BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

NI WAKATI WA “FREEZE” KUTOKA KWA AY October, 29, 2008

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Muziki,Single/Mpya — bongocelebrity @ 1:52 PM

Anaitwa Ambwene Yessayah.Kwa wengi anafahamika kama AY huku wengine wakiendelea kumuita “Mzee wa Commercial”.Kwake muziki ni burudani na pia ni kazi.Mafanikio yake katika game ni mfano wa kuigwa na wengi hususani wasanii wanaochipukia.Ni miongoni mwa “mabalozi” wazuri wa Tanzania nje ya nchi kupitia sanaa ya muziki.Kwa mara nyingine tena mwaka huu anawania tuzo maarufu za Kisima za nchini Kenya.

BC ina furaha kuutambulisha kwako wimbo mpya kutoka kwa AY.Wimbo unaitwa FREEZE.Amewashirikisha P.SQUARE kutoka nchini Nigeria. Wimbo umetayarishwa na kurekodiwa na Producer Hermy B kutoka Tanzania.Tayari wimbo huu unakamata chart katika vituo mbalimbali vya radio.Unaweza kuusikiliza kwa kubonyeza player hapo chini.
Advertisements
 

79 Responses to “NI WAKATI WA “FREEZE” KUTOKA KWA AY”

 1. binti-mzuri Says:

  dah mtoto kawekwa photoshop nini,softii! aisee your music is as beautful as you are. mi nakumind AY kwani kwanza una deliva,afu cha pili huna ma bifu ya kijinga. go on mzee wa commercial!big up

 2. Hombiz Says:

  Hapa mimi nna tatizo kidogo!. Huyu AY anachokiongelea hapa ni kitu gani? Au ili mladi nyimbo tuu!. Sisikii ujumbe wowote kwa jamii hapa. Hakuna kitu kinachonitibua mimi ktk BONGO FLAVA kama kusikiliza nyimbo zisizokuwa na ujumbe wowote kwa jamii zikipewa promotions za nguvu wakati nyimbo zinazoongelea vitu ya maana ktk jamii zikizimwa bila sababu.

  Ndio maana mpaka dakika hii mimi wasanii ninaowaona wako safi ktk muziki huu wa kizazi kipya ni Profesa Jay na Mr 2. Wengi wao naona wanapeperusha steam tuu!
  Mnazikumbuka nyimbo kama- wapi tunakwenda wa Mr.2 na ule wa Chemsha bongo by Prof. Jay? Hata Feruz naye yuko safi. Ana ujumbe kibao.
  Lakini huyuanayejiita mzee wa kumesho na wenzake wengi, hakuna kitu kabisaaaaaaa. Ni upuuzi mtupu!

  Kuna mambo mengi sana ya kuzungumza ambayo yanakera jamii k.v. kukumbatiwa kwa ufisadi ndani ya serikali, kero za walimu, mauaji ya albino n.k. Wanashindwaje kuongelea mambo haya muhimu na kutaka kukimbilia ku-freeze tuuuuu!. Meeeeen Please!give me a break!

  Wasanii wa bongo flava hebu umizeni vichwa na kuandika mashaili yenye akili sio huu upuuzi wa ku-freeze bila hoja za msingi.
  Huu nii mtazamo wangu!
  the One and only…Hombiz!

 3. piusmickys Says:

  Aaaaaaaah Dogo salute
  Nimeikubali hii kitu ina kiwango si mchezo na Big up kwa Producer ameonyesha ukomavu Beat iko tofauti na tulizooea za ki Bongo Flava!!
  AY Once again Big up kaka.

 4. BLACKMANNEN Says:

  Kitabu kimo kichwani lakini? Maana tusirukie kumsifia kwa kiburudisho chake kizuri. Tutakuwa tunam-lostisha kijana wetu, katika maisha yake ya baadaye. Kuna msemo usemao “Education Is Power, It Can Not Be Taken Away From You”.

  Vijana wengi waliojiinua mapema katika shughuli zao, mara nyingi husahau kitu “ELIMU”, kama tulivyomwona Marehemu Marijan Rajab Shabani – “Jabali la Muziki” na hata Dada Saida Karoli na wengine.

  Nawaombeni vijana wote, wake kwa waume, mshikeni kwanza huyo “ELIMU”, akae vichwani mwenu mapema, halafu mambo mengine baadaye.

  This Is Black=Blackmannen

 5. Kaka K Says:

  namfagilia sana bwana mdogo, naamini ipo cku atakuwa mbali saaana.

 6. Matty Says:

  Binti-mzuri na wewe unamacho kama mimi mhh ngoja nisiseme sana maana naona kijana no pimposi hahahahahah!

  ila sasa ujumbe wa huo wimbo ndo sijauelewa kabisa!

 7. sisterTZ Says:

  BLACKMANN; mimi na mind sana comments zako kwa sababu zimeenda shule…ujua hawa wadogo zetu hataki shule wadhani musiki bila shule ndio watapata mafanikio ujinga mtupu.. na jamani lazima tufute huu ujinga ndio tutapata maendeleo..we angalia Saida Karoli alikuwa na kipaji na sauti nzuri ila kwa sababu hakuenda shule akatapeliwa mpo hapo??

 8. ooohhh so this is the track anewashirikisha P^2. Lovely, loveky I must say. Always had mad love 2 Ambwene… from back in the days when he used 2 perforem @ Kilakala’s concerts… Kipi kikusitishicha…? hahah. Ifunda buoy!! Got to know him through some friends at Mzumbe who’d come from Ifunda!!!

  Been a fan ever since. mToka Raha Tu mpaka Raha Kamili mpaka Usijaribu!!!

 9. star Says:

  jamani wanamusik wa TZ nendeni shule Kofi Olomide na digrii mbili na music anapiga ambao unafanana na shule yake..

 10. Matty Says:

  jamani ni sawa arejee shule ila mbona kwa Inspector Haroun hakuna aliyemshauri arejee shule???au tunaangalia vigezo gani???pls anyejua aniambie!

 11. kaboka Says:

  Naona Bwana Hombis huenda hufahamu kazi za fasihi.Muziki kama part mojawapo ya fasihi inaweza kutoa ujumbe ila si lazima sababu kazi nyingine ya fasihi ni kuburudisha ,kuriwadha nk,sasa kama ukisikiliza nyombo hii iwapo utaburudika ,hiyo inatosha ,kama fanani ametimiza kazi yake.

 12. kahindi Says:

  mi nampenda.na nampa tu ushauri aumize kichwa,atoke na mashairi yenye ujumbe wa maana..yapo matatizo mengi sana miongoni mwetu ambayo wanamuziki kama kina ay wakiyawakilisha through muziki yanaweza yakapata ufumbuzi,na sio kuimba 2 mashairi ya mapenzi mapenzi kila mara…kuhusu elimu yake mi sina idea ila ni rafiki wa karibu sana wa mwana fa….na nafikiri mwana fa hawezi kumwacha rafiki yake abaki m2pu bila hata kacertificate kokote….ni hayo 2….

 13. halima Says:

  hana makuu wala perepere full comercial hata akon amepiga salut hapo

 14. halima Says:

  Matty jamani nachanganyikiwa nikiangalia hako kamdomo mhh sijui bado yupo yupo duh mhhhh

 15. aligator Says:

  kwako hombiz,

  nina swali la kizushi! ujumbe wa wanamuziki wa marekani hasa ni upi? na wakati watanzania ndio tunaongoza kwa kununua kazi zao? kama sio kusifia gari zao,wanasifia mademu zao.sasa mbona mnamsema AY kwa kuimba nyimbo inayojielekeza kwake? naomba kuwasilisha

  aligator bunuzi

 16. binti-mzuri Says:

  kweli blackmannen umeongea! na star pia! – ujumbe huo AY.

