BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

HAPPY NEW YEAR! December, 31, 2008

Filed under: Editorial,Sikukuu — bongocelebrity @ 11:21 AM

header1

Hatimaye siku 365 za mwaka 2008 zimefikia ukingoni.Ninavyoandika ujumbe huu tayari kuna sehemu mbalimbali za dunia ambapo tayari sekunde za mwisho za mwaka huu zimeshahesabiwa na tayari takwimu mpya zimeshaandikwa.Kwa maana hiyo leo ni mwaka mpya. Kwa heri mwaka 2008 karibu mwaka 2009.Kwa wengi leo huwa ni siku nzuri kwa maazimio mapya ndani ya matumaini mapya.Kwa jinsi hali ya uchumi duniani ilivyoishia mwaka tunaoupa kisogo,basi sio ajabu kwamba malengo ya wengi ni kulinda zaidi mifuko yetu kwa kuwa makini zaidi na matumizi hesabu za mapato na matumizi na pia kulinda zaidi kazi zinazotuingizia kipato.Nakutakia kila la kheri katika hilo.

Bila kujali hali ya kiafya,kiuchumi,kisiasa wala kijamii, ukweli kwamba mwaka mpya umewadia huku wewe na sisi sote hapa BC tukiwa hai, ni jambo la kufurahia na kumshukuru Muumba.Ukivuka mwaka unakuwa umeandika historia mpya katika maisha yako. Vitabu vya kumbukumbu vitaandika kwamba uliuona mwaka 2009! Ni jambo la kumshukuru muumba kwani ni wazi wapo wengi sana waliotamani kuuona mwaka huu na wasifanikiwe.Kama huamini, fikiria kidogo tu ni watu wangapi ambao umehudhuria mazishi yao au kusikia habari juu ya misiba yao?Unaona? Hatuna budi kumshukuru Mungu.

Wakati huu tunapoingia mwaka mpya wa 2009,tungependa kwanza kukutakia kila la kheri wewe msomaji,mtembeleaji au mchangiaji wetu.Mwenyezi Mungu akuongoze na kukubariki katika kila jambo utakalolifanya ndani ya mwaka huu wa 2009.Kama mwaka 2008 haukuwa wenye mafanikio kwako au haukutimiza malengo yako,usikate tama.Fungua ukurasa mpya huku ukiwa na fikra chanya zaidi na utaona mabadiliko.

Tungependa pia kukupa shukrani zetu za pekee kwa kuwa mtembeleaji,msomaji au mchangiaji mzuri wa BC.Kama kuna mafanikio yoyote ambayo tumeyapata tangu kuanzishwa kwa blog/site hii,ni wazi kabisa kwamba mafanikio hayo yametokana na mchango wako wewe msomaji,mtembeleaji na mchangiaji wetu.

Shukrani nyingi ziwaendee celebrities mbalimbali ambao bila maringo,kinyongo wala ngendembwe walikubali aidha kufanya nasi mahojiano au kutokuwa na kinyongo nasi pale tulipoweka picha zao na kukaribisha mvua ya maoni kutoka kwa wasomaji huku wengine wakiwa chanya na wengine hasi.Celebrities kama hao wanakuwa wametambua vyema nafasi au mchango wao katika jamii.Wametambua pia kwamba haiwezekani kuwa bondia ulingoni halafu ukawa unaogopa ngumi za uso.Tunawashukuru na kuwaomba tuendelee kushirikiana.

Shukrani za pekee ziwafikie bloggers wenzetu mbalimbali,vyombo mbalimbali vya habari ndani na nje ya Tanzania,wapiga picha mbalimbali na wengineo wote ambao wanaendelea kushirikiana nasi katika jukumu hili zito la habari na mawasiliano.Asanteni sana.Bila ninyi,haiwezekani.BC inathamini sana mchango wenu.

Kama binadamu inawezekana kabisa kuna wakati tunatokea kutoelewana au hata kukwazana.Bila shaka hata sisi hapa BC inawezekana kuna wakati tulikukwaza.Yawezekana hatukuweka maoni yako kwa sababu moja au nyingine,yawezekana tulichelewa kuruhusu maoni yako yaonekane,yawezekana wewe ni celebrity na tuliruhusu maoni ambayo kimsingi uliona kama umetusiwa nk.Mifano ipo mingi.Lakini kwa wote hao,tunaomba samahani.Yote hayo ni katika kujitahidi kuitenda vyema kazi yetu.

