BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

PROF.JUMANNE MAGHEMBE January, 7, 2009

Filed under: Elimu na Maendeleo,Serikali/Uongozi,Swali kwa Jamii — bongocelebrity @ 9:36 PM

maghembe

Pichani ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Profesa Jumanne Maghembe.Huyu ni miongoni mwa mawaziri ambao wizara zao zimekuwa zikikumbwa na vimbwanga mbalimbali.Utakumbuka mwaka huu jinsi mitihani ya kidato cha nne ilivyovuja.Kwa upande mwingine kumekuwepo na kuongezeka kwa lawama kwamba kiwango cha elimu nchini kinazidi kushuka.Profesa Jumanne Maghembe ni Mbunge wa CCM akiwakilisha Wilaya ya Mwanga iliyopo mkoani Kilimanjaro. Unakubaliana na mtazamo kwamba kiwango cha elimu nchini kinazidi kuporomoka siku baada ya siku?Kama jibu ni ndio,nani unadhani anatakiwa kubebeshwa lawama?Nini kifanyike?


Advertisements
 

35 Responses to “PROF.JUMANNE MAGHEMBE”

 1. Kafura Says:

  Elimu inaporomoka. Wa kulaumiwa ni serikali, wazazi, walimu na wanafunzi wenyewe. Serikali inaendesha mambo kibabe na ya kifisadi. Walimu wamekata tamaa, wengine wanazaa na wanafunzi. Wazazi wanafikiri kuelimisha ni kazi ya mwalimu tu. Wanafunzi wamekosa nidhamu. Wanaishi au kutamani maisha ya kinyumba wakati bado wako mashuleni.

  Cha kufanya ni OPPOSITE ya niliyoyataja hapo juu.

 2. Gervas Says:

  Unategemea nini kitatokea kwa mwanafunzi kama mwalimu anafundisha kwa miezi mitano bila mshahara, ukaguzi wa mashule haupo tena, vifaa…sababu eti serikali inasema bajeti ya wizara ni kubwa kuliko pesa iliyopo. Wkati Kwa sasa serikali inatumia pesa nyingi katika kampeni mara dufu ya ilivokuwa huko zamani, Magari ya Mamilioni yananunuliwa na serikali. Pamoja na uchumi mdogo wa serikali, wakati naanza darasa la kwanza, tulikuwa tunapewa penseli nne, madaftari manane,vitabu kibao, vikiisha unapewa vingine na kila mwalimu alikuwa na nyumba yake n.k…hapo ni kijijini.

  Wizara ya Elimu inahitaji Bail Out, Mitaala iliyopo kwa sasa iwe formated, na walimu wapewe malipo na manufaa yote wanayotakiwa kupewa kwa mujibu wa sheria inayoongoza wizara no matter how much it costs. Haya ni matokeo ya ubinafisi/siasa na sio utaifa.

 3. kahindi Says:

  Huyu kaka yangu kila mara yupo jimboni kwake mwanga na Shangingi lake la uwaziri…sijui ofisini anakaa muda gani,huyu ndiye awe wa kwanza wa kubebeshwa hizo lawama za kushuka kwa kiwango cha elimu nchini,hana mchango wowote katika hiyo wizara,blaa,blaa nyingi tu…mimi napendekeza atolewe.badala yake awekwe Magufuli…au nyie wenzangu mna judge nini?…

 4. Mattylda Says:

  WATU WA EPA wamefikia wapi??wako wangapi mpaka sasa??anayejua tafadhali!!!!!!!!!

 5. binti-mzuri Says:

  ya elimu inazidi kuporomoka,si nasikia wanafunzi wa darasa la 7 half of them wamefeli. huyu baba hamna lolote,pochi nene pekee, mchezo umeishia apo

 6. anne Says:

  professor !
  Time to start dieting mate!
  This pic doesnt show you very healthy at all
  (sorry)

 7. fatma Says:

  tuzilaumu serikali za CCM tu na vingozi wetu, hawa binadamu hawatekelezi wajibu wao.