 17. Edwin Ndaki Says:

  Haya bwana vijana wanataka kufika sijui ndio mnaita “platinamu”(mtanisahihi lugha watoto st schools na english medium)si unajua wengine tumesoma zile S.L.P S/M(shule ya msingi)

  Nimependa ala za huo wimbo ingawa kwa bahati mbaya sina ze oxfodi dishenari maana ze lugha waliotumia ukweli wameniacha kilomita kibao..achilia mbali ze braza wangu niliemuacha Longido sijui kama atanunua kazi hiyo labda …

  Wasanii wajitahidi kwanza kuhimarisha masoko yao ya ndani ndio kufungua mabano kwenda za majuuu …

  Kila la kheri Ambwene ila jitahidi kuwa na kaujumbe kaliko nyoka mbona wimbo wa Binádamu ulifanya fresh..au umeamua kurudi kwenye zile nyimbo zako za NI RAHA TU?

  Tutafika tu ..ingawa Matty anaogopa kufika kachoka..Hombiz mfumo unasemaje?

 18. queenchillah Says:

  nitumieni picha yake kwenye email adress yangu pliz kwsababu nampenda sana.

 19. pierre Says:

  yap yap hombizzo ifunda buoy…… big up*2 en keep it up bro……………

 20. Hombiz Says:

  Kaboka na Aligator! Napenda niwajibu kama ifuatavyo:
  Naanza na wewe kageta! Darasa langu la kipindi cha Kiswahili nilichosoma O-Level, linanitosha sana kuijua kazi ya fasihi simulizi ni nini. Still hiyo isiwe sababu ya mimi kupinga upuuzi mwingi uliopo kwenye muziki huu wa kizazi kipya. Hata siku moja mimi siwezi kukubali kupenda nyimbo kwakuwa ina mpangilio wa vyombo mzuri wakati msanii anaimba ugolo. Najua kuna nyimbo nyingi sana zilizotolewa na wasanii wa bongo ambazo ni za kuburudisha zina beats nzuri na mashaili sio ya ujumbe kwa jamii lakini yanaleta maana. Mtililiko wa mashairi ni mzuri na kinachosemwa kinaeleweka. Kwa mfano, nyimbo piga makofi ya professa Jay, of course nyimbo ile sio ya kuelemisha jamii bali kuburudisha tuu. Still kinachosemwa kiko kwenye mpangilio maalum unaoleta sense na unaeleweka pia.Sasa upuuzi huu wa freeze! hakuna kitu chochote kinacholeta maana kwenye mashairi anayo-flow nayo! He needs to change this nonsense and address important issues +ve writing.

  Aligator! Jibu langu kwa swali lako la kizushi ni kwamba, ujumbe wa wanamuziki wa kimarekani unategemea na mwanamziki unayemzungumzia na aina ya muziki anaojihusisha nao. Kuna wanamuziki wa miziki ya aina mbali mbali hapa marekani ambao wana ujumbe tofauti tofauti ktk miziki yao. Kwahiyo jaribu kuwa specific kwenye swali lako ili niweze kulijibu kulingana na uelewa wangu mimi.
  Unaposema wamarekani wanaimba nyimbo zinazosifia magari na wanawake zao tuu! Hapo sikubaliani na wewe hata chembe!. Kuna wanamuziki wanaoongelea mambo mengi ya muhimu ktk jamii kuliko wewe unavyofikilia. Hivi umewahi kuisikia nyimbo iitwayo Why ya Jadakis? Bila shaka pia unaifahamu nyimbo ya Tupac iitwayo Dear mama?. Vile vile inafaa usikilize wimbo wa Pink uitwao Mr. President. Unamkumbuka Scarface na nyimbo yake zenye ujumbe kibao?.

  Unaponiambia kuwa watanzania ndio tunaoongoza kununua nyimbo za wamarekani walioimba nyimbo zinazoongelea magari na wanawake zao, mimi nasema hiyo sio kweli. Soko la nyimbo za wamarekani, linaongozwa na wamarekani wenyewe. Sidhani kama Tanzania ni inashika hata namba kumi ktk ununuzi wa nyimbo hizo. Wakati huo huo, ni lazima uelewe kuwa nyimbo zenye negative image kwa jamii hivi sasa zimeanza kupigwa vikali sana marekani kaskazini. Organizations mbali mbali zinazopinga upuuzi huo zimeanza kuwabana wamiliki wa record companies ili wabadili muelekeo wa kupigia debe utengenezaji na uuzaji wa nyimbo zenye ujumbe mbovu kwa jamii hasa ktk Rap Music. Baadhi ya nyimbo zinazoendelea kupigwa vita ni zile zinazodhalilisha wanawake na kuongelea uhalifu, mauaji, umiliki wa siraha na matumizi ya madawa ya kulevya. Nakumbuka Russell Simmons na baadhi ya wadau wakubwa wa music wa Rap, waliwahi kuwekwa kiti moto kwenye Oprah show na walikili kuwa muelekeo wa muziki huo si mzuri na unahitaji marekebisho ya hali ya juu kv kuwanyima record deals wasanii wanaotaka kuimba upuuzi kwenye nyimbo zao, ikiwemo na matumizi ya neon Nigga ambalo dhumuni lake halisi toka kwa wazungu wabaguzi lilikuwa ni kumdhalilisha mtu mweusi.
  Mwisho kabisa Aligator, napenda kukuuliza wewe hivi: Hizo nyimbo za wamarekani zilizojaa negativity wewe unazinunua za nini wakati unajua wazi hazijengi lolote ktk jamii? Uma na wewe una utumwa wa akili wa kuona kila anachofanya mmarekani ni cha kuigwa? Mimi sikufahamu wewe hapo ulipo lakini ningefanikiwa kukuona nisingeshangaa kuona umevaa suruali yako ikiwa inaning`inia chini ya makalio yako.

  Edwin Ndaki, mimi napenda tufiki lakini tukiwa na na energy ya kutosha na sio tukiwa choka mbaya!
  Stay up as always!

 21. mdau Says:

  kaka ujumbe wa wadau umeusikia,inabidi ukaze buti kaka AY.

 22. Kweliman Says:

  wooote mnaozungumzia elimu hapo juu ni upuuzi mtupu mnaouongea .kijana anakipaji hiyo ndio elimu yake
  sasa mnataka kila mtu awe accountant au md au lawayer?
  acheni mitazamo finyu AY yuko juu anakipaji na anakionyesha ktk kazi zake anazofanya
  elimu yake ndio hiyo hiyo shughuli anayofanya elimu sio lazima kuenda chuo kikuu au formal school hasa kwa wasanii bali kwa maoni yangu ni kwamba aendelee kujielimisha through non traditional ways adumishe na kuboresha muziki wake na ajifunze kwa ukamilifu yale yanyohusiana na muziki wake na takataka zingine za accounting,llb,md au diploma zisizohusiana na mziki wake labda hana kipaji au skills hizo za madiploma yenu ya business adminstration lakini ana elimu na upeo wa kujiendeleza along the lines of his music genre, au god given gift nk
  Na pia mziki sio lazima uwe na ujumbe kuna wengine wanapenda mziki fulani kwa sababau zingine kabisa na si lazima ujumbe isitoshe weather kuna ujumbe au hakuna AY amefanya kazi yake ya kiusanii ni juhudi imetumika anastahili recognition
  acheni wivu wenu give credit where credit is due
  Kwaliman
  Edmonton
  Canada

 23. BLACKMANNEN Says:

  Kwako Mkuu “Hombiz”,

  Kwa muda mrefu ndugu yangu, nimekuwa nikiziona comments zako hapa zilizojaa chuki na dharau kwa viongozi wetu wa Tanzania, na hata kwa watoa mada zao hapa BC, nilikumezea tu.

