BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

pazia la fiesta lafungwa zenj kwa kishindo November, 16, 2008

Filed under: Burudani — bongocelebrity @ 7:02 AM

bcccbc22bcc1b3Tamasha la fiesta jirambe 2008 jana usiku pazia lake lilifungwa rasmi ndani ya uwanja wa Mao Tse-Tung uliopo Michenzani,ambapo wakazi wa zenj walijitokeza kwa wingi kujiramba kwa namna ambayo waliita ya kujiramba kizenj.Pichani juu kabisa ni kikundi cha ngoma ya Kidumbaki kinachoongozwa  na Mzee Makame Faki (kwa wakazi wa zenj kikundi hiki shughuli yake wanaijua vyema),inayofuata ni Msanii wa kizazi kipya Mwana-FA akiwauliza wakazi wa Zenj kama nao bado wapo wapo kama yeye anavyodai ama la,Wasanii wa kundi la Tanzania House of Talent nao wakionesha kipaji chao cha kucheza mbele ya wakazi wa Zenj na mwisho kabisa pichani ni Prof Jay akiwakuna vilivyo wana wa kizenj ndani ya tamasha la fiesta jirambe ambapo kilele chake ilikuwa jana usiku ndani ya uwanja wa Mao Tse-Tung uliopo mIchenzani

Advertisements
 

23 Responses to “pazia la fiesta lafungwa zenj kwa kishindo”

 1. BLACKMANNEN Says:

  Waliokuwa wakitaka maguo marefu ndiyo hayoo. Sasa angalieni na kusifia kuwa watu wananidhamu ukilinganisha na enzi za siku hizi. Kila mtu anataka kuona vitu Bwana, sio maguo marefu, eti sema ndugu yangu “Majita”.

 2. binti-mzuri Says:

  hahahah @ blackmannen.. me no comment.. bazee jamani hilo!

  nimewapenda hao house of talent sijui,hao wanaume waliovaa white

  yule mwanaume kule juu nae kajifunga kitenge anakatika jamani..eeh!..kazz kubwa hii!

  inaelekea ilibamba haswa

 3. hombiz Says:

  Duuh!, hiyo staili ya kwenye picha ya tatu kutoka juu imetulia kweli!
  Prof Jeeeeze kamua…….mbongo nambali one mwenye alama ya ndui na sio tattoo. Hapo sawaaaaaaaa!

 4. michelle Says:

  Ndo nini sasa maguo marefu, wana mambo hao na hizo nguo zao ndefu, hakuna lolote wanafiki tu,matusi ndo zao hizo.

  Na hao hapo juu na masweta yao meupe, ndo nini sasa? mwisho ataumizana maana hata lishe ni duni.

 5. duh hao jamaa wa THT katika picha ya 3 style yao nimeikubali. Ila huyo wa nyuma inabidi awe na stamina kweli!!

  Haha, Blackmannen umenichekesha kweli mshkaji; you decided to say the truth that no one else would sio? Haya 🙂

 6. Majita Says:

  Blackmannen,
  Yaani nakumbuka enzi zetu pale Lasacachika Tanga ulikuwa ukiingia pale counter/mlangoni unakuta maguo hayo marefu na baibui kibao zimeachwa.Mtumeee!!!!vuka huo mlango na udumbukie kwenye muziki,yeyeyeyeye vitumbo nje.Yani nilikuwa nacheka hadi basi kumbe wavaaji wake walikuwa chicha.

  Ndaki uko wapi??Najua hapo nimegusa viwanja vyako manake ulikuwa unazunguka tu hapo mjengoni na kutumbukia ndani.

