BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

YONA NA MRAMBA KIZIMBANI! November, 25, 2008

Filed under: Breaking News,Developing News,Serikali/Uongozi — bongocelebrity @ 8:11 AM

yona-na-mrambabc

Mawaziri wa zamani (wote wamewahi kuwa mawaziri wa Fedha), Mheshimiwa Daniel Aggrey Ndhira Yona(pichani kushoto) na Mheshimiwa Basil Pesambili Mramba(pichani kulia) leo hii wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi ya Kisutu jijini Dar-es-salaam wakikabiliwa na mashtaka 13 ikiwa ni pamoja na kutumia vibaya madaraka yao walipokuwa mawaziri, kuingia mikataba tata ya madini nk

Pichani ni waheshimiwa hao muda mfupi baada ya kusomewa mashtaka yao.Wote wamewekewa masharti ya dhamana kwamba kila mmoja atoe fedha taslimu bilioni 3.9,wasalimishe hati zao za kusafiria,wasitoke nje ya Dar-es-salaam na kila mmoja wao awe na wadhamini wawili ambao mahakama itaridhika nao kuwa ni wa kuaminika.

basil-yona

“Pana joto sana hapa au”?

yona

Masharti ya dhamana magumu,siyawezi.

Picha kwa hisani ya Bongo PixAdvertisements
 

81 Responses to “YONA NA MRAMBA KIZIMBANI!”

 1. mr degree Says:

  huyo mchaga mramba ni kweli kabisa alikua anatumia madaraka yake vibaya.kajaza ndugu zake tuu pale benki kuu na taasisi zote alizowahi kufanya kazi! sheria ichukue mkondo wake kwake na wachaga wote wanaodhani binadamu ni wachaga tuu hapa duniani

 2. linga Says:

  mungu atutangulie kwa mambo haya,atusimamie kwa kweli,otherwise! ———–.

 3. Shankazulu Says:

  Imefika wakati sheria isibague matabaka ya watu sheria msumeno…;nadhani hii iwe mwanzo tu ..bado kuna wengi tu ambao wamelihujumu taifa hili na hawajachukuliwa hatua zozote ;inasikitisha sana.

 4. tgirl86 Says:

  Heeeeee!! mungu tuoneshe ukweli sisi watazania tusiokuwa na hatia kwa kufichua watu woooooooote wanaoturudisha nyuma kimaendeleo sasa kazi imeanza mpaka baba zetu pia watajwe kama wamo pleaseeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!.

 5. Matty Says:

  thats wat we want,mramba pls mention ur fellow ebooooooooooo ila sasa utashangaa watakavyotoa dhamana haraka utadhani wanamigodi ya accounts lol!
  Natamani wanyongwe tu kama sadam hussein!

 6. Frateline Says:

  Hi Guys kutoka Helsinki

  Kwa kweli ninapenda kuanza kwa kumpongeza JK na Pinda angalau mwanzo mzuri, pili ninapenda kuwapongeza watanzania wote hasa hasa makundi yafuatayo, walimu, wafanyakazi, wanafunzi na madaktari kwa migomo na maandamano maana nguvu ya wengi ni sauti ya mungu, bila kufanya hivi sisi wanahistoria tunaamini huu ndiyo ulikuwa mwanzo wa CCM kuanguka maana hasira ya wananchi ni kali kuliko jeshi lolote lile dunia, kama jeshi linanguvu mmarekani hasingechemsha Iraq lakini sauti ya UMMA ni kali kuliko sauti ya watawala.

  Baada ya pongezi- ninawarudia mafisadi, wametuuza hawa, madini hatupati kitu, yaani tunapata asilimia tatu 3% rayalties, hii ni mikataba iliyoingiwa na wale machifu wa zamani-magungo wa mzovero- , Yona na Mramba ni wezi na wakabila wa hali ya juu,

  wasiishie kupeleka mahakamani kama danganya dototo, Kikwete futa mikataba yote ya wizi- ili uweze kupata pesa za wanafunzi vyuo vikuu kusoma.

  Frateline

 7. Mh LUKAMBA Says:

  AZabu yao inatakiwa iwe KIFOOOOOOO
  UA maharmia hawa !!!
  Hawa walimilikishwa leseni za Wizi chuo kikuu mlimani !!
  sijui kama takukuru kama wanajua hotel zako 2 za kifahari Arusha?
  kibo palece na crown crane(mpya)
  na we mramba na Ngurdoto hotel !!!
  uko segerea mnatakiwa MFI #####we mpka mkija amuwezi kukaa.

 8. Oxalato Says:

  pua za watu wote zinaangalia chini,ikimaanisha chini tutarudi……..sasa yamefichuka

 9. Oxalato Says:

  “IKIBIDI HATA KULA MAJANI TULE ILA NDEGE YA RAISI LAZIMA INUNULIWE”…..by Basir Pesambili Mramba 9alipokuwa waziri wa fedha wakati wa mchakato wa kununua ndege ya raisi)……

 10. halima Says:

  wewe degedege hebu acha mambo ya ukabila hapa. ovyooooooo

 11. MLIO PIGA KELELE SASA NYAMAZENI TUMUACHE KIKWETE AONGOZE SHERIA KWA MIFAAANO HAI
  KILA LA KHERI

  JAKAYA MRISHO KIKWETE..

