BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MRAMBA NA YONA WAACHIWA KWA DHAMANA December, 2, 2008

Filed under: Breaking News,Serikali/Uongozi,Siasa,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 12:58 PM

yonamrambabc

Baada ya kusota rumande kwa takribani wiki moja,hatimaye mawaziri wa zamani, Daniel Yona na Basil Mramba leo wametoka rumande baada ya kutimiza masharti ya dhamana.Wameachiwa baada ya kuweka dhamana ya hati za nyumba zenye thamani inayozidi bilioni 2.9 kila mmoja!! Kumbe watu wana nyumba za mabilioni!

Advertisements
 

36 Responses to “MRAMBA NA YONA WAACHIWA KWA DHAMANA”

 1. - - - - - - - - - Says:

  ala sasa wewe bongo celebrity unashangaa nini nyumba za mabilioni watu wana nyumba za trilioni kina shekhe nkapa hata hivyo nimeshangazwa kwamba hawa mafisadi imewachukua wiki kutoka mimi nilidhani wangetoka baada ya masaa maana mambo yote walikuwa nayo tayari hapo malawyer wamefanya kazi ya ziada wameamua kuwaachia ndani wiki moja changa la macho ili kuonyuesha na wao ni wenzetu wanasota jela hawa wazee wametoka leo ndio wametoka moja kwa moja poleni sana wadanganyika

 2. Mattylda Says:

  MAFISADI WA RICHMOND-BOT-EPA-MAFISADI WALA UCHUMI WA NCHI…..guess wat next?mchakato ndo huo wataingia selo wengi tu nakutoka by the way yaliyopita tushaanza kuyasahau,wako wapi kina Jeet patel??wako nje kwa dhamana….soon tu hawa kina mramba watashinda kesi na watadunda mitaani kama kawa,ningekuwa na uwezo wangesota huko selo mpaka sura ziwe nzito kwa maisha ya jail,natamani Mungu asikie kilio cha wanyonge wanaoishi kwa machale bila kujua ni lini na wao wataishi kama binadamu nchi hii!!
  Pamoja na kutoka lakini mmeonja selo na kero yake!

 3. janbar Says:

  nani kakwambia kuna lisilowezekana bongo. hasa ukiwa kigogo. nyumbanyaweza kuwa na thamani ya 100mil. lakini kwa issue ya mahakama itaonyeshwa 3.0bil. utapeli mtupu. kwani mara ya kwanza hawakujua kama wana nyumban za thamani hiyo. waweza nambia kwamba walipenda kulala keko siku zote hizo au ujinga mtupu. sasa wadanganyika wenzangu subirini pale mtapoambiwa hawana hatia! kushangilia kote ni kiinimacho
  ……….yangu macho na masikio………………..

 4. hombiz Says:

  Hayo ma-pose vipi!?

 5. Bahati R. Mtui Says:

  Naomba niulize hivi, kwani hizo ‘mali zisizohamishika’ walizipataje? Na ka a hati za mashitaka zinaonesha kwamba walijipatia mali fulani kinyume na sheria, inawezekanae wakatumia mali hizohizo za walipakodi kujitoa mahabusu?? Naomba mtu anayeelewa sheria za nyumbani anifafanulie. Asante.

 6. Frateline Says:

  Hi guys kutoka Helsinki

  Kwa kweli hawa wazee wameumbuka sana, wamepoteza heshima kabisa kwenye jamii, sasa wataendelea kupambana na kesi yao wakiwa nje lakini wameumbuka sana tena sana, ukizingatia zile nafasi wamewahi shika,

  I have no comments on their bailout, but it is important to note , dhambi ya ufisadi ni sawa na dhambi ya uchawi maana inachafua ukoo, kabila na wakati mwingine taifa, hawa jamaa wamechafuka sana KTK SIASA ZA BONGO

  Frateline

 7. hombiz Says:

  Ndugu wasikilizaji. Hiyo picha hapo juu ilipigwa dakika 10 kabla mpira kuanza wakati wachezaji Mramba na Yona wakijiandaa kubadili jezi.
  Ni sekunde ya kwanza tu tangu mpira uanze
  Mkapa kasimama golini vema kabisa wasikilizaji. Anadunda mpira chini kisha anampasia Beki wake Edward Lowasa. Lowasa hapotezi muda anampasia Jeeta Patel. Patel anatuliza mpira kifuani kisha anaushusha chini na kupiga cross nzuri kabisa ambayo inamfikia Rostam Aziz… Rostam Aziz….Rostam aziz…Rostam Aziz anakwenda na mpira kwa kasi ya ajabu anakutana na mlinzi hatari wa timu ya TAIFA LETU anayekwenda kwa jina la mlalahoi. Hata hivyo Rostam anafanikiwa kumpiga kanzu ya nguvu na kusogeza mpira kwake Chenge.. chenge wa vijisenti…Chenge..chenge wa vijisenti wasikilizaji…chenge anaambaa taratiiiiiiiiibu kabisa na ngoma ile…. Kwakweli Chenge ana pumzi na kasi ya ajabu leo ktk uwanja huu wa national Stadium ya Kagoda. Chenge bado anatokomea na mpira kaskazini mwa uwanja wasikilizaji. Chenge hatimaye anatoa pasi kwa Daniel Yona. Yona anaonekana kabanwa sana na mchezaji nyota wa Segelea lakini hata hivyo anaweza kumponyoka na kuachia nduki kali kabisa ambalo linakwenda moja kwa moja kwake Basir Mramba. Basir anatuliza ngoma chini na kugeuka kulia na kushoto kuangalia nani wa kumpasia gozi.wasikilizaji naona mzee wa kula majani amejiatiti vema kabisa ndani ya wanja hili ambalo nyasi zake ni evergreen…hata ng`ombe hana haja ya kutafuna jinsi koka lilivyokubali…O.K! naona mzee wa kugegeda nyasi anasimama kidume kabisa hapa, Duuuuuuh!. Kweli Mramba ana nyonga nyepesi wasikilizaji kwani amegeuka kwa kasi ya ajabu na kupiga mpira kuelekea kwa Nazil Karamagi ambaye ni mchezaji wa kuaminiwa ktk timu hii ya FISADI UNITED. Kalamagi bila kupoteza muda anapiga cross safi kabisa inayomfikia Mahita. Mahita anaambaa na mpira taratibu na kufanikiwa kuwavuka washambuliaji hatari wa Taifa letu na anampasia gozi Abdalah Zombe ambaye bila kupoteza muda anapiga mpira ule kwa kichwa kuelekea Costa Ricky Mahalu. Huyu mchezaji bila shaka pengine wasikilizaji wengi hamumfahamu. Kwakweli ni mchezaji mpya kabisa ktk timu hii. Ila kwa muda mwingi alikuwa anachezea timu ya kulipwa huko Italia. Sasa karejea kwenye timu ya FISADI UNITED ili kuiongezea nguvu zaidi. Kwakweli mchezaji huyu amebobea sana ktk…..ooooooh wasikilizaji Costa Ricky na mpira…Costa Ricky na mpira..Costa Ricky na mpira wasikilizaji..Costa..costa..costa..la.laaaaa…la..laaaa goooooooooooooo!!!!!!!
  Washikaji katika dakika ya kumi tangu mpira kuanza, Mafisadi united inajipatia bao la kwanza na timu ya Taifa Letu, haijapata kitu!

 8. EDWIN NDAKI Says:

  Kwangu ningeona HABARI iwapo wangenyimwa Dhamana.Ila kupata dhamani ni jambo ambolo nilitegemea.Hii nikutokana na sababu zifuatazo.

  Kwanza.
  Ulishaona “steringi” kauwa?Labda sinema za kihindi.

  Pili:
  Ulishaoona wapi mtuhuhimiwa anaaamua tu mwenyewe KUTOKA RUMANDE BILA kibali kumruhu(removal order)…wakati kuna watuhumiwa kibao na wana hati za kutoka kuja kushugulikia dhamana zao wasota tu jela.

  Sipendi kuwahukumu kwa mashitaka yao ila UKWELI unabaki PALE PALE..safari bado ni NDEFU sana..naaamini wengine watajitoa..ila nawaomba tukaze buti tutafika tu HATA kama tutakuwa tumechoka.