  Binti Mzuri,yaani yule mshikaji kule nyuma ananikumbusha mambo ya wete,pemba na mji mkongwe huku unguja.Ulikuwa ukiingia disco yaani asilimia 98 ya miziki inayopigwa ni taarabu,sasa hapo ilikuwa haitoshi.Balaa ni pale unaposhitukia wanaume woote mle ndani wanacheza mduara na kupeperusha vitambaa vyao juu.Yaani wewe acha tu.Sisi eti wa bara wakawa wanatuita washamba na wao kujiona wamekulia maisha ya kifahari kama ya swaiba yangu binti wa masaki aka mtoto wa kishua.
  Kaaaaazi kwelikweli

 7. Matty Says:

  hatimaye dila latinga jukwaani lol! hata haina mvuto lol!!!!!!tushazoea kuoneshwa vitobo nyuma ya goti aluuuuuuuuuuuu!

  yes, Prf J, wape vituz!

 8. halima Says:

  Jamani hiyo style ya THT mmh kama umetoka kupiga nguna na maharage lazima hapo upumue.

 9. SaLaMa Says:

  kamua mwana prof. J
  nimependa sana hayo mavazi ya hao sijui wakinadada au niwaite wakina mama mmependeza sana.

 10. Mzee wa Changamoto Says:

  Tunapoangalia MAGUO ni vema tukaangalia maudhui na wakati wa kuvaa maguo hayo. Sijui hao wa mwanzo “maguo” yao yanaendana na wimbo wenye ujumbe gani. Labda si kawaida yao, waliamua kufikisha ujumbe tuu. Si mnakumbuka Video ya Mwinjuma ya Kilio cha Yatima. Wakaimba kama wako msibani. Ukiichukua ukai-freeze bila kujua kiimbwacho utaona mnafiki maana twajua anavyowavalisha ma-stage show wake.
  Kwa Mwana-Fa sina la kusema maana nadhani amevaa kulingana na maudhui mengi ya nyimbo zake. Ki-ujana ujana na akiuliza kama wapowapo anaweza kueleweka. Si anaonekana kama “bachela”?
  Hao THT naona ni njema maana ni nguo za baridi kiasi na ni usiku. Wamependeza.
  Prof Jay naye yuko “simpo” lakini sina hakika na hizo Safety Boots hapo. Lakini anyway, si kila mahala pahitaji usalama?

  Blackmannen tuwasiliane changamoto@gmail.com

 11. Gervas Says:

  Hao mabinti kama wanacheza sindimba vile,..hata Bi kidude havai hayo ati mjanja yule, ndo BASATA wanataka hivi sasa. Cheki vijana wakizenj walivo watulivu utafikiri wanamsikiliza Maalim Seif…. pangeimbwa taarabu naona pasingetosha. THT-naona ni good idea kwa aliyeianzisha, sio ajira tu bali kuibua vipaji pia. SWALI: Mbona Pemba na kule kwetu mchambawima, mwembe malingo, Kiwengwa hawaendi fanya Fiesta huko?

 12. any Says:

  UKISIKIA MTU UTAKULA KWA JASHO NI HAO, AMBU ONA HAO WAMAMA WALIVOSWETI KWA AJILI YA KUJITUMA.

 13. unajua maoni ya kaka Black=Blackmannen kuhusu kuvaa “maguo” ilikuwa utani, ila imenifanya nifikirie kidogo. Nakumbuka katika somo la kiingereza kidato cha nne tulisoma “Song of Lawino” na nakumbuka moja ya vitu ambavyo mwandishi Okot p’Bitek aligusia ni juu ya mavazi na utamaduni. Katika moja ya beti, Lawino anamzungumzia kimada wa mumewe, Ocol, anayeitwa Clemetine. Lawino anasema kuwa Clementine anavaa mavazi marefu yaliyoletwa na wakoloni, ambayo sio sawa na asili ya wanawake wa Kiacoli yanayoonesha uzuri wao.

  Swali langu kwa wadau ni kuwa uvaaji upi unaendana na utamaduni wa Mtanzania (kwa kuangalia kabila kwa kabila, na pia kwa kuangalia taifa kiujumla)

 14. halima Says:

  Mmewaonea tu kuwapelekea fiesta hao check wanavyotia huruma jamani. Check wanavyomtolea mijicho FA yaani wanaona anawazingua tu.

