BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

I CAN-NAS November, 6, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Siasa,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 10:00 PM

obama-michellebcHakuna ubishi kwamba jina la Barack Hussein Obama ndilo ambalo bado limetawala vichwa vya habari na vinywa vya watu ulimwenguni kote.Nikisema kwamba ushindi wa Obama bado haurindimi kwenye ubongo wangu nitakuwa naongopa.Itachukua muda kuamini na kukubali kwamba mabadiliko ndio yameshawadia.Ubaya wa historia ni kwamba huwa ina tabia ya kugeuka na kuwa kama sheria vile.Ilifikia mahali wengi tukapumbazwa na kuamini kwamba kwa sababu hakuna historia ya mtu mweusi kuiongoza nchi kama Marekani basi ni sheria kwamba haitokaa itokee! Leo hii Barack Obama amethibitisha kwamba kila siku ni siku mpya na kwamba historia mpya zinaweza kuandikwa.Na kubwa zaidi Obama amethibitisha kwamba inawezekana!

Leo hii tukiwaambia wanetu kwamba “you can be anything you want to be as long as you put your mind into it” tunao mfano hai.Inawezekana!Matumaini ambayo ameyaamsha Obama sio ya kupuuzwa.Ni matumaini ambayo hatuna budi kuyatumia kubadilisha maisha yetu,popote pale tulipo.Kama tunaona viongozi tulionao madarakani hivi leo nchini kwetu hawatufai,basi tunaweza kuwabadilisha.Inawezekana!Kama tunaona chama kinachotutawala hivi leo kimeshindwa kuleta mabadiliko yoyote ya kimsingi,basi utaratibu wa kidemokrasia wa kukipumzisha unaweza kushika moto hivi sasa.Inawezekana.

Lakini kama ambavyo mwenyewe Obama amekumbusha wakati akiupokea ushindi wake,mabadiliko ya msingi yataletwa au yanaletwa na watu wenyewe.Yeye peke yake hawezi.Serikali peke yake haiwezi.Hali sio tofauti hata kwetu Tanzania.Ni lazima kila mmoja wetu atumie kauli mbiu ya Obama kujiletea mabadiliko anayotaka kuyaona maishani mwake.Katika nchi zetu ambapo viongozi wamekuwa wakituangusha kila kukicha,ukweli huo una mizizi ya mbali zaidi.

Wakati dunia nzima ikiendelea kumuongelea Obama na kumtizama kwa makini kuona kwamba atafanya nini tofauti na waliomtangulia katika madaraka yake mapya,jambo moja ambalo hatuna budi kujikumbusha ni kwamba Barack Obama hivi leo ni Rais mteule wa Marekani,taifa ambalo limegubikwa na historia ya ubabe.Atakapokula kiapo rasmi tarehe 20 January 2009 ataapa kuilinda na kuitetea katiba ya Marekani.Wamarekani ndio waliomchagua na ataenda pale kulinda katiba yao na kutetea maslahi yao ulimwenguni.Akishindwa kufanya hivyo wenzetu wanayo demokrasia ya kumuondoa madarakani!

Hivyo ndio kusema kwamba matumaini yetu kwa Barack Obama yaendane na uelewa wa historia ya Marekani na misingi ya taifa hilo.Tukumbuke pia kwamba urais ni taasisi.Hatoongoza peke yake bali kwa kusaidiana na watu wengine tele.Tutegemee kitu lakini sio mengi.Lazima pia tukumbuke kwamba wapo waliomuweka alipo hivi leo.Nao wana matarajio yao na pengine hata ajenda zao za siri.Bado tunalo jukumu kubwa na kujibeba wenyewe na kuzibeba nchi zetu.Mkombozi anabakia kuwa sisi wenyewe.Mtaji wa Masikini ni Nguvu Zake Mwenyewe.Itaendelea…

Mtizame na kumsikiliza mwanamuziki Nas katika wimbo wake I Can.Nakutakia Ijumaa Njema.