 8. Mama wa Kichagga Says:

  Ni kweli Elimu imeshuka sana tena sana!

  Gervas umenikumbusha mbali sana, enzi zile za kupewa mgawo wa vifaa vya elimu! Kweli Mwl JKN alikuwa mwanaume wa shoka maana aliangalia sana mambo ya msingi na ya kujenga. Na hii iliwasaidia watu wengi sana (kitaifa) hasa maskini. Fikiria unaishi Moshi unasoma Tabora Girls enzi hizo za shida ya usafiri, na hakuna mwanafunzi aliyeadhirika kwa chakula, usafiri, elimu wala nini. R.I.P Mwalimu, you were a great man and the HERO of our Nation.

  Madhara ya kushuka kwa elimu ni pamoja na haya:

  1. a Kutokuyajali maslahi ya waalimu ktk ngazi zote kulikopelekea wao kukata tamaa na kufanya mambo “BORA LIENDE”

  1.b Kuendelea kuanzisha sera mpya mara kwa mara bila kubooresha zilizokuwepo matokeo yake ni kuifanya wizara kama sehemu ya majaribio ya sera zinazoshindwa kukidhi haja ya utaifa.

  2. KUpitisha sera angamizi za elimu – kama kuchoma vitabu vya zamani ilhali tukielewa fika hivyo vitabu ni hazina ya Taifa

  3. Viongozi katika sehemu husika kutojali maslahi ya Taifa kwanza na kujihangaikia wao na jamaa zao (Ubinafsi)

  4. Kutokuwapa wabunifu nafasi za uongozi walete changamoto na mabadiliko, badala yake kutumia kujuana juana na sijui niseme nini mie.

  NASEMA HIVI, TUYAKUBALI MATOKEO KWANI TUNAJUA FIKA NI NINI TULICHOKIFANYA. NA HAPA NI SEKTA YA ELIMU TU, BADO SEKTA NYINGINE MADUDU NI HAYOHAYO.

  Serikali isipopitia upya utaratibu wa utendaji na kuhakikisha kujuanajuana, ukabilakabila, udinidini na upendeleopendeleo wa kipuuzipuuzi vinarekebishwa, “MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA ITAKUWA NI NDOTO YA KUSADIKIKA”

  Naamini fika nchi haiwezi kuongozwa na vijana pekeyao, ila nachelea kusema wazee wetu wanatuangusha kiutendaji na kimaadili hasa kwa kuukosa uzalendo na utaifa ndani ya utendaji wao. Wanafikiria ndani ya km 1 wakati wanatakiwa kuwaza katika kipenyo cha km 1,800 (Mtwara hadi Kagera).

  Lets talk the talk may be one day they will get us!

 9. DUNDA GALDEN Says:

  Lawama kwa kweli si kwa waziri anaestaiki kubebeshwa lawama ni hao wasiolipwa mishahara yao na haata wakilipwa si muda muafaka
  hapa ughaibuni sijasikia eti mitihani imevuja we hilo kosa kubwa sana kwa hawa watu tunaoishi nchini kwao na ni aibuu

 10. Kwani bado vibosile wa wizara ya elimu wanawasomesha watoto wao katika shule zilizo nchini bongo au chini ya wizara ya elimu?

 11. Dr.Majita Says:

  Ikitokea nikawa Rais wa Tanzania kwenye Elimu nitafanya yafuatayo:-
  1.NITAHAKIKISHA NAONDOA/KUFUTA MITIHANI YA MWISHO YA TAIFA as STD VII,Form IV na form VI.