 12. eve Says:

  HAHAHAHAHAHAHAHAAAAAAAAAAAAA ENDELEENI KUSHABIKIA WADAU KAMA KAWA HABARI NDO HIYO!!!!!!!!!!!!!!!!! HADI MCHAGA MWENZANGU HUREEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!

 13. Mama wa Kichagga Says:

  Mr Madegree,

  Wewe ni msafi sana na huna dhambi yoyote? Mshukuru Mungu kwa kukufanya ulivyo na wasaidie wengine kuwa wasafi kama wewe. Hapo umeuona mchagga tuu na mwenzie hujamuona?

  Tuacheni chuki binafsi jamani na tuiache sheria ichukue mkondo wake. Tuhukumiane kwa makosa na sio kikabila au kidini!

  Kwenye orodha ya watoto wa vigogo bot uligundua wachagga wangapi? Mbona hukunguruma?

  Shame on you kwa kujibadilishabadilisha majina na kueneza chuki mitandaoni!

  Ukabila hautakufikisha popote ndugu yangu na kumbuka daima mwenye chuki hawafanikiwi ktk maisha.

  SIDHANI NI SAHIHI KUHUKUMU KABILA ZIMA AU DINI KWA KOSA NA MTU AU KIKUNDI CHA WATU! You are very wrong before God and man.

  Hebu jiulize tuanze kuwahukumu wasukuma eti kisa bwana vijisenti alituuzi au wachagga kisa eti Mramba hakutumia madaraka yake vema, au Wapare kisa Yona naye kama Mramba, wamakonde, wahehe, wahindi nk nk mwisho wake makabila yote yatakuwa ndani ya hukumu na halafu nini tunatengeneza kama sio VITA!

  Nawasihi watu wenye mtizamokama wako mkae chini mfikirie kabla hamjaanza kueneza chuki zenu zisizo na msingi wowote! Tuiachie sheria na mahakama zichukue mkondo wake na kama haki itatendeka basi huo msumeno ukate kote!

 14. hombiz Says:

  Now we can talk! Wahenga walisema:
  -ukitaka kumuua nyani usimtazame usoni (vita dhidi ya ufisadi isiogope sura za watu, mali ama vyeo vyao na hata kujuana)
  -“usipoziba ufa, utajenga ukuta” (MAFISADI wakichekewa, wataathili ustawi wa Tanzania na jamii yake)
  -bandu bandu, humaliza gogo! (Mafisadi wasiponyooshwa, watazidi kulifilisi taifa letu changa kwa tamaa zao binafsi)
  -mtaka mbili, moja humponyoka (unapepewa dhamana ya madaraka au uongozi, tafadhali heshimu kazi yako kama hayati Sokoine)
  -asiyefunzwa na mamaye, hufunzwa na ulimwengu (viongozi ambao wameshindwa kuheshimu madaraka waliyopewa na kulihujumu taifa, inafaa wachukuliwe hatua kali za kisheria ili wengine wenye nia kama yao wayajue madhara ya uongozi mbovu (rushwa na UFISADI)
  I’m kinda busy right now, but I will be back. However, I am a little bit pleased with how this issue progress! Moreover, I was happy to hear that President Kikwete reversed his statement that those who returned EPA money won’t be prosecuted. Neither who returned nor those who kept the EPA money, will be let free! That’s great! Don’t let them fisadiz bounce!

 15. binti-mzuri Says:

  mmh kikwete sasa naona jitihada zako…am proud of whats going on now,maana naona kweli sheria ni msumeno! please let the fisadis go to jail and repent their sins

 16. Mama wa Kichagga Says:

  Ngoja Sasa nichangie hoja:

  Hii ni hatua muhimu sana kwa taifa letu. Italeta maana sana kama wale wote waliotuhumiwa ktk sakata la EPA na ubathirifu mwingineo wowote wa Serikali kama kaka yangu hapa na mtani wangu wakachukuliwa hatua za kisheria.

  Mh. Rais wangu mzuri nakupongeza kwa hatua hii yenye changomoto kubwa kwa taifa hili kupita kipindi chochote ktk historia ya maendeleo yetu.

  Mh. Rais, mchakato uliouanzisha ni muhimu sana ktk nchi yetu kwa wakati huu na kipindi hiki mathalani. Mchakato huu ukitekelezwa kwa haki na kwa ufanisi ndio mwanzo wa kuiinua nchi yetu kimaadili na kimaendele. Aidha, kama mchakato huu hautafuata haki na maadili naamini taifa litakuwa limeengia katika hatua mbaya kimaadili na hati kiamani.

  Busara itumike na kila aliyehusika kulihujumu taifa hili na achukuliwe hatua za kisheria akiwa ni pamoja na kufilisiwa mali walizojilimbikizia ili wengine nao waige mfano.

  Mh. nakuomba sana usikilize sauti ya Mungu moyoni mwako ya kutenda haki na zoezi hili lianzia juu hadi chini maana uozo umeenea na mizizi yake ni mikubwa sana. Aliyoyafanya Mramba au Yona yanafanywa na KK, Mkuu wa mkoa, Mkuu wa Wilaya hadi mjumbe wa nyumba kumi kumi hadi ngazi ya familia.