  Ndugu yangu Hombiz, nakuomba ujaribu kuzirudia tena kuzisoma comments zako hapo juu, na ujaribu kuyatafakari kwa kina sana yale yote ambayo umeyasema hapa na huko nyuma, ambako nitakujibu pia.

  Mapenzi yako makubwa kwa nchi ya Marekani unakoishi wewe, (ambako wewe unajiona UMEFIKA), yasikufanye kukuweka pabaya na sisi Watanzania wenzako, ndugu zako tukupendaye. Watanzania (unaowadharau) wanachokifanya ni kujitengenezea kile wanachokitaka wao na kinakubalika na watanzania wenyewe, sio lazima ukipende wewe na Wamarekani wako. Kwa hiyo wewe kama kuna vitu Watanzania wanakifanya kina mapungufu ukilinganisha na Marekani, huko uliko wewe, nakushauri utuachie sisi wenyewe Watanzania. Sisi tunaiona Tanzania yetu tambarare, imenyooka, na hatuna makuu.

  Matumizi ya maneno kama “……upuuuzi……”, sio dharau tu kwa yule unayemwongelea, bali ni hata wale wapenzi wake umewaona “Wapuuzi”. Sisi sio wapuuzi.

  Unataka Wasanii wetu watunge mashairi yahusuyo “… kukumbatiwa kwa Ufisadi ndani ya serikali, kero za walimu na mauaji ya maalbino n.k.” Je, nyimbo za aina tunazotaka sisi, zinazozungumzia Ubabe wa Marekani katika kuvamia nchi zingine, na kuiba mafuta ya nchi hizo, na hata kuwachukia wafuasi wa dini ya “Kiislamu” duniani, kwa kuwapakazia Ugaidi, zina soko kubwa huko Marekani?

  Tukitaka kukuchambua wewe “Hombiz” hapa sasa hivi, utajikuta hata kile kiswahili ulichojisifia kukijua, utaona kuwa hukijui, maana pahali panapotakiwa kutumika “r” unatumia “l”, lakini kwetu sisi makosa yako hayo, hayatufanyi tukudharau na kuanza kukutolea maneno ya kashifa, tunachoangalia ni ujumbe wako kwetu. Nakuomba umtake radhi “Aligator”, kwa kumwambia kuwa “…..nisingeshangaakuona umevaa suruali yako ikiwa inaning’inia chini ya makalio yako”. Mimi sikupendezwa na maneno yako hayo. Nimeona umemtusi MwanaBC mwenzako.

  Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitawashukuru “SisterTZ, Binti-Mzuri, Kaboka na Aligator”, kwa coments zenu nzuri.

  This Is Black=Blackmannen

 24. Matty Says:

  Halima shosti huyu nasikia hayupo hayupo namaanisha kinyume cha yupo yupo sijui kama unanipata maana ashajicomit kwa watani zetu mungiki upo mpaka hapo shosti???
  Hombiz gazeti lako mzalendo walai limekwenda shule point bila kificho no mafumbo hapo BIG 5!

 25. XXX Says:

  AY anatarajia mtoto (cjui km keshazaliwa) na amani wa kenya!

 26. XXX Says:

  hizi foto labz za bongo bwana zina over dot!mtu una editiwa mpk sura inakuwa haina uhalisia bwana ….

 27. star Says:

  Kweliman nadhani ndugu yangu hakuelewa what we meant by elimu..
  na kama uliota vile maana umetaja profession yangu kwenye hiyo comment yako.. unajua ELIMU we meant not only studies na LLB or ACCOunts ila hata elimu ya usanii upo hapo ?? Maana kama unavyosema labda kichwa chake ndio kichwa maji basi aende kujielimisha zaidi, wewe upo huko Canada sijui kama unakujaga TZ mara kwa mara,, ukiwaona hawa vijana ndugu yangu utawaonea huruma kwenye interview yeyeto akifungua mdomo tu then you will know uwiiiiiiii FORM FOUR FAILER au std 7.. We angalia wezetu wakenya kuna degree holders kibao ni wanamusic and they are doing better na hata huku ulaya wanaonekana wa kwetu ndio kila siku mnasema music wetu bado mchanga mchanga mpaka lini?? lazima hao wanamusic wetu we international ndio watapata pesa ya kutosha tusidanganyane hapa kwenye hii colum .. na eti unasema sisi tuliosema wanamusik wa TZ waende shule tunawaonea wivu (yaani ungejua tu hatuna shida ya pesa ila hao wanamusik wanashida na pesa sana wengi wao si wanakaa uswazi) ..yaani wewe kaka yangu ndio haulewi kabisa issues..na kumbuka kwamba -constructive critism- ndio inajenga kuliko kusifiasifia tu..

  BLACKMANN nakaribisha busara zako maana wewe kaka yangu naona we are speaking at the same level

 28. halima Says:

  Kweliman before hujawaambia watu wapuuzi unatakiwa utafakari kwanza inawezekana wewe ndio mpuuzi kuliko hao unaowaona wapuuzi.

  Dunia ya sasa bila elimu nafikiri ni sawa unatembea barabarani huku umevaa suruali aina mkanda wala kifungo nini kinachofata utamalizia……. Kwako wewe kama unaona elimu haina maana basi ni vema na haki usipowapeleka watoto wako shule wasubirie bahati yakuja kuwa milionea asiyekwenda shule.

  HABARI NDIO HII

 29. sisterTZ Says:

  Kwelimann,Hombizz nawaomba sana uheshimu mawazo ya watu katika forum hii..maana umesema sisi wote tunaongelea elimu kwa hawa vijana si sawa…mimi naomba nitofautiane na wewe..

  unajua watu wengi hawaelewi elimu inasaidiaje ktka maisha..unajua kuwa na elimu sio kwamba ndio unakili sana kupita wengine BUT inakusaidia kufikiria na kuona vitu/mambo vingi kwa mtazamo tofauti na wale ambao hawajaenda shule …na pia elimu inasaidia kukubali kukosolewa…(maana naona watu wengi hapa hawapendi comments za kukosolewa mwanamusiki)

  ..sasa wewe unavyosema sisi hatutaki kumpa-credit huyu mwanamusiki ni sawa kabisa, ila sisi kama wasomi tunaona ni vema pia apewa constructive critism ili aone makosa yake ect…na ndugu yangu believe me mtu ambae hataki kukuonyesha short coming zako sio mtu mzuri, kwa sasababu NO ONE IS PERFECT..mimi wanamusic wa Bongo na interract nao mara kwa mara jamani elimu zao ni zero jamani..tuwaonee huruma..because vijana wote wanaoshindwa shule wanaingia kwenye music…mimi kwa upande wangu ningependa sana ktk corum hii tutoe comments ambazo zinajenga na sio comment za kuradharau,kugombana ect

  BInti mzuri, Blackmann,halima kwani nasema uongo?

  nipo tayari kukosolewa (siogopi maana i know i am not perfect)

 30. Gervas Says:

  Wanaoshauli Aende shule, hivi mnaposema shule mnamaanisha shule katika level gani? Chamsingi hapa ni Kuwa na elimu tu reasonable ya kujua mambo ya msingi, hasa hasa communication ndio cha maana. Maana waweza kuandikiwa verse then una-flow. Kumbukeni mziki ni art, nikipaji na sio lazima ili uwe mwanamziki bomba lazima ukakomae na midigrii ndo ufanikiwe….tafadhali msiwachanganye vijana Ebo!!!