Tunapouanza mwaka mpya wa 2009,tunakusihi uendele kututembelea,kuchangia,kutukosoa tunapokosea na pia kumwambia mwenzako kuhusu uwanja huu ili naye asipitwe na yanayojiri.Tunakutakia kila la kheri.HAPPY NEW YEAR 2009.

Advertisements
 

20 Responses to “HAPPY NEW YEAR!”

 1. BLACKMANNEN Says:

  Ahsanteni sana BC kwa maneno yenu mazuri ya kuumaliza mwaka 2008 na kuukaribisha mwaka 2009. Mimi pamoja na wale wote wenye fikra kama zangu, tunawashuruni sana kwa kutuleletea blog hii. Maana nimepata marafiki wapya wenye mawazo mapya na yaliyoenda shule kupitia hapa.

  Naomba tuendelee na mshikamano wetu wa Kitanzania, katika majadiliano, maoni na maelimishano endelevu katika kijiwe chetu hiki.

  Krismas ilienda vema kwangu, ni mategemeo yangu pia wengi wetu ilienda vizuri. Kama kuna mtu haikuwa hivyo, ni bahati mbaya, ilikuwa ni mipango yake Mwenyezi Mungu.

  Mimi pamoja na marafiki zangu wanaoniunga mkono katika maneno yangu haya, nawatakia kila la kheri katika mwaka mpya wa 2009. Mungu asikilize sala zenu, zifanikiwe kama mnavyoomba. Nawatakia Afya Njema na maisha marefu yenye furaha. Happy New Year 2009!!!!!

  It’s Great To Be Black=Blackmannen

 2. Mama wa Kichagga Says:

  BC

  Tunamshukuru sana Mungu kwa kutuweka hadi mwaka huu mpya wa 2009. Ni wengi walipenda kuuona Mwaka 2009 lakini hawakubahatika kuipewa zawadi hii kama wewe na mimi.

  Tusameheane kwa yale yote yaaliyotukwaza 2008 na tudhamirie kuwa na mitizamo na mawazo chanya ya kujenga ndani ya mwaka 2009.

  Zaidi sana tumuombe Mungu awape hekima ya pekee viongozi wetu katika ngazi zote za utendaji ili waweze kufanya na kutoa maamuzi ya kizalendo na yakujenga zaidi nchi yetu nzuri. Pia afukuze zile roho zote za ubinafsi, uchoyo, chuki, ukabila, udini na ufisadi ndani ya jamii yetu na awape watoto na wajukuu wetu mwanga na ufahamu wa kutenda mema.

  Tanzania bila umaskini inawezekana – Tutimize wajubu wetu na tujibidiishe katika kazi mimi na wewe na wengineo wote.

  HERINI YA MWAKA MPYA 2009 WANAFAMILIA YA BC WOTE – TUMEJALIWA KUUONA!

 3. DUNDA GALDEN Says:

  NAWATAKIENI KHERI YA MWAKA MPYA WADAU NA WAPENZI WA BONGO CELEBRITY KOKOTE MLIPO DUNIANI
  MATTYLIDA,BINTI MZURI BLACKMANNEN.MAMA WA KICHAGA NA WENGI WENGINEO SIKUWAANDIKA
  AMANI KWENU MWAKA UWE WA MAFANIKIO AMINI

 4. any Says:

  kwani mwaka tiyari, huku china bado kabisaaaaaaaaaa

 5. watubwana Says:

  watu bwana,nashukuru MUNGU kwa kuuona huu mwaka sababu wapo waliopenda fika mwaka huu ila hawakuweza fika.nashukuru kwa waandaaji wote wa blog hii na wachangiaji.nashukuru sana.
  twende kazi mwaka ndio umeanza huo…

 6. binti-mzuri Says:

  thanx dunda.. happy new year to all BC members. mwaka umeisha,and now am stuck with the reality of life..back to work.

 7. Mh.Dr Madman (phD) Says:

  Nimechaguliwa tena.binti-mzuri ninavutiwa sana na jina lako.Nina imani kuwa u mzuri kama jina lako.Heri ya mwaka mpya.Kwa upande wangu naona mambo ni yaleyale tu.

 8. Mwanamke wa shoka (UK) Says:

  ohh!!!…ndio tunauanza mwaka 2009….(naona mwandishi ameturusha hadi kufikia mwhisho wa 2009!!!!!!!!!! ((…first line…sixth word…!!!)….YOooote heri…!!!!!!!!!

