BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

BABA WA KAMBO-THE NGOMA AFRICA BAND November, 16, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Single/Mpya — bongocelebrity @ 8:09 PM
Tags: , ,

ngoma-africabc1

The Ngoma Africa Band(pichani),bendi ya muziki wa dansi yenye makao yake nchini Ujerumani bado wanaendelea kuwa mabalozi wetu wazuri katika anga za muziki na burudani hususani katika nchi za Ulaya.

Hivi karibuni wamekuja na wimbo unaokwenda kwa jina la Baba wa Kambo ukiwa ni utunzi wake kiongozi wa bendi hiyo Ebrahim Makunja aka Ras Makunja. Wimbo umeimbwa na yeye mwenyewe Ras Makunja akishirikiana na mpiga solo guitar wa bendi hiyo Chris B.

Unaweza kuusikiliza wimbo huo kwa kubonyeza player hapo chini.Sikiliza jinsi The Ngoma Africa walivyopeleka kesi kwa Mkuu wa Wilaya ya Tegeta,Issa Michuzi. Salamu kwa wote huko Ujerumani wana The Ngoma Africa Band.


Advertisements
 

21 Responses to “BABA WA KAMBO-THE NGOMA AFRICA BAND”

 1. BIG UP NGOMA AFRICA BAND,LAZMA SHUKENI BONGO MKA PROMOTI MIZIKI YENU REDIONI NA KWENYE STESHENI ZA TV’s KAMA MWENZENU VUMBI DEKULA ALIVYO TAMBA OKT DAR NA KUNDI LAKE LA ZAMANI MAQUIZ,BC AHSANTE

 2. halima Says:

  Huyo wakati kati jamani kacheka au kafurahi? maana meno thelathini na nje yote yako mbili. hahahahha

 3. hombiz Says:

  Asante sana BC kwa burudani hii toka kwa The Ngoma Africa Band. Message is delivered. Wazazi wote wa kambo wanaotesa watoto wa kambo ni vema wajifunze kupitia ujumbe kama huu.
  Watoto wanaoteswa na wazazi wa kambo ni vema waanike ukweli hadharani kwa wazazi wao. Na wazazi tusipuuze yanayosemwa na watoto hao. Ni vema kufanyia kazi wasemacho watoto. Mara nyingi maneno ya watoto huwa ni kweli pasipo kusingizia.
  Mkuu wa Wilaya ya Tegeta, Issa Michuzi. Tafadhali kampige picha mtoto wa kambo ili uanike mateso yake hadharani. Hata mimi sikuwa na akili hiyo nilipokua youngstar. Otherwise ningekufuata Mheshimiwa Michuzi ili uokoe jahazi lililotaka kuzama kutokana na “mama wa kambo”. Anyway, I forgave her but will never forget!

 4. mkulu kulu Says:

  Hiii!Ngoma Africa! hongereni kwa kumshushua baba wa kambo,beat zenu kali tena kali na tishio.

 5. Somo Says:

  Ngoma Africa hii kali kuliko zote!?
  mambo yamemgeukuia baba wa kambo!?
  mnatuacha hoi

 6. Jose Ntila Says:

  haya Baba wa kambo ! vichaa hao wamekujia juu!
  kama unaweza jibu hoja zao!

 7. DUNDA GALDEN Says:

  Makunja baba wa Kambo kakufanya nini?
  mbona alikulea vizuru tuu au yule wa Tegeta
  alie leta mizengwe pole sana hahahahaha

 8. Sensei Romi(Rumadha) Says:

  Makunja(Ras-Kunja)
  Hongera sana! Wimbo unaujumbe mzito sana.
  Kazi safi, nasubiri tu website ya kununua CD au video.

 9. kiwila Says:

  Ras makunja !hii kali ya mwaka! vipi baba wa kambo
  mmekorofishana nini?tena ?naona unamsemea hovyo!
  hivi uhogopi kuwa utanja ndoa ya mama

 10. BLACKMANNEN Says:

  “Sensei”, habari za ‘Jambo?’. Karibu BC…..!!!

  This Is Black=Blackmannen

 11. Jane Says:

  hi!Kaka Brother Ras Makunja! hili sasa soo jipya! tena linanikumbusha mbali nilipokuwa nalelewa na baba wa kambo…halafu alikuwa noma na mnoko kishenzi!!!!
  lakini huu wimbo wako umenitoa machozi kwa kunigusa hisia zangu ! wimbo wenu huu umekuwa dawa ya kutibu mawazo yangu yalikuwa na hasira !kuanzia leo naona mmewakilisha kilio changu adharani.Nami nimemsamehe baba wa kambo.
  kazi yenu nzuri sana.
  Jene
  Goterborg,Sweden

 12. Tabia Says:

  hallo! ras Makunja?! vipi hapa kulikoni mbola vidole machoni!
  na Baba wa Kambo? ndio tuseme umeamua kumsemea ovyo?
  Lakini nyini si milipewa onyo na mjomba wenu Msondo ngoma
  kuwa tabia ya kumzomea wakubwa ni mbaya! halafu militubu na kusema amfanyi utukutu tena! sasa leo vipi mnarudia tabia zenu za watoto wa Kariakoo?

