BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

KESI YA EPA YAANZA KUUNGURUMA November, 5, 2008

Filed under: News,Special Interest News — bongocelebrity @ 8:07 PM

epabc

Baada ya kushuhudia historia mpya ikiandikwa huko nchini Marekani jana,macho na masikio leo yalielekezwa katika mahakama ya Kisutu jijini Dar-es-salaam ambapo watuhumiwa wa ‘EPA’ wamefikishwa hapo ili kuanza kujibu shutuma nzito zinazowakabili.

Blog ya Michuzi imeandika kwa undani kuhusu kesi hiyo na kuambatanisha picha kibao.Bonyeza hapa uende moja kwa moja kwenye post hiyo.

Advertisements
 

40 Responses to “KESI YA EPA YAANZA KUUNGURUMA”

 1. binti-mzuri Says:

  pashakucha!

  ila huyo muhindi wa pili kulia,ndio anajutia makosa yake au?

 2. BLACKMANNEN Says:

  Ndugu zangu Wana BC,

  Kama nilivyokuwa nikisema kuwa, Rais Jakaya Kikwete ni mtu makini sana, na anajitahidi kwa upande wake, kufuata utawala wa sheria. Matakwa ya wachangia mada hapa BC, na wengine wengi nje ya hapa, walitaka Rais akurupuke kwa kutumia madaraka yake katika kushughulikia swala nyeti hili la EPA.

  Kutokana na Watanzania kukomaa kisiasa, kidemokrasia na uhuru wa kusema, hilo haliwezekani. Kiongozi yeyote Tanzania, hawezi kutumia madaraka yake bila ya kufuata sheria za nchi yetu, au hawezi kuwa “dikteta”, kwani, kwa kufanya hivyo, ni yeye ndiye atakayeingizwa matatani na wananchi.

  Najua watu wengi wataanza kusema kuwa, mbona vigogo wenyewe wa serikalini ambao wamekuwa wakitajwa sana, katika sakata zima la EPA, hawamo katika kundi hili lililofikishwa Mahakamani?

  Eleweni kuwa, kwa kukamatwa watuhumiwa hawa wa EPA tunaowaona hapa leo Mahakamani, ni hatua ya mwanzo itakayofanya kukamatwa pia na washirika wao walioko serikalini, kwa njia ya kutajana. Kwa kufanya hivyo, itakuwa imekatwa mizizi ya mtu kusema kuwa kaonewa ama kabambikiwa kesi kutokana na cheo chake ama itikadi yake kisiasa.

  Nawaomba tuwe na subira, safari ndefu ndiyo kwanza imeanza, tutaona mengi yanaibuliwa hapa Mahakamani.

  Mimi binafsi natoa pongezi zangu za dhati, kwa Rais Jakaya Kikwete, kwa kutimiza ahadi zake kwetu, japo watu wengi na hasa wanasiasa, wamekuwa wakimbeza, wakilitumia sakata la EPA kujinufaisha kisiasa na kuwachanganya Watanzania, kwa kutumia matatizo ya kiuchumi nchini na dunia nzima, ili kuiyumbisha serikali na viongozi wake.

  Nawaomba Watanzania wenzangu tuwe macho, na watu wenye nia mbaya na nchi yetu, waliomo Tanzania na wale walioko nchi za nje, wanaojifanya kuijua sana Tanzania kuliko wanavyoijua viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kutuongoza. Kama kuna mtu ana sera zake nzuri kushinda sera za Chama kilichopo madarakani, ama anaona yeye ni kiongozi bora zaidi anayewafaa Watanzania kuwaongoza, anakaribishwa kuzimwaga sera zake hadharani mwaka 2010.

  This Is Black=Blackmannen

 3. Matty Says:

  Ahhaaaa hayo ndo yakutuambia,waone na nyuso za haya pichani lol!!!!!!!!!mnainamisha sura chini ili iweje??????natamani hao maponjoro hapo pichani watiwe hatiani wafungwe maisha, watu wanakufa na njaa wao wanakula good time alaaaa!!!!!!!!!
  Halafu isiwe geresha sio leo wapo kisutu kesho wamehamia Marekani na familia zao tunataka hakiiiii wadau nashika bango kubwa lililoandikwa “MAFISADI WACHOMWE MOTO AU WANYONGWE”
  Hebu ngoja kwanza niwaache kina Hombiz,Blackmannen,Binti- Mzuri,Gervas,Edo,Mtu na wengine waseme then i will be back!