  Hapo angekuwa ni mzee yusuph yupo ahhh ungeona mijanaume inavyozungusha nyonga. Mwakani kwenye fiesta kuwe na taarab ili iwe haki sawa kwa wote.

 15. BLACKMANNEN Says:

  Nalitolela na Watanzania wenzangu hapa BC,

  Tanzania hatuna vazi maalum la kitamaduni. Lakini kabila la Kimasai wao wanalo vazi linalojulikana, kama tunavyowaona kila mahali. Watanzania tumejitahidi kupata vazi letu wenyewe, kwa kuiga mavazi mbalimbali, tumeshindwa kupata vazi rasmi la kitaifa.

  Nionavyo mimi, ni heri tulivyokosa vazi maalum la Kitanzania, maana kama tungekuwa nalo, lingeleta mijadala isiyokuwa na maana na tungeachana nalo, kutokana na kuibuka kundi la watanzania roho mbaya, wanaojitahidi kuwavuruga wenzao kwa kuibua mambo ya ajabu, yasiyokuwa na kichwa wala miguu.

  Kila mara, swala la mavazi tunapolizungumza, na kuliingiza kwenye maadili ya Kitanzania. Mtazamo wetu wengi, tunauelekeza zaidi katika mavazi ya wanawake. Huu ni ubaguzi wa kijinsia, nionavyo mimi. Sijaona mwanaume kapigiwa kele za jinsi alivyovaa, ukilinganisha na mwanamke. Tabia hii, sisi wanaume, nawaomba tuiache, mara moja.

  Natoa mifano yangu miwili; 1) Waje vijana wetu wawili, wakike na wakiume, na wote wametinga suruali za kata “K”, nani atakayeshambuliwa zaidi na watu? Jibu: Ni msichana.
  2) Waje watu wawili, mwanamke na mwanaume. Mwanamke kajaliwa umbile la kufa mtu, na kifuani mwake ziwa linaonyesha saa sita kamili za mchana, saa za Tanzania. Mwanaume ni pandikizi la Baba, mabega mapana, kifua kipana cha kuua mtu, na tumbo lenye matuta na matako ya kiume.

  Watu hawa wawili, wanajipenda sana, na wamevaa mavazi ya kubana, kuonyesha kila kitu walichojaaliwa, na Maulana Mweniazi Mungu!!! Nani atakayeshambuliwa zaidi? Jibu: Ni mwanamke.

  Mavazi sio umalaya, bali tabia ya mtu ndicho tunachotakiwa kukiangalia. Tamaa za wanaume ndizo zinazosababisha wanawake waandamwe, wasipewe nafasi ya kuvaa kile wakitakacho. Wanaume sharti tujifunze ku-control hisia zetu za kimapenzi (ngono). Sio kila mwanamke alivyovaa na kuonyesha sehemu kubwa ya mwili wake, anatakufanya au anafikiria “ngono”. Hayo ndiyo maoni yangu kwa leo.

