BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

KAMA UNAMPENDA UTAMLINDA December, 1, 2008

Filed under: Afya — bongocelebrity @ 12:05 AM
Tags: ,

aidsLeo ni siku ya ukimwi duniani.Ni mwaka wa ishirini sasa tangu maadhimisho ya siku hii yaanze hapo mwaka 1988.Ni siku ambayo dunia nzima inajumuika kukumbuka ndugu,jamaa na marafiki zetu wote walioathirika na hata kupoteza maisha kutokana na ugonjwa huu hatari ambao mpaka hivi leo bado unaendelea kuwa tishio.

Lakini muhimu kabisa ni kwamba maadhimisho ya siku hii hutumika pia kutafakari mambo mbalimbali kuhusiana na ugonjwa huu.Ni siku ya kutizama kwa makini maendeleo ya tafiti mbalimbali za tiba kuhusiana na ugonjwa huu,hatua ambazo tumeshapiga katika mapambano ya kuutokomeza ugonjwa huu na mipango ya mbeleni katika vita hii.Zaidi ya watu milioni 33 duniani wanaishi na virusi vya ukimwi.Ni siku nzuri pia kudhamiria,wewe na mimi,kwamba tutaongoza mapambano dhidi ya ugonjwa huu.

Takwimu mbalimbali za kitaalamu zinaonyesha kwamba maambukizi ya ukimwi yameanza kupungua ikilinganishwa na miaka kadhaa nyuma. Hili ni jambo la kujivunia ingawa halitakiwi kuachwa kuwa kama mafanikio ya mbalamwezi ambayo hupotea pindi tu jua linapoanza kuchomoza.Kazi kubwa bado ipo.Ukimwi bado upo,ni hatari na unaua.Sote tuna jukumu la kujilinda,kuwalinda tuwapendao na kuilinda dunia yetu.Dunia bila watu si dunia!Kama unampenda,utamlinda!

 

19 Responses to “KAMA UNAMPENDA UTAMLINDA”

 1. Mattylda Says:

  Mungu atusaidie sitaki kukumbuka ukimwi ulipoanza kule Bukoba lol!familia ziliisha jamani mweeeeee unakuta baba,mama,kaka,dada,shangazi,mjomba watoto wanabaki nba babu na bibi tena nao wameathirika inauma sana!
  Namkumbuka pia rafiki yangu mpendwa Eva na kakake waliondokewa na baba na mama wakaishi maisha ya shida sana kwa kweli ukimwi unatisha!
  WAPUMZIKE KWA AMANI WOTE WALIO AGA DUNIA KWA GONJWA HILI HATARI LA UKIMWI!

  NB:KAMA UNAMPENDA NI KWELI MLINDE!

 2. binti-mzuri Says:

  r.i.p to all those we’ve lost to this disease. wale waliojitakia, hawakujitakia na waliozaliwa na kulipia makosa ya wazee wao.

  mi kwakweli nampenda,hivo ntamlinda. r’mba no glove,no love..au mpenz 1 mwaminifu… yakikushinda,basi mapenzi tuachie sisi.

 3. Pearl Says:

  ni kweli kama unampenda utamlinda.
  Huu usemi ume-base sana upande mmoja wa shillingi kwa sababu kuna mifano ipo ambayo mtu anakufa kwa ukimwi kwa sababu alikuwa namuhudumia mgonjwa wa ukimwi.

  Mi nadhani tuweke mkazo pia kwenye kutoa elimu kwa wanaowahudumia wagonjwa wa ukimwi ili nao pia waweze kukingwa na hili janga la ukimwi hasa huko vijijini kunatisha jamani,watu hawana elimu ya kutosha ya namna ya kumuhudumia mgonjwa wa ukimwi,unakuta bibi anamuuguza mtoto wake halafu at the end wote wanakufa na ukimwi.
  Elimu isiishie kwenye namna ya kuishi kwa matumaini ila iguse maeneo yote ambayo yanauwezekano wa maambukizi.