 4. trii Says:

  wadozi kibao.

 5. trii Says:

  swali:na wale viongozi wetu waliojiuzuru wako wapi?
  au upelelezi bado haujakamilika kama kawaida.
  mi nafikiri TZ imekuwa inawapa urai wageni kirahisi sana
  ndo madhara yake,pia inawaamini sana wageni.

 6. Bob Sambeke Says:

  E bwana Big Up kwa Kikwete kwa Kutekeleza ahadi aliyotoa ya kuwafikisha hao wezi wa Kodi Zetu mahakani! TUnaomba Mh.Rais uwachukulie hatua kali hao wezi wa fedha za EPA hili iwe fundisho kwa wengine.Hao ndio wanaohujumu uchumi wa nchi yetu.
  Pongezi hakimu kwa kutoa Dhamana kali sana kwa Wahalifu hao(nusu ya fedha walizochukua ndio dhamana).
  Pili JK, Na hao waliorudisha fedha tunaomba wachukuliwe hatua za kisheria.
  Ushauri wangu hao kina patel na jamii yake hiyo wafutiwe uraia na wafilisiwe warudi kwao wakauze migahawa.

  PDD na Jk tunawaomba muwachukulie hatua kali sana hao Mafisadi .Lakini mbona wapo wachache hivi? wengine wako wapi? Kina Meremeta,green na bwana mkubwa(Baba Watoto Mama,B.W.M Naye VP?)
  Ni Hayo tu Wadau!

 7. solange Says:

  huyo wa pili kutoka kushto atafia rumande, lakini sidhani kama hawa ndio wale wahusika wakuu

 8. first lady Says:

  I realy don’t think if those are the right people, sijui may be am right may be am rong , hii ni DANGANYA TOTO TU. Wenyewe wamehifadhiwa tu.

 9. Gervas Says:

  Sijui bei ya magari ila huyo mshikaji wa tatu kutoka kulia, huwa namuona na gari moja chafu sana, nafikiri zaidi ata ya million mia mbili ivi, afu msosi wake faivu sitaa…..kumbe duh!!, anyway, they are just suspects and not guilty yet. Huyo wa kushoto naona EPA kaihifadhi tumboni, wapili kushoto na tatu..wanaonekana wanazo bado benki….afu huyo mdosi Jeetu anaonekana akisema…mamayangu weee wakistukia ile michongo yangu mingine itakuwa soo. Najua vidume wengine bado hawajapatikana. Change we need!!

 10. DMX Says:

  Wadua tunaomba majina ya hao jamaa nasi tupate picha kamili.
  Naomba kuwasilisha

 11. Halisi Says:

  Mbona serikali inatufanya sisi wajinga? kwanini hatujawaona wale viongozi wetu, mi nlitegemea kumwona mtu kama lowasa, karamagi, rostam na manji.

  sasa mmetuletea hawa ambao walichukua hela kwa ajili yao na kuwaacha wale waliochukua kwaajili ya chama cha ccm.

  Haya ni matokeo ya uongozi mbaya, na tutawakomesha 2010 kama marekani.

 12. halima Says:

  Kemchoo Patel, kudadadeki cheki alivyochoka utafikiri amekosa penalt.

  Kweli siku hizi tumegawana madaraka mpaka wanawake mafisadi aisee tulienda Beijing kihalali hahahahah

 13. mtu Says:

  wanafaa kupigwa mawe wafe, kwani wao ni majambazi, sasa wanapelekwa mahakamani halafu watagawana mafao na procecuter na mahakimu baada ya siku mbili haaaooo mitaani na mapajero yao na benzi zzao. Hongereni kwa kkushinda kesi MAFISADI WA KUBWA

 14. Hombiz Says:

  Hapa ndio nnapopataka haswa!. Nasubiri mpaka nisikie hukumu yao ndio nitoe mtazamo wa mawazo yangu juu ya hukumu yao. Lakini ktk wote hawa, sijamuona hata kigogo mmoja(fisadi) ambaye alihusika ktk mchakato huu. Hao vigogo(mafisadi wako wapi)