  Kwa kifupi, Watz tunahitaji mabadiliko makubwa sana ya kiroho, kifikra, uwajibikaji na kiutendaji.

  Wakati unatekeleza zoezi hili pia usiwasahau wafanyabiashara wakubwa wanaolinyonya taifa hili uchumi wao ukianzia na biashara ya mafuta ya petroli na wengine. Hainingii akilini nchi zilizoendelea wanunue lita moja ya petroli kwa sh. 600 hadi 750 kwa wastani halafu taifa maskini kama letu tununule lita hiyo hiyo kwa sh. 1500 – 3000/= (hii ya juu nenda Loliondo). Naamini sekta ya petroli ni mbaya kuliko EPA maana hii inamgusa kila raia na ni sekta endelevu. Yumkini aliyeiua TPDC hana budi naye kuionja mahakama maana uamuzi wake umelikosesha taifa maendeleo makubwa kwa zaidi ya miaka 20 sasa!

  We need big changes and this is the right time for that changes. AND ONLY THE TRUTH WILL SET US FREE.

  I STRONGLY BELIEVE MY CCM WILL BRING IT.

 17. mafungua Says:

  sasa natambua kuwa TAKUKURU ipo. kabla ya leo nilidhani TAKUKURU ni MSAMIATI tu. Basili na Yona wametafanua na kudhihirisha kuwa sio msamiati ila ni chombo kinachofanya kazi dhidi ya rushwaaaaaaaaaa.

 18. Babukadja Says:

  Kuna bwana mmoja aliwahi kuulizwa, “Hivi inawezekanaje wewe uwe spika halafu hapohapo uwe mwenyekiti wa bodi ya kampuni fulani ya simu za mkononi?” bwana akajibu, “Acheni wivu wa kike…” Hivi alikuwa nani tena?

  Majibu kama haya ndiyo yanawafikisha watu kama hawa sehemu hizi. Madaraka kitu kibaya sana, unajusahau kabisa kwamba siku moja utashuka.

  Hawa watu waadhibiwe sana tu lakini sio kuwapa adhabu ya kifo, adhabu ya kifo ni ya kinyama na ni uuaji uliohalalishwa.

  Naomba kuwasilisha!

 19. Majita Says:

  Mr.degree ya chekechea,
  Nimependa maoni yako kuwa Mramba ni Mchaga.

  Mmhh sasa naanza kupata shida ya kusoma maoni yako

 20. ROss Says:

  Nilisema Mengi sio Obama na wachagga hawawezi sema “Yes we Can” kwa Tanzania ya sasa , mkaniona ni mbaguzi , haya sasa watu wanaanza ooh “Mramba kaweka ndugu zake” , ooh “BOT kumejaa wachagga” , haya hapo sasa Mama wa KIchaga

 21. usinijue1 Says:

  isiwe kimasomaso cha ccm then jamaa wakashinda kesi zote 12wabongo tufungue macho hawa jamaa ni wahalifu na lazima wafungwe tusijesikia wameshinda kesi kimtindomtindo tu……..haya yangu macho

 22. Fukara Says:

  Yametimia,
  wanamereeeeeeeemetaaaaaaaaaa…..
  wanameremeta…,
  mafisadi wanameremeta……..
  wanameremeta

 23. Renee Says:

  Labda ya kusweat kidogo watafikiria kurenovate hiyo mahakama.
  Ama kweli hujafa hujaumbika! …Where is BWM?!

 24. freedom Says:

  jamani kama mnakumbuka huyu mramba halikisha nunua pantoni la jano yani tishari lililo kuwa likivushia vifaa vya kivita vitata kuu ya pili ya dunia likipigwa rangi likaja bongo wikimbili lote linakutu na kufanya kazi halifanyi nyerere hakamwamisha wizara na walikuwa wamedai ni jipya

 25. BLACKMANNEN Says:

  WanaBC wenzangu!

  Kwa kipindi kirefu, kila tulipokuwa tukiongelea maswala ya MAFISADI, nimekuwa nikiwaambia kuwa, Mh. Rais Kikwete ni mtu makini sana na anajua akifanyacho katika kazi yake. Tuvute subira, mengi tutayaona katika safari hii, ndefu na ngumu ya kupambana na Mafisadi na wanaokula Rushwa.

  Wakati kikundi cha kwanza cha Mafisadi kilipopandishwa kizimbani, watu wasioitakia mema Tanzania walibeza kwa kusema kuwa huo ulikuwa ni usanii. Watu wadogo kukamatwa na wakubwa kuachwa. Katika kuwaona leo, Mawaziri Basiri Mramba na Daniel Yona wakipandishwa kwa “Pilato”, wapinzani na wale wanaoichukia Tanzania na viongozi wake sijui sasa, watasemaje?

  Katika nchi zote, zenye kufuata Utawala wa Sheria, Tanzania chini ya Utawala wa Rais Kikwete ikiwemo. Viongozi wake hawakurupuki kuyashughulikia maswala nyeti kama haya ya wezi wajanja wa EPA na wala Rushwa. Umakini wa hali ya juu unahitajika, ili kuwapata wahusika wote.

