BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

SIKUKUU ILIKUWAJE? December, 30, 2008

Filed under: Burudani,Sikukuu,Swali kwa Jamii,Zilipendwa — bongocelebrity @ 11:54 AM

comedi-orijinobc

Naam!Xmas kwa mwaka 2008 ndio imeshaisha.Kwa bahati mbaya siku kama hizi huwa hazirudi tena.Ilivyokuwa Xmas mwaka huu sivyo itakavyokuwa mwaka ujao na mingine itakayofuata.Ulipokuwa mwaka huu si ajabu hutokuwepo mwakani.Ndio maana huwa tunasisitiza kwamba Make The Most Use of It when/whenever you can(nimetia kizungu hapo kuonyesha msisitizo).

Najua wengi wenu bado mpo kwenye hali ya sikukuu.Wengine nasikia bado wanatibu mning’inio wa ziada(hangover).Kwa wengine huu ni wakati wa kutafakari jinsi matumizi yalivyokwenda.Ni wakati wa kukagua risiti huku macho yakiwa yamekutoka na simanzi likiwa limetanda usoni.Usijali,ndio maisha.Si ushasikia ule msemo usemao Ponda Mali kwani Kufa Kwaja?Sasa?

Lazima pia nikiri kwamba hata sisi wenyewe tupo kwenye holiday mood bado.Ndio maana mwendo kidogo unakuwa taratibu ingawa sio kama wa kinyonga.Bahati nzuri hatubadiliki rangi pia.Tunajongea huku tukiandaa mambo makubwa zaidi kwa ajili ya mwaka ujao ambao kimsingi tunataka uwe mwaka wa BC!

Sikukuu ilikuwaje?Uliserebukia wapi?Mambo yalikwendaje?Tungependa kusikia kutoka kwako msomaji.Wakati unatafakari jinsi sikukuu ilivyokwenda,hatungependa kukuacha hivi hivi.Burudika na wimbo Ndoa Fungo la Imani kutoka kwa Bima Lee.Pata burudani


Tumeshindwa kupata maelezo au caption ya hiyo picha.Unaweza kutusaidia?

Advertisements
 

17 Responses to “SIKUKUU ILIKUWAJE?”

 1. Majita Says:

  BC athante ama avacha kwa kichina kwa hii picha na kupiga kimombo.Uwe una kandamiza bwana kiingilishi,si unajua ndo kimefanya mimi nikapewa Phd?????

  Caption ya picha iko hapo kwenye kufungua soda hapoooo.
  Yaani hapo ndo penyewe.Mengine tisa ila kumi hilo kopo lilivyoshikwa na kufunguliwa hope yataandikwa mengi.bwaaaaa hahahahah.
  Either Heri ya mwaka mpya ndg zangu woote hapa BC
  Dr.Majita

 2. hombiz Says:

  joyous

 3. papuu Says:

  dah naona huyu mpoki anabonyeza kizenji.. mashallah

 4. Mattylda Says:

  mimi make up za mpoki ndo zinanimaliza khaaaaaaa!

  wishing u all a happy new year!

 5. viola Says:

  mbona mwashangaza watu na yote uloyasema ni kweli dhahiri

 6. DUNDA GALDEN Says:

  HOME SICK
  SIKUKUU ILIKUWA SAFI
  JÄTTE FIN SOM FAN

 7. rasto Says:

  bc jina la wimbo kama sijakosea ni Ndoa ni fungo la hiari.ni burudani safi la wana magnet tingisha.x-mas ilikuwa poa tu labda leo.all the best katika mwaka mpya wadu wote.iwe ya mafanikio mema na afya njema

 8. BLACKMANNEN Says:

  “Roy”=Rweyemamu, niliwahi kuimba naye katika moja ya bendi za hapo Dar, ni mwimbaji mzuri sana. Aliiacha kidogo Bimalee na kujiunga nasi katika bendi yetu. Baada ya hapo alirudi tena Bimalee na alitunga na kuimba ule wimbo wa “Sophy”.

  Black=Blackmannen

 9. binti-mzuri Says:

  jamani blackmanen kumbe we musician.. i always knew there was something about you..tukumbukane basi lool

 10. FIFI Says:

  SKUKU ILIKUWA SAFIIIIIIIIIIIII SANA.
  NAWATAKIYA WANAINCI WOTE UYU MWAKA UWE WA KHERI NA AFYA NJEMA:

 11. Mattylda Says:

  Blackmannen kumbe unaimba?safi sana kaka mimi natamani kuimba ila sina sauti ya kuimbia!

 12. angel jk Says:

  huyo mpoki angebadili mekups coz watoto wanaogopa

 13. Mwanamke wa shoka (UK) Says:

  hizo make-up zao zimeniacha mbavu sina…(teh teh teh…)….nakipenda saana kipindi chao hao mabwana…kuna wakti kulikuwa kunatokea kama coincidence hivi…kwani kila kipindi kikikaribia umeme unakatika….not sure if it was a black out in all places…or what…whether a planned one….not sure….ila nondo zao kali….wana ujumbe mzito kila wakati…lol

 14. bugi Says:

  sikuku muhimu lakini tusije tukasahao sababu ya kuisherehekea

 15. cityboy Says:

  Mmmmm!! Mattylda wacha longo longo!!!nimekusia ukiimba kule uwani!!! unasauti nzuri bana!!!hahahaaaaa

 16. cityboy Says:

  Mattylda, yaaaaani ndo tuseme make up za Mpoki zimekua hoi bin taabani!!!, hahahahaaaaaa!!!!!

 17. Mattylda Says:

  Cityboy cityboy visa hivyo ninaimba uani kivipi??fafanua hahahahaha,nakwambia mimi make ups za mpoki sina usemi utadhani anataka kukata roho hahahahah!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s