BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

Kampuni ya Kagoda ni ya nani? November, 19, 2008

Filed under: Watu na Matukio — bongocelebrity @ 9:48 AM
Tags: , ,

mengi

Mwenyekiti wa shirikisho la wenye viwanda Tanzania (CTI) na Baraza la biashara la Afrika Mashariki (EABC) Reginald Mengi akiongea kwenye maadhimisho ya 19 ya siku ya viwanda Afrika na maadhimisho ya miaka 10 ya taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF) kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam jana.Kupitia shirikisho hilo,Mh Mengi wamemtaka DPP aweke wazi nani mmiliki wa kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd inayodaiwa kujichotea bilioni 40 kutoka katika akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA),ambayo mpaka sasa hajafikishwa mahakamani !?.

Advertisements
 

69 Responses to “Kampuni ya Kagoda ni ya nani?”

 1. mtu Says:

  I hope nia yako bwana Mengi ni ya kweli kutetea haki za wanyonge na sio kuwavalia njuga wenzio kwasababu mgao huo haukukupitia na wewe.
  Nikitendo cha kupongezwa na juhudi zako zisiishie hapo tu, bali mpaka mafisadi walio jificha wafikishwe mahakamani. Binafsi nachukua nafasi hii kukupongeza. HONGERA SANA

 2. halima Says:

  Hapo ndipo patamu hapo kudadadeki mmoja baada ya mwingine watatajana tuu.

 3. Simba Says:

  Fanyeni mambo its about time tumechoka na Polisi wanaoogopa vigogo na kukamata samaki wadogo.Keep it up Mengi!

 4. DUNDA GALDEN Says:

  Hiyo kampuni ya Matty,Binti-mzuri,Pandu pamoja na mama wa kichaga

 5. Hombiz Says:

  That’s what I’m talking about! Heko mzee Mengi! Shiaka bango hadi kieleweke! Kanyaga mafuta ,mazee! Usiogope tuta wala shimo. Funika… funika… funika…
  Vita dhidi ya ufisadi si ya mtu mmoja tu! Everybody needs to play his part. Zama za kuogopa kufumbwa midomo, zimepitwa na wakati. Kuhusu swala hilo, hata mimi nasubiri jibu kwa hamu. Nani mmiliki wa Kagoda!? Kwanini iwe siri juu ya mmiliki wake!? Mimi siamini kwamba hajulikani. Hii sio kweli.

  Kwawana BC Blog ambao hawajasoma juu ya utata wa Kagoda, wanaweza kupitia hapa ili kupata maelezo zaidi http://www.raiamwema.co.tz/08/02/27/3.php

  Pia nadhani ikiwa ufumbuzi utapatikana ama laa, mimi ningeshauri tujaribu kutumia kanuni ifuatayo ili kuepusha ufisadi kama huu siku zijazo:
  M+P+R=RR nikiwa nina maana kwamba Monitoring + Programming + Response = Reduced Recidivism Naamini serikali inaijua vema kanuni hii. Ikiwa itatumika ipasavyo, wizi, udokozi na ufisadi wa mali ya umma, utapungua kwa kiasi kikubwa sana. Hivyo basi utajili wa nchi, utamfaa kila mtanzania.
  Stay Focused y`all!

 6. Fukara Says:

  Ni ya mafisadi wote wanaokingiwa kifua na Serikali

 7. Majita Says:

  yaani hizo bilioni 40 zinavyotamkwa utafikiri ni sh.1,000/=
  Yaani hamuwezi kuamini,mimi hata kuiandika hiyo bilioni 40 sijui.Sasa kuna wajanja wamejichotea mihela yote hiyo.Yaaani nahisi ukinipa kuihesabu hiyo bilioni 40 nahisi nitahitaji watu wa kuniazima mate manake ya kwangu yatakauka kwa kulambia vidole.Grrrrrrrr

  Ningekuwa mimi nipewe nchi siku tatu tu wangekiona cha moto.Wizi gani huu??huh??fyuuuuuuu.
  Avache Mengi

 8. ROss Says:

  Huyu Mengi anataka kuendeleza UCHADEMA wake hapo TUU

  Hebu Mengi tulia ,acha siasa kula pesa yako, utajisumbua bure wewe sio Obama, Wachaaga hamuwezi sema “Yes We Can” kwa BOngo.