  MAELEZO AS WHY NITAFANYA MAAMUZI HAYO MAKUBWA KIASI HICHO.
  Inaonekana kuwa credibility ya mitihani hiyo ni 0%.Utafiti wangu umeonyesha kuwa mitihani hiyo ya Taifa ranking yake haionekani kuwa na uhalisia wowote.Utakuta anaekuwa wa kwanza kila siku darasani anapata Div IV wakati ambae amekuwa anakuwa wa 20 kila mtihani anakupata Div I.Hii ina maana kuwa ama mitihani hiyo haikidhi hadhi ya kuwepo au wanaofaulu wamekuwa wakikariri baadhi ya vijisehemu vinavyotoka kwenye mitihani tuu.Hapo sijagusia hata chembe kuvuja kwa kuitisha kwa mitihani hiyo.
  SOLUTION:-
  Nitahakikisha walimu husika wa masomo ya madarasa hayo husika ndio wanatuchagulia wanafunzi wanaofaa kulingana na jinsi wanavyowaona na kuwajua wanafunzi wao kipindi wawafundishapo,so walimu hao tuu ndo watakaotoa ranking.

  2.NITAPANGUA WATU WA TIE WOTE (Tanzania Instistute of Education)
  3.NITAHAKIKISHA MITAALA WA ELIMU INAANGALIWA UPYA NA WADAU MBALIMBALI ili ikidhi kiu ya elimu nchini.
  4.NITAHAKIKISHA ELIMU YA TANZANIA INAKUWA STUDENT CENTRED na kutilia mkazo elimu kwa vitendo.
  5.KWA LEVEL YA TANZANIA NITAHAKIKISHA NARUDISHA VIBOKO MASHULENI.

  acheni hizo nyieee,yaani siku hizi vitoto nimeona vimekuwa sugu utafikiri nini.Vitoto vinawakwida maticha utafikiri ni washikaji wao.
  Mie nakumbuka enzi zetu ukienda disko ukamkuta mwl duuuu yaaaani kama ni jumamosi basi jumatatu jiandae kwenda ukiwa umejaradia kigozi.Lakini siku hizi hawa akina ROSS hawa watoto wa masaki ni shida tupu.Vibishiii utafikiri mshipa wa ngiri.

  Ngoja nikatafute lubisi kwanza nirudi nimalizie sera zangu za “Kama nikiwa Rais” manake naona ndoto hizi za mchana jua kaliii nazo ni nzuri.Ila wajita wanasema “If you belive,it will be miracles”.Ile pyeeeeeeeeeeeeeeeeeee Dr.Majita ni Rais watu weweweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee,mbuzi meeeeeeeeeeeeeeeeee,Wadau hoooooooooo
  Dr.Majita (PhD)

 12. Hombiz Says:

  Kwakweli hoja ya kiwango cha elimu nchini kuzidi kushuka, hata mimi siipingi. Uthibitisho juu ya swala hili uko wazi hata ukiangalia matukio mbali mbali ya kila siku yahusuyo sekta ya elimu. Mathalani: walimu kufanya kazi ktk mazingira magumu k.v. kufanya kazi kwa miezi mingi bila kulipwa mishahara na posho zao, wanafunzi na walimu kujiingiza ktk mahusiano ya ngono na walimu au wanafunzi wenzao, ongezeko la mimba za wanafunzi mashuleni, maambukizo ya ukimwi kwa wanafunzi na walimu, wazazi wenye uwezo wa kifedha kukimbizia watoto wao ktk shule za kulipia na nje ya nchi (Uganda Kenya, Asia, Ulaya, Marekani na kwingineko duniani), kuongezeka kwa kiwango cha wanafunzi kufanya vibaya ktk mitihani yao ya mwisho, migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu wakidai posho zao za kujikimu, mazingira mabovu ya kujifunzia, zana duni za kufundishia, mitaara iliyopitwa na wakati, wazazi wengi kudhani kuwa jukumu la kumfundisha mtoto ni la mwalimu peke yake n.k.
  Hata hivyo hili ni swala nyeti la kitaifa. Sio la kucheza nalo kabisa. Ndio maana wenzetu walioendelea, wanalipa kipaumbele sana swala la kuboresha elimu. Kwa hapa kwetu Tanzania ni jukumu letu wananchi wate kulitilia msisitizo juu ya uboreshaji elimu kama tulivyoanza kufanya ktk vita ya kupambana na ufisadi kwa kasi ya hali ya juu.
  Leo sina muda mwingi wa kuongelea suala hili. Nawaachia wadau wengine mtoe mchango wenu.
  Pia napenda kuwawekea mchango wa muandishi wa habari maarugu Ndugu Jenerali Ulimwengu ambaye amewahi kulizungumzia swala hili siku za nyuma.
  Pata mawazo yake kwa kuingia hapa tafadhali http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=43

