BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

It’s Only BONGO RADIO December, 6, 2008

Filed under: African Pride,Bongo Flava,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 12:21 PM
Tags: ,

bfradio_logo_230x130Mara kwa mara tumekuwa tukipata e-mails kutoka kwa watu wanaouliza au kutaka kujua kama kuna radio za kibongo ambazo zinapatikana mtandaoni(online).Kwa bahati nzuri jibu tulilonalo ni kwamba kwa upande wa radio za burudani radio pekee ya kibongo inayopatikana mtandaoni 24/7 ni Bongo Radio.

Kwa hiyo kama unataka kuburudika na Bongo Flava,Zilipendwa,Muziki wa dansi na muziki wa kiafrika kwa ujumla huku ukiendelea na kazi zako,basi Bongo Radio ndio jibu lako.Bonyeza hapa kuitembelea Bongo Radio.

Kimsingi Tanzania tupo nyuma kidogo katika uwanja huu wa radio ambazo zinapatikana pia mtandaoni.Tatizo sijui liko wapi kwa kweli.Sio mbaya kama radio zingine za kibongo kama vile Clouds FM,Radio One,Times FM nk nazo zikaangalia uwezekano wa kuwepo mtandaoni pia kwa maana ya kusikika mtandaoni.

**Kama kuna mtu anazifahamu radio zingine za kibongo zilizopo mtandaoni tafadhali tujulishe.

Advertisements
 

11 Responses to “It’s Only BONGO RADIO”

 1. Seydou Says:

  Si utani Bongo Radio ni mwendo mdundo yaani hapa ni full mzuka namsikiliza Dj Dennis hapa LIVE anafanya mambo si ya kawaida. Hakuna nyingine zaidi za Bongo Radio na kila jumampili sikosi kumsikiliza Dinah kwenye kile kipindi cha mahusiano na ngono.

 2. K-U Says:

  Jaribu http://nukta77.com/burudani.aspx for more swahili radios

 3. Laswai Says:

  Si kweli radi bongo PEKEE IPO MTANDAONI TANZANIA, HATA RADIO YA WAKATOLIKI IPO MTANDAONI. INAITWA RADIO MARIA KAMA SIKOSEI

 4. BLACKMANNEN Says:

  WanaBC wenzangu,

  Karibuni katika redio za mtandaoni. Mimi ni mwakilishi wa “Radiomaria.or.tz”. Sauti Ya Enjili Nyumbani kwako. Hii ni redio yako “Live”, na ni wakati wote 24hrs. Sio kwa Wakristu pekee yao, ni kwa kila mtu, maana inatoa mafundisho na kukupa habari mbali mbali. Taarifa ya Habari kutoka TBC-Live, utasikiliza hapo.

  Pia tunayo redio nyingine, ambayo ni kijiwe cha Watanzania wote, ni “Jambonetwork.com”, ni washikaji wangu hawa. Hapo uta-chat na Wabongo wenzako masaa 24, ingia sehemu ya kuchat, utakutana nao.

  Ili kupata redio zingine zaidi ya hizo nilizowatajia, jaribuni kuingia, “nukta77.com”, bonyeza “Burudani”. Redio zote utazikuta hapo, ikiwa ni pamoja na Bongoradio kutoka Chicago. Kuna redio zingine pia, lakini hizi nilizokupeni, mtafurahiwa nazo na kuburudishwa nazo sana.

  Kuhusu Radiomariatanzania. Kama kuna mtu anacho cha kuniuliza niko tayari kuwajibu, wakati wowote, ila situmii jina la “BLACK”, kwani Mwenyezi Mungu, hafanyiwi dhihaka, na mimi simtanii katika kueneza “neno” lake. Mama wa Kichagga, tuwemo, karibu “www.radiomaria.or.tz”, kwa sasa inakarabatiwa, lakini bonyeza upande wa radio, inafanya kazi kama kawaida.

  It’s Great To Be Black=Blackmannen

 5. DJ Dennis Says:

  Live shows schedule (all times are Central Time – GMT +6)
  FunkHouse Mixes With DJ Dennis Live from the Twin Cities on Saturdays @ 1 PM.
  Slowjams with GQ Live from Chi-Town on Tuesdays @ 10 PM.
  Mapenzi, Mahusiano & Ngono Live from the UK with Dinah on Saturdays @ 12 PM.

 6. pompidu Says:

  jaribuni newenglandumoja.net,utapata midundo balaa

 7. Baraka Says:

  Mbona hio radio haina ratiba? haina taarifa ya habari live kutoka tz

 8. Presenter Says:

  Hakuna taarifa za habari kwa vile habari zote za kibongo ziko kwenye magazeti mtandaoni na blogs.

  Tunajaribu kuwa tofauti ili tusiwa-bore wasikilizaji.
  Karibuni sana.

 9. Soldier Says:

  pamoja na bongo radio kua hewani shukurani za pekee ziwaendee waanzilishi wa radio za kwanza za kiswahili mtandaoni live ni Radio free africa na Jambo Radio hao ndio walitoa changamota kubwa tokea mwaka 2001 hadi leo sijui kuhsu radio free africa lakini jambo radio wapo hewani hadi hivi ninaandika hapa tena wanarusha channel tatu jambo live miziki ya flava, Jambo Gold miziki ya dansi na Jambo Plus kwa ajili ya mziki ya Taarab na Jambo Vibez kwa wapenzi wa reggae. Hongera kwa wote mnaochukua juhudi za kutuburudisha live mtandaoni mungu ibariki Tanzania……..

 10. Maxence Melo Says:

  Nawashukuru wote mloweza kutupa shavu (Jambo Radio) na kuwakumbusha wengine kuwa tumesimama imara tangu 2001 (ila ni tangu 2003). Kwa kutambua umuhimu wa kuwapa kilicho bora zaidi tumeamua kujipangilia upya zaidi.

  Mwaka mpya utakuja na kitu kipya kabisa na cha kufurahisha zaidi.

  Tunawashukuru kwa kuwa nasi kwa miaka hii mitano na tunawaahidi kuendelea kusimama imara, tunaamini katika ushirikiano na ushirikiano huo tunautarajia toka kwenu. Kunapokuwa na tatizo tafadhali tufahamisheni. Simu yangu iko hewani 24hrs na wote wanaotutumia maoni kwa njia ya barua pepe hujibiwa!

  Maxence


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s