 31. hombiz Says:

  BLACKMANNEN, BC huu ni uwanja wazi wa kutazama picha iliyobandikwa na kisha kutoa maoni yako binafsi. Mtazamo wangu mimi juu ya mambo mbali mbali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii si lazima ulingane na wako wewe. Na kukosea ktk kuandika mambo kadhaa ktk lugha yangu ya kiswahili, hili halininyimi utanzania wangu. Pia, kukosoa mambo yasiyofaaa ktk serikali ya Tanzania na ufisadi wake, havinifanyi mimi kutokuwa mtanzania. Mimi ni mtanzania mwenye machungu na nchi yangu na kila ninachokosoa juu ya jambo lolote, nasimama ktk mtazamo wa kujenga na si kubomoa. Umedai kwa muda urefu umekuwa ukizisoma Comments zangu kwenye mtandao na kutopendezwa nazo. Mimi sikulazimishi upendezwe nazo au kutafuta redhaa kwako. Bali naandiki kile ninachokiona ni cha maana in a constructive way, kulingana ni uelewa wangu wa mambo na upembuzi wangu yakinifu wa mambo mbali mbali. Sasa kama umeguswa na comments zangu kwa njia moja ama nyingine, ushauri wangu kwako ni kuyafanyia kazi niliyoyaongea ktk mtazamo wa maendeleo.
  Ila usitegemee hata siku moja kuwa mimi nitaacha kutoa maoni yangu kila ninaposoma posts mbali mbali kwenye uwanja huu. Nitaendelea kufanya hivyo kwa moyo mkunjufu na kulingana na vile ninavyofahamu mimi.
  Hakuna ninalolijutia juu ya yote niliyowahi kuyaandika huko nyumba na wala sitaomba radhi juu ya lolote nililokwisha liandika hapa BC.
  Blackmannen!, Hombi ni mtanzania halisi ambaye sina tattoo bali alama ya ndui. Tanzania naipenda lakini viongozi mafisadi,mabilionea wa vijisenti siwapendi na sitowapenda kabisa mpaka watakapoacha ufisadi wao na kufanya kazi kwa manufaa ya nchi.
  Blackmannen, Hivi kero za viongozi wabovu wewe huzioni?. Wazee wastaafu wanaohangaika kudai mafao yao miaka nenda miaka rudi wewe huwahurumii?, pesa za misaada zinazotolewa na mataifa makubwa kwa ajili ya kusaidia wagonjwa wa ukimwi lakini wajanja wachache wanazitafuna huku wagonjwa wakiendelea kuteseka wewe unaona ni burudani kwako?, mikataba mibovu ya kufisadi nchi hiyo inakufurahisha wewe?, walimu kulipwa mishahara kiduchu isiyolingana na kazi yao hiyo ni heko kwako?, Kiongozi kuuwa raia mwema kwa kumpiga risasi na sheria kumuachia huru, wewe unaona ni poa tuu!?
  Kwa upande wa wasanii wa marekani ambao wametoa nyimbo ambayo inapinga, vita, ugaidi na ambayo ilipinga wazi wazi kutojali umaskini na ukimwi uliokithili duniani na ikatamba sana hata marekani inatoka kwa kundi liitwalo black Eye pea. Lisome hilo kundi na nyimbo yao ambayo ilifanya vizuri sana nchini marekani kwa kubonyeza hapa http://en.wikipedia.org/wiki/Where_Is_the_Love%3F
  Wakati huo huo unaweza kupata JADAKISS LYRICS wa nyimbo yake iitwayo WHY hapa chini:
  “Why”
  (feat. Anthony Hamilton)

  [Jadakiss]
  Aha
  It’s dat real
  Yo, why is Jadakiss as hard as it gets
  Why is the industry designed to keep the artist in debt
  And why them dudes ain’t ridin’ if there part of your set
  And why they never get it poppin’ but they party to death
  Yea, and why they gon give you life for a murder
  Turn around only give you eight months for a burner, it’s goin down
  Why they sellin’ niggaz CD’s for under a dime
  If it’s all love daddy why you come wit your nine
  Why my niggaz ain’t get that cake
  Why is a brother up North better than Jordan
  That ain’t get that break
  Why you ain’t stackin’ instead of tryin’ to be fly
  Why is rattin’ at an all time high
  Why are you even alive
  Why they kill Tupac n’ Chris
  Why at the bar you ain’t take straight shots instead of poppin Crist’
  Why them bullets have to hit that door
  Why did Kobe have to hit that raw
  Why he kiss that whore
  Why

  [Chorus: Anthony Hamilton]
  All that I been givin’
  Is this thing that I’ve been living
  They got me in the system
  Why they gotta do me like that
  Try’d to make it my way
  But got sent up on the highway
  Why, oh why
  Why they gotta do me like that

  [Jadakiss]
  Why would niggaz push pounds and powder
  Why did bush knock down the towers
  Why you around them cowards
  Why Aaliyah have to take that flight
  Why my nigga D ain’t pull out his Ferrari
  Why he take that bike
  Why they gotta open your package and read your mail
  Why they stop lettin’ niggaz get degreez in jail
  Why you gotta do eighty-five percent of your time
  And why do niggaz lie in eighty-five percent of they rhymes
  Why a nigga always want what he can’t have
  Why I can’t come through in the pecan Jag
  Why did crack have to hit so hard
  Even though it’s almost over
  Why niggaz can’t get no jobs
  Why they come up wit the witness protection
  Why they let the terminator win the election
  Come on, pay attention
  Why sell in the stores what you can sell in the streets
  Why I say the hottest shit but we sellin’ the least

  [Chorus]

  [Jadakiss]
  Uh, yea, yo
  Why Halle have to let a white man pop her to get a Oscar
  Why Denzel have to be crooked before he took it
  Why they didn’t make the CL6 wit a clutch
  And if you don’t smoke why the hell you reachin’ for my dutch
  Why rap, cause I need air time
  Why be on the curb wit a “why lie I need a beer” sign
  Why all the young niggaz is dyin’
  Cause they moms at work, they pops is gone, they livin’ wit iron
  Why they ain’t give us a cure for aids
  Why my diesel have fiends in the spot on the floor for days
  Why you screamin’ like it’s slug, it’s only the hawk
  Why my buzz in L.A. ain’t like it is in New York
  Why you forcin’ you to be hard
  Why ain’t you a thug by choice
  Why the whole world love my voice
  Why try to tell ’em that it’s the flow son
  And you know why they made the new twenties
  Cause I got all my old ones
  That’s why
  BLACKMANNEN! I`m not done yet!
  I`ll be back!