 13. any Says:

  Hakuna wawekezaji wanaweza kubinafsisha sekta ya ELIMU?

 14. any Says:

  aah, nimesahau, DAWA ARUDI MKOLONI, WATU WACHAPWE BAKORA NDIO TUTASHIKA ADABU.

 15. Mwanamke wa shoka (UK) Says:

  mhhh hapa naona ninapata school mate….samahani “mama wa Kichagga”…hivi umesoma Tabora girls ama…I am just interested…(if you dont mind..)

 16. Mwanamke wa shoka (UK) Says:

  Dr. Majita (PhD) umenifurahisha…aidha na wengine woote mmechangia vilivyo kuhusu elimu….inaumiza kichwa ukifikiria hali ilivyo sasa hapa Bongo…

 17. Dr.Majita Says:

  Kwako Any #14,
  Tuko pamoja kwa pendekezo lako ilo la watu wachapwe Bakora, ila tofauti ni kuwa mimi sitaki warudi wakoloni.Puliiiiizi nipigie chapuo niwe RAIS WA TANZANIA.bwahahahahahahah
  Dr.Majita (PhD)

 18. Renee Says:

  Mimi nadhani swala hili ni swala nyeti sana:

  1. Waalimu kutolipwa mishahara yao wakati unaostahili ni kitendo cha kinyama na cha kusikitisha sana. Ni wizara gani nyingine imekuwa ikikopa nguvu za mfanyakazi hadi hapo itakapojiweka sawa? Mnategemea huyu mwalimu ambaye amelala na njaa au hajui watoto wake watakula nini aone umuhimu wa kutoa elimu kwa watoto wa wenzake? please!!

  2. Wakubwa kuwa na share kwenye shule za binafsi na kusahau wajibu wao katika shule za jumuiya. Pia hizo shule za binafsi zimeachiwa uhuru mkubwa sana kusimamia “curriculum”; sijui hata kama kuna wakaguzi toka wizarani wanaofuatilia viwango na kuona kuwa wanafunzi katika shule hizo hawapotoshwi au wanasoma katika mazingira yanayotakiwa! Viongozi katika shule za binafsi nyingi hawana ufumbuzi mkubwa katika maswala ya uzalendo, mila, na uananchi. Pia wamekuwa wakisisiza kufaulu kwa mitihani tu bila kujali michezo ambayo ni sehemu kubwa sana ya nidhamu mashuleni.

  Kudharau mila na lugha zetu siyo kiwango cha kujisifia cha maendeleo na kama tutaacha wageni waendelee kutuelimishia watoto wetu bila kuwamonitor tutakula hasara kubwa!
  3.Viwango vya nidhamu kwa walimu na wazazi vimeshuka sana. Wazazi wanataka kuwa marafiki wa watoto wao badala ya kuwa wazazi. Wanaogopa kuwaudhi au kuchukiwa na watoto wao. Mzazi anayeshindwa kumkosoa mwanae hajampenda bado. Kwa sababu ya kukosa nidhamu, watoto wameshindwa kuwajibika. Tukumbuke kuwa maendeleo/civilization siyo kufumbia macho vitendo vya upotovu kwa watoto wetu. “Civilization is a highly developed society with a high level of culture and social organization”.

  Mimi sielewi pale mwalimu wa kigeni (US/UK) anapo organize sherehe ya Halloween kwa watoto wetu na mwalimu mkuu anaruhusu bila kuuliza maana halisi ya sherehe hiyo. Don’t we have enough ghosts and witches already?!

