BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

KILA LA KHERI NASREEM December, 13, 2008

Filed under: Fashion,Urembo — bongocelebrity @ 12:12 PM

miss-tanzania-08

Leo ni fainali za kumtafuta mrembo wa dunia wa mwaka 2008(Miss World 2008). Shindano hilo linafanyikia nchini Afrika Kusini ndani ya jiji maarufu la Johanesburg katika ukumbi ujulikanao kama Sandton Convention Centre.Tanzania inawakilishwa na mrembo wetu Nasreem Karim(pichani).

Shindano la mwaka huu ambalo mwanzoni lilikuwa limepangwa kufanyikia huko Kiev nchini Ukraine kabla ya kuhamishiwa Afrika Kusini kutokana na mgogoro wa kisiasa uliokuwa unafukuta baina ya majirani Georgia na Urusi,limevunja rekodi ya kuwa na washiriki wengi kushinda miaka mingine yote katika historia ya miaka 58 ya shindano hilo.Jumla ya washiriki 109 wanashiriki shindano la mwaka huu.

Mrembo wa dunia wa mwaka jana,Zhang Zilin kutoka China ndiye anatarajiwa kumkabidhi mrembo mpya wa dunia taji.BC inamtakia kila la kheri Nasreem Karim ambaye katika mashindano hayo anajulikana zaidi kwa jina la Nasreem Ndiye.Kila la kheri.


Advertisements
 

28 Responses to “KILA LA KHERI NASREEM”

 1. BC Editor Says:

  Mashindano ya urembo ya dunia mwaka 2008 yamemalizika nchini Afrika Kusini.Mrembo kutoka Russia,Kseniya Sukhinova,ndiye ameibuka mshindi.Mshindi wa pili ni kutoka Trinidad and Tobago na wa tatu ni kutoka India.Wa nne ni kutoka Afrika Kusini na wa tano ni kutoka Angola.

  Haya,tusubiri tena mwakani.

 2. mimi Says:

  Asante.kama kawaida yetu kusindikiza!!

 3. majita Says:

  Huu mwezi ni mbaya kwangu.mamaa Nasreem ndo hivyo tena keshamaliza kwa matokeo ya “kama kawaida”

  Mimi nae babaa “muchumba” huku majita ni balaa.Imenyesha mvua ya aina yake na kuangusha miti na kuharibu kila aina ya miundombinu kitu kilichopelekea “vibatari” vyetu kuzima kabisa na kibaya na kikubwa zaidi ni kuwa hii aina ya mvua imesababisha sasa hakuna kuni tena na hivyo HAKUNA KUPIKA.Mama ntilie baadhi wenye akiba ya kuni nao wamepika chakula kiiingi lakini kwa wingi wa watu tuliopo hapa kijijini kwangu imekuwa ngumu kutuhudumia.Kwa mara ya kwanza hapa kijijini kwangu naona watu wanakula kwa foleni ndeeeeeefu kiasi kwamba ni shida kwani hakuna kuvumilia kukaa kwenye foleni kutokana na baridi kali iliyopo.

  Balozi wa kijiji tayari anatembelea wananchi wake huku sungusungu na mafundi vibatari wakifanya kazi usiku na mchana kuokoa jahazi hili.Sehemu za kujazia upepo kwenye baiskeli zetu nazo hazifanyi kazi sasa hapo ndo balaa linapolalia.

  Matty,Pearl,Binti mzuri,Mama mkwe mama wa kichaga,Any,Hombizi,Mkuu blackmannen,Watu bwana,Mzee wa finland,Kiongozi Ndaki,na washikadau wengine ambao sikutaja majina yenu HEBU NIPENI POLE na nawatakia mwisho wa wiki mwema.
  Majita.

 4. any Says:

  Kongrats nasreem, umejitahidi kadri ya uwezo wako.

 5. Sikujui Says:

  Yes!!! Nasreem you just take the way of others models.

  I would like to advise the goverment to stop the models system because we didint get anything from this.

 6. sisterTZ Says:

  kwa kweli inabidi tusubiri mwakani..mimi nimeona interview ya miss TZ 2008 kwenye internet..mhhhhhhhhh well no comment..hana kitu kabisa..ila mimi ningesharuri tujiandae vizuri angalau tushinde awards nyingine kama ´talent show´ect nimeona miss kenya ameshinda one of the awards..yaani inaniuma sana mamiss wetu kwa kweli hawana kitu kabisa yaani baada ya Hoyce Temu kushinda ile award ndio hamna tena mwingine yaani si amini..but that is life….hivi kwanini Maria Sarungi asiingizwe kwenye team ya kumtafuta miss TZ mama mimi namuona yeye ana fahamu na choice nzuri..