  Wachaga Bongo mnaonekana kama ni Masters kwenye Plantation, so usilete kimbelembele ukajiharibia

  Unataka uraisi wa nini wakati Unahela zako nyingi tuu za kubalisisha maisha watu? ,au unataka ziongezeke zaidi? acha baba, unajina teari , fanya maendeleo kwa charities sio kujifanya una uchungu na EPPA kumbe ni gea ya kujijenga jina ili ugombee Uraisi kwa ticket ya CHADEMA ,Mengi tunakupenda sana!

 9. any Says:

  huyo mpiga picha? mh, sina mengi mie.

 10. BLACKMANNEN Says:

  mtu,

  Karibu sana ndugu yetu, maana mimi na Majita, hata na Binti-Mzuri, sasa tutapumzika. Maana Matty ilikuwa kila saa, jamani “mtu” yuko wapi? Kila siku “mtu”, tukigeuka huku, “mtu”!!! Oooohhhh “mtu” yu wapi? “mtu”….”mtu”….”mtu”!!!! Khaaaaaa!!!!!!!

  Sisi wengine ukijumuisha na “miwivu” yetu……Dah!!! Mbona ilikuwa balaa??? Kama usingekuja hapa wiki hii “mtu”, mimi nilikuwa nimeamua kujiondokea zangu hadi Majohe, nje kidogo ya Gongo la Mboto nikajipumzishe.

  Maana mimi wivu wangu, acheni tu, hauna mchezo kabisa!!! Haya, “Mengi” hapa anasemaje sasa, maana nilipoona jina la “mtu” sikuwa na haja ya kusoma kitu kingine. Nitamsoma “Mengi” baadaye!

  My Name Is Black……..Blackmannen

 11. Majita Says:

  Jamani wana BC wenzangu,
  Siyo kwamba nina chuki na huyo mwenzetu aliyetoa maoni hapo juu namba 8,ila duuu hayo maoni yake ni babu kubwa.

  Mimi ninaloamini sasa ni kuwa hata kwenye msafara wa Mamba kenge hawakosekani.Tuvumile tu tutafika.Duuuu haki ya nani huko masaki kuna kazi.

 12. Mama wa Kichagga Says:

  Uchangiaji wa huyo Ross mbona umekaa kaa mrengo wa kushoto sana?

  Ingefaa zaidi kama michango yake inalenga kujenga kuliko kujikita kwenye anga za upondaji zaidi na zenye kugawa watu kidini/kikabila!

  Kumbuka Ross Mungu hakuumba kabila wala hakuweka mipaka ya kutenganisha nchi! Ni watu wa aina yako ndio wametufikisha hapa tulipo!

  Nakuombea Mungu akupe moyo wa nyama ujue kuwaongelea wenzio katika mtizamo chanya daima! Ubarikiwe.

  “NO ONE IS PERFECT, THEREFORE I’AM PERFECT”

 13. Pearl Says:

  Ross, now i can read your mind even more that you are of unsound mind,wewe nadhani uliangushwa ukiwa mdogo halafu akili yako ikasogea from the origin. Mwenye akili timamu hawezi kuandika ulichoandika wewe. Na kama ndio gia yako ili wana BC wakutambue nadhani utakuwa umepotea njia kwasababu tutaku-ignore muda si mrefu.

  Jukumu la kuwafichua mafisadi ni la kila mtu na Mengi amegundua hilo ndio maana amechukua hatua kuuliza pale anapohisi kuna mashaka.

  Halafu Dunda Galden hiyo Kagoda nahisi ni yako,Majita,Hombiz,Blackmannen a.k.a wivu boy,hehehehe
  Jamani hayo yote ni utani kina kaka msinipige mawe humu.

