BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

WAPI BESTA? January, 4, 2009

Filed under: Bongo Fleva,Burudani,Muziki — bongocelebrity @ 6:15 PM

bestabc1

Msomaji wetu mmoja ametuandikia akitaka kujua alipo mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya,Besta(pichani) kwani hajamsikia kwa muda mrefu.Ukweli ni kwamba hata sisi hatuna jibu la uhakika ingawa fununu tulizonazo ni kwamba Besta alirejea nchini Uganda kumalizia masomo yake aliyokuwa ameyakatisha.Alikuwa anasomea masuala ya Habari na Tekinolojia.Besta aliwahi kutamba sana na wimbo wake Kati Yetu ambao unaweza kuutizama kwenye video hapo chini.Kama kuna mtu ambaye ana habari za uhakika zaidi,tusaidiane tafadhali.


Advertisements
 

30 Responses to “WAPI BESTA?”

 1. cityboy Says:

  Jamani makwapa hayo!!!!!,yaaaani we acha tu, hahahaaa!!!!!!!!

 2. domo kama upawa Says:

  duh mtoto mswafi hadi raha kwapa nyeupeeeeeeeeeee utafikiri za baby huyu nilimuona wakimuhoji star tv ila ana albamu yake sijui inaitwaje vile kawashirikisha watu kibao.

 3. Mwanamke wa shoka (UK) Says:

  teh teh teh…..”City Boy” na “Domo kama upawa” ….mmenifurahisha…
  Happy New year to all of you at BC

 4. kahindi Says:

  mi mgongo tu….kajaliwa jamani…..ila style ya nywelwe cjaipenda….wadau wenzangu kina bint mzuri,,matyy,hombiz na wengine wengi,nawapa hi sana….nimewamissss….

 5. mchangiaji Says:

  Jamani msidanganywe na teknolojia ya picha huyo Dada hapo juu si kweli kwamba ana kwapa laini huyu demu namjua sana hapo imetumika ile kitu inaitwa PHOTOSHOP inayokuwezesha kuonekana soft as natural. Ila kzi yake imetulia kimziki.
  Amkeni kutoka ktk usingizi.

 6. DUNDA GALDEN Says:

  Baadhi ya nyimbo zake nzuri sana

 7. Dinah Says:

  Tena sio yeye tu, Ray C, Keisha, Kwini Doreen. Tunaupungufu mkubwa wa wasanii wa kike wa muziki wa kizazi kipya ukilinganisha na wanaume……Mwasiti na Jide wanajitahidi kuwepo mchezoni.

  Hivi yule Mshindi wa Bongo sachi 2008 nae kaishia wapi? Hata singo bado au mimi ndio sijaipata??

  Heri ya mwaka mpya wapendwa!

 8. kisiio Says:

  unamjua??? mdau wa hapo juu unamjuaje jamani au ndio umbea huu

 9. Mattylda Says:

  cityboy na domo kama upawa makwapa hahahahahaha mimi hoi!!!!!!!!!!
  pamoja na maphoto shop mnayosema ila ukweli utabaki pale pale mtoto softiiiiiiiiiiiiiiiiiiii kiuno bila mfupa huyu sijui sasa tumforwadie nani?miongoni mwa kaka zangu wa hapa BC,anyway ngoja nitafakari kisha nitarudi kuwapa jibu!
  Kabla sijatoka nishapata jibu,Bob Sambeke kifaa hicho nimekuchagulia teh teh teh teh

  Kahindi bibie karibu tena ulikuwa wapi shosti???

 10. Gervas Says:

  Cityboy na wewe Mchangiaji, mbona mnakuwa haters tu pasipo msingi? mara kwapa, mara sijui sio soft? nyie hamna kwapa? au nyie mko soft? mbona kila mtu anamapungufu yake? jinsi alivo siye tunamfuagilia, wabongo(Africans) wengi hatupendi vyetu, maanake ni nadra sana kukuta wezetu wanapondeana pasipo msingi. Ni lini hasa tutajikubali jinsi tulivo na kusema kuwa we are beautiful/handsome? JAMANI, wadau woote wa BC nafikiri mambo hayakuwa mabaya saana katika kuupokea mwaka mpya, Mattylida, Blackmanen na wengineo asanteni kwa salaams!!!

