BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

HONGERA MWL.ARNOLD CHIWALA December, 30, 2008

Filed under: African Pride,Watanzania Kimataifa — bongocelebrity @ 11:30 AM

chiwala1bc

Wapo watanzania ambao pengine hawajulikani sana miongoni mwetu ingawa mambo wanayoyafanya ni makubwa na ambayo huiletea nchi yetu sifa na heshima kubwa achilia mbali kuitangaza kwa mapana na marefu.

Ni jukumu letu kuwatambulisha kwa jamii pana zaidi na pia kuwapa shukrani kwa mchango wao katika jamii.Ukiangalia sana,kimsingi,watu hao ndio celebrity wa kweli.

Leo tunapenda kumpongeza Arnold Chiwala,mwanamuziki/mwalimu wa Kitanzania anayechukua Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu Cha Muziki Cha Sibelius (Sibelius Academy).Hivi karibuni Arnold ametunukiwa Tuzo ya Dhahabu ya muziki wa Ala ya Kantele 2008. Kantele ni ala ya kiasili ya Finland. Tuzo hii hutolewa kila mwaka na Wizara ya Utamaduni ya Finland kwa mwanamuziki bora ambaye amechangia katika utunzi(composition) na uendelezaji (promotion) wa ala ya Kantele ndani na nje ya Finland.

chiwalabc

Arnold Chiwalala ni muhitimu na mwalimu kutokea Chuo cha Sanaa Bagamoyo. Vile vile ni mwanamuziki, mtunzi, muandishi wa nyimbo na mbunifu wa miondoko (choreographer).

Kazi za Mwalimu Chiwalala zinatambulika kimataifa ambapo ameshiriki katika warsha, matamasha na makongamano sehemu mbali mbali ulimwenguni ikiwemo Tanzania, Zambia, Zimbabwe, Msumbiji, Uingereza, Ujerumani, Marekani, Urusi, Norway, Denmark,Sweden,Finland, Estonia na Yugoslavia.

Hongera sana Arnold.Tunakutakia kazi njema na tafadhali endelea kuwa balozi mzuri wa Tanzania.

Pichani juu katikati ni Mwalimu Arnold baada ya kukabidhiwa tuzo.Wengine ni wakufunzi wa chuo anachosoma Arnold.

Advertisements
 

12 Responses to “HONGERA MWL.ARNOLD CHIWALA”

 1. binti-mzuri Says:

  nice..congrats

 2. hombiz Says:

  Hongera mwalimu A. Chiwala. Nakubali usanii kama wako uliokwenda shule.
  Kanyaga mafuta mtu wangu!

 3. eva Says:

  Hongera zake, lakini akumbuke kupromoti mziki wa tanzania badala ya kantele.

 4. EDWIN NDAKI Says:

  HONGERA SANA MWALIMU CHIWALALA..

  Tuzo uliyopata ni stahili yako kabisa.Kazi zako ni nzuri sana.

  Nakutakia kila jema katika harakati za sanaa na kuitangaza nchi yetu.

  WADAU habari ya siku ya leo..

  Wazima wote..nilipata mgao wa umeme ndio maana nilikuwa kimya..

  tutafika tu

 5. Mattylda Says:

  hongera sana kaka, kila la heri!

  Edwin Ndaki pole na mgao wa umeme rafiki yangu ila missing u so baadddddddddd!

  happy new year!

 6. mr degree Says:

  kazi nzuri,big up!

 7. DUNDA GALDEN Says:

  SAFI SANA CHIWALALA WAKILISHA TAIFA
  LAKINI HUSEIN MASIMBI NA FRANK WAKO WAPI?
  HAKIKA WATU WAMETOKA MBALI

 8. Ndugu yangu Chiwalala hongera sana kuutangaza mziki HALISI WA TANZANIA,wewe haswa ni BALOZI wa Tanzania Music ao MISIONARI unaye fundisha Mziki wetu kwa Wazungu,kama wao walivyo tuletea Dini la Kikristo,God bless you

 9. BLACKMANNEN Says:

  Hongera Arnold, lakini mimi bado nina wasiwasi na Elimu yako, maana tuzo hili ni la vitendo katika mambo ya sanaa. Nitashukuru na kujisikia vema kuwa baada ya wewe kumaliza darasa lako la saba hapo Lugalo, uliendelea na sekondari?.

  Najua tangu miaka ya 1991, wataalamu wa muziki na maigizo kutoka Sweden, wamekuwa wakiwasaidia sana hapo Chuo Cha Sanaa Bagamoyo vijana wote waliokuwa wakijishughulisha na sanaa ya muziki Tanzania. Elimu ya Vitendo katika sanaa na Nadharia ya sanaa, ni vitu tofauti kidogo. Moja kati ya hayo ni rahisi kuliko nyingine.

  Tanzania, tumeshawahi kuwa na maestro, Mayagilo wa Police Brass Band. Mayagilo hakuwa na elimu ya juu ya nadharia ya muziki, lakini, alikuwa na hiyo Elimu ya vitendo ya Muziki kama hiyo uliyopewa tuzo wewe huko Finland. Lakini pia, alifanikiwa kutunga na kuimba nyimbo zote za dunia.

  Kinachotakiwa katika sanaa, ni kuwa na Elimu zote. Elimu ya nadharia na Elimu ya vitendo. Hapo utakuwa na eneo kubwa sana la kuwaelimisha Watanzania katika sanaa. Vinginevyo, utakuwa sawa na akina Mwinamila, Makongoro au Mayagilo. Ambao kwa sasa hivi kwa Tanzania, wanahesabika kuwa ndio Waasisi na Viongozi mashuhuri wa ngoma za kitamaduni za Tanzania.

  This Is Black=Blackmannen

 10. Frateline Says:

  Hi Guys

  Bravo, ninakupongeza maana hiyo ni hatua kubwa sana umepiga ktk maisha, sasa ninakushauri kumbuka kurudi Tanzania ambao hiyo Elimu yako wanahitaji sana kuliko huku Finland,

  Asante mwalimu umewakilisha

  Nakutakia mwama mpya mwema

  Frateline

 11. Dinah Says:

  Hongera Mwalimu!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s