 14. Gervas Says:

  ROss/loss….kwa saikologia ndogo tu inaonyesha ni jinsi gani ufisadi umekufaidisha. Nachelea kuamini kwamba wewe ndo moja ya watoto wa mafisadi mliojificha ng’ambo na nawashauli TAKURU waanze nawewe. Watu watakushangaa at this point kutetea ufisadi. Inatia nguvu sana watu wazito kama kina Mzee Mengi Kushikia bango Ufisadi maana kama watu wenye nguvu ya maamuzi na utawala serikalini watakaa kimya, unafikiri nani atamsikiriza maskini?. Ross….hata kama unafaidika na huo umasikini, kaa chini na ufikirie masikini wanaoteseka na kufa kwa kukosa chakula au dawa ya sh,1000 kule vijijini.

 15. Gervas Says:

  Saa nyingine huyu Ross….nafikiri hapa tunajaribu kufukuza mwehu aliyekwapua nguo zako wakati unaoga Beach!!

 16. Matty Says:

  Mtu welcome back kakangu!

  DUNDA GALDEN unatafuta maneno mchana kweupe shauri yako!!!!!!

  Blackmannen ni kweli nilimmiss sana MTU!

  Kuhusu hiyo Kagoda sijaelewa vizuri kama ni kweli mmiliki haonekani, au ndo hizo fix zenyewe!Mimi naona mmiliki yupo na anajulikana but amewikwa kwenye brackets!we are tired of that bwana!

 17. Mayu Says:

  Jamani hivi kampuni iliyobaki au inayotafutwa ni Kagoda tu au kuna zingine

 18. mr degree Says:

  anautaka urais huyo mchaga Ross umenena Vyema! lakini hana sifa ya urais hata kidogo huyo mchaga.kila siku analalamika tuu kama mtoto anaona yeye anaonewa tuu.aende zake bwana.yeye kama ana uchungu wa kuendeleza maisha ya watu aende akaboreshea mishahara ya watumishi wake.wanamkimbia kila siku kwa kuwalipa mishahara mbuzi ndo maana amebaki na wachache wenye elimu ndogo tuu wengi wamemkimbia.

 19. halima Says:

  Pearl shost uwiiiiii jamani nimecheka mpaka mbavu zinaniuma yaani kama ni dozi ya malaria haki ya mungu inauwa mpaka taifod. Hebu mpe uyo mbeba box Ross asituletee za kuleta hapa.

  Mimi nafikiri huyu Ross anamatatizo ya kisaikolojia sio mzima huyu wana BC nasikia anachet cha mirembe muulizeni Papuu anamjua.

 20. Mh LUKAMBA Says:

  kampuni ya KAGODA ni ya KAGODA !!
  Mengi piga kimya !!
  sisi ni WADANGANYIKA inatosha,mengi subiri kipande kinageukia muda siyo mrefu

 21. pablo Says:

  anachofanya mengi ni haki yake akiwa raia wa bongo na mlipa kodi japokiuwa watanzania wengi wamekata tamaa na kuamini kuwa wanasiasa wana haki kufanya watakavyo na baaadhi yetu tunauelewa mdogo kiasi cha kutojua madhara yaubadhirifu achilia mbali wanaonufanika kwa kutokana na ufisadi ndio maana kuna huyo mchingiaji anamtaka mengi akae kimya wakati kuna wananchi wanakosa matibabu,watoto wanakaa chini kwa ukosefu wa madawati nk na mtu mmoja na familia yake wanachukuwa 40bil!!! shame on him

 22. Pearl Says:

  mmhhhhh!!!! ila jamani kweli huyo mpiga picha wa hiyo picha ya mnato ya Mengi mmmmmhhhhh!!!!! mie sisemi ila iangalieni hiyo picha. Sijui Raque yuko wapi aliyekuwa anawapiga picha wale “Visura Wanaojitambua wa Face of Tanzania” aje aseme neno kuhusu hiyo picha. Matty na Binti mzuri nadhani mpo hapo nikimtaja “Rakii”

 23. leini Says:

  Hehee nyie mmemsahau Ross alikatazwa kuoga kwenye vidimbwi kule kijijini kwao mtoto wa magetini masaki. Kweli bora usiwe unaandika kitu. Somethiihg is very wrong with you ndio maana unachuki na mafanikio ya kila mtu kweli walikuangusha ukiwa mdogo

 24. buddaboo Says:

  Kagoda ni ya Manji na Rostam Aziz,so mchaga anatumia nafasi hiyo kutafuta kuungwa mkono na waTanzania kwenye beef lake linalojulikana la muda mrefu sasa na bwana Manji..tunaunga mkono juhudi zake kwenye kupiga vita ufisadi yes,lakini kwenye hilo beef yao naomba ajue halina maslahi kwa Taifa so halituhusu!period.