 11. binti-mzuri Says:

  mh binti mzuri jamani huyu

  kahindi shosti welcome back

 12. kahindi Says:

  mashost wenzangu…mattyida na binti mzuri…nilikuwa kijijini vumari same…..c mnajua tena maswala ya mitambiko ya mwisho wa mwaka?….nimerudi full gado.kujiachia kwa raha zangu….mattyida,pole nimeona umelalamika mdau mmoja kakuibia jina lako…jamani mbona majina yapo mengi tu ya kujiita,why lakini….mimi cjapenda….pole bibie…

 13. domo kama upawa Says:

  Gervas soma vizuri comment zetu hakuna alikandia hapo.

 14. cityboy Says:

  Tulikua tunaulizana apa ni nani huyu!! haaa!! kumbe ni wewe Binti mzuri!!!!, sasfiiiii, hahahaaaaa!!!!

 15. Talib Kweli Says:

  we Maty nifowadie mimi,kitoto ‘kitamu’ hiki jamni loh!

 16. any Says:

  kaka Gervas mi kwa mtizamo wangu, naona kama umemkoti citiboy vibaya, Citiboy alivo navomfahamu tangu Dhb, sidhani kama kaponda, mi naona kama amemsifia mdada wa watu kuwa ana kwapa swafi kuwa anajua usafi binafsi, Vinginevyo citiboy njoo apa ukanushe nilivoona mie.

 17. binti-mzuri Says:

  hahahaa city boy umeniacha hoi!..sio mimi huyo,sema ni mwenzetu tu..mzuri na anajitambua,au nakosea… ndio 2009 hii..upo

  kahindi shostito mbona umerudi mikono mitupu wajameni, hebu tupe vya huko vumari .. happy new year to you

 18. chapombe Says:

  tatizo mnakimbia kujibu swali,mmeambiwa anayejua alipo abaelezee.sasa mmeanza kummaliza kijinsia,hoo makwapa,hoo kiuno…mweh,wajameni mbona mnakuwa hivyo,hivi hiyo picha kama ingekuwa ya lidume limenyoosha mikono juu hapo,macho yenu yengelenga kwenye kwapa?

 19. BLACKMANNEN Says:

  “Besta,” ni msichana aliyejaliwa vitu vingi. Sio kwa kipaji cha usanii pekee, bali pia ikiwa ni pamoja na sura yake, iliyoshehenezwa na umbile lake lisiloelezeka kwa uzuri, likisindikizwa na mtazamo wake wa macho ya huba, na mengine mengi nabakiza kuyasema!!!!

  Ndugu zangu wana BC, katika salaamu zetu za mwaka mpya, tulisema tuuanze mwaka na mawazo mapya “ENDELEVU” kwa kila mmoja wetu.

  Je, mawazo hayo hapo juu, yanaweza kumwendeleza vipi msanii wetu “Besta” katika harakati zake ngumu za kisanii? Maana kubwa ya kuletwa hapa BC “Ma-celebrities” wetu, ni kuwapa nafasi ya kujielewa nafasi zao kwetu sisi wapenzi wao.

  Hakuna kosa katika kumsifia mtu kwa kile alichopewa na Mwenyezi Mungu, k.m. kipaji, sura, mawazo yenye busara n.k. Hiyo itakuwa tunampa moyo aendeleze kitu hicho kinachowafurahisha wengi. Pia sio mbaya kama tutamchambua makosa yake kwa nia njema ya kumwendeleza na siyo kumdhalilisha. Utani kidogo pia unaruhusiwa.

