. I’ll always criticize things that I believe to be wrong and give five to the decent comments or ideas.

 37. Matty Says:

  wape wapeeeee vidonge vyao wakimeza wakitema ni shauri yao!!!!!!!hahahahahhaa sms delivered!

 38. halima Says:

  matty hako kawimbo ni kazuri repeat again kwikwikwi

 39. Matty Says:

  Halima shosti nawewe nae unatafuta……………..shauri yako watu wa jazba wakija hapa utalijua jiji na mataa yake hahahahahaha!
  wknd njema shosti!

 40. halima Says:

  iasee wewe acha tu sio mataa nitaonyeshwa mpaka lami zake

 41. hussein Says:

  Waandishi ni wachoyo, hawataki kuguswa wakiguswa wanakimbilia kususa, hivi kila mtu akisusa mpaka tukasusa kusoma hivyo wanavyoviandika watafanyaje? Nafikiri wanapopotoka na kuandika visivyokubalika katika jamii inabidi wakubali wanapokosolewa sio kutumia kalamu yao kung’aka


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s