 25. Hombiz Says:

  Aaaaa wapi dada Pearl. Hombiz hawezi kumiliki KAGODA! Uwezekano wa mimi kuwa FISADI ni 4×4-16. Bila shaka jawabu umelipata. Yaani mimi hasira zimenijaa sana dhidi ya mafisadi. Nadhani itanibidi nikazipunguze kwa kusukuma treni toka Dar hadi godegode….kwi-kwi-kwiiii!!

  Na nikisharudi kutoka godegode, nakula plate moja na MAFISADI through BC Blog mpaka kieleweke..
  Mtetezi yeyote wa mafisadi akikasirika, itabidi achukue uzi wa buibui akajinyonge kwenye tawi la mpapai…..kudadeki!
  One love Pearl!

 26. binti-mzuri Says:

  mh lukamba kagoda ndio nani,au u meant kigoda? jamani let us know tuwajue mafisadi wa bongo.

  dunda galden lol .. naona umewachoka madada zako! – blackmannen our wivu boy,sio siri matty alimmiss sana mtu! pearl nipo nimekupata,ndo tatizo la unprofessinal photographers..mambo haya yahitaji ujuzi jama.

  mengi all the best katika ukweli wako,pia kaa hima wasije wakakugeuzia na wewe kibao..bongo watu roho mbaya!

 27. ROss Says:

  To mama wa KIchaga

  Mimi sio Mbanguzi na weza oa demu wa kichaga sina tatizo na wachaga, ila ukweli hauto badilika kuau kiwa na jina “Mushi,Laswai, Macha,Munisi,Kimario,Masawe ” Sahau kuchukua nchi kwa Tanzania ya sasa , ndio mana nasema wachaga hamuwezi sema ” YES WE CAN “

 28. halima Says:

  Matty mimi naamua kuwafungisha ndoa hapa mr degree na Ross naona kama akili zao zinafanana hahahahah Bint mzuri hapo vip?

 29. Matty Says:

  Pearl picha hiyo mimi mwanzo sikumtambua muhusika kabisa mpaka niliposoma ndo nikaelewa, anyway utaalamu huo noma!

  Mtaniwia radhi na wasiwasi kama ROSS anastress za kuachwa na bf wake ndo maana anapayuka ovyo lo! tupishe bibie!

 30. Pearl Says:

  halima nakwambia kweli huyo mtoto wa masaki iko shida.

  hombiz nakuaminia kaka fichua mafisadi tuijenge tanzania yetu.

 31. binti-mzuri Says:

  kumbe ross mwanaume! hahahhahahahhahhahahahhahahahah

 32. Matty Says:

  hahahahaa ustadhati Halima shosti wafungishe ndoa ya mkeka hao, ila sasa mbona ROss kashout kwa mama wa kichaga as if yy ni kudume???mhh i wonder asijekuwa Lesbian tu!

 33. Pearl Says:

  kumbe Ross ni “DUME”!!!!!!!!!?????? hehehehehehe

 34. halima Says:

  Nimepata mshtuko kugundua kwamba ROSS ni kidume uwiiii mwanaume gani huyo anaakili fupi kama miguu ya sisimizi mmmmh

  Baada ya kudondoshwa akiwa mdogo nahisi wazazi wake walishagundua kwamba hiki ni kimeo so hata katika harakati za kumpatia jina ikabidi wampatie jina la utata utata yaani halieleweki kama ni lakike au kiume. kwikwikwikwikwi

 35. Gervas Says:

  Swala la Mafisadi itabidi mambo ya haki za binadamu, sijui utawala bora yawekwe kando. Kwanza wanatakiwa wacharazwe bakola kwanza za matako kabla hata ya kupewa dhamana…nyambafu kabisa hawa. Wanasumbua mtaani navijigari vyao kumbe vya udokozi. Tena hizo bakola wanatakiwa wachalazwe na mwalimu wangu wa Primary…liwe fundisho, hii ni kama kweli JK anataka Change.