 13. Suzan Says:

  Kaka Ras Makunja !ununda bado ujaacha?
  kwani tabia hii ya kurushia mawe wakubwa na kusema ovyo uliahanza ukiwa mdogo,kumbu kumbu zangu nakujua nilipokuwa naishi jirani na marehemu baba yako! kule osterbay aka masaki! wewe hilibidi uhondelewe pale na kuahamishiwa ktk nyumba ya familia yenu Kinondoni kutokana na tabia ya kuwakorofisha manjagu waliokuwa
  wakilinda geti la baba yako,na siku moja ulihamua kuwarushia
  mawe,wakati walinzi walikuwapo kwa usalama wenu!
  leo hii sioni hajabu ukimsemea ovyo baba wa kambo.

 14. Tindwa Says:

  Kaka braza makunja pasua pasua ukweli,
  akina baba wa kambo wengine ni wakatili tena wana roho mbaya.

 15. Amir Says:

  We! halima,
  mtoa maoni namba 2 unasema huyo jamaa wa kati ras makunja kacheka? au katabasamu? huyo Simba !na simba ni simba tu ukimwoana atoa menu usifikilie anakuchekea!
  ukimsogelea atakutafuna,jamaa ana kipaji tena ana noma katika kazi yake,tungo zake zimezaa matunda katika jamii na kuleta changamoto.

 16. Hombiz Says:

  Pole sana dada Jane. Let me pass some tissuezzz 4 U!
  Msamaha ni dawa nzuri sana! It`ll help you let all that anger out and be a new person again!
  Have a fresh start please!
  Be cool ma sista!

 17. dino Says:

  kaka ras makunja,umewagusa wengi!lakini mimi binafsi nilikiona cha moto kwa malezi niliyoyapa kutoka wa baba wa kambo,yaani hata mama yangu mwenyewe hakuweza kunitetea! katika huu wimbo wenu unaliza pale unapoimba:
  “Mama kalewa mapenzi kanisahau mwanawe!” na unasisitiza
  “Muyaone walimwengu mahajabu ya ulimwengu” Kaka bro!
  umenigusa maini yangu,lakini any way nimewasamehe wote yaani Baba wa kambo paamoja mama yangu aliyelewa mapenzi na kunisahau mimi,naleo hii nipo hapa U.K aka ukelewe nabeba mabox na nampa msaada sana mama yangu,
  kwa hayupo tena na yule mpenzi wake.
  kaka ras makunja nashukuru kwa kuweka uwanjani yale ´machungu yaliyo jificha miyoni mwetu.
  Big Up

 18. Michuzi Says:

  Awali ya yote naomba nitoe hongera sana kwa wana Afrika Ngoma Band kwa kuendeleza libeneke kisawasawa huko waliko. Hawa jamaa, chini ya Ras Makunja, ni noma kama wanavyosema watoto wa mijini.

  Napenda pia kutoa shukrani kwa shavu kali walilonipatia pamoja na jukumu zito la kuamua kesi hii.

  Kwa kweli ukisoma maoni utakuta songi hili limegusa wengi na hivyo basi mtunzi wake anastahili pongezi kwani ni nadra sana kukuta jambo hili likitokea. Hongera sana Ras Makunja. Nakukumbuka sana enzi za mtaa wa Aggrey chini (mie niliishi Aggrey juu) ambapo ulikuwa mtu wa mihangaiko kuliko kawaida. Sishangai kuona mafanikio uliyoyapata

 19. hombiz Says:

  Kaka michuzi mbona hujatubainishia kama ombi la mtoto wa kambo utalifanyia kazi ama laa!. Je, utakwenda kutwanga hizo picha na kuanika mateso yake hadhalani!?

 20. kileo Says:

  Kaka! michuzi ?hamua kesi basi hijulikane nani mkosa?
  maana ujaweka wazi uhamuzi kati ya Baba wa Kambo na
  watoto wa Kariakoo akina Ras Makunja,na ali we we ukweli unaujua kuwa kulea watoto wakufikia ni kazi ngumu!
  Tena watoto wenyewe wakiwa watoto wa kariakoo wenzio
  aka watoto wa mjini,nani mwenye makosa ?watoto watukutu? Mama aliyelewa Mapenzi? au dikteta baba wa kambo?

 21. chapombe Says:

  we bwana weee,najua hao wazungu huko wala hawajui maana ya baba kambo,sema hizo beat zimetulia kisawasawa,najua wakilewa wanakatika kwelikweli,miziki ya kiafrika we acha tu


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s