 7. Pandu Says:

  Nasreem umemaliza kutalii, rudi bongo uje tukumege…maana nyie walimbwende huwa hamna mpya

 8. hombiz Says:

  Uuuups!

 9. binti-mzuri Says:

  sasa mbona majina tofauti.. mara karim mara ndiye! au ndio mambo ya terrorists.mmh..haya tusubiriage tena..sjui 2020?ah tutatoka tu kimasomaso..if nancy could do it..then yeah

 10. Michelle Says:

  Nilijua tu, jibu lilikuwa wazi nje. hongera dada na Nasreem Tz oyeeeeeeeeeeeee.

 11. eve Says:

  Mie toka mwanzo nilijua tunatimiza wajibu tanzania hakuna kitu ubishooo umezidi bora wafutilie mbali mambo ya umiss ushuzi mtupu bora waanzishe miss chaubaya hapo tanzania inaweza kuwa kwenye list ya tano bora hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

 12. Mattylda Says:

  Heee nimechelewa kumuwishia kila la heri Nasrim, anyway usijali hayo ndo matokeo..

  SisterTz naomba nikukumbushe pia tunaye mrembo wa kujivunia NANCY SUMARI aliyetuwakilisha vema mwaka 2005 na alifanikiwa kuingia TOP 6!!

  Kuna kushindwa kama kushindwa, BUT pia uongozi wa MISS TZ na wenyewe jamani sio, its time now wanatakiwa wabadilike, nadhani Maria Sarungi ni mtu makini sana kwenye suala la urembo wangemshirikisha hasa ktk kamati ya Miss Tz ndo tungevuna, unless otherwise kila siku blah blah tupu!!!!!!

 13. COSTA Says:

  issue siyo Nasreem, issue ni waandaaji wetu wa miss bongo, mimi nina wasiwasi na proffesional zao, yaan preparation was very poor, kama vp tuwe ki-proffesional zaidi, dada yangu Nasreem usikate tamaa, yet u can make on the other way around.

 14. johnny Says:

  Nilikuambieni kwamba angella lubala ndiye angeweza kutupa taji lolote huko.

  tatizo la nasreen ni lilelile hana uwezo wa kujieleza na angukuwa angalau amefikia nusu tu ya uwezo wa angela lubala wa kujiamini basi labda ndio angeweza kufanya vizuri.

  mimi sija shangaa kushindwa kwa nasreen,ningeshangaa kama angeshinda kwasababu ana mapungufu mengi tu.

 15. Gervas Says:

  Karibu ila…Mapedejee wa bongo wanakusubiri kama mpira wa kona km kawaida yao kuharibu na vijisenti vyao……. who is next?

 16. any Says:

  ACHENI HIZO ANGERUDI NA TAJI MNGEKUWA WA KWANZA KUMPONGEZA, AKISHINDWA MLIJUA TU~ KWANI NA NANCY MLIJUA ATAFIKA ALIKOFIKA? KOJOENI MKALALE. KHAA.

 17. cityboy Says:

  Nimeona nikusifu, umetoka sexxyy mama!!!

 18. Bob Sambeke Says:

  Hamna kitu! Wizi mtupu! Kaenda Kula hela tu!
  Katika warembo ambao Nawakubari Kwa Uzuri Wa Sura
  Huyu Mtoto Nancy ni Bomba Sana,Sema cpo kwenye system ya EPA kama ningekuwepo ningempa hata Ka-vogue kama Zawadi ili aendelee kuwa mrembo acpigwe na jua ngozi yake isiharibike iwe ivyo ivyo nyororo kama fur!

 19. BLACKMANNEN Says:

  Dahhhh!!! Watu kweli wanakupenda unapokuwa na kitu tu. Shemeji langu la nguvu “Nasreem” kwa Majita, kurudi bila ushindi. Watu imekuwa ni ishu ya kusema hili na lile. Khaaahhhh!!!!! Heri alivyowaambia “any” kwenye comment # 16. Ila “any” hakufafanua wakojoe mkojo upi? Mkubwa au Mdogo?