  Lakini sisi wachangiaji tunapojikita kuchangia kitu kisichoendeleza kama mnavyoona Comments # 1-5 na zingine. Tunapoteza nafasi nzuri sisi wenyewe Watanzania, wachangiaji pamoja na wahusika (Celebrities) ya kuendelezana kimawazo. Pia kupoteza maana nzima inayokusudiwa na “Blog” hii.

  Beyonce anakwapa safi na kiuno kizuri, lakini Wamarekani ikiwa ni pamoja na Watanzania wenzetu wapenda kusifia Wamarekani, sijawaona wakijadili kitu kama hicho tunachokijadili hapa kwa “Besta” wetu.

  Ushauri wangu kwa “Besta” ni kwamba, akaze buti kweli kweli katika shughuli zake za kisanii popote alipo. Asitegemee kupata mawazo endelevu kutoka popote. Kila mtu anajali maisha yake, na hasa sisi Watanzania na maneno yetu mengi, kama anavyoona hapa nilivyoandika maoni marefu mchosho.

  Kazi kwako Bob Sambeke Mattylda kakuchagulia chombo, comment # 9. Thanks Gervas, comment # 10, mimi najikubali kuwa “Black”, na ninajivunia saaaaaana rangi yangu hiyo.

  It’s Great To Be Black=Blackmannen

 20. kahindi Says:

  bint mzuri….havache…to you to….huko vumari ni maboga na msele tu(mboga flani hivi,unakula na ugali,inatelezaaa…)vinginevyo namshukuru mungu kunilinda mwaka jana wote,na kuniwezesha kuiona 2009,wana bc wote nawatakia heri mwaka mpya,tukaze boot,kazi ndo kwanza inaanza….changieni kwa sana bila kuhide anything…na mkumbuke UCHAGUZI 2009 ndio huo hapo usoni…change we need au vipi?

 21. Mattylda Says:

  Kahindi bibie ok, karibu tena, ndo maana sikukuona zhong garden teh teh nakwambia ulimiss mengi mpaka kuibiwa jina langu asante mwaya!!!!

  Talib kweli, don worry warembo wanazaliwa kila siku wako anakuja tu this time lazima nikuchagulie kifaa cha uhakika.

  Chapombe bwana una visa wewe khaaaaa anyway hatujui alipo habari ndo hiyo sasa ulitaka watu wafe na tai shingoni wakati wanaona binti anaita ?????

 22. BLACKMANNEN Says:

  Ahsantenisana pia na ninyi “Bongo Celebrity” kwa mchango wenu mkubwa katika jamii yetu ya Kitanzania. Tupo pamoja nanyi.

  Blackmannen

 23. cityboy Says:

  Habari ndo hiyo hiyo, utakufaje na tai shingoni!!!! haaa!! wakati kifaa cha nguvu kinaita!!! hahahaaa, received Mattlda.

 24. BLACKMANNEN Says:

  Duh!!!! Jina lako # 24, linatuchefua kinoma ndugu yangu. BC inatembelewa na watu wengi. Nakuomba tuwaheshimu watembeleaji wake kwa kujiheshimu wenyewe kwanza. Nadhani umenielewa!!!!

  Blackmannen

 25. halima Says:

  hili jina # 24, ni noma mhhhh

 26. Frida Barthazary Says:

  Naunga mkono mtazamo wak, pia napenda uamuzi wako

  Frida

 27. watubwana Says:

  watu bwana,siri ya mtungi aijuaye ngata…popote ulopo besta weka kipaumbele elimu kwanza mambo mengine yafuate baadae.muziki kwa TANZANIA NI BADO,sawa umeimprove kwa kiasi chake ila bado safari ni ndefu inahitaji uvumilivu na ujasiri.maisha mema

 28. betha shao Says:

  jamani besta unanipaga raha kiuno chako unavyokuzungusha? mimi natamanigi kuwa kama wewe sema ubonge unaniboaa

 29. chapombe Says:

  sasa we bethe shao,sasa uzungushe kiuno halafu ndio iwaje?


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s