BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

UNITY ENTERTAINMENT November, 11, 2008

Filed under: BC Investigative,Burudani,Mahusiano/Jamii,Muziki — bongocelebrity @ 7:54 PM
Tags: , ,

Hivi karibuni tulipotambulisha single mpya ya AY inayokwenda kwa jina Freeze, palitokea mabishano makali sana kuhusiana na kama ni kweli AY ni established artist ambaye ana mpaka ofisi yake inayohusiana na suala zima la burudani na muziki. Umuhimu wa elimu ya darasani (formal education) pia ulizua gumzo.Nadhani wote tunakubaliana kwamba elimu siku zote ni suala muhimu na lisilofaa kubezwa hata kidogo.Kama mtu ana nafasi na uwezo kusoma tunamshauri afanye hivyo!

Lakini pia kulikuwepo na maelezo tofauti tofauti kuhusiana na kuwepo au kutokuwepo kwa ofisi ya AY na sehemu ilipo.BC iliamua kuwatuma baadhi ya wanachama wakereketwa ili kujaribu kupata undani kidogo wa suala hili.Tuliamua kufanya hivi ili kuwapatieni ukweli baada ya kuona kuna maelezo mengi yanayopingana au kupishana.

Ukweli ni kwamba AY anamiliki kampuni inayokwenda kwa jina la Unity Entertainment Company Limited.Ipo Mikocheni kwa Nyerere,Rose Garden Road pale Jued Business Centre Wing B 2nd Floor. Kampuni hiyo inajishughulisha na Event Coordination and Organizing(kuandaa na kuratibu matukio) na pia ni Events Booking Agency.BC pia ilifanikiwa kupata picha kadhaa za ofisi hiyo kama unavyoziona hapo chini.

BC inapenda kumpongeza AY kwa ujasiriamali na umakini huu katika masuala ya muziki na burudani.Ni matumaini yetu kwamba wengine nao watafuata nyayo za AY.

unity1bc

Unity Ent.

unity2bc

Unity Tanzania

unity-entertainmentbc

Advertisements
 

24 Responses to “UNITY ENTERTAINMENT”

 1. binti-mzuri Says:

  mmh safi sana! pamekaa kama ofisi!

 2. BLACKMANNEN Says:

  Ahsanteni sana Jeff na Uongozi wote wa BC, kwa kuyasikiliza maneno yetu kuhusu kijana wetu AY, na mmetupa ukweli halisi wa mambo yote.

  Kwa sisi tusiomjua sana kijana huyu, japo ni wapenzi wa miziki yake sana, tulibaki tuking’aang’aa macho tu, na tusijue la kusema, wakati waliokuwa wakidai kumfahamu walivyokuwa wakisema hapa. Sasa, ninyi mmetufungua macho, na tunampongeza sana AY kwa hilo. Ofisi yake ni nzuri sana, mie nimeipenda. Hongera AY.

  Kitu kilichobaki ni kujua kama AY ana “kitabu cha kutosha kichwani”, kitu ambacho ndiye mimi niliyeuliza, na nikaungwa mkono na watu wengi. Mimi napendekeza swali hili kwa sasa, atujibu yeye mwenyewe AY, ili tuone kama kweli, nasaha zetu kuhusu kitu “ELIMU”, alizipata. Pia tutafurahi kuona kuwa AY pia, ni MwanaBC mwenzetu.

  Obama pia, atakapotulia Ofisini kwake, tutapenda aje hapa BC, kutushukuru jinsi ambavyo tumekuwa pamoja naye katika shughuli ya uchaguzi, hadi kuibuka na ushindi wa kishindo USA, bila kumsahau Miriam Odemba pia tunamhitaji hapa BC, tusikie neno lake kwetu, kuhusu ushauri wetu kwake, na misifa kedekede tuliyomwagia alipoibuka mshindi namba mbili.