 36. Mama wa Kichagga Says:

  Ross asante kwa kujidhiirisha wazi ujinsia wako na ulivokuwa mbabaishaji.

  Chuki yako kwa wachagga wee endelea nayo halafu ukifanikiwa tuambie. Sie wenzio tunasonga mbele na maisha na wala hatutaukasirikia ujinga wako kwani hatuko tayari kupotezewa muda na watu wenye mawazo kama yako.

  Point zako ziko hopless na tena hazina utafiti wa data za kuback up! Hivi nikuulize mara ya mwisho mchaaga kuwa rais akaboronga ilikuwa lini? Na je tukihukumiana kwa ujumla wa kiukabila au udini tutafika? Nakushauri kwa MARA YA MWISHO” penda kuzungumzia wenzio kwa mtazamo chanya kwani itakusaidia pia na wewe kukua kiakili na kimaendeleo.

  Basi kwa vile unaamini mchaga hawezi nenda wewe kugombea urais 2010 au chagua kabila lako nasi tuko tayari kuongozwa!

  Maneno yako yanaonyesha jinsi gani ulivokuwa na chuki na hili kabila pole sana maana itakuuwa!

  Kumbuka huo ujinga wa kumchagua mtu kwa kabila hauna maendeleo yeyote na pia TZ ni ya watu wote bila kujali kabila, rangi au dini. Kwa taarifa yako tuu ni kwamba kama yupo mchagga na sera ambazo watu wanazikubali usishangae akawa pia ni rais wako!

  Yaani nakutizama kuwa mtu mwenye roho mbaya kama mkaanga sumu vile au uko stressed ile mbaya maana kila ukikohoa hapa BC unachefua wenzio kwa kiwango cha juu.

  Ok nikutakie kila la kheri na chuki yako kwa wachagga na Mungu akusamehe kwa dhambi hii ya utengano wa watu wake unayoieneza kwa njia ya mitandao wewe na mwenzio Buddaboo!

  MKIKUA MTAACHA

 37. Hombiz Says:

  Ross alibemendwa utotoni nini!?
  Mmmh! Kweli kunguru hafugiki!!

 38. mwandiga Says:

  Mengi kaongea kama mtz. na kila mtz anakabila,sijui kosa ni kuwa mchaga.!!! mbona warioba akaisema hamsemi mkurya,mbona mkap kakwapua hamsemi mmakonde.
  Ni kweli tunataka kujua kagoda ni mnyama gani.
  Hapa kama akina Lowas,mrambee,meghjiiz,ben na familia,kama hawapo sijui!

 39. Matty Says:

  hahahahaha Mama wa Kichagga asante kwa kunikumbusha mstari nanukuu “MKAANGA SUMU “mtoto mshua wa masaki ROSS unakaanga sumu waachie wenye meno watafune lol!

 40. ROss Says:

  Mama wa Kichagga.

  Nadhani huja nielewa nilichotaka kusema, nachosema ni kwamba sina chuki na wachagga. Naamini demu wa KIchagaa ni wazuri na hata kam wan sifa ya kupenda hela mimi hilo nalinisumbui, napenda mademu wa kigaga na hata kam una Binti ambaye umri umefika sito sita kumposa kama ikiwezekana.

  Kuhusu suala la Uchaga , ukweli i kwamba watanzania hawako teari kwa wakati huu, kumpa Mchaga uraisi.. hilo lipo na kama hulijui lifanyie utafiti. ndio maana nikasema Mengi sio Obama (Obama alisema “Yes we can” ) na Mengi hata akisema “Yes We can” kwa waTanzanzania muda bado haijafika kwa TZ kuwa na Mchaga Presdent.

  Hii inatokana na imani iliyopo kwa wachaga (Kama wewe ni Mchaga huwezi jua hilo ) kuwa ni wabaguzi na wanukabila kupindukia, Ukiangalia CHADEMA waBunge wa kuteuliwe ni majina yake yale tuu ya kichagga kibao, Ukiangalia popote kweney Mchaga kama Kiongozi, utakuta wwachaga kibao Angalai TRA na kwingine utakua wachaga kibao, ina wezekana ni coicendence ila Watanzania wengi wana amini kuw ahuo ni Ukabila.

