BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MWISHO WA MWEZI-VIJANA JAZZ BAND October, 31, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 12:30 AM

Maisha yetu yanaboreshwa kwa pesa ambazo zinapatikana nyakati za malipo (kwa wafanyakazi, wafanyabiashara n.k).Malipo hayo huwa yanatokea kwa nyakati tofauti. Lakini uwe unalipwa mwisho wa siku, ama mwisho wa wiki, ama mwisho wa kila baada ya wiki ama mwisho wa mwezi, dalili ni kwamba siku ya leo wengi watakuwa wamelipwa maana sio tu mwisho wa siku,na wiki, bali ni Mwisho wa mwezi.Tumeingia ngwe ya lala salama ya mwaka 2008.Unaweza dhani utani vile ukiwambiwa karibuni watu tunakula Xmas.

Unakumbuka vituko vya mwisho wa mwezi?Binafsi nakumbuka kisa cha mzee mmoja ambaye ilikuwa kila mwisho wa mwezi unapofika haonekani nyumbani mpaka alizonazo zikishamuishia.Siku moja mke wake akagundua kule jamaa anapoenda akishakamata “mshiko”. Kilichotokea huko mpaka hivi leo ni simulizi lenye mafunzo.Kwa kifupi jamaa alitoka huko bila sehemu muhimu ya viungo vyake vya uzazi!

Wasikilize Vijana Jazz wakizungumzia mambo ya mwisho wa mwezi katika kibao chao kilichotamba saana cha MWISHO WA MWEZI. Wikiendi njema kwenu nyote.


Burudani ya leo imeletwa kwenu kwa hisani ya http://www.changamotoyetu.blogspot.com

NB: Kwa wasomaji na wapenzi wote wa BC ambao walimiss burudani ya kila Ijumaa kwa majuma kadhaa,tunawaomba radhi.Hiyo yote ilitokana na sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wetu.Tekinolojia ya 3G ilituangusha kwa majuma kadhaa tulipokuwa hukooo kwenye semina elekevu.

Advertisements
 

20 Responses to “MWISHO WA MWEZI-VIJANA JAZZ BAND”

 1. halima Says:

  kudadadeki!!!!!!!!!!!!! mwisho ukifika eeehh habari gani ugeuka kuwa, How are you? tehetehe tehehhe

 2. maranta Says:

  were nice guys…but i think most of them are gone by now! we will always remember them for there contribution in music industry of our country…!

 3. majita Says:

  Jamani yule atakayewiwa na haya maandishi yangu hebu aniandikie majitabrain@gmail.com tuongee zaidi.Sipendi kutaja majina kwani naweza kusahau ya wadau wenzangu wa karibu ila ndg zangu hebu tuwasiliane na pls taja jina lako unalotumia hapa ukumbini ili niwajue nisomapo mail zenu.Nahisi kama nina neno la ku-share na ninyi wapendwa.

  Zaidi mwisho wa mwezi kuna mambo.Usiseme hakuna tabu bali sema no problem,sawa Maty??ukawii kuulizwa habari zako,wewe ukajibu hakuna tabu.Hapana, jibu ki mwisho wa mwezi

 4. Matty Says:

  Asante BC kwa kibao murua tulimiss vionjo!
  huyo wa kulia kwangu vipi jamani ameoa???naona kama kanyosha kidole juu na pale nyuma nae kidole juu mhh mipasho na hapo tena???
  Wknd njema wote!!

 5. Matty Says:

  swali tena huyo wa kushoto na miwani ni Kitime??wadau naomba jibu naona kafanana!

 6. kindo Says:

  Matty, huyo ni Kitime. Ametokea mbali

 7. binti-mzuri Says:

  thanx BC … wkend jema to all.

  majita mbona na ka ‘mobitel’ kako hujaweka???