  Kwa mujibu wa Rais Kikwete, idadi kubwa ya wahusika katika kashfa hiyo, wamerudisha fedha walizoiba kutoka EPA. Mafisadi hao walirejesha Sh 69,326,437,650 kati ya Sh 90,359,078,804 walizoiba kwenye EPA, kwa maana hiyo hawatafikishwa mahakamani kwa kuwa wametekeleza agizo lake la kurejesha fedha kwa muda aliowapa hadi ilipofika Oktoba 31, mwaka huu. Badala yake, mafisadi walioshindwa kurejesha Sh 21,032,641,154, ndio tu watakaofikishwa mahakamani, baada ya mchakato wa mashitaka kukamilishwa na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP).
  Kisichoingia akilini kwangu juu ya kauli hii ya raisi Kikwete ni kwanini hawa mafisadi wasishitakiwe hata kama wamerudidsha fedha walizoiba!? Najaribu kuweka picha akilini kwangu inakuwaje mwizi (FISADI) aachiwe huru kisa amerudisha pesa alizoiba!? This does not make any sense to me!. Hawa mafisadi. Mafisadi wote should be taken to court to answer charges against their offenses. Mualifu ni mualifu (awe kigogo ama mlalahoi) na anastahili adhabu kulingana na kosa lake. Tunataka tuanze kuwaona vigogo(MAFISADI) nao wakienda gerezani kutumikia vifungo kwa kuvunja sheria za nchi. Kasusura alifungwa miaka kibao kwa kuliibia taifa fedha zilizo chini ya hizo za mafisadi. Mbona yeye hakuomba kuzirudisha ili aachiwe huru?. Sheria inapaswa kuwa msumeno kwa kila mwananchi anayevunja sheria za nchi bila kujali dini, cheo, kabila, jinsia, wala umri.

  Watanzania wanzangu, tulivalia njuga swala hili mpaka wahusika wote wapande kizimbani!
  Stay focused

 15. binti-mzuri Says:

  hahahhaha @ halima! kumbe na we umemuona!

 16. Christabell Says:

  Safi sana. JK Umejitahidi mno. Yataka ujasiri wa hali ya juu kufikia uamuzi huo. “Ukitaka kumchinja kobe mlie timming” Huo ni mwanzo tu. Hao ndio waliotumiwa kuzichota na waliozichota. Awamu ya pili na nyinginezo zaja ktk kutajana. Watatajana tu. Big Up Jk kwa kukamata hilo li “Tycoon” la Kidosi Jeetu Ujanja mfukoni.
  Bahati nzuri mmejengewa VIP rooms Segerea la sivyo mngejisaidia ktk madebe na kuona chungu ya jela za Bongo.

 17. XXX Says:

  haa hawa ndio wana wali wapya sio?watoto wazuriiiiii washakaribishwa na njemba za lumpango! watoto si rizki tena hawa!!!

  huyo muhindi wa pili anawazia zile kachori alizoacha home sasa ni uji wa chumvi na maharage yenye wadudu…MNALO! sasa tunamngojea yule bwana MVi nyingi na mafisadi wenzao wapandishwe kizimbani!

 18. hilly Says:

  MI KWAKWELI NASHINDWA KUWAHUKUMU MAANA HAWAJAWASPECIFY,WANGETAJA MAJINA KWANZA….
  HALAFU CJUI HUU UJASIRI WA KUIBIA NCHI WAMEUPATA WAPI…
  HUU NDIO UGAIDI WENYEWE!

 19. halima Says:

  Bint – mzuri best nilipagawa baada ya kuona kimini cha kitenge nach kipo kwenye kambi ya mafisadi duuh matty umeiona hiyo mhhh kweli ni balaaa

 20. halima Says:

  lakini mbona hizi sura hazionyeshi kama zimechukua mabiilioni ya fedha? duhhhh mbona wale wazee wananihiiii sijawaona? mhhh kama huyo wa pili jamanimhhh,
  Kahindi na sistertz nimewamiss kishenz sioni maoni yenu why??????????

 21. Matty Says:

  Halima shosti hebu usinivunje Mbavu zangu mie, nilimuona kwa michuzi huyo bidada na kimini cha tenge kashika kiuno lol!was wondering hizo nyodo zake yule bidada maana hata haya hana …mara nasikia wasamaria wema wakamrushia kanga upo mpaka hapo???????