 4. Gervas Says:

  NI SIKU YA UKIMWI..TUONGEE UKIMWI !!
  BC- tusipeane moyo kabisa kuhusu gonjwa hili, ngoma bado mbichi kabisa, unajua African Countries South of Sahara ambapo kuna nchi kama 40 hivi ndo inaongoza kwa maambukizi na wagonjwa wa ngoma duniani? Imefikia saizi kati ya Watu watano kwa Mswati mmoja lazima ana ngoma. Tanzania saizi si mijini tu hadi huku kwetu vijijini watu wanavuta vibaya sana. Tatizo gonjwa lenyewe limeijia pabaya;

  Tujiulize kwa nini iwe hivi?

  1. Elimu ya AIDS bado haijatosha. Hapa kijijini kwetu hata lile
  duka linalouza condom tu halipo. kwanza nani atanunua?

  2. Tamaa ya pesa/maisha mazuri/kuolewa na kufuata vipimo vya macho, kutoridhika na mpenzi mmoja..nini kifanyike?

  3. Inasemekana walioko kwenye ndoa ndio wanaongoza…
  kwa nini inakua hivo?

  4. Hiyo slogan..”kama unampenda utamlinda” naona haisaidii
  maanake siku hizi kufanya mapenzi sio lazima mpendane
  unaweza hata ukafumba macho.
  EFFECT;
  Population ya nchi itapungua, nguvukazi, market, Amani, uchumi wa nchi zitaporomoka. UKIMWI-huu huu umetafuna maprofessor, madaktari, wanasheria, ma-engineer, wakulima na wafanyakazi. Sheria ya ukimwi itapitishwa lini? maana kuna watu wanasambaza nasikia kwa maksudi.

  Tujiulize baada ya miaka 20, itakuwaje kama tiba itakuwa haijapatikana?

 5. hilly Says:

  “mh ni kweli,..huu ugonjwa Mungu atuepushie!!”

 6. DUNDA GALDEN Says:

  MSTAAFUUU WETU ALISEMA UGONJWA UMEKAA PABAYA
  HAPO HAPO KWENYE UTAMUUU.NA HATA HIVYO MASIKIO TUMETIA PAMBA LAHAULAAAA MUNGU TUAMSHE ILI TUJALIANEE

 7. hombiz Says:

  Tatizo la ukimwi Tanzania Afrika na Dunia nzima, haliwezi kutokomezwa kwa maneno tu!. Kazi ya pamoja mithili ya mchwa, ndiyo inayohitajika.

  Kwa hapa kwetu Tanzania mimi nina mtazamo wangu kama ifuatavyo:
  Kwanza kabisa, nakupa 5 dada Pearl na Gervas kwa comments zenu. Ni kweli inafaa elimu juu ya gonjwa hili hatari ipewe kipaumbele na ifikishwe zaidi vijijini ambako wanavijiji wengi bado hawana ufahamu wa kutosha juu ya janga hili.

  At the same time, badala ya taasisi husika kuchukua pesa za wafadhili na kufanya makongamano na wasanii kuimba majukwaani tu na kasha kujilipa posho, pesa hizo zitumike kuwapeleka wataalamu wa afya kuelimisha wananchi juu ya janga hili nationwide, bila kuchoka.

  Zaidi ya hapo, badala ya NGOs kuchukua pesa za wafadhili kwa manufaa binafsi, serikali inapaswa kuzihakiki NGOs hizi na kuhakikisha pesa za wafadhili zinamnufaisha mlengwa na sio matumbo ya ma-bwanyenye wachache! NGO-fisadi, zidhibitiwe na kuchukuliwa hatua.

  Wanaobainika kueneza gonjwa hili hatari kwa makusudi, inafaa wachukuliwe hatua kali za kisheria pindi wanapobainika. Please don’t be selfish you idiots!

  Moreover, maneno bila vitendo hayasaidii lolote. Hata useme “I love you” a thousand times a day,still haitakuwa na maana iwapo wewe msemaji ni mzinzi na humaanishi kwa dhati. Cha muhimu ni kujali kwa vitendo.