  Vile vile namna ya kutayarisha mashitaka ya wahalifu hao, ni tofauti. Pia tofauti ukilinganisha na watu wengine walivyokuwa wakifikiria. Hii yote ni kuhakikisha kuwa washitakiwa wasipate mianya ya kujinasua katika sakata zima, linalowasubiri mbele.

  Kitu kinachofanya shughuli hii MAFISADI kwenda taratibu ni unyeti wa sakata na wahusika kutiwa hatiani kila mtu kutokana na sehemu yake inayomhusu. Pole pole ndiyo mwendo, tutafika tu. Nawaomba wale watanzania wasioipenda Tanzania yetu, watuachie sisi watanzania tuipendao! Waache chuki zao.

  It’s Great To Be Black……………………..Blackmannen

 26. hilly Says:

  nyie mbona mna mpa rais wakati mgumu sana lakini…,jamani hata mambo ya epa hayajaisha nanyi mshajitokeza …!

 27. pound Says:

  holiday season kwa magazeti sasa! alafu kuna watu wananichefua kwa ukabila humu ndani…….. SAY NO TO TRIBALISM IT IS A DEVIL THAN THE WAY U THINK THOUGH IT IS SIMPLE 2 SAY…. ALWAYS SAY AM TANZANIAN, FIRST.

 28. Betty George Says:

  Kwa kufupi inafurahisha na kutia moyo sana kuona hata vingunge navyo waingia lupango. Hii itakuwa fundisho kubwa kwa watu wanaopenda kujirimbikizia mali za serikali nakuwaacha walengwa wa hizo pesa wakiumia hata wengine kupoteza maisha kwa sababu ya watu binafsi wanaojijali wenyewe na familia zao. Itakuwa fundisho kweli kweli kama serikari itawahukumu na wakaanga ndani kwa muda mrefu. Imefika wakati wa kuwacha wadogo wasio na vyeo wao pekee kufungwa na kuwatetea mafisadi. Asante sana kwa juhudi zenu andeleeni kujenga Taifa letu lilinaboboka kwa miaka mingi. Mtanzania USA

 29. mr degree Says:

  apelekewe majani huko segerea ale!

 30. ThinkBig Says:

  Huu ni mwanzo mzuri but ningependa kuwaona yule nguli wao(mkuu wa awam ya tatu) pamoja na huyo pia tunawataka wale waliochukua pesa kwa maslahi ya chama nao wapandishwe kizimbani….

  Mambo ya ukabila tusiyalete kwenye hii ishu coz kwenye hizi ishu za EPA,Richmond,Madini wapo watu wa makibila mbalimbali.

 31. Pearl Says:

  kwani LOWASA yuko wapi mbona simuoni hapo!!!!???? au shida ni nini mbona ye hakamatwi!!!???

 32. kevin Says:

  nasikiaaa rahaaaaaa!utamu…poa mzeiya mramba haina kwereee tutakula majani tu..sasa mzeiya imefika zamu yako na wewe ya kula ugali maharage na kusahau mazagamazaga mapiza mabaga..ah!nipeni dili masela..ah!niwamwage hawa maboya jela..it z wat t z…cpati picha waliobaki mapigo yao ya moyo yanavyo pa pa pa pa..kama ni upande wa magari basi ni vog,, na kama ni mnyama basi ni cheetah..kipara eh jiandae hii ni wiki ya vigogo.

 33. Aunt D Says:

  Jamani lol mnichekesha mnavyosema etii JK kafanya kazi….hahaha changa la macho ilooo.
  Naomba niwaambie hivi kelele zetu watanzania ndio zimetusaidia kufichua hayo mambo…hebu tunyamaze muone kama hatujauzwa!!!!!!!
  Hv jamni hilo pozi la mramba mbona kama mama mjamzito kwenye benchi la kiliniki
  Tunalo wa-TZ
  Mramba baba kalee na wewe maharagwe yenye wadudu kidogo kama sisi tulivyokuwa tunakula majani kipindi kileee….unakumbuka?usijidai umepoteza memory
  Hata kama hutachukuliwa hatua atleast umeaibika japo kidogo
  Yona alizoea AC ofisini hahahhaha hizo ndio mahakama zetu bado huko keko sijui mara segerea mkakutane na mbu
  R.I.P (Rest In Prison) waheshimiwa

 34. any Says:

  Mr degree, Its very unprofessional to judge someone based on his gender, race, and or his origin. Its sad to see people generalizing sh.it like this.Mchaga anaeiba ahukumiwe kama individual, na sio kwa vile katokea Moshi!
  ivi makabila mengine hakunaga wezi kabisa nini? nahisi wote mnalala milango wazi kisa hakuna mchaga sehemu hiyo! haaaaaaaaaaaaaa! nicheke mie, Pole bro Mramba kama hujaiba, ila kama umeiba, shauri yako, watakuvizia segerea, shauriyo.

 35. Matty Original Says:

  Jamani kumbe Matty tuko wengi eee??am sorry matty # 7 unaonaje ukitofautisha kidogo jina?in order 2 avoid any enconvenience? if not possible basi mimi nishabadilisha kama unavyoona hapo juu!