  P.S. Walio kuwa hawajui Ross ni nani. Ross ni a Handsome boy , mixed wa Ki Pare,Kipemba,Kikuyu na KIjerumani.

 41. Malingumu Says:

  Hi Mzee Mengi

  Mimi nazani umefanya kazi ya maana sana kuuliza hilo swali, lakini na sisi tuna kuuliza , yale madeni yako ya NBC uliishia wapi ? ule pia ulikuwa ufisadi , mimi nazani likiisha hili la EPA tuanze kuitazama na NBC nayo unasemaje mzee!!!!!!

  Ze comedy

 42. binti-mzuri Says:

  lol haloo halooo, bc mwanipata? kumbe ross ni half casti aka afri casti.. kaaazzzzzzz kweli kweli!!!!!

  ross watu walidhania we ndiye,siye coz of the pumba u uvurumishad in ze u kno wat…iz i dont wana chapia too much!

  ila mbona wajisifia kaa demu..mmh..au ndio ubishororo wa masaki huu. gudluck

 43. ROss Says:

  Amin MaliNgumu , , maana Mafisadi wengi tuu wapo, wasijifanye wao wasafi.
  Hawa matajiri wengi utakuta chanzo cha utajiri wao ni ufisadi au njia zisizo na uhalali, Martha Stewart ali shock watu baada ya kugundulika sio msafi kihivyo na wewe Yesu wa wachaga Mengi tuanze kuku chunguza.

  Slaa hana lolote ni wale wale tuu, mbona hakemei posho ya Kutoka Conservative party inayo ishia makao makuu na kukarabadi Billicanas na kwingine haiendi huko CHADEMA ,kashikishwa au?

  Binti sio na jisifia ila ukweli mimi ni handsome, ni vizuri kujitambua na kujipenda, kwani kama umejaliwa lazima ukubali na ufurahie.

 44. halima Says:

  Mpare+Mpemba+Mkikuyu+Mjerumani= hazikutoshi

 45. Matty Says:

  i wonder if all MAN would stand to proud themslf through their beauty hahahahaha uhandsome lol!ROSS mshikaji noma!

 46. jamal Says:

  Jamani mimi co mchaga…ni mzenji lakini panapo ukweli tuseme. wachaga wapo sehemu nyingi nyeti coz wamesoma na si kama wachangiaji wengi msemavyo….

  nawajua sana hawa watu, angalieni institution wanazoongoza zikoje….sio mnaongea tu. hata hivyo sidhani kama anahuo mpango wa kugombea uraisi, na hata akigombea atatokea ccm.

 47. BLACKMANNEN Says:

  He he he he heeeeeeeeeeeee! Duh!!!!! Joooooooob True Trueeeee!!!!!

  Black=Blackmannen

 48. Pearl Says:

  huyu mtoto wa masaki ndo mambo kama ya kina “elton john” nini tena au!!!??? wa kunielewa atanielewa

 49. leini Says:

  Kwa kweli Ross ni rafiki wa damu wa elton John kwasababu wanaume hawajisifiagi na comments zake za kidole juu na huo mkorogo wa damu ndio kabisaaa unadhihirisha ni mtu wa aina gani. Ndio maana mama yake alilipukwa na roho alipogundua kaenda kusasambua mtoni

 50. Fukara Says:

  Kwani wa Dau Kagoda ni nini?
  Mzimu?,haioinekani?, Haipo kwenye mafaili ya brela?
  Nafikiriri kila mtanzania anjua ni mchongo tu wa wakubwa kujitwalia fedha zetu wanyonge
  Bila shaka hata Bwana Mengi analijua hilo
  Kila la kheri
  Mdau

 51. Mama wa Kichagga Says:

  Kwa kifupi Ross ni anti-upinzani so anamwaga ujinga wake humu mtandaoni akidhania watu watamsikiliza.

  Toa data muhimu na kama wewe kidumu na unauhakika na uropokaji wake basi usisite kwenda mahakamani.