  This Is Black=Blackmannen

 3. papuu Says:

  swali langu hasa,ni kwamba yeye ni shareholder,partner au full owner and CEO?hii mizinguo tu bwana. hii ofisi kwanza HUWEZI ITA KAMPUNI..sijaona cha kampuni hapo,ni sawa na mimi nikodishe chumba kimoja pale haidery plaza na kuuita papuu company,its very simple. sisi tunataka mambo ya maana ya utandawazi -RUDIA KISOMO AMBWENE.. kampuni inaweza filisika any moment. what a lousy idea – entertainment events company ziko ngapi bongo. yeye kama AY anaweza walipa wasanii WENZAKE more than what those companies offer? pumba tupu tu hapa

 4. Matty Says:

  safi sana kijana! though Papuu hajaona kama ofice sio??????sijui unakusudia nini labda sijaelewa ur lines!

 5. halima Says:

  Mwenye wivu ajinyoge hahahaha papuu habari ndio hiyo hata kama kakodi au kaazima lakini ni yake upo hapo?

 6. XXX Says:

  wabongo nyie ni HATERS!!!!appreciate the niga iz doin good!

 7. Papuu,
  Ni vizuri kumshauri mtu asome na kujiendeleza anapoweza. Ndio maana nafurahishwa na artists kama CP na a friend of AY’s, MwanaFA ambao walihakikisha wanapata vyeti vyao na wana ujuzi wa kuwasaidia kuzalisha kipato zaidi ya muziki. Pia wapo wengine kama Simple X, n.k.
  Lakini kwa mwendo na lugha unayotumia wewe naona unakuwa negative sana kiasi kwamba kama ndio njia ya kumpa ushauri itakuwa ngumu kuusikiliza. Ni kama unaponda, sio kushauri.

  Kampuni sio lazima iwe na maofisi kibao, cha muhimu anazalisha kiasi gani kwa mwezi. Ukubwa wa ofisi sio wingi wa hela. Na kumbuka kuwa things start small and grow always. Kwa biashara ambayo nina-assume is solely owned by him, that is a moderately sized office, I have been to less impressive looking business places that bring in a considerably handsome pay cheque every month. Wasanii wengi wa Bongo wanategemea sana matamasha kuwaingizia kipato, na si uuzaji wa CD. Sasa kama ana kampuni ambayo hopefully ina-organize show zake mwenyewe badala ya kutegemea mapromota matapeli, it only means more money for him. Kibiashara I only hope wanadiversify shughuli zao ili kuongeza kipato. Akiweza afanye shughuli za usambazaji wa nakala za CD zake mwenyewe, n.k. This is the way to go. Hata wasanii wakubwa wa Hiphop marekani ambao wamefanikiwa kiuchumi kama Master P, P-Diddy, Jay Z, etc., waliwekeza katika kampuni nyingine sio kutegemea muziki tu.

  Nakumbuka not too long ago wakati niko A’ level, I used to see AY come perform at concerts in Moro. It’s nice to see he has already made it this far, and I only wish him more success.Mwishowe nakubaliana na wewe kuwa AY na wasanii wengine pindi wapatapo nafasi wajiendeleze kielimu. Sijui how amefika, ila najua at least amefika form IV. A friend of mine and classmate from Mzumbe, alisoma na AY O’ level Ifunda, ingawa he (AY) alikuwa nyuma. Hata kama yuko busy na biashara/muziki, kwa form IV yake, he can start taking evening Diploma/Certificate classes, zipo nyingi to Dar, then afterwards anaweza kusoma BBA evening Mlimani. Ni ushauri wangu tu.

  Best of luck on the success achieved thus far, na endelea kukazana, usiridhike.

 8. dina Says:

  Papuu ndugu yangu, hata mbuyu ulianza kama mchicha, sioni ubaya wa mtu kuanza kampuni na ofisi moja, ukienda kwa registrar kusajili kampuni si atakupa usajili, hata kama una chumba kimoja na bado itajulikana kama kampuni…maduka ya nguo yapo tele mjini lakini kesho bado mtu atafungua biashara ya duka..bado nafikiri itategemea mtu ameongozwa vipi na mawazo yake…..

