BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

HARD BLASTERZ KUZALIWA UPYA? January, 1, 2009

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Muziki — bongocelebrity @ 7:44 PM

hbc1

Bila shaka unalikumbuka kundi maarufu la Hard Blasterz Crew(HBC).Hilo ni mojawapo ya makundi ambayo tunaweza kabisa kusema yalichangia kwa kiasi kikubwa kuuweka muziki wa kizazi kipya hapo ulipo.Sasa kuna habari njema ambazo zimeripotiwa na Full Shangwe kwamba huenda mwaka 2009 ukashuhudia kurudi kwa kundi hilo baada ya miaka kadhaa kutokuwepo hewani ingawa mwenzao Prof.Jay aliendelea na game kwa muda wote huu.

Kundi lile lilikuwa linaundwa na Joseph Haule aka Prof.Jay,Willy Shundi aka Big Willy na Terry aka Fanani lilikuwa na makazi yake maeneo ya Upanga jijini Dar-es-salaam.Tunawatakia kila la heri HardBlasterz.BC itaendelea kufuatilia maendeleo ya kuundwa upya kwa kundi hilo.

Pichani juu kutoka kushoto ni Big Willy,katikati ni Profesa Jay na kulia ni DJ Choka ambaye ni mmojawapo miongoni mwa producers wanaotarajiwa kuwatoa upya HBC.Kwa undani wa habari unaweza kubonyeza hapa.

Advertisements
 

16 Responses to “HARD BLASTERZ KUZALIWA UPYA?”

 1. Dinah Says:

  Sio mbaya kujaribu zali, si mnajua maisha ni kuchukua risk, kama kundi haliku-hit those years nini kimebadilika 2009?

  Nionavyo mimi ni kuwa Prof J rudi kundini kwa muda ili uone itakuaje (isije ikawa ile kitu ya kukutumia kwa vile umefanya vizuri kwa muda mrefu, so kundi will sell copies b’coz Prf J yumo)…..yote kwa yote nadhani Prof J uko fit on ur own…u should keep that way 🙂

  Kila la kheri!

 2. Bob Sambeke Says:

  Da c mchezo nakumbuka mbali miaka ya 1999-2000,HBC mambo ya “KUBWA KULIKO” kama itarudi poa aina Kwele,ila wakirudi wawe Pamoko wactengane tena kwani inavyoonekana FANANI kachoka ndo maana Prof.J akamuimba kama msanii wa kweli kwanini ufe na Njaa(Mtazamo).

  1.chemshabongo
  2.mamsap
  3.kubwakuliko
  4.niamini

  Jipangeni Je mtaweza Kuvipiku hivyo Vibao? Au mmekuja Kuuza NYAGO ili muuze album zenu(Prof.J)

  Happy New year! 2009!

 3. hombiz Says:

  Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. Nawaaminia watu wangu! Jay, Simba na Terry vichwa makini. Kamateni tena 2009. Nawapa baraka zote.

 4. papuu Says:

  hivi haya mashati ya hi hater ndiyo yametoka bongo nini naona kila mtu anayavaa mpaka kero sasa mara profesa jay mara mwana fa no offense ila sasa wamezidisha

 5. Ebwana mwake! yaani mzuka kikweli kweli coz what im expecting is what i used to feel in those years when they were conquering stage! Unajuwa washkaji walibamba haswa miaka ile 2000-2001 washkaji walikuwa juu zaidi ya wote hapa Bongo simchezo nakumbuka sana! BOB SAMBEKE amejaribu kuorodhesha baadhi ya Track! ile albam ilisimama haswa yaani track zote sio siri! Kuna track ile FANANI, wanasema ni nani Fanani wa uhakika kwenye fani anasikika akishika mic ni patashika! Kweli jamaa walikuwa wakishika mic ni patashika kweli! .Hey guys you’re welcome back!

 6. mdau Says:

  big up guys wishing you all the best 2009!ila kazeni si mnaona underground wanakuja kwa kasi ya ajabu!

 7. kahindi Says:

  kwako professor j…thamani ya huo mnyororo ni kubwa sana….sijakusikia hata cku moja umesaidia watoto yatima au wagonjwa hospitalini,,,unaonaje kama ungetumia at least robo ya pato lako kwa kuwapa watoto yatima?kuliko kuvaa mnyororo kama huo shingoni?…wadau ni mawazo yangu tu…

 8. kisiio Says:

  wewe mdau kweli hayo ni mawazo yako tena finyu,badala ya kuomba mafisadi yatoe hela kwa yatima unakuja kuyayapa profesa j atoe kwa yatima wewe unajua jinsi gani wassanii wa bongo flaver wanaranguliwa huko bongo hawa wote choka mbaya hilo limnyororo unaloliona la thamani ni la kuchovya

 9. Ebwana HBC ilibamba sana na tunaitakia kila kheri!

 10. kahindi Says:

  kisiio….nimekupata?je unataka nikujibu?

 11. cityboy Says:

  Kisiio, mbavu yangu imebakia moja tu, usijeukaimaliza!!!hahahaaaa

 12. ramona Says:

  ha ha ha at commentator number 8

 13. binti-mzuri Says:

  hey bob sambeke thank you kwa kutukumbusha..i liked that song mamsapp,nipoze roho mama,nimechanganyikiwa na penzi lako la mahaba..mapenzi si upweke,mapenzi sijui nini nini

 14. mzawa wa upanga Says:

  we dinah kweli haujui kabisa hardblaster eti kundi alikufanya vizuri nini.hardblaster walianza kwa kutaalifa yako muziki kabra prof jay hajulikana ni prof j mwenyewe ndio aliomba ajjiunge na kabra jay hajaingia kundini hardblaster walikuwa willy,telly,frank na wengine 2 na wakachukua ubingwa wa rap prof jay alikuwa hayumo umesikia useme tu prof jay aliongeza nguvu zaidi nakundi kufa ni jambo la kawaida hata marekani kutakuwa na mtu mmoja ambae atatoka kimziki kushinda wenzake

 15. mzawa wa upanga Says:

  unajua hardblaster ilianza tangu miaka ya 1991 wakati huo wako marafiki 5 ambao ni willy,telly,frank,ngida na tuff jam wakati wanatamba na vibao vyao kama twapendeza,mambo ya mjini,cheka nao huyo prof jay alikuwa hayumo na ajulikani kabisa baada ya tuff jam kwenda usa na frank kwenda london na ngida kuachana na music ndio prof jay akajiunga lakini hardblaster ilikuwa na mafanikio makubwa tu ukitaja makundi kama gwm,kwanza unit,da young mob nk lazima mtu alikuwa anafatilia rap ya kibongo atasahau kulitaja kundi la hardblaster kwahiyo kusema kwamba hardblaster alikuhit ni ukilitimba uliza ujue sio unasema vitu ambavyo vinauzi watu

 16. hombiz Says:

  mzawa wa upanda usisahau kuwa hard blasters walimsaidia sana Too Proud a.k.a Mr Two, a.k.a. Sugu, ktk kukulu kakala zake za fani. Ile nyimbo ya Mr 2 iitwayo-” ni mimi”-niko kwenye microphone, hata unipe nini sitamani sioni”, ilifanyiwa chorus na Terry wa Hard Blasters!
  Dinah! Leave HBC alone!, hawa jamaa hawabahatishi. Ni wakongwe wa fani. They always come out with the real stuff. And if they bring a new Album out, i bet you it is gonna HIT again!
  Receive all my blessings HBC


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s