  With that said, waziri na timu yake yote, wazazi, na hata watoto wenyewe wanatakiwa kubadili mwelekeo.

  Piece of advise kwa mheshimiwa waziri: Fungua viwanja vya michezo wizarani kwako na uanze mazoezi; afya yako inatia mashaka. I am sorry kama una tatizo la kiafya.

 19. BLACKMANNEN Says:

  Well done wanaBC wenzangu,

  Maoni ya namna hii yamesubiriwa kwa muda mrefu na Watanzania wote. Hapa nilipo sina cha kuongezea katika mada hii, maana wachangiaji wenzangu wote hapo juu mmezungumza kila kitu.

  Sababu za kushuka kwa ELIMU nchini Tanzania zipo nyingi sana, lakini zilizoelezwa na wachangiaji, zinachukua sehemu mkubwa zaidi kuliko sababu zilizobakizwa kutajwa hapa. Hata kama Wizara ingefanya uchunguzi wa kina, kwa kuwauliza wananchi wa kawaida sehemu yoyote Tanzania. Wangepata maelezo kama hayo hapo juu.

  Waziri “Prof. Jumanne Maghembe” na viongozi wenzako huko wizarani, hayo ndiyo maoni halisi ya Watanzania wa nje na ndani ya nchi. Yachukulie kama changamoto kwenu nyote na ni barua ya “Wazi” kwako, na uyafanyie kazi.

  This Is Black………….Blackmannen

 20. mwandiga Says:

  Serikali ya kulaumiwa.
  1. Mwalimu anafuata mshahara mail 60 na hapati,anafundisha saa ngapi.kwa mwezi anatumia siku 10 kufuatilia haki yake.

  2.Siasa. Mtaala wa elimu unabadilika kila waziri ajaye. mtaala unatengenezwa na wataalam wa mambo ya elimu,sio wanasiasa kama mzee ma-rope.
  3.Ufisadi. Pesa zinatumika katika mambo ya hovyo. mfano [A ]uchaguzi tarime ccm peke yake 1 Bilioni. Hizo zingenunua madawati,vitabu,mishahara ya walimu na shule ngapi.
  [B].kuna tume inachunguza wanawake wangapi waingie bungeni kana kwamba wingi wao utaondoa shida ya mimba za watoto wa kike.mapesa yanatumbuka,watu wanamalizia mahekalu mbezi.

  Solution
  1. Walimu walipwe stahili kwa muda muafaka.
  2.Tume chafu zisiundwe,na pesa zipelekwe elimu kwa usimamizi maalum
  3.Bunge lipunguze vikao 2 na pesa iingie bajeti elimu.
  4.Hela za mfuko wa jimbo zifutwe zipelekwe elimu
  5. Hakuna ruzuku vyama vya siasa.
  6. Elimu iangaliwe na wataalamu si bashy na ma-ropes.

 21. H.Y. Mganga Says:

  Kuporomoka kwa elimu ni mlolongo wa mambo mengi, sio suala la waziri tu, bali ni suala la mfumo mzima(system) wa serikali husika hata kama waziri akiwa genius kiasi gani kama system haitakia anacho hitaji waziri ni bure. Mambo mengi sana bila ya kuhukumu yana hitaji Utafiti kwanza na sio kuangalia juu juu tu, Kwa upande wangu naona wakulaumiwa ni makatibu wakuu zaidi kwasababu wao ndio wenye siri kubwa ya offisi husika, mawaziri ni watu wa kuhama hama, ni nadra sana kuona katibu mkuu ndani ya mwaka kubadilishwa, lakini kwa mawaziri ni jambo la kawaida.
  jambo la msingi watu wajadili nini kifanyike kuinua elimu na si kulaumu tu haita saidia hata kidogo.

  Regards:
  H.Y. Mganga.