 8. kindo Says:

  jamani mie huu wimbo ukifika katikati hauendelei au komputa yanguina tatizo… nahitaji msaada kwenye tuta

 9. binti-mzuri Says:

  ivi dunda golden yuko wapi siku hizi?au ndio mambo ya winter vacation. anyway, shout out to you if your still around. tumekumissi

 10. Matty Says:

  Majita na wewe nae sasa una issue tukuandikie ili?????????unaenda wapi?????pangoni????hahahahahahaha(jokes)

 11. kahindi Says:

  jamani si haba….kwa kweli old is gold…nimependa na hivyo vibanda vyao vichwani…..sijui kama enzi yaweza rudi au la….

 12. debra Says:

  Mwishoo wa mwezi hata lugha hubadilika habari gani hugeuka kua HAWA YUUU
  Hakuna tabu wanasema NOO PROBLEM
  samahani wansema sore ohh sore..
  Heheheee Edo wea a yuuu!!
  Mi spiking ingish coz izi mwisho wa mwezi leo!!
  BC…sante sana

 13. EDWIN NDAKI Says:

  Matty ni kwli huyu ni aliyesimama toka kushoto, John Kitime alikuwa muimbaji na pia mpiga guitaa ila kwa sasa yuko Kilimanjaro Band-Wananjenje.

  Wanne kutoka kushoto ni Abuu Semhando anakaanga chips(yaani anapiga Drumms katika bendi ya Twanga Pepeta na pia namuona Said Mnyupe mpuliza mdomo wa bata(trumpet) nafikiri bado yupo msondo.

  Jamaaa walikuwa wakali sana namkumbuka enzi za marehmu Maneti pamoja na kina kida waziri..duh..ilikuwa patamu enzi hizi huku ukipata mirindimo kupitia radio tanzania..aaaaa aaa

  wiki endi njema ndugu yangu

 14. Gervas Says:

  Nakumbuka nilikuwa darasa la saba hivi..mchana mwema, nasubiri lunch nirudi shule tena….Nikitizama vizuri namuona mzee Kitime hajavaa mkanda, au mshikaji wa kati katinga naona kamba flani nyeupe(mshipi). Wanaonyesha umoja japo fedha inaonekana ilikuwa haba enzi hizo lakini hawa ndo walijenga msingi ambao bendi za sasa zinaukalia. Tofauti kati ya mwisho wa mwezi wa zamani na saizi ni kwamba zamani mshahara ulipigwa jeki na huduma kibao za bule kama mahospitali, maji, umeme, chakula havikuwa tatizo sana. lakini siku izi, mwisho wa mwezi umetawaliwa na VAT, kodi kibao kwa kifupi bure amekufa kabisa…Anyway… Big up Vijana jazi bendi

 15. usinijue1 Says:

  jamani edi shegy ndio mbona simuoni hapo,btanks bc… msaada tutani kwenu bc tutafutieni na za washirika tz stars watu njatanjata

 16. hombiz Says:

  Thankz BC! Nyimbo inanikumbusha mbali sana. Kuna jamaa yangu fulani aliwahi kuniambia kuwa kuna familia moja mwisho wa mwezi, watoto hawachezi mbali na nyumbani. Sababu siku hiyo msosi ni wali na nyama! teh-teh-teh!
  BC huyo jamaa aliyenyofolewa nyeti zake kwakweli alifikwa na maswahiba makubwa mazee! Hiyo haijakaa sawa. Bola wangemnyofoa walau jicho kuliko hiyo bidhaa nyeti..no more ligwaride.. …ha-ha-haaa!.

 17. Matty Says:

  Asante wadau kumbe Kitime alianzia mbali…hongera baba!

 18. hilly Says:

  dah huu mziki unanikumbusha mbali kweli,lkn mwisho wa mwezi kweli ni balaa…

 19. innocent Says:

  ebwana hawa watu nawakubali sana ni vigumu kukuta vijana wadogo kama mimi wanapenda nyimbo za zamani kama mimi. binafsi nawapa shavu sana hawa watu


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s