  It’s Great To Be Black=Blackmannen

 16. Gervas Says:

  Mdau Nalitolela, umeuliza swali la Msingi hapa. Ninavofahamu, Hatuna vazi lolote linaloendana na utamaduni wa kitanzania. kwanza utamaduni wa kitanzania ni upi? Ukitaka kuongelea kitu ni vizuri utizame historia yake kwanza: Kumbuka Tanzania umejengwa na muungano wa makabila zaidi ya 150, na kila kabila lina utamaduni wake hii ni katika chakula, sherehe, harusi, mavazi nk,
  Historia inatuambia kuwa nguo zililetwa na wakoloni. Hivo kila kabila lilikuwa na style yake. Kutokuwa na vazi la Kitaifa/utamaduni siokosa letu ni historia. Nafikiri kitu kinachotuonyesha historia ya mavazi ya makabila yetu ni ngoma za Kienyeji zinazochezwa kwa sasa. Ukiangalia ngoma kama Sindimba au zile za Bidada saida kaloli…zinakuonyesha ni jinsi gani nguo zile zilivo fupi yaani ni vimini vya either majani, tumbo wazi, mgongo nk na wala sio ndefu za kufunika magoti. Hivo hata mimi nawashangaa sana BASATA kudai baadhi ya nguo eti haziendani na utamaduni wa kitanzania…hebu wau-define kwanza huo utamaduni.
  Wakumbuke kuwa jamii inabadilika kwa sasa, Maasai wanarudi mjini na wananyuka suti kama kawa(na wanavaa chupi..ashakum si matusi), Mawaziri wakike wananyuka vikuku siku hizi, shangaa kwa nini wasivae shanga kuonyesha utamaduni? Namaliza kwa kusema kuwa, Utamaduni wa kitanzania ni “Masala” na hivo uvaaji wa kitanzania pia ni Masala…provided kuwa humwagi radhi!!

 17. nashukuru kwa majibu yenu Gervas na Blackmannen, na niseme naungana nanyi 100%.
  Ila labda kwa kufafanua tu Blackmannen, naelewa kuwa hatuna vazi rasmi la kitaifa, na wengi wetu mara nyingi tukiwa nje, tukitaka “kuwakilisha” tunakimbilia vazi la kimaasai maana kwa kiasi kikubwa utamaduni wao umehimili mikiki mikiki ya ukoloni, na vazi linatambulika hadi leo. Lakini asilimia kubwa ya watanzania tuna utamaduni tofauti na wamaasai. Asilimia kubwa ni wabantu, lakini hata miongoni mwa wabantu tunatofautiana pia; hatuko wote 100% sawa. Hivyo basi swali langu lilikuwa halilengi kutambua kuwa vazi rasmi la taifa ni lipi, bali kuangalia kuanzia ngazi ya kabila moja hadi jingine, tuone vazi la kitamaduni ni lipi, kisha tuweze kusema kiujumla kama sisi ni watu wa “maguo” au la.

  Na pengine ikiwezekana, kutokana na mitazamo ya wadau, BC inaweza kuwa chanzo cha kuibuka kwa vazi rasmi la kitaifa litakalokubalika na wote.

 18. BLACKMANNEN Says:

  Gervas, Nalitolela na wanaBC wote!

  Majumuisho yako Gervas kuhusu mavazi, ni mazuri sana, na pia ni darasa kamili kwa Watanzania wengine hapa BC na BASATA.
  Nashukuru pia kusikia kuwa Nalitolela, unakubaliana nasi 100% katika uchambuzi wetu huo wa mavazi.

  Kuhusu pendekezo lako Nalitolela, la BC kuwa chanzo cha kuibuka vazi rasmi la Kitaifa, litakalokubalika na wote. Mimi naona tupate mchango wa kutosha, wa wanawake kuhusu swala hili, maana mimi naona ndiyo wao wanaotazamwa zaidi namna wanavyovaa na watu wengi.

  Mifano yangu miwili hapo juu (Comment #15), japo sio kwamba inawakilisha mawazo ya wengi, lakini pengine inaweza kusaidia kuwa kianzio, katika mjadala wetu huu.

  Dada zanguni, hapa ndiyo nafasi yenu ya kujieleza madukuduku yenu yahusuyo mavazi na kutupasha vema sisi wanaume wenye mawazo mafupi, hadi somo lituingie, ambao kwa maoni yangu naona tunawaandama sana ninyi. Mama wa Kichagga, Matty, Binti-Mzuri, halima, Pearl, Lalola, michelle, any, SaLaMa na wengine, tunasubiri maoni yenu hapa! Wanaume pia, Majita, Tommy, Mzee wa Changamoto, Edwin Ndaki, Mtu, tuwemo katika mjadala.