 36. Saligwa Says:

  Yaani kwa utaratibu huu, maisha bora kwa kila Mtanzania yatawezekana; kwani hata sheria ikitumiwa na kufuatwa vizuri ndiyo maisha mazuri aliyokuwa akimaanisha rais wetu. Baada ya rumande ifuate kutaifishwa mali zao. Heko Mwankenja

 37. Saligwa Says:

  Mramba Majani uliyokuwa ukiyasema wananchi wale; nadhani radha yake utaiona ukiwa keko.

 38. salma Says:

  halima mchaga ninimbona imekuuma!!!!!!!!

 39. Mayu Says:

  Utafanya yote duniani, utajishebedua na kujiona mjanja lakini ipo siku moja na yupo mmoja tu Mungu atakuumbua. Ndo hayo wa bwana mrambaji hatimae naye karamwa

 40. Mummy Says:

  Mi naona adhabu nzuri kabisa kwa hao mafisadi viwembe ni kufilisiwa wao na familia zao zote kwani wengi wao wameandikisha mali kwa majina ya watoto wao na ndugu zao ili hata wakifilisiwa wasiishiwe kabisa. Sasa wawafilisi hadi (block B) zao (nyumba ndogo) kwani wakianza kutembea na ndala ndo watakapoona uchungu wa kula pesa ya mvuja jasho!!!

 41. Mummy Says:

  Matty kama mtu anachukua jina lako adhabu nzuri ni kumuachia na wewe kuanzisha jina jingine ni kama wanaume wakware wenye kupenda kuchukua wake za watu, basi ukimnyaka tu na mkeo adhabu yake unamuachia huyo mke. Unadhani atakuwa anamtaka tena?!?!?!?!?!? Semeni wanaume

 42. Frateline Says:

  Hi guys kutoka Helsinki

  Mimi nimefarijika na hatua hiyo kwa sababu hao ni watu wamekuwa madarakani kwa muda mrefu, Mramba amekuwa waziri karibu serikali zote, pia Yona amekuwa waziri serikali mbili, Kwanza kitendo cha hawa mawaziri kushitakiwa ni tishio kubwa kwa mawaziri waliopo madarakani, pia hawa ndiyo tumwewazika kisiasa hata watoto wao hawawezi kupitia mgongo wao kuchukua madaraka kirahisi na hii ni hatua nzuri kisiasa.

  Kwa sasa tunaongeza idadi ya wafu wa kisiasa
  1. Lowasa-politically dead-
  2. Mramba -politically dead
  3. Yona- politically dead

  Ukweli wa mambo hata kama watatumia pesa kutoka kifungoni hawa watu majina yao kwisha kazi ktk siasa za Bongo, Kwa kweli ninavipongeza vyombo vya habari wanastahili pongezi kwa kazi nzuri ya kupambana na mafisadi

  Mwisho, dhambi ya ufisadi na sifa ya ufisadi ni mbaya kama vile sifa ya uchawi maana haitoki miongoni mwa umma, lakini kibaya zaidi dhambi hii inatabia ya kuchafua ukoo na familia nzima wakati mwingine kabila zima la mlengwa- sasa hivi wachagga hili mnalo na hivi kuna watu wanadhani wachagga walio wengi ni wezi ingawa mimi binafsi siamini hivyo, ninao marafiki zangu wengi wachagga ambao ni watu safi kuliko hata mimi mwenyewe.

 43. Frateline Says:

  Hi guys kutoka Halsinki

  Mramba, Yona na Lowasa hii dhambi ya ufisadi itawatafuna mpaka ktk familia zetu, ukoo na hata wakati mwingine kabila,kwa mfano nakumbuka kabla ya kashifa mtoto au watoto wa hawa waheshimiwa walikuwa wanatesa sana na maisha ya kifahari na magari ya kifahari, sasa kila wakifanya jambo jamii itawaona ni wezi tu, hata kama watapata vitu kwa jasho lao , tatizo hii dhambi ina tabia ya kutafuna mtu mpaka anaingia kaburini na hivyo hawezi tena kupata maisha ya kisiasa.

  Aruta kontinua…. mapambano bado yanaendelea,

 44. Oxalato Says:

  TAFaKARI;kama Mramba na Yona wameshitakiwa,na moja ya tUhuma zao ni kutumia mamalaka waliyopewa vibaya na kuisababishia nchi hasara……sasa vipi kuhusu Lowasa,Karamagi na Msabaha nao si walitumia madaraka yao vibaya kwenye mikataba ya RICHMOND na MADINI?…….TAFAKARIII

 45. chezasalama Says:

  we mama wa kichaga hata kama we ni mchaga huwa hatung’aki hivyo mtu wangu. Mbona hata mie mchaga lakini niko poa na sijaona baya alosema Mr mdegree.Ni kweli ukienda pale BOT na benkind institution nyingi hapa bongo ni sisi wachaga na ukiangalia sana wengi sana tuliingia humu kipindi cha Mramba,so hapo Mdegree anavyosema huenda akawa anadata au anatania tuuuuu, si unajua tena si watanzania tumeshazoea mambo ya matani mtu wangu.

  pole sana mama wa kichaga na Halima japo nahisi halima sio mchaga ila ni mwana harakati anayepinga issue za ukabila tz au sio mtu wangu.

