BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

BACK TO SCHOOL December, 2, 2008

Filed under: Blogs,Kabumbu/Soka,Michezo — bongocelebrity @ 10:13 PM

pawasabc

Mchezaji maarufu aliyewahi kuichezea Simba Sports Club, APR ya Rwanda na ambaye kwa sasa alikuwa akiichezea timu ya Azam FC Club inayoshiriki ligi ya Vodacom Boniface Pawasa (Baba Ubaya ) amejiunga na Chuo Cha Biashara (CBE) cha jijini Dar-es-salaam mwezi mmoja uliopita ili kuongeza elimu.

Akizungumza na blog ya Full Shangwe hivi karibuni,Pawasa amesema kwa sasa umri wake umeenda hivyo anahitaji kutengeneza maisha mapya na yenye malengo ya baadae na ndiyo maana ameamua kufuata nyayo za wachezaji wenzake waliopita kwa kujiendeleza kielimu.

Pawasa amesema kwa sasa anasomea mambo ya utawala wa biashara ambapo atakuwa chuoni hapo kwa mwaka mmoja akisomea cheti katika fani ya utawala wa biashara yaani Business Administration. Pawasa pia amesema akimaliza anatarajia kuendelea na elimu yake ya Diploma mpaka atakapokamata digrii yake ya kwanza hapo ndiyo ataangalia afanye nini.

Pawasa amesema kuwa pamoja na kwamba kocha wa timu yake ya Azam Santos anamuhitaji ili arejee kundini kuipigania timu yake katika mzunguko wa pili wa ligi ya Vodacom hataweza kurejea tena kwa sababu pia ana maumivu ya misuli ambayo yatamchukua muda mrefu kupona hivyo ameona asipoteze muda kusubiri apone wakati anaweza kufanya kitu kingine cha maendeleo.

Amewashukuru wachezaji wenzake kwa kumpokea chuoni hapo na anasema kwa sasa anafurahia sana maisha ya chuoni kwani rafiki zake wa karibu Ally Mayay, Aron Nyanda na Wilfred Kidilu wamempokea na wanampa sapoti ya hali ya juu na kama wao wameweza kwa nini yeye ashindwe “najua nitaweza tu na nitasoma kama nilivyojiwekea malengo yangu” anamaliza Baba Ubaya.

Pichani juu Boniface Pawasa a.k.a Baba Ubaya(kulia) akiwa na mwenyeji wake na Rais wa serikali ya wanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE) Bw. Ally Mayay ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa Yanga.

Habari na picha kwa hisani ya John Bukuku anayeendesha blog ya Full Shangwe.Mtembelee.

 

24 Responses to “BACK TO SCHOOL”

  1. Majita Says:

    Haya ndo mambo nataka mimi.
    Ningeweza ningewasikia wooote mliokuwa mnaponda Mr.Blue kurudi shule mnasemaje.Si mnaona wenzenu wanavyo focus???

    Haya tunarudia tena Mr.Blue nenda shule na baba Ubaya big up.Bravo mkubwa Pawasa

  2. eve Says:

    Hahahaha ishi! ndo unashtuka saivi kwamba kuna kusoma?? haya kazana maana ndo dili sikuizi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  3. Mattylda Says:

    All the best bro!ELIMU HAINA MWISHO!

  4. queen Says:

    well done pawasa(baba ubay) katha buti elimu haina mwisho usiofu utafanikiwa tu.

    ila inatakiwa uwe na moyo mana watoto wa CBE wizi mtupu!!!

  5. BLACKMANNEN Says:

    Umefanya uamuzi muhimu na wa busara sana, katika historia ya maisha yako, kwa sababu “Education Is Power”. Mtu hawezi kukunyang’anya ELIMU yako katika maisha yako yote. Nakutakia kila la heri katika maisha yako!

    This Is Black=Blackmannen

  6. Hombiz Says:

    Yes you can-baba ubaya!
    Ila tuu..chonde chonde baba ubaya,
    Usije kushawishika kuacha masomo na kukubali kujaza formz za kujiunga na timu ya MAFISADI UNITED ikiwa watakuhitaji
    Stay Focused baba Ubaya!
    PEACE!

  7. gisela Says:

    wewe queen no. 4 katha buti?

  8. watubwana Says:

    siri ya mtungi aijuaye ngata,big up baba ubaya kwa kurudi shule,
    big up MAJITA,saana tuu mtu wangu,umeona eee ndugu yangu!?watu wanaangalia mbali bwana,tuangalie FUTURE jamani,sio hapa tulipo…ELIMU HAINA MWISHO.

  9. halima Says:

    Yap! hayo ndio maneno baba ubaya nenda kasome bro faida utaiona. BIG UP

  10. Pearl Says:

    OMG!!!! this is good news,hongera kijana uamuzi wa busara,shule ni ya maana sana nadhani umegundua hilo ndo maana umeamua kurudi shule,ALL THE BEST,YOU WILL MAKE IT.