 22. kindo Says:

  Blackmannen point yako ni nzuri sana…nakuunga mkono. kwa kuongezea ni kuwa hao vibopa wako makinisana kwani wao hawako frontline vidampa wao ndio wanaofanya kazi…..its difficult because they make sure they cover their tracks…wao transaction zao zote zinafanywa in cash, wao sio ma-directors kwenye makampuni yanayohusishwa na EPA, sasa utawapataje?

 23. eve Says:

  Ivi nyie mnacomment nini ndo maana mtaendelea hivyo hivyo kufanywa mabwege hadi mingie kaburini ivi hao watu hapo mnafikiri ndo mafisadi danganya toto yani hapo mafisadi wa Epa wamekaa pembeni wametulia wanacheka hahahaha wamewatumia hao ili wapigwe picha wachukue chao! watimukie nje.Mie sidhani kuna fisadi hapo zaidi ya patel basi hao wengine wameenda kwa niaba ya watu tu! nyuso zenyewe hazioneshi kama zina hela hata sijawahi kuwaona wakitoa mchango wowote sehemu yoyote endeleeni kufanywa mabwege tu kucoment upuuzi usiokuwa na kichwa wala miguu.Mnadanganywa kaa watoto walishwa pipi weye subiri uone hatma ya hao watu watahukumia ila ndugu yangu ila baada ya mwezi wanakwea pipa byeeee!!!!!!!!! tayari mmefungwa vinywa ebu watanzania na kwa akili yenu kweli wale watu wanaweza chukua fedha zote hizo halafu wapo hapa nchni hahahahahaaaaaaaaaa majinga kabisa mnaowasagia hao simon wa kirene shaurienu mtaendelea kuwa majinga hivyo hivyo

 24. Matty Says:

  Eve u shld be more explainable! inaelekea unawajua MAFISADI ORIGINAL WA EPA!kwani hapo pichani hawawezi kuwa mafisadi?????????????????????????
  msaada tutani Eve!

 25. Sakina Says:

  Kusema Ukweli wa TZ bado tumelala unajua hiyo ni kiini macho hawo ma EPA sijui mtaona kesi haitoisha labda baada ya 2020 mpo???so hiyo kuwekwa ndani ni danganya toto tu mnyamaze HABARI NDIO HIYO!

 26. sellanda Says:

  Hivi nyinyi mnaodai hawa sio watajeni basi hao mnaowajua nyinyi kabla hawajakamatwa mlidai ohh JK ana urafiki na hao mafisadi wametajwa ohhh sio mnatakaje.

  Hii kesi ni kubwa na ina mlolongo mrefu kwa hiyo siku hadi siku wataendelea kutajana mpaka atapatikana aliyekuwa kinara katika kundi lao.

  Au mnataka akurupuke tu awataje hao mnao wataka nyinyi na mkitakiwa mkatoe ushahidi ulio kamilika je mtaenda kuutoa au mnaropoka tuu hapa .

  JK fanya kazi yako achana na hao wabeba mabox wasukutue vinywa.

 27. kahindi Says:

  mlaaniwe na mkifa mteseke na moto wa jehanamu…maisha ya watanzania yanakuwa magumu kila kukicha kwa sababu watu kama ninyi,ingekuwa enzi ya nyerere nyie mngefichwa 2 kimya wala kucngekuwa na haja ya kupelekwa mahakamani….kenge weusi nyiee..

 28. Pearly blackberry Says:

  JK keshajishtukia kuna kikundi ndani ya ccm watampiga chini 2010…amezinduka lkn huyo bwege BLACKMANNEN Says: November, 5, 2008 at 9:24 pm aliyesema jk mtu makini kachemsha, jk bitoz hawezi kuwa kiongozi wa nchi yenye matatizo na wananchi waliopoteza tumaini kama tz, kama sikosei aliendakia comment hy ni unc Salva.
  JK kama kweli kidume awafikishe mbele ya sheria mpaka wale waliolipa ( hapa ndo utawaona kina edo, vijisenti, rostam, beno mwenye yumo asijishauwe) na watakapotiwa hatiani wafilisiwe mpaka ndululu

 29. binti-mzuri Says:

  mi naomba tu mwezi huu JK achukue likizo from his world tour, na kukaa na kuangalia kwa undani hii shuguli ya EPA hata kwa siku 3..lol…. maana kila kukicha mwenzetu anaruka majoka tu nchi za watu! si ajabu ikulu yupo once a week.