Advertisements
 

21 Responses to “I CAN-NAS”

 1. BLACKMANNEN Says:

  Ahsante Jeff kwa majumuisho yako kuhusu Obama, umesema kweli na ndivyo ilivyo. Mambo ya Siasa na Uongozi wa nchi, ni magumu sana. Unatakiwa mtu uwe mkweli kiukweli, na nia ya kweli ya kufanya ukikusudiacho kukifanya, sio kufanya kitu kwa manufaa yako. Uchoyo, Tamaa na Ubinafsi viwe “Mwiko”, ndipo unaweza kufanya vitu kama alivyovifanya “Black Obama”.

  Hata hivyo, nguvu za binaadamu pekee, hazitoshi kukufanikisha nia yako ya kufanya uyakusudiayo. Ni muhimu kuomba maelekezo ya vitendo vyako vyote kwa “Mwenyezi Mungu”. Yeye ndiyo muwezeshaji wa kila kitu. Omba kwa Imani ya kweli kweli, utajibiwa maombi yako.

  Wakati tukiendelea kumpongeza “Rais Mteule Barack Obama”, kwa mafanikio yake hayo, pia tumshukuru sana “Mwenyezi Mungu” kwa kuyaitikia maombi ya Obama, na ya watu wote waliokuwa wakimwombea kwa Mwenyezi Mungu, kupitia katika Imani ya dini zao mbali mbali, ikiwa ni pamoja na WanaBC wenzangu wote. Habari yenyewe ndiyo hiyo ndugu zanguni, nafungulia kusikiliza Mziki wa Nas – Wikiendi Njema Wote!

  This Is Black=Blackmannen

 2. binti-mzuri Says:

  its another friday..another weekend

  i know i can, be what i wanna be… zubaeni zubaeni wenyewe,sie twasonga mbele ohooo!… next female president mie … if i work hard in it, i’ll be where i wanna be

 3. Matty Says:

  Uongozi mgumu jamani!

  All the best OBAMA!

  TUTAFIKA!

 4. kindo Says:

  Jeff and Blackmannen you have summed it all. Mmetuwakilisha! Obama ndio kwanza kazi imeanza…baraka za Mwenyenzi Mungu ziwe nae.

 5. Nakubaliana kabisa uliyonena!

 6. Matty Says:

  Kudadadeki Binti-mzuri u strike a chord to me today is another friday!yes i blv i can fly!and yes i can!
  BEIJING FOR BETTER LIFE,
  WOMENS LETS WAKE UP,
  Nice wknd to u all!

 7. halima Says:

  Ni kweli blackmannen bila mungu hili jambo lisingewezekana hata kama waafrika wote tungeruhusiwa kumpigia kura Obama.

  Hatuna budi kumshukuru mungu wetu kwa jambo hili na mungu amuongoze barack obama katika kusimamia haki ya mtu mweusi ambayo ilikuwa imeshaondolewa katika dunia hii.
  Have a good week end matty,bint mzuri, kahindi, hombiz blackmannen, mama wa kichaga, sistertz, mtu, bob sambeka . Pamoja tutafika

 8. Mama wa Kichagga Says:

  Hii habari bado ni pevu kabisa.

  Tujifunze kupata mafanikio kupitia mifano hao toka kwa huyu shujaa wetu kwa kweli.

  1. Angalia kuanzia familia , angekuwa kule kwetu wapambe wangesema oooooo mtoto wa mwanamke hawezi kutuongoza ooo mama yake oooo baba yake! Wachaga hasa mijidumu mpate fundisho hapo na kamwe siwatetei maana kuficha ujinga ni sawa na kuficha maradhi hadi kifo kikuumbue.

  2. Maisha yake ya kifamilia ni kioo tosha kwa jamii

  3. Shule na kujituma kwa kujiamini kwake hakuna mfano

  Mwisho na funga kazi “Kuwa mwaminifu ktk maisha yako ya ndoa au mahusiano” ni jambo jema ili kuweza kuwa confident maana wakati mwingine tumeshuhudia watu wanashindwa kusimamia ukweli maana na wao sio wakweli. Sasa hapo inapotokea kunyooshea kidole uonge anaogopa maana na yeye yumo kundini.