 32. Bob Sambeke Says:

  E bwana nyie mnaozungumzia kama ay ana shule? mbona mkomalia shule sana,hivi mnajua kwamba kila m2 anadream ya kuma-fortunes na mnazijua njia za kumake-fortune,Nadhani hamzifahamu.kwani mngezijue msingekomalia shule shule! Kwa taharifa yenu kunav2 vingi m2 anaweza akafanya akamake-fortune kwamfano
  1.Kurithi mali,kwa mfano CMB $prezzo$
  2.self-made eg Prince Alwaleed Bin Talal Alsaud
  3.kupitia sanaa eg Tiger wood
  4.Ufisadi(Fraud) Nadhani mnawajua hilo cwezi kuliongelea
  5.Kusomea fani flani na kuwa mtaalamu

  na vi2 vingine cwezi kuvimaliza,kwahyo mckomaile tu ay kasoma au hajasoma,hyo aikuhusu.Ay ni Entreprenuar wa kufa m2 na rafiki yake Prezzo(Msanii Tajari kuliko wote EA)
  Hanawapita wote wabeba box na Degree Zenu hizo
  Ay Ameamua Kupitia Sanaa ili amake-fortune,Na nyie wabeba box mmeamua kupitia shule,Je mnaishi fresh kwa kutumia hiyo elimu yenu? Ay Anaishi fresh sana na Ana kampuni yake fresh kwahyo msimlazimishe kusoma wakati anatumie other means kumake mawe!
  Habari ndo hiyo

 33. Carlito Says:

  AY anafanya vizuri katika medani ya music hapa nyumbani na hata nchi za jirani!Ana kipaji na kipaji pia ni Elimu hivyo swala la kusema kwamba akasome ni kila mtu anatakiwa akasome kama mtu unaona kuna ulazima wa kufanya au kuitafuta hiyo Elimu kwa sababu Elimu haina mwisho!Anafanya vizuri katika kazi zake na nyimbo zake kibao zinahit kwenye vituo mbali mbali hapa kama ambavyo tunaona ingwa safari bado ni ndefu na siyo yeye tu wanamuziki kibao ulimwenguni,
  Mimi kama mimi huu ni mtazamo wangu na nimtakia mafanikio mazuri katika safari yake ya kimuziki tuache kuponda poanda kila kitu siyo lazima u-comment utumbo tu kwa sababu tu unataka u-comment sometimes tuone aibu dah

 34. halima Says:

  Aiseee Bob sambeka wewe ndio umechemka kabisa kwasababu hizo ndoto unazoota za kurithi mali au kuwa na rafiki tajiri sio za dunia hii ya sasa.

  Jua kuwa elimu ni kitega uchumi chako ambacho hakuna mtu ambaye anaweza kukitaifisha. usitoe mifano ambayo haina mbele wala nyuma hapa all in all lazima kijana apate elimu.

  Hata kama nikurithi mali utaziendeshaje without education? au ndio nyinyi ambao mtaajiri watu kwa ajili ya kukuangalizia hizo mali?

  Bob sambeka unataka kuniambia wewe hujaenda shule au ndio wale ambao wanapenda kuwapotosha watoto wa wenzao

  Sister tz habar umeongea point lazima dogo awe na elimu sio blablaaa hapa
  HABARI NDIO HII

 35. binti-mzuri Says:

  wewe Bob Sambeke my friend, prezoo (msanii tajiri kuliko wote EA kama ulivyosema) kwa taarifa yako hiyo hela ameirithi kwa baba yake, yeye akiwa mtoto pekee, na baba yake alisurubika shule kujakutengeneza ilo kampuni na kuliendesha as C.E.O he has been lucky to have a hard working father,aliemrithisha hizo mali, yeye hajazitafuta from scratch, kaja kuchukua madaraka baba yake alivotangulia. hizo hela hajazipata from muziki. please usichanganye watu humu ndani

  ila mjadala wa leo humu,kaaz kweli kweli, naona pande zote wanatoa points heavi!

 36. binti-mzuri Says:

  oh my bad bob, u do say kwamba kazirithi. kumradhi! naanza kupofuka mie lol

 37. papuu Says:

  wewe queenchillah,picha si ukopi pest apo,au unataka tu umaarufu! kwanza ana mke huyo a.k.a amani, mwanamuziki wa kenya. naanzisha mada ‘ hivi ni lini wanawake wa kitanzania wataasha kushabikia wanamuziki?’

 38. papuu Says:

  bobu sambeke, AY ana kampuni gani?tafadhari nijibu haraka sana, kabla sijaongeza zaidi ya kukuumbua.

  AY fanya kazi,piga buti, mziki waburudisha, ila punguza pombe mshkaji

 39. kijiwe Says:

  ushauri wa bure jamani someni kitabu kinachoitwa “Capitalist Nigger” that is all we need siyo kupigiana porojo za kwenda shule au nini.
  Yes shule inaweza kusaidia kwa namna moja au nyingine especially katika kuchangamsha akili I mean unaweza kuwa na options nyingi katika jambo fulani kama umeenda shule lakini pia hii haimlimit mtu mwenye kipaji kuwa enterprenuer e.g A.Y
  na katika suala la kuchana mistari yes katika huu mwimbo probably alifikiria vitu 2 local market(TZ),western africa & africa nzima kwa ujumla.
  hawa jamaa aliofanya nao collabo wameuza sana katika soko la africa (they are extremely succesful)lakini wanachoimba ni mademu na kujirusha tu!then kama A.Y kafanya nao collabo anaangalia usawa pia ndiyo maana kachana mistari ya kujirusha rusha!
  he knows what he wants and he gets it most of the time.wengi wetu tunamkosoa jamaa wa watu na tuna midegree chungu mzima but the main problem is we dont really know what we want so tunaishia kulipa bills,rent na matumbo!
  do we have some savings at any given sunday?am afraid not.
  make sure you see it in your swag brothers and sisters and stop hating!

 40. hombiz Says:

  Blackmannen!,Kaboka na Aligator: nyimbo nyingine ya RAP toka kwao Black Eyed Peas ambayo ilivuma sana marekani na kupelekea hili kundi la muziki wa RAP MUSIC kushinda tozo kede-kede ni ule uitwao “Where is the love” ambao lyrics zake ni hizi zifuatazo:
  What’s wrong with the world, mama
  People livin’ like they ain’t got no mamas
  I think the whole world addicted to the drama
  Only attracted to things that’ll bring you trauma
  Overseas, yeah, we try to stop terrorism
  But we still got terrorists here livin’
  In the USA, the big CIA
  The Bloods and The Crips and the KKK
  But if you only have love for your own race
  Then you only leave space to discriminate
  And to discriminate only generates hate
  And when you hate then you’re bound to get irate, yeah
  Madness is what you demonstrate
  And that’s exactly how anger works and operates
  Man, you gotta have love just to set it straight
  Take control of your mind and meditate
  Let your soul gravitate to the love, y’all, y’all

  People killin’, people dyin’
  Children hurt and you hear them cryin’
  Can you practice what you preach
  And would you turn the other cheek

  Father, Father, Father help us
  Send some guidance from above
  ‘Cause people got me, got me questionin’
  Where is the love (Love)

  Where is the love (The love)
  Where is the love (The love)
  Where is the love
  The love, the love

  It just ain’t the same, always unchanged
  New days are strange, is the world insane
  If love and peace is so strong
  Why are there pieces of love that don’t belong
  Nations droppin’ bombs
  Chemical gasses fillin’ lungs of little ones
  With ongoin’ sufferin’ as the youth die young
  So ask yourself is the lovin’ really gone
  So I could ask myself really what is goin’ wrong
  In this world that we livin’ in people keep on givin’
  in
  Makin’ wrong decisions, only visions of them dividends
  Not respectin’ each other, deny thy brother
  A war is goin’ on but the reason’s undercover
  The truth is kept secret, it’s swept under the rug
  If you never know truth then you never know love
  Where’s the love, y’all, come on (I don’t know)
  Where’s the truth, y’all, come on (I don’t know)
  Where’s the love, y’all