  Mkumbuke pia kuna shida kweli kumrudisha mtu darasani kama yeye mwenyewe mawazo yake yamegoma kwenda huko…Mara nyingi wengi hujuta baada ya muda kuwa umeshawatupa mkono…anyways, huo ni mtazamo wangu tu….

 9. Veshimi Says:

  mhhh!!! haaaya!!

 10. hombiz Says:

  mimi binafsi mziki wa AY haunivutii kabisa.
  Ila nampa tano kwa kuanzisha kampuni yake ya Unity Entertainment. Kila la kheri ktk shughuli zako za biashara.

  Kuhusu swala la elimu, mimi naona ni vema uzingatie jambo hilo muhimu. I don`t care how busy you are, you still need to find time to hit them books

  Ushauri wangu kwako AY ktk fani ya BONGO FLAVAR ni kwamba, “tafadhali anza kuandika mashaili yaliyosimama labda nami nitakukubali”. Fata nyayo za wakongwa Mr. 2, Prof. Jay, na Simba Mzee!

 11. hombiz Says:

  Nalitolela, nakumbuka mstari mmoja wa Simple X, ktk kibao iitwacho Hakuna noma aliposema……hakuna noma bado nipo chuo kikuu nasoma!…
  Mstari huo unadhihilisha ni kiasi gani alipenda fani lakini pia hakuitupa elimu na hatimae kahitimu shahada yake ya kwanza pale UD. Big up simple X!

 12. BLACKMANNEN Says:

  Nalitolela, ulipotelea wapia? Karibu tena ndugu yangu. Vijana wanakosa kupata nasaha educative za watu kama wewe. Badala yake wanajikita katika malumbano yasiyokuwa na maana, kwa kukosa mwelekeo wa kimawazo.

  “papuu” nadhani, somo limemwingia, baada ya watu kama wewe, dina, Matty, halima, na wengine watakaoendelea kumpa “dozi” kali na zile za kutuliza kidogo mizuka yake inavyomwelekeza kuwazukia ovyo wenzake, hapa BC.

  Ofisi ya kijana AY mbona naiona inapendeza na imeisogea ile Ofisi ya Ikulu ya Marekani “OVAL”. Hongera sana AY, Ofisi yako ni nzuri sana. Tunakusubiri pia uje, kusema na sisi hapa BC. Nina hakika Binti-Mzuri, Matty na halima, watafurahi sana kusoma utakachoandika juu yao hapa BC.

  This Is Black………….Blackmannen

 13. amina Says:

  Du mdogo wangu AY hongera sana waache hao wenye wivu labda wakajinyonge watashangaa utakavyokuwa matawi ya juu juu zaidi ha ha ha

 14. debra Says:

  Mweeh EI WAI…………..Kama Dinah alivosema hata mbuyu ulianza ka uyoga
  Tutafika tuuu!!

 15. Gervas Says:

  Jamani mnaopiga kelele za ELIMU, kila siku nasema elimu ya kawaida inatosha jamani, Biashara zitaenda tu kama pesa ipo, sasa kila mtu akisoma nani atamwajili mwenzake? Mnajua kama mmiliki wa “Imalaseko Supamaketi” Dar, Arusha na Mwanza hajui hata masomo ya form one yakoje? lakini ni mfanyabiashara maarufu ambaye amewekeza hata nchi za nje na anatengeneza fueza kwa kwenda mbele? nani anamjua Professor Shaba? anaishi karibu na Holiday inn-Hotel (iliyokuwa). Kuna mkongoman mmoja anakata viuno stejini lakini ana degree ya Economics, wala hana mafanikio saana maana kwa miaka nane saizi tunabanana naye tu kwenye dala-dala. nawasilisha….