  Wachaga,wapare,wasukuma,wahehe,wamachinga………….. wote ni kitu kimoja ndugu zangu.haya ni makosa yanayo weza kumpata mtu yeyote au sio???

 46. ISMA KABENGO Says:

  MIMI USHAURI MAONI YANGU NI KUWA NAONA RAIS ANATUMIA MADARAKA VIBAYA KUINGILIA VYOMBO VYA SHERIA ,UKWELI UNABAKI PALE PALE HAWA NI WATUHUMIWA TU WANABLOG NAWAHAKIKISHIA HAWA WATAKUWA HURU MBONA HATUONI ROSTAM AZIZI,MANJI,NK KIKWETE UKWELI NCHI IMEMSHINDA MIGOMO,UMASIKINI BADALA YA KUPUNGUA UNAONGEZEKA HALI YA MAISHA NI MBAYA SANA HIVYO NAOMBA MSIWAHUKUMU HAWA HAWA JAMAA WAKATI HAWAJAPATIKANA NA HATIA MAANA NAONA MNAWASHAMBULIA TU.TANZANIA INABIDI IJE ITAWALIWE NA WATU WENYE UCHUNGU WA NCHI KAMA IDI AMINI,ALIIPENDA SANA NCHI YAKE UKIFANYA FYOKO UMEIBA HUNA MAISHA NDIYO INATAKIWA

 47. Chris Says:

  Watanzania tuu short-sighted sana! Na viongozi wetu wanajua hayo. Hili ni changa la macho tu.

  Those guys, Mramba, Yona, Meghji etc are ticking-bombs. Hakuna hatua zozote zinazoweza chukulia against those figures. That chain involves Mkapa na huyo Vasco Da Gama wenu, unafikiri na wao watapelekwa mahakamani?

  Naona kama wanataka jenga chama chao kuelekea 2010. Japo wameshashindwa kukijenga kwa baadae. Kikwete atarudi japo kwa shida sasa baadae kazi ipo hapo.

  I don’t believe in these dirty politics za huyo Kikwete wenu.

 48. binti-mzuri Says:

  Mramba bwana izo pesa kazichuchumua,mtu ana mihoteli kibao..the man makes millions..mramba kuwa na aibu,huoni credit crunch hii watu wanakufa na njaa,wanao wanatesa na ma bima. PLEASE GO TO JAIL AND REPENT YOUR SINS. mi nakushikia bango mzee wewe usie kua na soni,nyoo!,limekushuka shuu mbele ya hakimu!

  jamani hili sio changa la macho,si hao wapo kwa pilato hapo, bdae wameenda segerea kula nyasi aka hamburger za mramba..ujue wakiachiwa hivi hivi,wananchi nao watachachamaa,plus i think JK needs our votes 2010 inakuja,so he wouldnt mess up..this world of today,where even people wamemrushia mawe.anaogopa kubugi stepu mzee mzima..bongo people sio wajinga anymore

 49. minor Says:

  ni vijimambo tu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
  Ndiyo mzeeeeeeeeeeeeeeeeeee

 50. eve Says:

  JAMANI JAMBO MSILOLIJUA MSISHABIKIE ACHENI SHERIA ICHUKUE MKONDO TENA NAANDIKA KWA HERUFI KUBWA NA NIMEKOSA BOLD JAMANI HII TABIA YA KUKASHIFU KABILA LA MTU MMETOA WAPI HATA KAMA KATOKA UCHAGANI LAKINI ISIWE SABABU YA KUKASHIFU KABILA LA MTU HII INALETA CHUKI BAINA YA MAKABILA HAKUNA SEHEMU ISIYOKUWA NA KIBAKA HUMU DUNIANI WADAU MNAOTOA MAONI NAWAOMBENI ACHENI HIYO TABIA UTASHANGAA SIKU UNAISHI NA JAMBAZI NDIPO UTAKKAPOJICHEKI HALAFU MANENO MACHAFU JAMANI SI MAZURI NIMEKERWA SANA NA HII SENTENSI HIv jamni hilo pozi la mramba mbona kama mama mjamzito kwenye benchi la kiliniki SIYO VIZURI AUNT D TENA UNAJIITA AUNT HATA KAMA WAMEIBA MKISHADADIA KWA MANENO MNALIPWA NINI WENZENU WASHAJICHANA MTABAKI PIGA KELELE TU HAMJUI MTAPOTEZWA MABOYA BADALA TAIFA LIFIKIRIE VITU VYA MAANA NA MAENDELEO LINASTRUGGLE KUCHOTA MAJI YALIYOMWAGIKA NA WAKATI NA WAKATI WALIOPO MADARAKANI WANAENDELEA NA UFISADI

 51. Mambo Says:

  Asante mungu

 52. any Says:

  NA NYIE KWELI MNAAMINI WATALALA SEGEREA? HIYO NI KIINI MACHO JIONI WANARUDI HOME KULALA KWENYE MANSION ZAO, WHERE IS UR BRAIN NYIE WADANGANYIKA?