  Nakukumbuka mwalimu NYERERE

 9. ..................... Says:

  nmnatakiwa kurudi tena rumande mnaonyesha kiasi gani nyie ni wezi sasa mtakoma kumbe sisi tunataabika nyie mnakula kuku na familia zenu tu kiama cenu mafisadi nyie hamuoni aibu mnalisha familia zenu haramu mababa mazima wezi wa kodi za wananchi tena masikini kweli nyie mnauzi ngoja tu lakini na bado mungu atawaumbua tu kama wewe mramba unaniuzi wewe umeinua kichwa kama unaogelea bila aibu mnacheka mngetakiwa mlie!

 10. BLACKMANNEN Says:

  Dah!!!! Daniel Yona, kageuka kuwa “Monki”. Anatusalimia kimonks, kama afanyavyo “Dalai Lama” wa Tibet, ” Wakubwa kwa watoto , itikieni wote – Markhabaa Jambazi Yona”. Lakini haka ka Mramba, naona bado kajeuri, kaoneni kalivyoinua kichwa chake, kama tumbiri anayeiba karanga za “Majita” shambani.

  Black=Blackmannen

 11. any Says:

  I told ya! it wasnt WOW to me, as I knew what will be next. kama mlivoona, so we were not supposed to celebrate, the guys are out for good, dont expect them back to selo, sawa? Ndio maana i said wadanganyika msianze kushanglia kabla.

 12. any Says:

  Pozi la Mramba la KIMISS! mmeliona lakini>?

 13. Majita Says:

  Nimependa hiyo body language.
  Angalia machoni pa Mramba,you can tell.Naamini pale kwa Yona wakati hakimu anajiumauma kusoma juu ya dhamana pale chini lilikuwa linaitwa jina la Yusufuuuuuuuuu!!!!Halafu hakuna alosikia harufuuuuuuu

 14. Pearl Says:

  mie sina la kusema ila Mungu anaona uovu wote huu,sijui watu watasema nini huko kwa Mungu!!!???

 15. mrdegree Says:

  daah! mchaga yupo nje? kosa kubwa sana hili!

 16. Mkate Says:

  Watanzania wenzangu..kitendo tu cha kujiita ‘wadanganyika’ ni kuonyesha udogo wa fikra na mawazo yetu…
  Tulichukulie hili suala kwa mtazamo mwingine kwani serikali inajitahidi iwezavyo kutatua shida ya mafisadi (nakubali kwamba kati ya hao wanaotatua shida, wengine ndiyo wenye shida) ila tusiilaumu sana serikali. Mbona wenzetu wenzetu Kenya wana kashfa nyingi za wizi lakini bado uchumi wao unaendelea????Mbona hatujiulizi hivyo…ni kwamba wenzetu wamegundua kwamba in as much as we depend on the government, it is not going to help us in no way..Tuangalie ishu nyingine za kuongelea kujiendeleza kiuchumi tuachane na kesi ambazo hata wakirudisha hizo pesa..hazitafika mifukoni mwenu..
  Let us think outside the box my fellow Tanzanians…!!!!
  God bless Tanzania…God Bless Tanzanians!!?

 17. halima Says:

  Hombiz aisee ilo ball limeniacha hoi nimecheka mpaka machozi kwikwikwikw big up kaka. huyo mchezaji aliefunga ilo goli nimatata sana maana sijawahi kumsikia.

 18. halima Says:

  Hilo poz la mramba mhhh utafikiri yupo kliniki anasubiri zamu yake hahahahahah

 19. Madman Says:

  Hivi hizo bil ni kwamba wanamiliki mitaa ama?Halafu inawezekana hizo kandambili alizovaa Yona kanunua Laki tatu tu!Pia kuna tetesi kuwa hiyo picha imepigwa wakipanga mgomo kama ule alioongoza Mramba enzi za Nyerere alipodai kuwa bora mkoloni kuliko uongozi wa Nyerere.Sasa niwaulize…,tuseme kuwa bora utumwa kuliko uongozi wa Mramba?