  HUYU JAMAA NI SOMO TOSHA KWA KILA NYANJA YA MAISHA TUNAYOTAKIWA KUYAISHI HAPA DUNIANI

 9. Mama wa Kichagga Says:

  MASAHIHISHO:

  UONGE = UONGO

  MIJIDUMU = MIJIDUME (MAANA INAKOSOA HADI INACHEMSHA)

 10. Mama wa Kichagga Says:

  ANGALIZO:

  1. HESHIMU MTU BILA KUJALI MAKUZI WALA ALIKOTOKEA (KABILA, RANGI, UMBILE) MAANA HESHIMA HUJENGA TAIFA

  2. CHUKI BINAFSI HAZIWEZI KUKUJENGEA MAFANIKIO MAISHANA WEE KAZANIA ULICHONACHO HUKU UKIWEKA MALENGO YAKO MBELE

  3. CHUNGA MDOMO WAKO USINENE MAKUU

  4. KUWA MWAMINIFU ILI UWE NA UWEZO WA KUSIMAMIA HAKI PINDI UTAKAPOPATA HIYO NAFASI

  I WANT ONE DAY TO BE A POWERFUL WOMAN LEADER IN TANZANIA WHO CAN BRING THE CHANGES NEEDED IN TANZANIA BY TANZANIANI

  YES I CAN BE WHAT I WANT TO BE! AND I AM WORKING HARD

  WAJUMBE NIPENI KURA ZENU NIWALETEE MABADILIKO (NDOTO NYINGINE HUSUMBUAGA MCHANA HAHAAA)

 11. majita Says:

  Ama kweli hii ni weekend kabambe.
  Haya Binti Mzuri for presidency na Matty ataka kupaa.Pliz Msinisahau mimi kama moja ya ma-strategists wenu.Na Yes We Can meet your wishes

 12. mtu Says:

  Nimeona maoni ya wadau wengi yenye ‘hope’ na ndoto ndani yake but ‘Yes we can’ Binti mzuri Yes we can. Lakini sidhani kama kumuweka Mungu mbele kutasaidia kuleta maendeleo au kumsaidia Black Obama kuleta mafanikio Marekani. Sifa ya kubwa ya nchi zilizo mweka Mungu mbele ndio zinaongoza kwa umasini. Na hizo nchi zilizo leta hizoo dini na huyo Mungu wala habari hawana na huyo Mungu mwenyewe. Chakufanya hapo ni kuchanganya akili na kusonga mbele. Tafuteni maendeleo kisha mleteni Mungu na sio kinyume chake. Kujenga familia ni maadili ya uadilifu ambao mtu anatafuta ndani yake, na siyo nguvu inayotoka sijui wapi. MNANIUDHI SANA WADAU AMKENI JAMANI. Blackmannen vipi wewe?

 13. Hombiz Says:

  In my opinion, nadhani President-elect, Barack Hussein Obama, ni the most inspirational figure juu ya hii duniani kwa hivi sasa.Jitiada, juhudi na maarifa alivyovitumia kufikia hapo alipo, kwakweli sio mchezo. Ana kipawa cha kuwa charismatic and courageous ktk kufanya mambo. Of course, amepitia maisha ya ujana ambayo kwa kiasi fulani hayakuwa mazuri, kama vile matumizi ya madawa ya kulevya(bangi, na wakati mwingine cocaine) na ulevi wa pombe. Kwa mujibu wa kitabu cha historia yake, mheshimiwa Obama aliyafanya haya akiwa high school huko Hawaii takribani miaka 20 iliyopita. Lakini kabla hajachelewa, alibaini kuwa njia anayokwenda nayo siyo sahihi na hivyo akabadilisha tabia na mwenendo wake na kuanza kuishi maisha ya kuwa productive member of society. Naamini President-elect Obama, ni mtu anayependa Social Justice ndio maana alisomea sheria na baadae kuitumikia jamii kama Community Organizer.Lakini kubwa zaidi ya yote, mtu wa shoka kapambana kufa na kupona, “kwa njia ya nguvu za hoja”, mpaka kaingia Ikulu na kuwa the first AFRICAN-AMERICAN US PRESIDENT. What a life story! If Obama, why not us!
  NB: Mimi naona Obama kapatia sana kumchagua Illinois Rep. Rahm Emanuel. I think this guy will have things done.
  BC, Thanks 4 the positive Song (I know I can) from NAS. It is very inspirational.
  By the way, thanks Halima for wishing me a nice week end. You do the same, OK!
  In my opinion, nadhani President-elect, Barack Hussein Obama, ni the most inspirational figure juu ya hii duniani kwa hivi sasa.Jitiada, juhudi na maarifa alivyovitumia kufikia hapo alipo, kwakweli sio mchezo. Ana kipawa cha kuwa charismatic and courageous ktk kufanya mambo. Of course, amepitia maisha ya ujana ambayo kwa kiasi fulani hayakuwa mazuri, kama vile matumizi ya madawa ya kulevya(bangi, na wakati mwingine cocaine) na ulevi wa pombe. Kwa mujibu wa kitabu cha historia yake, mheshimiwa Obama aliyafanya haya akiwa high school huko Hawaii takribani miaka 20 iliyopita. Lakini kabla hajachelewa, alibaini kuwa njia anayokwenda nayo siyo sahihi na hivyo akabadilisha tabia na mwenendo wake na kuanza kuishi maisha ya kuwa productive member of society. Naamini President-elect Obama, ni mtu anayependa Social Justice ndio maana alisomea sheria na baadae kuitumikia jamii kama Community Organizer.Lakini kubwa zaidi ya yote, mtu wa shoka kapambana kufa na kupona, “kwa njia ya nguvu za hoja”, mpaka kaingia Ikulu na kuwa the first AFRICAN-AMERICAN US PRESIDENT. What a life story! If Obama, why not us!
  NB: Mimi naona Obama kapatia sana kumchagua Illinois Rep. Rahm Emanuel. I think this guy will have things done.
  BC, Thanks 4 the positive Song (I know I can) from NAS. It is very inspirational.
  By the way, thanks Halima for wishing me a nice week end. You do the same, OK!