 16. binti-mzuri Says:

  papuu ndugu vp … au AY alikuibia demu,maana hayo maneno ni machungu ka fansida

 17. papuu Says:

  Huyu jamaa This Is Black………….Blackmannen mbona haeleweki haeleweki na messeji zake. Nimepewa dozi gani sasa, ya malaria au ya pumu? Tupo tunatoa mawazo kama wewe,sasa sijui kwanini unaleta inshu zako.

  Kwa wengine namaanisha AY bado ana njai ndefu na hicho kichumba kimoja

 18. Pearl Says:

  papuu # 3, comments zako zinaonyesha wivu na roho ya kwanini.

  haijalishi AY ni shareholder,part shareholder,full owner,CEO or the like na pia haijalishi ofisi ni ndogo kachumba kamoja,pia haijalishi bongo ziko kampuni ngapi kama hizo,PAPUU WE VALUE HIS(AY’s) IDEA kwamba he can go extra miles. At least for him(AY) he can think of ways to improve his life and all that.

  pia papuu fahamu kuwa kwavile eti kuna kampuni kama hizo nyingi bongo basi asifungue kwa vile ziko nyingi. Kwani hujui maana ya market share na product differentiation!!!???
  halafu wewe kwa wazazi wako si ulizaliwa ukiwa mtoto mchanga unajisaidia kwenye nguo,haya wazazi wako nao wangesema kuna watoto wengi wanazaliwa na watanzania wengine kwahiyo wao wasizae kwavile watoto wengi wanazaliwa na watu wengine!!!!!???? lakini walizaa.
  najaribu kukuonyesha kuwa watu wasiache kufanya kitu kwavile wako wengine wanafanya kila mtu hupenda kuona ana kitu amekipata kwa jasho lake na ndio inaleta SENSE OF OWNERSHIP, na ulipozaliwa ulikuwa mdogo na leo umekuwa mtu mzima na utafika mahali “Mungu atakupenda zaidi” na hutakuwepo tena,watu wanakufa sembuse kampuni!!!??? kwahiyo papuu let AY make the most of it while he can.
  AY MI NAKUPONGEZA SANA,KEEP THE GOOD WORK.

 19. halima Says:

  Ni sawa papuu bado ana njia ndefu na kachumba chake kamoja lakini siameshatoka? je utafananisha yeye na wewe?

  Sikuzote binadamu mwenzako anapopata maendeleo unatakiwa umpe hongera zake sio kila kitu wewe unakosowa tu. jamani tupendane lol………

  Safi sana AY acha hawa wabeba box waoshe vinywa wakichoka watatafuta sabuni ya mbuni wakaoge.

 20. MKULU Says:

  mie nawaona mnamsakama tu papuu ofisi kama hizo mjini ndio zinazoongeza utapeli tu zimejaa kila kona,AY eti CEO mbona hatuwi serious kidogo?nilipoona zile picha za wale watuhumiwa wa EPA nikapigwa na butwaa iweje tuibiwe na watu wanaoonyesha kuchoka vile ?lkn sasa najua tuna matatizo kwenye bongo zetu wabongo na ndio maana tunamuona kama papuu anaponda lkn the guy is right AY mziki wake mwenyewe analipua tu ndio akajifiche kwenye kampuni?vikampuni kama hivyo si ndio vilivyomngòa lowassa tena basi vikubwa vyake sio kama hicho chake kidogodogo

 21. usinijue1 Says:

  hongera AY kimsingi umepiga hatua hata hao wanaosema wewe mzushi lakini ni mwenye mipango maana wanasema hata ukiwa muongo basi uongo wako ufanane na kweli,so wewe ni artist ukiwa na ofice inayohusu mambo ya entertainment basi wenyewivu wajinyonge

 22. nipo Blackmannen, nilikuwa bado nafika BC everyday kama kawaida, just had no time ku-comment and read back the replies; school’s been keeping me quite busy!

 23. trii Says:

  jamani kila kitu kinaanza kwa hatua.

 24. Bob sambeke Says:

  Mambo vipi? BC ebwana big up ay! BC vp mbona unabania comments zetu! Peter Nalitolela mzumbe boy vp mkuu! Mbona Kimya!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s