  People killin’, people dyin’
  Children hurt and you hear them cryin’
  Can you practice what you preach
  And would you turn the other cheek

  Father, Father, Father help us
  Send some guidance from above
  ‘Cause people got me, got me questionin’
  Where is the love (Love)

  Where is the love (The love)
  Where is the love (The love)
  Where is the love
  The love, the love

  I feel the weight of the world on my shoulder
  As I’m gettin’ older, y’all, people gets colder
  Most of us only care about money makin’
  Selfishness got us followin’ our wrong direction
  Wrong information always shown by the media
  Negative images is the main criteria
  Infecting the young minds faster than bacteria
  Kids wanna act like what they see in the cinema
  Yo’, whatever happened to the values of humanity
  Whatever happened to the fairness in equality
  Instead in spreading love we spreading animosity
  Lack of understanding, leading lives away from unity
  That’s the reason why sometimes I’m feelin’ under
  That’s the reason why sometimes I’m feelin’ down
  There’s no wonder why sometimes I’m feelin’ under
  Gotta keep my faith alive till love is found

  People killin’, people dyin’
  Children hurt and you hear them cryin’
  Can you practice what you preach
  And would you turn the other cheek

  Father, Father, Father help us
  Send some guidance from above
  ‘Cause people got me, got me questionin’
  Where is the love (Love)

  Where is the love (The love)
  Where is the love (The love)
  Where is the love (The love)

  Where is the love (The love)
  Where is the love (The love)
  Where is the love (The love)
  Wakati huo huo BLACKMANNEN napenda kukukosoa kuwa mimi sijasema nafananisha muziki wa Tanzania na Marekani. Pia sio kweli miziki ya kitanzania mimi siipendi. Where did i say that!?. Tangu awali nimeainisha kuwa napenda miziki ya wasanii wa bongo flavar ambao wanaimba nyimbo zenye ujumbe mzuri kwa jamili na wenye mashaili yanayokubalika mama Profesa JAY na nyimbo yake Nang`atuka,Bongo Dar-es-salaam, Nang`atuka n.k., Mr. 2 (na nyimbo yake wapi tunakwenda na ule mwingine wa -ana miaka ndani ya 18). Pia kuna msanii wa Injili Rose Mhando na album yake ya “nakaza mwendo” na nyimbo nyingine nyinge za wasanii wengine zenye kuleta maana. Lakini sio upuuzi wa FREEEEEZE! wa AY!. Naludia tena nyimbo hii FREEZE ya AY, ni upuuuuuuuuuuuziiiiii!.

 41. Kweliman Says:

  jamani mimi nauliza how do we define ELIMU as related to AY’s case.
  ukiachia mbali suala hilo la elimu bado mimi nasisitiza, kwa maoni yangu ni kwamba kijan understands exactlly ni nini anachotaka na anachofanya kwa kweli anakipaji na mziki wake ni mzuri ofcourse ktk mtindo anaoufanaya
  AY nakupa hongera nyingi you have come a long way to get where you are now
  ushauri wngu kwqko AY ni kwamba jitahidi kutafuta na kuanzisha mbinu za kulinda kazi yako na compasation inayoendana na jasho lako hasa uktilia maanani sual zima la teknolojia
  kaka AY endelea ku- stay focused.always believe in nobody but youself kam ambavyo umekuwa ukifanya siku zoote
  great job!
  Kweliman
  great job!

 42. Bob Sambeke Says:

  Ay ana kampuni nenda Millenium Tower utaona tu! Uliza Walinzi nataka Niende Ofc ya Ay watakupeleka,Na wewe halima Navyozungumzia Kwamba Kuna Aina Nyingi za kumake fortune Mojawapo ni Kurithi Mali! Na cjasema kwamba prezzo kapata pesa kwa ajiri ya Music,The Guy is The CEO wa Herbal Makini,Mbona manji na yeye karithi? Nazungumzia Kuna Njia nyingi za kumake $$$$

 43. halima Says:

  Hivi watu bado wanaota ndoto za kuwa na rafiki mwenye pesa au kurithi pesa za marehemu? duuuhhh ni kichekesho mwenzio akaze mkanda kutafuta wewe uje tu urithi mtangoja milele.

 44. Matty Says:

  Leo i can’t open ma mouth, just reading and singing from u guys!!!!!!!!!!

 45. sisterTZ Says:

  dada Halima hi comment 35 imeipenda sana.. Bob Sambeke wewe umeenda shule kweli? kwanini unapinga elimu

  Yaani mimi nishindwa kuelewa watu wengi wanavyopinga Elimu humu ndani, eti simple bec kijana anakipaji… kuna mambo mawili AY hao unaokushauri usisome either hawakutakii mema au wenyewe pia shule hawajaenda, na jamani wanzangu mimi najua sana kwamba vijana wengi wa TZ huko USA hawasomi wanafanya kazi za kuosha wazee na kufagia barabara.. (jamani home hata sisi mbona tumekaa miaka mingi tu huko USA?)

  Sasa mdogo wangu mtu ambae anakaa USA na hasomi we unadhani atakushauri nini? si ndio hao wanakwambia usibiri urithi..ujinga mtupu..

  Mnajua mimi binafsi nilikuwa nafikiria huyo kujana asome ili awe na plan B kama musiki usipofanikiwa..yeye anaweza kuendeleza na kitu chochote ambacho anaweza…unajua kuwa very honest mimi naona kipaji chake sio kama ndio eti kitamtoa ktk huo umasini wake (bado sijaamini hivyo)..ndio maana namshauri huku akiwa anafanya music asome kitu chochote au ajiendeleze katika usanii..kuna kaka mmoja hapa kwenye maoni alitoa hoja nzuri sana nadhani jina lake ni MLEBA na inaelekea yeye haya mambo ya usanii ni fani yake amesomea na anaelewa issues..mawazo yake yalikuwa mazuri sana..(Angelieni kwenye maoni ya the comedy mtaona maoni yake mazuri)…

  Ila mdogo wetu AY wewe ni mtu mzima na una haki ya kukaa chini na kufiria kama uende shule au la…ila kumbuka kwamba hawa watu wanaokushauri hawakujui ila wanakutakia mema..U R AT LIBERTY TO ACCEPT OR DECLINE AN ADVICE kazi kwako..

 46. mtu Says:

  Binti mzuri, Matty na Halima, mna nishangaza sana, badala ya kuuchambua ujumbe wa nyimbo, nyinyi mnazimikia urembo wa mtu, kweli mnanifanya nione ujumbe wa Mwana fa, kwenu kuwa ni wa kweli, yaani mmeona kijana hana pinpoz tu ndio dili, hatu katai kumtamani mtu lakini angalieni na mada.
  Mzee Hombiz nakupa big up kwa mchango wako, na katika list ya wanatoa msg zenye busara muongeze Afande Sele, ambaye nakumbuka ni mwanafunzi wa Mr. 2 usisahau kundi la Mandojo na Domo kutoka A town.