  Niwatakieni mwaka wenye baraka , upendo, AMANI na afya tele……(amin)

 9. Mattylda Says:

  Asante BC, happy new year na nyie pia NA WADAU WOTE WA bc!!!!!!!!!!!
  Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunifikisha 2009, ni wengi walitamani kufika kwakweli lakini ilishindikana.
  Tuanze mwaka kwa malengo yenye amani,upendo,furaha na kujituma zaidi!!!
  Asanteni sana Dunda, mama wa kichaga,Binti mzuri na mwanamke wa shoka…tuko pamoja!

 10. kindo Says:

  Heri ya Mwaka Mpya wapenzi wote wa BC. Mungu wabariki BC na mashabiki wake, Mungu ibariki Tanzania.

 11. Lalola Says:

  Happy new year wana BC wote. Have a blessed 09.

 12. hombiz Says:

  Uongozi wa BC na wadau wote, nawatakia kheri ya mwaka mpya uliosheheni mafanikio ktk ndoto ya kila mmoja.
  By the way, according to Albert Powell, the top 10 New Year’s Resolutions are:
  1. Spending more time with family and friends
  2. Fit in Fitness
  3. Tame the Bulge
  4. Quit smoking
  5. Enjoy life more
  6. Quit Drinking
  7. Get Out of Debt
  8. Learn Something New
  9. Help Others
  10. Get Organized
  Kuna inayomgusa mdau yoyote!?

 13. binti-mzuri Says:

  haha Mh. Dr. Madman hongera kwa kupata awamu ya pili..na asante.lol mimi hombiz kuna lililo ni gusa kuroho hapo..ila i doubt we ever stick to our resolutions,so i’ll just shut up

 14. kahindi Says:

  any…haha haha…nimecheka sanaaaaaaa….

 15. kahindi Says:

  hombiz no 7 imenigusa….tel me how?

 16. hombiz Says:

  Binti-mzuri try your best sticking to your resolution, remember “YES YOU CAN!

  Kwa upande wako kahindi i believe-” YES YOU CAN TOO!”
  Nionavyo mimi, itabidi uzingatie zaidi matumizi ya fedha kwa umakini mkubwa. Ningeshauri tumia fedha zako kwa matumizi yaliyo ya lazima zaidi na pesa nyingine zote zielekeze kwenye kulipa deni ulilonalo, hasa kama ni la credit card!
  Natamani ningekuwa nna uwezo wa kukusaidia kwa hilo, lakini na mimi nachechemea ndugu yangu. Labda tumuulize ROSS, mtoto wa masaki kama ana jeuli ya kupiga jeki kidogo. Dr Majita sidhani kama ataweza kwani ameshabainisha kuwa sikukuu zimemchapa hadi mifukoni vibaya mno, na sasa anaugulia maumivu.

 17. kahindi Says:

  hombiz shukrani…lakini,mhh cjui,kwa usawa huu?i doubt.

 18. hombiz Says:

  Kahindi Ingia hapa kisha download hiki kitabu cha suzie Orman kuhusu utunzaji wa fedha. Ni kitabu kizuri kwakweli. Ametoa muda mchache sana wa ku-down load kitabu bure
  http://www.oprah.com/article/oprahshow/20081119_tows_bookdownload
  Good luck

 19. kindo Says:

  hombiz…umenichekesha especially resolution No. 3…he he he

 20. watubwana Says:

  watu bwana,siri ya mtungi aijuaye ngata…tunashukuru MUNGU tumeuona huu mwaka…HERI YA MWAKA MPYA KWA WATU WOTE.
  NAWAOMBA JAMANI WENZANGU:-
  1)tuwe na ma
  wazo ya kujenga zaidi kuliko ya kubomoa
  2)utani sio mbaya,ni mzuri ila usipotoshe maana ya hii blog
  3)tuwe tunatoa mawazo ya kuendeleza jamii na sio kuponda tuu kuponda hadi mwisho.PONDA,ELEWESHA,FUNDISHA.
  4)leteni mawazo yanayoweza kumjenga mtu,watu,kufundisha.kumuinua mtu,kumpa njia za kumletea maendeleo zaidi na zaidi sio kupondana saaana,utani uliokithiri na nk.
  asanteni.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s