 22. heya – i stumbled upon your blog, but you need a translator for us english speakers

 23. Mwanamke wa shoka (UK) Says:

  “Any”: wakoloni mbona wamesharudi siku nyiiingi tu ….ila wapo katika sura nyingine…..sio zile zao za zamani……kwa sasa hawana shida na kutupiga bakora migongoni…..wapo wanatupiga bakora kiaina -aina…..kama vile kiuchumi…etc etc….wakitupaka mafuta kwa mgongo wa chupa now and then….(si unajuwa panya huuma akipulizia ……)…..lol

 24. chapombe Says:

  ukweli uko palepale,tanzania kila mtu kivyake naomba msinibishie.hakuna mtu yuko pale kujitolea kwa ajili ya taifa,wote ni maslahi binafsi kwanza,ndio maana hata wanafunzi wanaanza huko chini ku-cheat.lawama apewe nani?jibu ni sisi watanzania kwa ujumla,nani amfunge paka kengere?

 25. TEACHER-DENMARK Says:

  mimi mwenyewe nilikua mwalimu bla bla bla za uwalimu nilizichoka nikaingia zangu mitini duu naona huruma sana nikukumbuka wenzangu Nyerere alitupa heshima na alithamini elimu

 26. kindo Says:

  Yote yaliyosemwa hapo juu kuhusu kushuka kwa elimu ni ukweli mtupu! Zamani waalimu walikuwa watu wa kuheshimika sana lakini sasa hivi ndio watu wanaodharauliwa kuliko wote katika jamii. Hii inachangiwa na jinsi serikali inavyo wa-handle na vilevile jinsi wazazi tunavyowachukulia waalimu wenyewe. Matokeo yake wanafunzi na jamii kwa ujumla hatuoni kama mwalimu ana thamani. Dharau hii husababisha mwalimu kufanya analoona ni best kwake na hasa kwa manufaa yake. Kwa mfano, mtoto akigombezwa na mwalimu, mzazi anakuja the next day anamtukana mwalimu mbele ya wanafunzi bila hata kujua kiini cha kugombezwa kwa mtoto wake. Na akijaribu labda kuongea na mamlaka zinazohusika kuhusu tabia ya mzazi kama huyu hapati ushirikiano wowote. Sasa waalimu nadhani wamechoka, wameamua bora liende, liwalo na liwe, as a result elimu inashuka. Halafu je kuna mtaala wa refresher courses kwa ajili ya waalimu? maanake waalimu wengi wa TZ (has vijijini) wamebaki nyuma kimaendeleo wakati dunia iko mbele sana katika kila hali. Wengine bado wanavaa nguo za krimplini!! Wengine wakiona computer wanasema video …sasa watamfundisha nani hawa? Toka amalize chuo mwaka 1970 hajawahi pata hata seminarya kumfungua macho…Jamani! Elimu ya TZ inahitaji uhakiki wa hali ya juu. Mungu ibariki TZ!

 27. Mama wa Kichagga Says:

  Kushuka kwa elimu nchini kuna mikondo mingi sana. Kwa kiswahili fasaha ni sekta tango “Cross-cutting sector”. Tunapozungumzia elimu hatuna budi bia kuangalia wadau/sekta zinazohusiana na elimu pia. Hapa nitachangia kuhusu sekta ya usafiri na utumishi(ajira). Sekta ya usafirishaji inachangia sana kushuka kwa elimu na maadili ya wanafunzi na waalimu kwa ujumla.

  Tusitegemee muujiza wa maendeleo kielimu iwapo watoto wetu wanasafiri ndani ya mabasi asubuhi na jioni waendapo na warudipo shuleni pamoja na watu wazima tena waliochanganyikiwa kwa jinsi ya kauli zao zilivyo . Katika mazingira ya usafiri kama huu, watoto wanajifunza mambo yasiyowahusu kunako umande wa udogo wao na hii inachangia sana kushuka kwa elimu/maadili nchini.

