Bila shaka utakubaliana nasi tukisema kwamba viwango vya ubora wa video za miziki kutoka Tanzania vimekuwa vikipanda siku baada ya siku.Siku hizi video nyingi zinakuwa zinaonyesha sio tu uhalisia bali pia zinabeba maudhui mazima ya nyimbo husika.Kwa hilo ni lazima tuwapongeze wasanii na pia waongozaji au watengenezaji wa video hizo.
Hali hiyo ndiyo tuliyoishuhudia hivi karibuni tulipotembelea kambi ya Prof.Jay wakati wa kutengeneza video yake ya wimbo Sauti ya Ghetto ambao umekuwa ukikamata mawimbi ya radio nchini Tanzania kwa muda sasa.Video hiyo inatarajiwa kutoka rasmi mwishoni mwa wiki hii.Hizi hapa ni baadhi ya picha kutoka katika shooting hiyo.Unaweza kuusikiliza wimbo huo kwa kubonyeza player hapa chini.
Prof.Jay(kushoto) akiwa na DJ Choka.
Sauti ya Ghetto:The Making
Prof Jay akiunguruma kutokea Ghetto.Hapo ni maeneo ya Magomeni Kagera.
Nawapongza wana mziki wa nyumbani kwenda na wakati
hakika mnasataili pongezi safi sana
bata hanyi magumu hata ukimlisha kokoto, teh!-teh!-teh!
Ukimlisha “peputobizimo” au “aisodiamu” jee!, itakuwaje!?
Komaa na fani toka Ghetto-Prof.
Kila la kheri!
sio aisodium, namaanisha-imodiamu! Hebu tumpe bata tuone matokeo prof!
oyaa jasho hilo prof jay,jimwagiage basi hata tu maji..maana harufu si haba hapo
haya ngoja tuione hiyo vedeo itakuaje ila hawa wasanii wana tatizo moja, mtu anaimba anaishi maisha magumu lakini anavaa kimambo safi macheni makubwa hata ukimuangalia anang’ara halafu anaimba yeye mgumu wa gheto,hata ukiangalia hiyo picha namba3 utaona kuna utofauti ya hao watu waliomzunguka pro jay walivyovaa na alivyovaa yeye! sasa ameenda kuwawakilisha au kuwasanifu?
hongera prof j kazi nzuri!!!!!!
Kisiio bwana harufu tena??
hahhaha wewe kisiio umenichekesha
hongera prof J,i’d like to see the video..song imekaa fresh
Bc huyu dj choka anapatikana wapi?nina deal nataka nimpe..please help me to get him….
Prof Jay ukiweka mtundiko ktk YouTube waambie jamaa zako ktk TAGS watangulize neno maarufu Tanzania ndipo kazi yako itaonekana kiurahisi kwa search: Tanzania music…………. mfano wa TAGS: ”Tanzania music Prof Jay – sauti ya ghetto”.
Mpaka sasa hivi wasanii wengi wa Tanzania hawaonekani ktk several initial search kwa vile TAGS/Video zao wanatanguliza majina yao ya kisanii badala ya neno kubwa TAGS: Tanzania music/ Prof Jay/AY/Segere/TMK/Banana Zoro/Karoli/marijani rajabu/kasheba/mlimani/kilimanjaro/Sekidia/Muhando/mamajusi/n.k n.k
watu bwana,siri ya mtungi aijuaye ngata..KWANZA NA KUPONGEZA SANA PROFESA J.
NAKUPONGEZA MWENYE BLOG
NAKUPONGEZA WEWE HAPO JUU UITWAE SALSA.
tunahitaji watu kama nyie duniaa hii,watu wenye upeo na akili kama hizo.
kweli nimeliona hilo tatizo kwenye youtube na naomba wasanii mkitaka kazi zenu zisikike vizuri bila shida tunayoipata mlifanyie kazi hilo.sio watu wote wanaofahamu blog za miziki ya kibongo,you tube wanaangalia watu wa mataifa mbalimbali itawasaidia wasanii kufahamika zaidi na zaidi na kupewa dili zenye akili nchi tofauti tofauti na sio nyumbani tu kila siku.asanteni
SAFI SANA PROF JAY,HAYO NDIYO MASHAIRI YANAYOTAKIWA…`DUNIA HAICHAKAI VINACHAKAA VILIVYOMO`,KWELI WEWE WA GHETTO…TUACHE KUKARIRI KUKAA GHETTO HAINA MAANA KUVAA VIBAYA…
Yeah! Thanks “salsa”, comment # 9. Maoni yako ni ya kuendeleza, na ndiyo mbiu yetu ya mwaka huu 2009. Mtu analetwa hapa kupanuliwa mawazo, na sio kudhalilishana kama comment # 4 anavyotoa maoni yake.
Black=Blackmannen