  Akili tupu mno hii jamani! Waswahili wanasemaga mtoto sio riski huyu khaaaa. !

 52. eve Says:

  nyie pigeni kelele kagoda kagoda msifanye shughuli zenu huyo anayekomaa na kagoda watu wana mabifu yao ndo maana anakomaa kumharasi mwenzie pilipili msiyoila yawawashia nini? fanyeni kazi bwana acheni kushabia unaa wanajuana wenyewe jambo msilolijua usijaribu kuongeza sukari waacheni maddp wafanye kazi yao kwani wakikamilisha si mtasikia tu!!!!!!!!!!!

 53. Mwinjuma Says:

  Naungana na jamal kwa hili, sisi wengine tumezidi kulaum wachaga huku tukiwaficha watoto wetu kwenda shule.

  huko knjaro kuna shule za sekondari kila kata, zingine zina mbilimbili kwanini wasipate vyeo vya maana?

  Tuache kutapatapa, tuwapeleke shule watoto wetu….

  Akhsante

 54. hombiz Says:

  eve you need to STOP!. Be concerned about the prosperity of Tanzania when these evil people misuse the power that voters gave to them!

 55. ROss Says:

  Masaki ndio tunakaa sisi watoto wa kishua, kwani kuna ubaya, mbona mna poteza lengo mnaanza kuni attack sababu mimi ni handsome, au mna wivu?
  Mimi ni handsome na najitambua hivyo, kama wewe unadhani mimi ni Elton John like dude, basi mlete demu wako au sister wako, halafu uone kama hata babaika na mimi .

 56. BLACKMANNEN Says:

  “eve” comment # 54 point yako ni kubwa sana, kwa mtu mwenye akili yake na anayejua issue yote ya Mengi na Wahasimu wake. Mengi ana wasiwasi ya kwamba, “Hasimu” wake anayemtuhumu, anaweza akajinasua katika sakata la “Kagoda”, sasa alifanya kama kumshitaki kwa Makamu wa Rais na pia kuwataarifu wachonga maneno wanaojua na wasiotumia vichwa kuchambua mambo.

  Kazi ya wasiojua mambo na kazi yao kuropoka, wanapenda kupandikiza chuki zao kwa Watanzania ili lionekane swala la Kagoda kuwa ni jambo ambalo sheria inataka kupindishwa ili kuwanasua wahusika. Mengi anajua fika kuwa mambo ya sheria hayapelekwi kwa kubabaisha au kumdhania mtu. Ili mtu umtie hatiani ni muhimu upate ushahidi wa kutosha kuhusiana na kosa alilofanya.

  Mtu kama Mengi, kuja hadharani na kuongea vitu vya ajabu kama hivi ndiyo maana watu wengine wamepata wasiwasi na yeye, kuwa alikuja na agenda ya siri.

  Mengi alichofanya katika swala la Kagoda ni sawa na kurukia treni kwa nyuma kama wachongaji wa humu walivyosema siku moja. Mengi kama angeona shughuli yote ya Kagoda, imeisha bila kukamatwa anaowashuku, ndipo angehoji. “eve”, nakupongeza kwa maoni yako mazuri.

  It’s Great To Be Black=Blackmannen

 57. hussein Says:

  Huyu Mengi ana matatizo na wafanyabiashara wa hapa nchini na hasa wakiwa ni wakibila lingine mbali na wachaga. Kila wakati na magazeti yake yamekuwa yakiwaandama wafanyabiashara kwa kuwazulia na kuchochea, waelevu tumeishaangamu kuwa huo ni wivu unamsumbua Mengi hana lolote la maana kazi kuchonga kwa kutumia vyombo vyake vya habari na vibaraka wake. Akome asituletee za kuleta

 58. halima Says:

  Eve toa kichefuchefu hapa kama wewe huna uchungu na hizo pesa basi nyamaza sio unaongea pumba hapa au baba yako ndio mwenye hiyo kampuni?

  Hata kama wanamabif yao sisi haya tuhusu tunachotaka hapa ni mmliki wa kigoda ni nani? sio blablaaa hapa.