  11. Chris Says:

    Ni zao la mfumo wa soka ya sasa? Au ni zao la kuacha shule by then na kuona mpira ndio unalipa kwa wakati huo, bila ushauri wa wazazi, walezi, makocha waliomsajili etc?

    Mfumo mzuri wa hizi shule za soccer hutoa fursa ya elimu ya soka na elimu ya kawaida. Hivyo mchezaji anakuwa na qualifications mbili, ya soccer na elimu nyingine. Mabadiliko yanatakiwa ili mchezaji anapoacha/staafu mpira/au mchezo wowote awe na cheti at hand.

    Hajachelewa though muda unakimbikia sana! All the best Bro!

  12. Mayu Says:

    Safi sana, maana hiyo misuli imekuanza inawezekana ndo mwisho wa mpira. Pata ellimu uendelee maisha mengine

  13. mrdegree Says:

    hawezi kusoma huyo mr misifa! huu mwaka wa tano sasa anajitangaza anaenda chuo! mara ya kwanza kumsikia ilikua 2003.sasa ni mwaka wa tano anarudia tena kujkitangaza! watu wangekua wanasoma kwa kuandikwa tuu kwenye vyombo vya habari basi watanzania wote tungekua wasomi! aende zake

  14. Pearl Says:

    halafu jamani kweli tutembelee blog ya full shangwe kama Jeff alivyoandika kwenye sentensi yake ya mwisho hapo juu.
    mi binafsi sikuwa naifahamu ila leo nimetembelee baada ya kusoma hapo jeff alipoandika,yaani wadau kule hakuna oni hata moja,tumtembelee bukuku jamani.

    ni hayo tu,ila msinishikie bango hapo na kuanza kunitungia mistari ya kashfa,kwasababu watu wengine wataanza kuniponda kisa kwa hako kashauri kadogo nilikokatoa, tuwe na mapenzi mema na watanzania wenzetu na tuwape support inapobidi.

  15. EDWIN NDAKI Says:

    POWER SIR..safi sana kurejea ubaoni.

    Ila usisahau kwenda pale CBE “kantini” japo kujinywea naniiihii inasaidia sana kuongeza pato la TBL etc.

    Kingine msalimie huyo bwana mdogo wangu wa kirumba Aron

  16. halima Says:

    Hivi wewe Mr Degree, hiyo degree yako umechukulia chuo gani nahisi hata huyo mwalimu wako darasani alikuwa anapata shida sana. kila kitu kwa kwako kibaya hakuna hata unachoweza kusifia mmhhh wewe ni tatizo.

  17. Majita Says:

    Halima # 16 wenye degree huwa hawajitangazi.

  18. Ed Says:

    Ally Mayai watu walimwambia wakati akiwa pale Jiteute, jamani somoni yeye akaona kama muda wake ndio huo. Hii inabidi iwe somo kwa wale wote ambao wanadhani sports inaweza kuwa asset.

    Good move vijana

  19. halima Says:

    Nimekupa majita hahahahahh

  20. halima Says:

    Majita nimekupa mkubwa hahahhahah

  21. mrdegree Says:

    teh! teh! unanichekesha sana majita no.17

  22. Laswai Says:

    HATA HUKU ULAYA SPORTS INALIPA TU UKIWA KWENYE GAME, UKISHAONDOKA MAMBO YANAANZA KWENDA MRAMA KAMA AKILI YAKO SI SAFI, MFANO NI MINGI SANA HAPA UK NA USA PIA WANASPORT WENGI BAADA YA KUSTAAFU MAMBO YEMEWAENDEA KOMBO. WENGI WANCHOKA NI KULEWA TU AKINA BEST, GAGA OJ SIMPSON ALIYEFUNGWA LEO HUKO U.S.A. MICHAEL JACKSON MUFULISI PESA HANA TENA

  23. watubwana Says:

    watu bwana,siri ya mtungi aijuaye ngata,ni mtazamo wangu kuwa kila mtu anauhuru wa kuandika anachojisikia na kufikiria.kila mtu ana mtazamo wa tofauti.
    baba ubaya kama kuna lolote lililo tofauti tafadhali jirekebishe,sababu muda nao haukungojeii,kazania masomo yako sana umalize ufanye ishu nyingine.hayo ndio maendeleo.wengi wanaenda shule ila wanaishia njiani sababu shule ya bongo yataka moyo,ni ya kujituma sana, jitahidi ufike unakotaka fika bila kumsahau MUUMBA wako akusaidie na kukuongoza

  24. ustadh Says:

    ali mayay ndugu yangu tuliachana ten yrs ago ununio high school, unakumbuka enzi za bewni la mecca na samaki wa ununio kijijini tuwasiliane email = soudnorman@yahoo.co.uk


Leave a reply to halima Cancel reply