 20. Madman Says:

  Aah… I’m sorry nimesahau kuwaambia kuwa Kikwete ametangaza kuwa fedha zote zenye saini ya maiti Balali au mafisadi Mramba na Yona ni haramu na hazitumiki tena kwa hiyo msijisumbue kudai mishahara yenu ya mwezi huu hasa walimu.Kudai mshahara ni kushiriki kulifisadi taifa.Mazee hamkusema kama kocha wa FISADI UNITED alishangilia lile goli tulilofungwa.Na ni nani huyo sisi wengine tunaisikia tu hiyo mechi wala hatuioni.Na je kuna uwezekano wa kupata namba kwa mafisadi niuze mechi?

 21. queen Says:

  jamani hivi wajamaa hawarudi tena ndani

  wizi mtupu!!!

 22. kekue Says:

  Jamani hawa wananchi wana hasira sana ss tufanyeje mzee, “Nendeni mkaongee na hao wahusika muwaombe wakaonekani tu pale kizimbani then wapelekwe keko pale wakae cku mbili tatu then wapewe dhamana” nafikiri itasaidia kdg kupunguza jazba kwa wananchi na wataona tunafanya kazi.

 23. Kafura Says:

  Huyu mzee vipi, mbona kapozi kama Dalai Lama vile? Au ndo shukurani kwa pilato kwa kumtoa keko? Hawa wazee walishakusanya. Sasa katika nchi kama yetu hii mtu unawezaje kuwa na mali ya billion hizo kama za Yona? Kweli tunaishi katika nchi mbili tofauti.

 24. Mchaga Says:

  There’s certainly more dirt where that came from..it’s so freakin funny how these tycoons wana poromoshwa madarakani. Kinachokera even more is wale wakina lowassa and company they still hold their bunge positions.. watakiwa warudi vijijini permanently maanake inaonekana kabisa they all just got a slap on their wrists..bongo inamambo, hatukai kuendelea–still, some credit to the current pres.. he can still do more!

 25. Hombiz Says:

  Halima huyo Costa Ricky Mahalu, alikuwa ni balozi wa Tanzania Italia. Alichokifanya yeye ni kuliingizia Taifa la Tanzania hasara ya mabilioni ya pesa za mlipa kodi kwa kununua jengo la kisanii kwaajili ya ubalozi wa Tanzania huko Italy. Unaweza kupata habari zake zaidi kwa kuingia hapa http://www.thisday.co.tz/News/3667.html

  Ndugu Madman, kocha wa timu hii ya MAFISADI UNITED, hata mimi simfahamu. Nilikuwa namfahamu kucho msaidizi tu ambaye hivi sasa ni marehemu. Anaitwa Daudi Balali. MOLA ammmmmm…re..hemu!. Kuhusu Kocha mkuu, itabidi nikamuulize mtangazaji kama anamfahamu anipe jina lake kisha tulianike hadharani. Nasikia mtangazaji alisahau kutangaza wakati kocha mkuu akishangilia kwa sababu macho yake mtangazaji, aliyaelekeza kwa washabiki wa timu hii waliokuwa wakishangilia kwa fujo,hasa familia za wachezaji ambazo ziliingia hadi mitaani huku zikiimba…”sisi ndio sisi….hakuna kiboko yetu……sisi ndio sisi…hakuna anayetuweza….Palikuwa hapatoshi mazee!. Sijuwi itakuwaje katika mechi ya maludiano…

 26. hombiz Says:

  Madman!, mimi naona kupata namba kwenye timu ya MAFISADI UNITED ili uuze timu sio kazi ndogo. Kwanza itajili ujaze fomu za usaili ambazo zina maswali magumu ile kinoma.
  Halafu, watakufanyia majaribio waone uchezaji wako wa ufisadi una kiwango gani. Mpaka usainiwe mazee, duuuuh! kazi ipo!, hapo utakuwa umeiva kinoma babu!. Hata kuuza timu hautakumbuka tena.
  Ila sikukatishi tamaa! Unajua tena hakuna lisilowezekana mtu wangu!. Jaribu bahati yao, unajua tena-“yes you can!”