 59. Matty Original Says:

  ROSS tuma picha pls hahahahaha nyooooooo mwanaume anajisifu?get a life!

 60. innocent Says:

  huyu mzee ni waiana yake kwa kweli! anajitahidi sana kubeba matatizo ya watu kila siku kusaidia masikini naamini pia mungu anamuona! mzee mengi tunakupenda na tunakuombea! ivi kumbe nchi yetu pia ina ukabila? uchaga ndo tatizo kwa huyu mzee sio? kwakweli watanzania tunaelekea kubaya sana! lakini sishangai sababu hata mimi kuna watu wananichukiaga bila sababu! najua ni wivu tu! MZEE MENGI GOD BE WITH YOU

 61. Maty ORigino Says:

  mungu akubariki mzee mengi, tupo pamoja sana tu.

 62. Maty ORigino Says:

  wewe ni wa ukweli…hakuna kama wewe hapa bongo. wengi wanatumia utajiri wao kwa starehe na anasa zao lakini wewe unatusaidia wanyonge mungu akuzidishie

 63. Mattylda Says:

  Maty Original, # 63 and 64

  U better get a life, kinachokushinda kujitofautisha na mimi ni nini???ninaitwa Matty na ndo utambulisho wangu hapa, umekuja na wewe unajiita Matty, after all nimekuachia nikajiita Matty Original unarudi tena kunitafuta, sasa najiita Mattylda kama unalipenda na hilo pia chukua!

  watu wengine mkuwage sometimes, utoto tu,anyway ukikua utaacha!

 64. hombiz Says:

  Eve point # 54 ni pumba tu. You need to disappear in the darkness with the short minded people who support your nonsense.

 65. DOMINICK EMMANUEL Says:

  Inaniuma sana pale tu ninapoona Ufisadi unafanyika WAZIWAZI, NA WALA HAKUNA ANAYE CHUKULIWA HATUA ZA KURIDHISHA.
  sasa nakubali kuwa nchi hii ni ya mwenye PESA, Kweli imeshindikana kumchukulia hatua za kinidham aliye chota pesa hizo zote? inamaana wakati pesa hizo zinatolewa aliye zitoa kwenda kwenye kampuni hiyo hamfahamu alikuwa nani anazipokea, kama anamfaham je ilikuwaje hamtaji, hatakama ni .. bado anafaa kuchukuliwa hatua za kinidham.tunashindwa kusema majina hayo kwani ukusema tu, kesho unajikuta matatani,
  ufisadi hauta isha kamwe hadi wote wanao fanya maovu hayo wachukuliwe hatua kali za kisheria,ndo nawatakao kalia viti hivyo watakalia kwa nidham.

 66. DOMINGO EMMANUEL Says:

  kuna watu wanajifanfa kumbelembele eti hawana na fedha za EPPA.hao ndo wajinga. unadhani nchi za wenzetu kama kule walipo mvalia njuga kiongozi mpaka atoke madarakani, na wakaamua kupiga kambi kwenye kiwanja cha ndege, unadhani wale ni viongozi, wale ni wananchi kama wewe na Mengi, Mengi ni sauti ya wanyonge, kamahujui angaza kwenye magazeti yake. ndo yanayo oongoza kwa kuwasema mafisadi, inaonyesha wewe unayepinga Basi roho ya ufisadi unayo,TEMA MATE.Mzee sema, wapingao wapinge lakini endelea, kwani Hata baba wa taifa aliwasemaga Hakuna upemba wala uzanzibar na ubara, sote ni wamoja, Isitoshe apingae huyo kama ni wakati wa ukoloni bado angeendelea kutawaliwa, tulipata haki zetu baada ya baba wa taifa kulivalia njuga, HIVI HAO WACHACHE WANAO TUMIA NAFASI ZAO KUJICHUKULIA FEDHA KILAINI, HAWAMWONI BABA WA TAIFA HAKUYAFANYA HAYO? KAMA ANGETAKA NANI ANGEMZUIA? EMBU ACHENI TAMAA. INAUMA SANA LAKINI SINA UWEZO.ILA KWAKUWA SHERIA YA TANZANIA INANIPA UHURU WA KUSEMA BASI NITASEMA.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s