  It’s Great To Be Black=Blackmannen

 19. Matty Says:

  Blackmannen # 15 POINT YAKO NIMEIPENDA NA IMENIGUSA SANA, sie wengine tushazoea vipedo na vimini lakini hapo tunaambiwa ni nusu uchi na si mila na desturi za mtanzania, ziko wapi mila za mtanzania??ni vema kama hata kule kijijini let say Bukoba ngoma zingechezwa na hayo madila may be ndo tungeonekana hatujapoteza mwelekeo, lakini hapo wenye madila pia tukubali nao ni asili yao mwambaoni kuvaa hivyo, basi kama tunavaa vibwebwe na vibywaya vifupi namna ile na kishort pensi kwa ndani sioni kama kuna sababu ya kusema msichana aliyevaa kimini/pedo kavunja maadili!
  Mila na desturi zipo kulingana na makabila ndo utapata hayo mavazi ya asili, ngoma,nyimbo na vyakula vya asili!

  Vazi la taifa rasmi halipo ni kweli ila sasa nadhani hata kama lingekuwepo naona kama watu muhimu ndo wangetakiwa wavae na kwa sehemu maalumu si kila mahala mfano.livaliwe ktk sherehe mbalimbali hasa za kitaifa,mikutano ya kitaifa,mazishi n.k

  Pendekezo langu naona kusiwe na vazi la taifa, kama litakuwepo basi liwe na flavour ya makabila yote ya Tanzania ndo tupate kitu kimoja!
  Je ni nani ataweza kulibuni hilo vazi??

 20. binti-mzuri Says:

  jamani blackmannen mi sijui nisemeje,am happy with your comments ulichosema ni vizuri na kweli kabisa! mi sioni kama ni women abuse or whateva mtu kuvaa miniskirt au ki pedo pusha.. mi navaa na sioni kama am abusing my body. vaa kile kitu roho inapenda.. yani tulazimishane ma bazee tuu? aah! wabongo tuamke,na tuache kasumba za zamani.. this is 21st century,lets live accordingly. kila mtu ana rights ya kufanya kile atakacho,kama you are not happy with it,deal with it. if you are not confident with your body or feel its abuse etc,do not wear such materials..ila it doesnt mean uende kuwasema wale wanaovaa vile..kwani wewe hayakuhusu!.. habari ndio hiyo! mi nashangaaga akija beyonce watu wanashangilia kishenzi,kaja ray c wanaanza kusema mmh huyu ana biashara nyingine zaidi ya kuimba coz ya mavazi aliyovaa.. how come you dont say the same for intl artists!.. if its culture,tulianzia huko huko kwenye vibwebwe!

  like what blackmannen said, mavazi sio umalaya,angalia tabia ya mtu

 21. any Says:

  BLACKMANNEN point nzuri, fashion ina depend na weather, time, personal choice and or financial position. So it depends unavaa nini na wapi na hali ya hewa inaruhusu?
  Ukivaa kwa hiari yako poa tu, hata ukiamua kwenda nusu naked its ur business, ila kama unalazimishwa kuwa ndio vazi la kazi? mh, apo sijui uhuru wa mtu kuhusu avae nini inakuwaje. Mf. dada zetu wanacheza show/dance/whatever, wengi sidhani kama ni hiari yao, Njaa nayo inachangia wakubali kuvalishwa kama midoli. My opinions though! as u know opinion is like an as.shole, kila mtu analo. mwingine ana makubwa, mwingine madogo, na wengine cherema. haaa.

 22. BLACKMANNEN Says:

  He he he heeee “any”!!!!!! ………opinion is like an *******, kila mtu analo. He he he he, Kaaaaaazi kweli kweli!!!!

 23. any Says:

  Hukuwa na habari kwani? size za opinion zinatofautiana, haziwezi kulingana, so tako was a simple example kuelezea. mfano wako wenye ya kihindi ya kichaga, kihaya, etc.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s