 53. Gervas Says:

  Mmmh..mimi leo sioshi kinywa, huwa pia ni burudani tosha kusoma wadau wanavocheza na maneno ya kiswahili. Sasa Matty original na Matty bandia ni yupi? ebu wekeni labda picha tujue kabisa!!

 54. kiki Says:

  mimi nina usongo na ROSTAM…..BADO ROSTAM,WAJAMENI

 55. Gervas Says:

  Chris, Any,.. na wengine woote mnaotilia mashaka kitendo hiki…..lets give the fela time as we approach election, hata Zombe, Dito wakati wanapelekwa selo watu walisema hivi hivi kuwa watatoka tu jioni. Najua Jk anaelewa moto wa ufisadi utakavomuumbua sio kwa wananchi, wapinzani, bali hata ndani ya ccm yenyewe ambamo makundi hasa hasa ya wabunge hayakubali tena mchanga wa macho. JK anajua kabisa kwa sasa kuwa “people needs change” otherwise hataweza kuiona ccm inameguka even before the coming uchaguzi.

 56. Gervas Says:

  Eve…nani huyo anatuchesea sisi wachagga? basi tumsameheni tu maana halijui lile alitendalo, yaani hajui kama tokea uhuru sisi ndo tumejenga inchi hii!!??

 57. XXX Says:

  PAY BACK TIME IDIOTS! may u ROT IN jaiL!

 58. hombiz Says:

  Vyombo vya habari watanzania wenzangu wenye kupenda maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla. Tuzidi kushikia bango swala hili mpaka UFISADI, RUSHWA na maovu mengine, vitokomezwe ndani ya nchi yetu hadi kila muongoza na muongozwa aishi kwa kufuata maadili ya nchi yetu-yanayotakiwa. Chanda chema huonekana asubuhi! Changa la macho halipewi nafasi hapa! Ukabila lazima upigwe vita Tanzania na Afrika nzima kwa ujumla. Madhara yake Tunayaona toka Congo, Burundi, Rwanda, na kwingineko.
  Stay up!

 59. hombiz Says:

  Mwanakijiji ana report kuwa kagoda ni ya Rostam na wenzake. Mwana BC Blog ambaye angependa kupata taarifa hizi anaweza kuingia hapa ili kupata maelezo kiduchu
  http://www.forums.mwanakijiji.com/showthread.php?s=327296c9681b2ed8a4e569d8f0e9505f&t=140

 60. janbar Says:

  # u’r absolutely right. hizo dirty polytics za kikwete kujipigia cross kwa 2010 akidhani wabongo wa leo ni sawa na wale wa 60’s. watu wana access na facts. na ole wko uwasamehe kimtindomtindo kama ulivyo fanya kwa lowassa na nduguze akina sumaye.
  thanks

 61. name Says:

  any wewe ni mzungu? kuwaita wenzio wadanganyika,kwani na wewe ni mkenya?eve kwani wewe mtoto wa fisadi na bint mzuri hili ni shanga la macho,au umekujaa machoni sasa huoni. rostam azizi mbunge wa igunga,edward lowasa, mkapa, karamagi, meghji,mengi na hata wewe mwenyewe JK ufungwe! hili shanga la macho! WOTE WAFUNGWE! JK hili ni shanga la macho kwani edward lowasa ana sakata la richmonduli lakini mpaka sasa hajashitakiwa. tunajua ya kwamba mnajuana tokea muna miaka 16 na mmesoma wote hadi vyuo vikuu,SHANGA LA MACHO HILI

 62. Matty Original Says:

  Mummy,ni kweli nimeona nimuachie hilo jina la Matty then mimi nianze upya!

  Gervas, Matty original a.k.a nshomile ni mimi uliyezoea kuniona hapa tangu enzi zile >>>>> na huyo matty # 7 simjui so jamani nimeamua kujitofautisha na yeye!

 63. Maty ORigino Says:

  Poleni ndug zangu, ila wewe unaejiita matty origino umeiba jina langu nimekua nikikuangalia tu cku nyingi.

  Kama vp niteme basi sawa….?

  Maty Original

 64. kevin Says:

  yaheeeeee,,muosha huoshwa,,,,anayetakia wenzake kula majani je yakikauka!!!!basi tutamla yeye maana ana boga,,eeh kiboga..serikali ya msimu huu ni noma….jana waziri leo muuza nyanya…jana kupumulia ac leo joto kali….jana akili nzuri za kuvaa viatu leo waomba malapa tena ya sh.500….jana unatamani leo watamaniwa…

 65. kevin Says:

  ah ah siwezi!!! aha ah siwezi…….kikwete ametisha ametisha…ah ah siwezi

 66. kekue Says:

  Hii bado haitoshi sio muwaweke hapo kizimbani then wawekewe dhamana ndo kwa heri manake Mh!!!!!!!!!!!!!

  Sasa wewe unayesema wachaga wachaga…. hao wachaga walikufanya nini? Jitu, Manji, Chenge, Lowasa hao nao ni wachaga au ndo usemi wa kunya anye kuku akinya bata kaharisha…………… tuwe na ufikirio wenye manufaa kdg.