  Kwa ndugu zangu ambao ni waoga kupima ngoma, mimi nashauri mfanye hivyo kwani ni muhimu kujua status ya afya yako. Iwapo utakuta umeathilika, basi utapata ushauri nasaha toka kwa wataalamu wa afya ambao utakusaidia kurefusha maisha yako kwa kuishi na ukimwi huku ukizingatia kanuni za afya. Na iwapo utakuwa haujaathilika, basi hiyo itakuwa ni changamoto yako ya kujali na kutunza afya yako na ya yule umpendae.
  Nakumbuka mwanzoni mwa mwaka jana nilikwenda Angaza kupima ukimwi tena bure bila ghalama zozote. Lakini wananchi tuliojitokeza tulikuwa wachache mno. Kwakweli sikufurahishwa na uchache wa watu waliojitokeza!
  Mwisho kabisa, naomba tusiwanyanyapae wagonjwa wa UKIMWI hata kama wameupata ugonjwa huu kwa uzembe. Hakuna binaadamu aliye mkamilifu. Kila mtu ama mapungufu yake. Hivyo upendo wetu kwao, ni moja ya tiba muhimu.
  Wale waliopata maambukizo ya ugonjwa huu kwa bahati mbaya, nawapa pole.

  LET`S FIGHT AGAINST THIS CALAMITY TOGETHER AS ONE!

 8. ngosha Says:

  wewe Jeff unamlinda huyo demu wako?

 9. BLACKMANNEN Says:

  Pearl, comment yako # 3 ni nzuri sana, maana watu wakisikia “UKIMWI” wanawaza kuwa ni ugonjwa utokanao na ngono tu.

  Lakini kwa kweli, ugonjwa wenyewe una roho mbaya sana. Kwanini ujipachike sehemu hiyo??????????? Kwani hakukuwa na sehemu nyingine ya kujipachika mwilini isipokuwa hapo tu?????? Hii itakuwa ni plani au mawazo ya shetwani tu, asiyetupenda sisi wana wa Adam na Eva, tusifaidi matunda ya Eden.

  This Is Black=Blackmannen

 10. BLACKMANNEN Says:

  Watu wengi sana wanapenda BBC=Body to Body Contact, matokeo ni vifo.

  Black=Blackmannen

 11. Pearl Says:

  Hombiz kweli hizi NGO zinahitaji kufuatiliwa kwa karibu kwasababu wataishia kujilipa per diem halafu elimu na msaada unawafikia wachache.

  Kuna maeneo yanatisha jamani watu hawaelewi kabisa haya maswala ya ukimwi,nani atawafikia watu kama hawa!!!???
  Nadhani ni changamoto kwa hizi NGOs wasiishie mijini wanaweka shows kubwakubwa mi nadhani waendeleze hizo kampeni mpaka maeneo ambayo hayajafikiwa ya vijijini.

 12. Mama wa Kichagga Says:

  Ni sikio la kufa halisikii dawa.

  Njia pekee na ya bure ya kujikinga la hili sagamba ni kuwa mwaminifu vinginevyo utakwebebwa na maji mtoni kwa kina Ross.

  INAWEZEKANA TIMIZA WAJIBU WAKO

 13. halima Says:

  Kila nisikiapo gonjwa hili huwa na umia sana kwa sababu tumeshapoteza mtu muhimu sana katika familia hiyo basi huwa naumia sana.

  Ndugu zangu huu ugonjwa unatesa sana kama ukibahatika kuona au kuuguza mgojwa wa ukimwi basi hutapingana na mimi kwani akiwa katika hatua za mwisho za uhai wake huwa anataabika sana na maumivu anayoyapata akikuelezea basi lazima umuonee huruma.

  Watanzania huu ugojwa upo siku hadi siku unazidi kuenea kwa kasi hatuna budi kujikinga nao.

  UKIMWI UNAUA.

 14. - - - - - - - - - Says:

  ukimwi hauui,magonjwa yatokanayo na ukimwi ndiyo yanaua hamna mtu anaekufa kwa ukimwi bali watu hufa kwa malaria taifod na kazarika. sasa nyinyi mnasema wa vijijini wapewe elimu kumbe na nyie hiyo elimu bado mnaihitaji. ukimwi ni mapungu ya kinga kama cdk na white blood cell

 15. kekue Says:

  KAMA MNAPENDANA MTALINDANA!!!!!!!!!!!!!!!!

