BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MNANIONYESHA NJIA YA KWETU-DDC MLIMANI PARK November, 14, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 12:04 AM
Tags: , ,

ddc1bcKila ifikapo wikiendi huwa nafurahi.Nafurahi kwa sababu napata nafasi ya kupumzisha akili na mwili japo kwa masaa kadhaa bila kujali kama nitachelewa kibaruani au la.Ni wakati wa kuepukana na foleni za mijini.Wakati wa kukwepa kulikwea daladala kuelekea kibaruani ambapo ujira wake kamwe hautoshi.Ni wakati wa familia.

Lakini pia wikiendi hunipa hofu.Wikiendi humaanisha kwamba mwaka ndio unazidi kuyoyoma.Hofu yangu huingia ninapowaza kama mwaka huu ukiisha itakuwaje.Je nitakuwa nimeshakamilisha malengo niliyojiwekea usiku ule wa mwaka mpya au tarehe ile ya mwanzo kabisa ya mwaka huu?Mara tu niwazapo hivyo,kijasho chembamba huanza kunitoka.Kumbe nahitaji kukimbia na wala sio kutembea kama nifanyavyo sasa! Enewei,tutafika tu kama asemavyo Ndaki.

Ni siku nyingine ya burudani.Ni ile ijumaa tuipendayo sote.Ni wakati wa kukumbuka enzi.Leo tunao tena DDC Mlimani Park.Wimbo unaitwa Mnanionyesha Njia ya Kwetu. Ni utunzi wake King Enoch na Cosmas Chidumule.

Kama zilivyo nyimbo nyingi za enzi zile,wimbo huu umejaa mafundisho.Ni mafundisho mazuri ya kijamii.Kwa bahati mbaya mambo yanayozungumziwa katika wimbo huu bado yanatokea hata hivi leo.Mume anafariki na kuacha mali na watoto kadhaa.Badala ya ndugu wa mume kushirikiana katika kuwafariji wafiwa,wao wanaanza kugombania mali.Mbaya zaidi ‘wanamuonyesha njia’ shemeji yao!Kama wanavyoimba wana Sikinde,mila au taratibu za kimaisha za namna hiyo hazina maana kabisa na hatuna budi kuzipiga vita.Kama hali kama hiyo imewahi kukutokea wewe msomaji,rafiki au ndugu yako,tunakupa pole sana na kukuambia usikate tama.Nyanyuka pigania haki yako.Bonyeza player hapo chini upate ujumbe na burudani.Wikiendi Njema.


Advertisements
 

13 Responses to “MNANIONYESHA NJIA YA KWETU-DDC MLIMANI PARK”

 1. anony Says:

  mbona mwimbo wa zamani sana. nasikia ray c anamwimbo mpaya,ni kweli?

 2. Matty Says:

  asante BC kwa kibao hicho murua kwakweli kimenibamba haswaaaa!

  Nice wknd to u all!

 3. solange Says:

  “”mbona mmesahauu ya kuwa mali iliyoachwa ni ya watoto na msimamizi ni mimi mama yao ambae leo mnanikana”

  mziki mtamu wenye mafundisho tele.

  nawatakia wkend njema.

 4. Matty Says:

  anony unatoka wapi???maana daaaaa si mchezo kazi ipo!

 5. pyupyu Says:

  Ujumbe huu uwafakie wote wale wenye hizi tabia za unafiki.

  unanikumbusha alipofariki baba yangu ndugu upande wa baba walijifanya mali zote ziko chini yao na sie hatuna kitu pale.

  Duu hadi vijiko walizuia!!!! wakati uhai wa baba ndugu ndo tulikua sisi. Binadamu!!!

  kama ni mila tuache kwa kweli.

 6. Hombiz Says:

  Kwakweli nyimbo ina ujumbe tele. Ni jukumu la kila kiongozi wa familia kuweka wazi kimaandishi na chini ya ulinzi wa sheria kuwa ikiwa uhai wako kiongozi wa familia utafika ukingoni(MWENYEZI MUNGU ANUSURU) basi urithi uende kwa mkeo na watoto uliowaacha. La sivyo familia yako itavamiwa na ndugu wasioeleweka na kudai kila kilicho chako huku mkeo na watoto wakitimuliwa na kubaki wakiishi maisha ya shida mno.
  uuups BC asante kwa kunikumbusha. Uuups, BC! Thanks for reminding me! Let me go update my beneficiary documents right now. See you later!

 7. nchekube Says:

  anony cha kale ni dhahabu, shukrani bc.

 8. debra Says:

  Ahhh nishaiona njia ya kwetuuuuuuu

 9. Dunda Golden Says:

  Home sick hiyo kweli mazala yake ni makubwa
  msikie jamanii
  chafosa

 10. usinijue1 Says:

  anony ndio maana yake hapa tunakumbushwa zilipendwa,karibu ujumuike nasi………thanks again bc kwa burudani yenye ujumbe muhimu kwajamii,nakumbuka rafiki yangu yalimkuta hayo mzee wake alikua mjeshi mavyeo ya juu kwao neema kibao ndugu wakumwaga kwao mzee aliwapa good life watoto wake,dah mungu alikujamchukua ghafla mzee kwa presha,mzee mtu wa mwanza huko sio siri ulipita kama mwezi tu kaka wamarehem ka takeover kila kitu,mjane katimuliwa watoto walibaki ila huduma mbovu ilibidi maskini shule iwe ngumu kwake mpaka naondoka bongo jamaa kawa msela mzurulaji noma yani,kweli kama mila basi si mzuka kabisa………usinijue1

 11. hombiz Says:

  Yes Aisha. Mimi nimeoa. Pamoja na kuoa, sioni kama kuna ubaya wowote wa kuwa na marafiki.
  Asante sana aisha kwa mualiko wako. I will e-mail you as you asked me to do so. It is always great to have friends.

 12. yohana kamisa Says:

  kwa kweli muziki wa zamani ulikuwa na ujumbe tosha, wanamuziki walijitaidi kutunga tungo zenye maana na ujumbe endelevu. hiyo ilikuwa miaka 1980 ambapo, tanzania tulishuhudia miamba ya muziki ikishindana kutunga nyimbo za kuelimisha jamii. nakumbuka sana sikinde ngoma ya ukae ilikuwa juu sana, pia nakumbuka jabali la muziki marijani shaaban, na nyimbo zake kama ukewenza, mwana meka, heshima kwa wazazi na masudi amekuwa jambazi nakwambia palikuwa hapatoshi. wana uda jazz, kibao kama nilipokuwa kwa mjomba na vinginevyo, nakumbuka biashara jazz band na kibao kama, mshenga katoloka. nakumbuka gwiji Zail Ally na bendi yake ya jeshi, nyimbo kama kabwe karibu nyumbani, ee bwana BC umenifikisha mbali sana.

  Wanamuziki wa sasa jifunzeni kutoka kwa wazee hao, si kutunga nyimbo na kuwatajataja majina ya marafiki zako mpaka mwisho wa nyimbo, bila ujumbe wa maana.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s