 47. mtu Says:

  Kamchango kangu basi, Music ni Industry kubwa sana, inafundisha na kufundisha, ina kanya na kurekebisha pia ina furahisha na kuburudisha nk.
  Wanamziki nao wamegawanyika katika mlolongo huohuo, wapo wanao elimisha, na wapo wanao burudisha na kukanya. Na wapo wanye mambo yote matatu. Wanamuziki wanakuwa influenced na mambo tofauti ili kuandika nyimbo ya muelekeo fulani. Kwamfano mwanamuziki akitetereke kimapenzi, na ikamuathiri basi akili yake itarespond to the problem, Mfano Juma Nature alipo toswa na Sinta, Lady JD alipokuwa na matatizo na mpenzi wake kabla hawajaowana nk, Pdiddy aliimba I need a girl pindi alipo achwa na Jlo nk. Na kwakuwa wapo wengi ambao wanakuwa katika same situation basi hao wote wanatokea kuupenda wimbo kwani umekuja in the hour of need. Wanamuziki wengine huimba burudani tu kwani wanakuwa katika peak ya furaha, wao huenda asiwe na ujumbe wa maana(mitungii, mikasi) lakini kwakuwa yuko happy basi ana express furaha yake. Na watu wengi katika situation hiyo basi watatokea kuupenda wimbo huo.
  Sasa basi hakuna ubaya kuimba wimbo kwa ajili ya burudani tu, kwani jamii inahitaji burudani sometimes we need to forget our problems and be happy, provided that they don’t segregate gender. Atleast thats how i understand

 48. mtu Says:

  Mimi nadhani music as music ni talent, tangu enzi za mababu zetu watu walikuwa wanaimba na kuburudisha kuelimisha na kukanya jamii through music. Asilimia kubwa ya wanamuziki duniani, marekani mfano mkubwa hawaenda shule. Michael Jackson, Madonna, Jlo, Snoopy tena hao marapper ndio usiseme woooooote hawajaenda skuli. Ila wengi wao wamejisomesha baada ya kupata mafanikio katika music. Talent is like a gift, you are just born with it beckham kwa mfano was just born to be, then you go to school for other reasons but not music. Music is to express feelings of love, oppression kama ubaguzi wa jinsia na rangi nk kiujumla kuexpress matukio katika jamii fulani.

 49. binti-mzuri Says:

  ‘mtu’ na wewe bwana. kizuri cha sifiwa! angekua kawekwa demu kama ray c hapo,am sure hata wewe ungecomment. maybe limekujaa coz wewe pia ni mwanaume,na naonaga wanaume wengi wanakua na kwanini anaposifiwa mwanaume mwenzao.. anyway,habari ndio hiyo.. AY mzuri tuuu!!! nothing we can do about it. kama watu walivyosema huko juu,tunajua ana mchumba wake, na wanatarajia mtoto. sasa ujumbe gani wa mwanaFA unaonihusu mie?kwamba mi kicheche? coz nimsifia mtu mzuri. we vp, unajuaje kama akinitokea sitamtolea nje? embu watch that mouth of yours before it takes you to hell. Maandiko yanasema,watu huponzwa na midomo yao.. in your case,i suppose your hands too.

 50. binti-mzuri Says:

  sister tz namba 29 wala hujasema uwongo… tema cheche shosti! PREACH!

  BLACKMANEN thanx for the shout-out

  hombiz thanx for the lyrics

 51. mtu Says:

  Binti mzuri, samahani kama nimekuboa, ila nilicho maanisha mimi ni kwamba topic, ilikuwa tofauti, wakati wagumu wanalumbana kuhusu wimbo, mwimbaji na maudhui ya wimbo, nyinyi mnaleta pimpoz, urembo, matamanio fulani, inshort it was out of topic. Kama ingekuwa ni kutoa sifa mbona hapo sawa. NIlitaka kukurudisha kwenye mada thats all. kwamfano Mzee Hombiz na masela wamehama kutoka kwenye hoja na sasa wanavagaana wenyewe, hiyo noma na wala haijengi, na mimi sijukuingilii wewe kama wewe, yaani ‘binti mzuri’ why would I do that to you cutie?, lakini ni topic ndo imesababisha.

 52. Matty Says:

  Mtu wewe unatafuta niongee wakati hapo juu nishasema am just reading and singing only!
  Sasa sikia mtu ukweli ni kwamba AY anavutia hata wewe muangalie uone so kizuri chasifiwa ma dear, sikuwa na point yoyote zaidi ya kumsifia naomba kuwakilisha nadhani am able and regret that!

 53. halima Says:

  Mtu sina lakuongeza nafikiri Bint-mzuri ameniwakilisha kizuri lazima kisifiwe. kula 100 Bint mzuri hahahhahah

 54. Toni Says:

  Jamani kama ni swala la elimu naomba niwape taarifa kiduchu wadau wenzangu. producer wa huo wimbo nasikia ni Dokta halafu ana degree ya music kama sound engineer.ukisikiliza vizuri utaona utofauti wa muziki wake na ma’prodyusa wengi wa bongo hasa kwenye quality.sijui kama amesharudi bongo au yupo huko alipochukuliwa na wazungu.na Aynae najua ana ka’degree flani ka biashara ndo maana anawapiga bao wasanii wenzake.kama wangekua na akili wangewafuata ay na huyo prodyusa wawasaidie.wabongo wapo wanaoweza kufikisha muziki wetu mbali tatizo badala ya ku’support kwa positive thinking sis ndio wa kwanza kuponda.inatia aibu jamani

 55. Talib Kweli Says:

  kaka black achana na wanaojifanya wajua kila kitu kumbe ‘magorofani’ hamna kitu.nimeickia nyimbo na imesimama ile mbaya!!!asituzingue huyo hombiz kama hajaikubali nyimbo kimpango wake,majani alimuita commercial kwa sababu bana,hakukurupuka tu,anajua soko linahitaji nini na anadeliver.huyo tupac wa dear mama ndo huyohuyo wa HIT’EM UP!!so sio kla wakati tutaskiza politiki au matatizo tu,tunahitaji burudani pia.ndo mana wako kina talib na lil wayne na wote wanamek kwenye soko hilohilo.kukaa us kusikufanye uone vyote vya home ni upuuzi,sanaa ina uwanja mpana sana!

 56. Talib Kweli Says:

  af nyie mnaomjadili prezoo tho hamjasema kama kaenda shule but the guy anasomea u-pilot na pia kusoma si lazima usome accountancy,eng.,law,com.scs and blah blah.kuna vingi vinavolingana na fani ya mtu husika.ni mchezaji mwenye ndoto ya ukocha badae atafanya elimu ya viungo na zinazofanana na hzo.AY ni mfanya biashara kuna vikoz vidogo/vifupi juu ya ku-manage biznes sio lazma asome BA na mengine ya hivo.huyu ni rubani lakini ni CEO wa kampuni flani.

 57. binti-mzuri Says:

  ok MTU nimekuelewa,my broda! 😉

 58. BLACKMANNEN Says:

  Hapo umesema kweli tupu Talib Kweli, mpe shua huyo limbukeni wa Marekani, hajui kuwa wenzake walishaishi huko na kupadharau na kujirudia zao Tanzania.

  Pia hapa BC hatuhitaji “magazeti” mchosho ya nyimbo za hao jamaa zake aliyoyanakili.

  “Black Eyed Peas in da BC???” No, ONLY Black…., I mean Black=Blackmannen

 59. papuu Says:

  wewe Black = Blackmannen usiwe racist!… Black Eyed Peas ina waimbaji wawili ambao ni ma Black.

  halafu Toni wewe unasema Hermy B ni Daktari? ha ha ha, Daktari wa nini? wa kukaa kijiweni na kupiga inshu, au daktari mwenye doctorate ya medicine?.. HONGEENI VITU MNAVOVIJUA, HUYU HERMY B JINA LAKE NI HERMAN BALITULILA,NI JAMAA NILIESOMA NAE PALE FORODHANI MSHKAJI KISHENZI, SASA HIYO MEDICINE KAITOA WAPI NA WAKATI ANAANZA MAMBO YA KUPRODUCE ALIKUA ANAKUJA KUPRACTICE KWANGU PALE KINONDONI??