 67. Mattylda Says:

  Matty Original #64 sijakuelewa unashout as if una hasira na mimi why madam??

  Jamani JEFF pls nisamehe niteme cheche kidogo!

  Tangu nianze kuingia BC utambulisho wangu ni Matty the short of Mattylda, nashangaa leo wewe matty unayesema nimekuibia jina lako how?anyway tulipewa majina sare sare kila mmoja na mzazi wake na kwa wakati wake so pls nimekuachia jiite uwezavyo am not arguing with a fool!

  WADAU, MASHOSTI,KAKA ZANGUNI,DADA ZANGUNI KWA SASA NITACHANGIA HAPA BC KAMA MATTYLDA!

 68. fatma Says:

  Hawa binadamu hawafai kuitwa waheshimiwa, na kama bado ni wabunge ni bora washauriwe wajiuzulu tu, aibu kubwa hii.

 69. hombiz Says:

  Kwa mujibu wa gazeti la nipashe, 11/27/2008, DPP anadaiwa kumkingia kifua Nazir Karamagi. Mwana BC ambaye hajasoma juu ya hili, anaweza kukongoli hapa http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2008/11/27/127197.html

 70. hombiz Says:

  Waandishi wa habari Mashaka Mgeta (Dar), na Thomas Mwanakatwe(Mbeya) wana-report juu ya habari yenye kichwa cha habari kisemacho ” JK amabebeshwa mzigo wa Mkapa-Lipumba” Mwana BC hajaipata hii habari, anaweza kujongea hapa http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2008/11/27/127196.html

 71. Dinah Says:

  Acheni ukabila, hao jamaa wameiba kutokana na roho zao za mbaya za kibinafsi na sio kwa vile ni Wachaga.

  ****Hivi ile sheria ya kuhukumiwa kifo bado tunayoTanzania?

 72. kiki Says:

  BADO BAZAZI ROSTAM ,LAZMA TUSHIKE BANGO MPAKA PONJOLI APANDE KIZIMBANI

 73. JOHN C Says:

  Mambo vp ndg zangu!unajua huyu kemcho Rostam nathadhi anaushemeji na mmoja wa vigogo mbona kisutu aletwi!
  Pia kuna kemcho mwingine toka hii kamata kamata yeye ni kuzidiwa tuu!aletwe kisutu wanazani TZ shamba la BiBI!warudi huko mumbai na kashmir …………….!
  WIZI MTUPU………………..!

 74. any Says:

  62#, mimi sio mzungu na sitamanikuwa mzungu, am BLACKWOMAN! and am proud to be black.
  wadanganyika ni wanaokubali kuwa jama watafungwa, hawafungwi watatesa tu.

 75. ----------------- Says:

  wameshatolewa kwa dhamana.bongo celebrity you need to update yourself

 76. binti-mzuri Says:

  wewe ‘name’ # 62, ‘shanga’ hizo zimeshakunyonga shingoni,ndo mana.

 77. any Says:

  MIMI ni mchaga piwa, na sitetei wezi, kama KAIBA sheria ichukue nafasi yake na waka rest in peace huko segerea! vinginevyo, poleni wazee.
  hivi kwa nini Masha ametembelea gereza ghafla baada ya waheshimiwa kupelekwa, ni coicidence, au was planned

 78. Dunda Golden Says:

  KAPU LA MJANJA HILO MJINGA ATII MKONO
  CHA MUHIMU NINI KIFANYIKIE KWANI UKO TUONDAKO
  WADANGANYIKA WENZANGU SAFARI BADO NDEFU SANA
  KULIKO TULIPO TOKA TUGANGE YAJAYO WAJAMENI TUSINZIE WALA KULALA JUA LISHAKUWA KALI SANA
  CHAI GODA

 79. Mwanamke wa shoka (UK) Says:

  Aunt D naungana na wewe….huu ndio unaitwa mchezo wa si-hasa…..elections zimekaribia. Wapiga kura wahamasishwe…..wezi wa epa na hao vibosile wa wizara ya fedha ndani…..halafu mengine baadae.

  Hilo ni changa la macho……mpaka tukatoe mchanga machoni mchuma umeshaondoka….wezi wa epa wenyewe wapo wanadunda….hao mawaziri walokuwa wa fedha nao wameshatoka nje….sasa kumbe…!!!!!!!!!!

  Halafu kitafuatacho ni ushindi wa kishindo….washasikia!!!!

 80. ntimizi Says:

  KUCHOKA TUMECHOKA NA HATUENDELEI NA MARUMBANO YA MANENO SHERIA ISIPOCHUKUA MKONDO WAKE KWA WOTE TUNAOWAJUA KUNDI LETU LIMEAMUA KUWAHUKUMU KWA JINSI TUNAVYOJUA KAMA KUNDI TUTAWAFUATA MAJUMBANI MWAO. IWE MASASI AU THE SO CALLED GENIVA OF AFRICA TUMEAMUA NAWAJULISHA HILO MAKE TUMEFANYWA WAJINGA MNO. NGOJA TUWE ONYESHO LAKINI MTAKAOBAKI MTASHUHUDIA SOMO TUNALOTAKA KUTOA.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s