 14. Hombiz Says:

  I`m sorry for posting my comment twice!

 15. Mtu mzima Says:

  JAMANI BARACK OBAMA AMEFANYA MPAKA WATOTO WETU WAJIAMINI SASA HASA SHULENI KALETA CHANGAMOTO AMBAYO HAITA SAHAULIKA KILA MTOTO SASA ANAKWAMBIA YES I CAN LIKE OBAMA…. AGH! HADI RAHA JAMANI…. THANKS BC WK END NJEMA WOTE WANA KIJIJI

 16. Matty Says:

  Mama wa Kichagga na changamoto yako imetoka chuo!nakupa 10000000000000!!wanawake na maendeleo jamani gombea mimi nitakupa kura yangu!!!!!!!!!!

  Majita hahahahahahha mimi nataka kufly kabisa lakini usijali basi nikifly nakuwa prezidaaaaaaaaa basi wewe utakuwa makamu wangu sawa nigga???????

  Yes we can!

  Wknd njema wote!!

 17. kahindi Says:

  binti mzuri ,mama wa kichaga wish u all the best muachieve goals zenu…..kumbukeni ule wimbo…wanawake wanaweza weza wezaaaaa wanawezaaa….sasa binti mzuri jitahidi basi kuanza kampeni na je wagombea kwa chama kipi shosti?..mind u 2010 c mbali..vinginevyo nampongeza mwana wa kisumu…viva viva Obama

 18. RebbyGod Says:

  Yes binti mzuri keep it up Beijing 4life!!!!!!!!!!!!! I know I can n’ I know I wanna be!!!!!! I’ll do ma best to support you!!!!!!! all the best!!!!1

  Rebby

 19. EDWIN NDAKI Says:

  Ni siku nzuri sana..yaani nilikuwa bado kwenye furaha hadi nikashindwa kutoa maoni jana.

  Kila la kheri Obama

 20. kisha Says:

  wanawake na maendeleoo,tufanye kazi tusonge mbele ooh
  yelelele yelelle wanawakee
  wololo wololo kinamama

 21. BLACKMANNEN Says:

  Jamani tuwe wakweli, hakuna mtu aliyekuwa anampenda Mzee Joji Pori. Heri achaguliwe mtu yeyote, lakini atuondokee huyu mtu mwuuaji, katili, mbaguzi wa dini, mwizi wa Petroli Iraq na shetani mkubwa! Jamani mimi kwa kweli simpendi, sijui ninyi. Msema kweli mpenzi wa Mungu! Sina mengi, karibu sana Obama, utuokoe kutoka kwas huyun shetani!

  It’s Great To Be Black………I Mean Black=Blackmannen


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s