  HACHA UWONGO WEWE TONI! UZUSHI SIO KITU KIZURI- USIWAPOTEZE WADAU WA BC,UKIJIFANYA UNAWAJUA WATU HUWAJUI!ALAH! BC PLEASE WAELEZE HAWA WATU!

 60. papuu Says:

  HALAFU TONI SIJAKUMALIZA! UJUE HAWA WASHKAJI MI NAWAJUA SANA! DEGREE GANI AMBAYO ANAYO BWANA AY?
  SITAKI KUKUCHOSHA SANA NA JINA LAKE,NITAJIE CHUO ALICHOMALIZIA. HUSIDANGANYE UMMA WEWE TONI, AY KAMALIZA SIX AU FOUR NA KINA MAREHEMU COMPLEX NA VIVIAN PALE MBEYA, AKARUDI BONGO WAKAANZA KUJISHUGULISHA NA MUZIKI( COMPLEX NA AY) NDIO MPAKA AKAJA KUTOKA NA NI ‘RAHA TU’ SASA UNAONGEA NINI?

 61. hilly Says:

  naona wote mnacomment elimu,elimu…!kwa taarifa yenu ay kasoma tena kasomea music. nyie mnataka aende shule gani? kusoma sio mpaka mtu usome commercial,science au politics.mtu anaweza hata akasomea kumburudisha mtu bwana kama ay anavyofanya.Kuna watu wanasomea hata kushona viatu.mwacheni ay.

 62. halima Says:

  hapa pameshakuwa patamu ngoja nicheke tuu kwikwikwikwikwi

 63. Toni Says:

  Papuu; nimegundua wewe ni kati ya wachache ambao mnarudisha nyuma maendeleo ya nchi yetu kwa kujifanya kujua watu…Hermy B sio Herman wewe..anaitwa Hermes Bariki tulisoma nae Tambaza akiwa anatokea uingereza. best sana wa elirehema doriye na chinko kichogo na tena alikua memba wa kundi la Wu Tamba.sasa leta hizo habari zako feki za kijinga.wivu utakuponza wewe nahisi wewe ndo wale wenye certificate feki,ukisikia mwenzako ana degree badala ya kuaprishieti kikorosho kinakujaa.
  Kijana amesoma unaona wivu,Haya sasa na mwana FA nae ana advanced diploma na anafanya kazi NBC bank.kitaakuuma mpaka ufe wewe. Ay ana kampuni.

 64. BLACKMANNEN Says:

  Duh! Kaaaazi Kweli kweli Hapa BC siku hizi. Kila mtu anamjua huyu na huyu!!! Sijui tumwamini nani. Sisi tusiowajua ni kung’aang’aa macho tu.

  This Is Black=Blackmannen

 65. Matty Says:

  nina tatizo nabaniwa ck hizi hapa BC jamani Jeff inakuwaje????????

 66. binti-mzuri Says:

  hahaha lool! ehe?.. endeleeni

 67. binti-mzuri Says:

  sasa tumwamini yupi? anaemjua hermy B embu atupe data zake basi.. maana mara herman, mara hermy, mara herry! eh!lol

 68. papuu Says:

  toni sina muda wa kupigiza kelele na watoto,ila ukweli unaujua wewe ndani ya mwili wako. halafu usiluke majoka, AY ana degree gani na kaipatia wapi? hilo swali dogo tu ndio pekee naomba unijibu! HERMY B hakusoma TAMBAZA na hilo jina sijui umelipekua wapi. ngoja nicheki,kama ameweza kuendelea hata kupata tecknolojia ya website yake,nije niwape mambo. sisi tunaongea facts, sio kufurahisha umati.. narudi kuposti linki ya web kama anayo.na hiyo degree yake ya medicine,sijui kaipatia chuo gani.labda kinondoni university

 69. Hombiz Says:

  Wewe BLACKMANNEN ndio limbukeni wa kutupa! Swala linabaki pale pale, pumba zote unazoongea hapa uwanja wa BC zitajibiwa kwa nguvu za hoja na sio hoja za nguvu. Fikiri kabla ya kuandika!

 70. nunku Says:

  du!!!!!!! kumbe hapa kuna mengi ya kujua namna hii??????
  endeleeni kutumwagia kimtindo,sisi twayasoma tu haina shida!!!!!!!

 71. Toni Says:

  Papuu: Kweli nimejua wewe ni mshamba,huyo hermy mbona amekua anakuumiza kichwa hivyo brother.nimekwambia haumfahamu unabisha sasa utaishia kuonekana kama pimbi kwa kutoa information za uongo. unabisha mpaka shule aliyosoma au unataka kusema kwamba maprodyusa wa tanzania hawajasoma,hebu punguza kikorosho na vyeti vyako feki vya kufoji. nani asiyejua wewe ulifoji vyeti au tukuache uchi huku?
  kijana nakwambia kaenda skonga ndo maana hana njaa na muziki wa bongo. umeshawahi kusikia ametoa utitiri wa nyimbo kama hawa maprodyusa wengine?anatoa kitu kimoja halafu kinakaa.yani hapa Ay,hapa FA halafu hermy b sikilizia mziki wake. hii ya psquare najua imewauma wengi sababu jamaa wana connections,badala ya kuwasifu hawa vvijana kwa kupeleka muziki wetu wa kibongo kwenye level za kimataifa unakaa kujadili elimu tuuu.wewe elimu yako imekusaidia nini.usingekua na muda wa kujifanya unamjua mtu kumbe hujui kitu.angalia kijana utapotezwa.
  mimi nawapa hawa vijana big up sana wanajitahidi kutufnya na sisi tujulikane,tuwaunge mkono,si unaona sasa hata akina profesa jay wanaingia kwenye mtv awards. Jamani tuwe na mawazo chanya na tuache kuona vitu vya home mavi. mafanikio ya nchi nyingine yamekuja kwa kupenda home kwanza. tuache ulimbukeni, upo hapo papuu?!!!!

 72. Matty Says:

  HOMBIZ & BLACKMANNEN KULIKONI?????????????YAISHE BASI KAKA ZANGUNI MBONA HIVYO!!!!!!!!!!!

 73. maryciana Says:

  mhh! mi naingiaga anonymous nicheke tu humu ndani.haipiti siku mshushuano.

 74. binti-mzuri Says:

  matty dia chuja maneno,si unajua tena tukishushua sana jeff hapendi.. weka ndimu kidogo,ukali upungue!

 75. hilly Says:

  AY I LYK YA MUSICS SO MUCH,BIG UP. GETTIN, AWARDS SHOW DAT UR THE BEST! BUT EDUCATION IS YOUR INVESTIMENT!

 76. Asha Juma Says:

  mtoto soft nimekumaind sana. keep it up boy

 77. BLACKMANNEN Says:

  Naona kila mdada anayeingia hapa anatoa dukuduku lake la moyoni la kum- maindi AY. Basi ngoja na mie nianike la kwangu kwa….., sijui kwa JiDe? Ah, lakini ana wa kwake wa moyoni!

  Ah!……………Sijui kwa………Ah! NEVER MIND!!!!!

  The Great Man………Black=Blackmannen

 78. Matty Says:

  sawa Binti-mzuri nitumie hiyo chachandu basi nizimue maneno maana daaaa nabaniwa si mchezo!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s