  Ndugu yangu “Majita”, mimi niko pembeni mwako kukusaidia kubeba zigo la matatizo unayoyapata katika kipindi hiki kigumu. Usipate tabu.

  Nasreem, karibu nyumbani Tanzania ndugu yetu. Wala usijutie kushindwa kwako, kwani katika mashindano yoyote usitegemee ushindi pekee, bali tegemea kushindwa pia. Kitu muhimu ni kwamba, una kwako Tanzania, una ndugu zako wanaokujali, una wapenzi zako wanaokupenda kiukweli.

  Kushindwa kwako mashindano hayo ya U-miss, hakutakufanya ukaishi maisha ya huzuni na ya aibu, kama wanayoishi WEZI wa mapesa ya EPA, akina Mramba na kundi lake. Kwa hiyo, wewe jione uko huru na mwenye furaha. Karibu hapa Blog ya Bongocelebrity uandike japo maneno mawili, ili tuone kama unafuatilia tunayokwambia. Watu wengi huingia hapa kujiliwaza na marafiki zao waliopo hapa.

  Hi Mattylda, binti-mzuri, Pearl, any, sisterTZ, Ndaki, Gervas, Frateline, bila kumsahau Mkuu Majita na wengine – Mpoooooooooo?????

  It’s Great To Be Black……………….Blackmannen

 20. trii Says:

  kwa kweli waandaaji ndo tatizo,nimeona picha yake kwenye internet yani kavaa blazia+sketi,yani blazia kama haimtoshi vizuri,au ndo alikonda akiwa kambini.

  kama hiyo picha hapo juu tofauti ya nywele+sijui banio au weaving kisogoni??hata kama ni weaving basi iwe inafanana na nywele zake isiwe rahisi mtu kugundua.
  ni wakati wa mdada awe ktk kamati ya miss tz yani woteeeee madume.

  kama kuna mtu alipata kumsikiliza Nancy S akiwapa darasa ma miss nadhani 2007 kama sijakosea,alisema huwa
  kuna watu wana waremba lkn alipo rudi chumbani akajitizama kwenye kioo hakuridhika akajifuta na kujiremba mwenyewe,kwa bahati nzuri maria odemba akamfata chumbani kumsalim,akamkuta anahangaika kujiremba,nae akamsaidi.

  kwa ufupi miss anapotoka tz ni vizuri akiongozana na mdada mtaalim mfano Maria Sarungi anakuwa ana msaidia.

 21. kindo Says:

  Eeeh! Sina la kusema…..!Maana hata ukisema au kutoa ushauri hawa Miss Tanzania wenyewe hawakusikilizi…bora liende!!!

 22. jackson Says:

  we any sijui una bahati huyo johnny uliye mtukana hapo juu inaonekana ni mtu aliye ingia mara moja na kuondoka ndio maana haja kujibu.

  lakini sio kwasababu wewe unajikojolea kitandani basi una fikiri kila mtu ndio hivyo hivyo,kwa sababu mimi nakujua tunaishi jirani.

  watu wanatoa maoni yao ya kweli sio ushabiki. ni kweli kwa sisi wafuatiriaji tuna mkubali angella lubala kwa kujiamini kwake na uwezo wa kujieleza.

 23. binti-mzuri Says:

  pole sana majita, and blackmannen hi right back atcha!

 24. halima Says:

  ohhhhh isha kuwa soo

 25. any Says:

  jackson, sijamtukana mtu, ni my opinion,sipendi watu fuata upepo., kama mlijua atashindwa si mngemuambie asiende, hata nancy watyu walimponda weee, aliporudi mkaenda uwanjani kumpokea. and by the way mi huyo angela simjui na sitaki kumjua, so its none of my business! my focus ni kwa aliekuwa Miss, huyo ambae mmeamua kumchagua wenyewe mkiwa bar kwenye stuli ndefu mi sipo.

 26. any Says:

  wee 22, sasa kama john haingiagi huku ndio kakutuma umjibie kwa niaba au wewe unauchungu sana, sikumtukana mtu, matusi hayasemwi yanatendwa upo apo. Alafu tena bora?t
  sisi hatumtambui angela wenu lubala, tunamtambua binti nasreem. waliobaki ni beki tu, hakuna jinsi labda mwakani

 27. msefip Says:

  UREMBO BONGOOOOOOOOOOO!!!

 28. zebraa66 Says:

  yaani kweli ni mzuriii,


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s