 30. hombiz Says:

  Kwa mujibu wa habari iliyochapishwa ktkt http://www.ippmedia.com-alasiri-11/11/2008, Mhadhiri wa Sheria katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Dk. Sengondo Mvungi, ametaka watu waliorudisha fedha za EPA nao wafikishwe mahakamani.

  Akasema taaluma ya sheria aliyofundishwa na ile anayoendelea kuwafundisha wasomi wa Watanzania na pia katiba ya nchi, inaeleza kuwa watu wote ni sawa mbele ya sheria.

  Akasema kwa mtaji huo, haoni sababu ya kuwaacha watuhumiwa waliorejesha fedha za EPA bila kuwaburuza kortini.

  “Kutowafikisha mahakamani wale waliorudisha fedha ni ubaguzi wa wazi mbele ya sheria. Kwa vile mimi ni mwalimu wa sheria, sivumilii kuona hali hiyo,“ akasema Dk. Mvungi.
  I agree with you Dk. Mvungi. Sheria inapaswa iwe ni msumeno kwa kila anayeivunja. Sheria inayotumika kitabaka mimi naiona ni nusu meno na si msumeno!

 31. binti-mzuri Says:

  jamani hawa maprofesa wa huko mlimani ndio wanaotakiwa! please come save us..washatufanya sie wajinga! Dk. Mvungi mie pia nakusapoti. JK ayafanyie kesi,au la..basi jambazi likipelekwa mahakamani kwa tuhuma za wizi, wampe tu option ya kurudisha vitu aachiwe.. habari ndo hiyo!

 32. binti-mzuri Says:

  afu that link doesnt work hombiz.

 33. hilly Says:

  Hivi wewe namba 24 unatype hizi comment ukiwa unasinzia au?Mzima kweli wewe? Sikuelewi unavyosema tunafanywa wajinga wat’ about u? we sio mtanzania? maana kama ulifanya kazi na kutoa kodi hapo na wewe umefanywa bwege na umeibiwa pia!!! sijui kama unanipata? Pili unavyokataa kua hao sio wahusika unazidi kunichanganya,we unawajua wahusika? kama kikwete alipangua baraza la mawaziri ,hashindwi kufuatilia hao majambazi wa EPA na kuwahukumu.Tatizo la nchi yetu ni responsibility,ila kila jambo tukiamua linawezekana. Tatu unavyosema unakwea pipa unaenda majuu,that’s not a solution,unakimbia matatizo halafu unajiona umewin Kumbuka ile ni nchi yako na hata kama umesafiri ipo siku utarudi,sasa hilo swala la Epa si utakuta limeota mizizi na imeshakomaa(sugu) .”mkimbia kwao ni mtumwa”

 34. hombiz Says:

  Uuups! Samahani kwa usumbufu binti-mzuri. jaribu kuingia hapa kumsoma Dr. Mvungi http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2008/11/11/126180.html

 35. binti-mzuri Says:

  ok poa thanx

 36. daniel Mabula Says:

  JE! MUNGU NA YESU NI MMOJA?
  Makanisa ya Kikristo yanafunza ya kuwa Yesu Kristo si kama kuwa ni Mwana wa Mungu tu, bali hakika ni Mungu khasa. Baba, Mwana na Roho Mtakatifu ni mmoja. Watatu katika mmoja, na mmoja katika watatu. Wote ni wa milele, wote ni sawa. Yesu ni Mungu, na Mungu ni Yesu. Hiyo ni imani ya Kikristo, ambayo inaaminiwa na karibu Wakristo wote. Hebu tuifunue Biblia tutazame inasema nini katika jambo hili?
  Mt Paulo katika barua yake ya kwanza kuwapelekea Wakorintho aliandika:

  Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi.
  1 Wakorintho 15.15

  Juu ya kuwa Paulo anaambiwa ya kuwa akiamini kuwa Masihi (yaani Kristo) na Mwenyezi Mungu ni kitu kimoja hapa anasema: “Tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo.” Ikiwa Mungu kamfufua Kristo, hawawezi kuwa wote wawili hao ni mtu mmoja. Mmoja alikuwa ni mtenda, mfufuaji, na wa pili alikuwa ni mtendwa, mfufuliwa. Kama Kristo ni Mungu mwenye uwezo wa kufufua basi maelekeo ni kusema: “Kristo kajifufua”, sio kafufuliwa. Mwenye kufufuliwa ni mfu asiyejiweza kitu.
  Katika kitabu cha Matendo ya Mitume inasimuliwa kuwa Mt Stefano alisema aliyoyaona yaliyo mbinguni. Alisema:

  Tazama! naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kuume wa Mungu.
  Matendo 7.56

  Mwana wa Adamu ndiye Yesu, na kwa jina hilo ndio mwenyewe akipenda kujiita, sio Mwana wa Mungu. Hapo basi huko mbinguni Stefano anasema anamwona Yesu kakaa mkono wa kulia wa Mungu. Mwenye kukaa mkono wa kulia wa fulani hawezi kuwa ndiye yule yule fulani. Hayo ni maelezo ya mbinguni. Ni wazi basi kwa ushahidi wa Biblia kuwa Yesu hakuwa Mungu mbinguni kama alivyokuwa si Mungu duniani.
  Yesu alipokimbilia kwenye Mlima wa Zaituni na huku akisakwa na Mayahudi alijitenga na wanafunzi wake. Huko faraghani aliomba hivi:

  Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.
  Luka 22.42-43

  Hapa tunaona mambo matatu muhimu:

  Yesu anamwomba Mungu. Yesu anamwabudu Mungu. Wawili hao ni mbali mbali, na vyeo vyao ni mbali mbali. Yesu ni mtumwa mnyonge mwenye kuomba na kuabudu. Na Mungu ni Mwenyezi Mungu mwenye uwezo wote na mwenye kustahiki kuabudiwa pekee, hata na Yesu, mwenye kutakiwa msaada pekee, hata na Yesu.
  Mapenzi ya Mungu ni mbali na yale ya Yesu. Yesu hataki kuuliwa, ananyenyekea na kuomba kwa Bwana wake: “uniondolee kikombe hiki” cha mauti. Yesu hana azma hata chembe ya kufa msalabani, kifo cha mhalifu, kifo cha laana kama maadui zake Mayahudi walivyoazimia kumpatilisha nacho. Lakini anakiri kuwa ni mapenzi ya Mungu sio yake yeye yatendeke. Yeye hana hila wala nguvu za kuzuia kudra ya Mwenyezi Mungu.
  Yesu, Mwana wa Adamu, anakata tamaa. Imani inampunguka. Kavunjika moyo. Ikabidi “Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.”
  Jee, yaelekea kuwa Yesu ndiye Mungu? Yaelekea kuwa yeye na Mungu kuwa ni sawa? Kama upo wasiwasi wo wote wa kujibu hayo, mwenyewe Yesu anajibu kama anavyo hadithiwa na Yohana kuwa kasema:

  Baba ni mkuu kuliko mimi.
  Yohana 14.28

  Na mwishoni naye yupo mslabani:

  Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha?
  Mathayo 27.46

  Yafaa hapa tujiulize: Yesu akimlilia Mungu gani hapo msalabani ikiwa naye mwenyewe ni Mungu? Au nini alikusudia aliposema: “Mungu wangu naye ni Mungu wenu”? Maneno hayo kama yanaonyesha cho chote basi yanaonyesha unyenyekevu wa Yesu mbele ya Mungu wake. La kustaajabisha ni kule kukata tamaa kwake na kuvunjika moyo. Huwaje mtu wa imani, licha ya nabii na mwana pekee wa Mungu, akate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Ama kuwa Mungu akate tamaa na Mungu, na kumyayatikia: “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha”, ni jambo ambalo halimkiniki kuwa.
  Kwa uthibitisho ulio wazi Biblia inatwambia kuwa Yesu si Mungu, wala Mungu si Yesu.

 37. - - - - - - - - - Says:

  daniel mabula una matatizo gani wewe

 38. halima Says:

  daniel mabula ulikuwa unasinzia maana ulichozungumzia wala sio mada ya hapa BC. tafadhali usiguse imani za watu hapa maana najua patakuwa hapatoshi sasa hivi hapa.

 39. Mattylda Says:

  # 37 Daniel mabula!
  bwana yesu asifiwe sana!!!!!!
  Naona mkuu umeshusha mistari ya bible kiaina BUT i do not get ur concept here on KESI YA EPA!

  Halima shosti naona Daniel Mabula ana preach the words of God here!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s