 16. sisterTZ Says:

  Homeboz i take notice of your comment ni nzuri sana..mimi binafsi nadhani elimu imetolewa na watu wengi wameelewa saana ISSUE ZOTE ZA UKIMWI..na vile vile hata vijijini jamani wanaelewa issue nzima ya ukimwi..THE ISSUE HERE NI KWAMBA sisi wenyewe kubadilisha TABIA ZETU..jamani hamuwezi kuamini sisi kazini kwetu tulikuwa tunahoja hawa mama DADA POA wengi wao wanakwambia wanaume wengi wanakuja kutaka HUDUMA kwao na wengi wanataka hiyo HUDUMA BILA KINGA YOYOTE…sasa jamani utasema kweli huyo mtu hajui issue ya UKIMWI? Au sisi akina DADA tunakimbilia MABUZI bila kujali kama ana ukimwi au la? CHA MSINGI SISI SOTE TUBADILISHe TABIA NA TUWE WAAMINIFU KTK MAHUSIANO YETU::JAMANI TUKUMBUKE TUNA WATOTO::

 17. BLACKMANNEN Says:

  WanaBC,

  Maoni yenu mengi yanaonyesha ni kiasi gani mmeguswa na balaa la UKIMWI. Maelezo yenu na ushauri wenu ni mzuri sana, lakini swali linabaki “Je, UKIMWI utamalizika na kutoweka kikweli?” Nawaomba msome umbea wangu hapa chini!

  UKIMWI hautaisha aslani, hadi tukubali mipango na matakwa ya “Waliouleta” hapa kwetu duniani.

  UKIMWI ni ugonjwa uliotengenezwa katika “Maabara” ya kitengo cha kijasusi cha nchi ambayo (leo) nimelisahau jina lake ili kuepusha mitafaruku kati yangu na watu waliowekeza huko.

  Sambamba na UKIMWI, wataalamu wa Kitengo hicho, walipendekeza kuwa nchi zote duniani, ziridhie na zihalalishe ushoga, usagaji na utoaji mimba. Utumiaji wa kondom pia lilikuwa ni moja ya pendekezo lao tangu mwanzo, lakini halikukidhi idadi ya watu waliopungua.

  Nia ya kushinikiza nchi za dunia kuridhia mambo hayo juu, ni kupunguza idadi ya watu. Kutokana na utabiri wa hali ya chakula duniani, baada ya miaka kadhaa ijayo, kitengo hicho kiliona kuwa uwiano wa chakula na watu havitaenda sawa, kutakuja njaa kubwa ya dunia yote, chakula kitakwisha. Kwa maana hiyo duniani hakutakuwa na chakula cha kumtosha kila mtu.

  Sababu ya kuongezeka kwa watu, inatokana na watu kuishi maisha marefu na kuzaaana sana bila mipango. Nchi maskini zinaongezeko kubwa la kuzaa watoto kuliko nchi zilizoendela. Nchi zilizoendelea watu hawazaani sana, lakini wanaishi maisha marefu zaidi, kutokana na maendeleo ya maisha bora wanayoishi.

  Sheria ya kuruhusu utoaji mimba umeridhiwa tayari na Tanzania katika “Maputo Protocol”. Mwulizeni Waziri Membe sababu zilizomfanya aridhie kwa niaba ya serikali. Sheria hiyo inasubiri kuridhiwa pia, na Bunge letu Tukufu katika siku chache zijazo. Kama mtapenda kuungana nami katika kuupinga mpango wa “Maputo Protocol”, mtanijulisha tuungane pamoja.

  Kwa hiyo, kutumia kondom, kama wengi mnavyopendekeza, hakitakidhi matakwa ya kitengo hicho, maana idadi ya watu, bado itabaki pale pale, na kama itapungua ni kidogo sana.

  Ngoma ya UKIMWI bado mbichi, na itaendelea, haiishi leo wala kesho!!! Habari ndiyo hiyo!

  It’s Great To Be Black=Blackmannen

 18. Maneno Mpina Says:

  This day is absolutely and very Unique as mark and reminds us of our daily resonponsilities; among of is to Be careful whatever any step wish to take ahead in life: Ukimwi really kills!! Lets us walk with calculated steps….My tribute on this sad day accross the globe goes to all have died by this desease UKIMWI….rest in peace…

 19. Hombiz Says:

  Tupambane na UKIMWI, tuache bla bla!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s