 27. hussein Says:

  Huyo aliyejitia kutuandikia timu ya mafisadi ni mtu mwenye chuki zake. Nafikiri tukubali kuwa mahala hapa ni kwa kila mtu kuonyesha chuki zake na wala si kwa masilahi ya taifa. Tusipoangalia tutafika mahala tutakuja kukosana kabisa lakini waandishi wa habari na waandaaji wa nafasi hizi wajue ndo wakulaumiwa na kubeba mzigo wakati nchi hii itakapoingia katika machafuko. Hii naisema kwa sababu mweelekeo uliopo ni kuchafuliana kwa ktumia vyombo hivi vya habari. Kwa tusiachie vyombo vyetu vya sheria vikachukua mkondo wake mpaka mtu ahukumiwe.
  Mimi naona tusipojifunza kutoka kwa wenzetu yatatukuta yaliyowakuta, maana chuki imeendekezwa na vyombo vya habari ambayo inaambatana na uchochezi wa ukabila. Mungu atunusuru

 28. julius Says:

  tunaelekea pabaya kweli kama tukiendelea kuendekeza chuki binafsi

 29. BLACKMANNEN Says:

  Mramba na Yona,

  Mtu mwenye ELIMU sio mwenzako. Elimu inakusaidia kupanuka kimawazo na kuweza kuona mbele. Mwenzenu Dr. Balali aliitumia elimu yake na kuyaona yote haya yanayowasibu ninyi sasa hivi.

  Yeye wakati mkifanya UFISADI wenu na yeye, alikwenda USA na kujipatia kabisa mapema, “NONDO” ya huko, ili mambo yakimbumburuka analala mbele. Dr. Balali, hela aliyoipiga “ukucha” BoT, hakupapatika nayo, kama ninyi (Mramba na Yona) kwa kununua magari ya fahari na kujenga majumba ya kifahari, kuliko hata White House ya Rais “Mfukuzwa”, Joji Pori.

  Dr. Balali, alipoona siri imebumburuka, alilala mbele, katika nchi yake ya pili (alikojipatia NONDO=Passport, yake) na kujibadilisha sura yake, na kutangaza kwamba “AMEKUFA”.
  Dr. Balali, alikuwa na maana ya kwamba, aliyekufa sio yeye bali, soo lote la EPA, upande wake LIMEKUFA.

  Mwenzenu anawacheka sana, anapowaona mkijifuta mijasho, mkiwa Mahakamani na kwenda kulala Keko. He he he he heeee!!!!. Mwenye ELIMU sio mwenzako. ELIMU kitu cha maana sana maishani. Habari ndiyo hiyo, na mkomage kupiga “ukucha” mali za watu.

  This Is Black=Blackmannen

 30. Hombiz Says:

  Hussein, inaelekea wewe ni kibaraka wa MAFISADI ndio maana hiyo timu huifagilii. Julius, chuki binafsi ni zidi? Kufichua wabadhilifu wa mali ya umma au? Anayemuona msafi hapo mtaje nasi tumwage data!
  Vyombo vya habari navipongeza kwa uzalendo wao wa kuanika uozo wa MAFISADI hadharani. Good JOB!. Endeleeni na wembe huo huo!

 31. binti mzuri Says:

  WEZI HAOOOOOOOOOOOOOOOOO

 32. Mayu Says:

  Shenzi zao – WIZI MTUPU

 33. binti-mzuri Says:

  HEY JAMANI WEWE BINTI MZURI WA NAMBA 32,NI BINTI MZURI GANI JAMANI!..I NEVER POSTED THAT COMMENT!ANYWAYS,MAYBE YOUR NEW,AU MAYBE ITS SOMEBODY WHOSE TRYING TO USE MY IDENTITY..NILIKUA NIMETOKA KIDOGO TU,NILIKUA NARUDI!!…USE IT OR LEAVE IT..EITHER WAY..MI NIPO TAMBARARE TU!COZ HATA KULIANDIKA UMEKOSEA

 34. JOYCE Says:

  TUKUBALI TU KUWA SISI NI WADANGANYIKA HAKUNA LA ZIADA ACHA WAFAIDI WAO NA FAMILIA ZAO.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s