  Wazo:

  1. Wanafunzi na Waalimu wao wapatiwe usafiri tofauti na wa public ili kuwaepusha na balaa la abiria wasio na maadili ndani ya mabasi/madaladala. Nakumbuka hata sie enzi hizo mabehewa ya kusafiria wanafunzi kamwe hapakuwepo na mtu mzima zaidi ya waalimu waliosindikiza msafara na wahudumu wa train kwa ajili ya usalama wa wanafunzi na hawakuwa wanasikiliza wala kuingilia mazungumzo yetu (hapo ni high school). Tena enzi zile Mwl JKN alihakikisha hata shule za mbali ambapo train hazikuwa na huduma, mabasi yalikodiwa na wanafunzi hawakujichanganya kwenye usafiri wa umla. Sasa hivi tunashuhudia mwanafunzi wa kike anasafiri safari ndefu tena anakaa ktk seat moja na mtu jinamizi linamsumbua njia nzima sijui usiku na mchana. Huyu mwanafunzi tunamtegemea awe muujiza wa maendeleo ya elimu au maadili mema wakati tumemfungulia mbwa mwitu wamrarue tena bila silaha ya kujikinga? Napatwa na uchungu sana ninapoona hali hii inatokea ndani ya jamii yetu.

  2. Tuition zinachangia sana ushukaji wa maadili maana huko hakuna control ya maadili wala elimu fundishwa, hivyo serikali izikomeshe hizi kwani wakati mwingine zinachangia pia waalimu kuwa wavivu/kujitafutia mapato ya ziada kwa njia isiyo rasmi.

  3. Mabasi ya kuhudumia wanafunzi yarudishwe ktk mikoa yote na yasimamiwe na halmashauri/manispaa husika. Wazazi wahamasishwe kuchangia huduma ktk mabasi hayo kwa njia ya nauli kama ilivyo utaratibu ktk shule za binafsi.

  4. Ikiwezekana na hili litakuwa jambo la maana zaidi kampuni za usafirishaji za mikoa kama ilivyokuwa UDA ya zamani ya DSM zifufuliwe upya ili kuweza kukidhi mahitaji ya kijamii ya usafirishaji na pia kuzalisha ajira mbalimbali badala ya hivi sasa ambapo watu binafsi wameendelea kuwanyonya na kuwasumbua abiria kwa utendaji wao mbovu. Binafsi ningefarijika sana kumoyo kama ingefikia siku moja kufikishwa mbele ya haki wale wote waliochangia katika kufilisika kwa kampuni ya UDA kwani hawa wamelirudisha taifa nyuma sana kimaendeleo. Nashauri mali zao zikamatike na waunganishwe kwenye makosa ya KIFISADI pamoja na washukiwa wa mashirika na makampuni mengine ya umma kama vile SUKITA, RTC, KNCU, nk ili kurudisha heshma na nizamu ktk utendaji. Hebu jiulize haya mashirika yangekuwepo hai hivi leo tungekuwa tumeokoa ajira za Watanzania wangapi? KNCU iliajira wafanyakazi ktk mkoa mzima wa KLM, RTC ilikuwa na matawi nchi nzima na shirika kama SUKITA lilitakiwa liwe ndiye mkombozi mkubwa wa soko la bidhaa za wakulima na supplier mkubwa wa bidhaa za vyakula nchini na hata nje ya nchi. Je, unazani mimi kama Mama wa Kichagga nitaweza kuuza pilipili hoho zangu au vitunguu kwenye soko la dunia bila kuwa na kampuni imara kama ilivokuwa SUKITA?

  Jamani shime shime tuacheni kulala usingizi na tubuni mbinu zitakazotutoa kimasomaso badala ya kulala milango wazi tukisubiria huenda JK atapita na MBKM (Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania). Kazi ya JK ni kuilinda haki na kuhakikisha usalama wa wewe na mimi kubuni mbinu mbadala wa kulikomboa taifa kutokana na huu umaskini uliokidhiri.

  Mwisho kabisa napenda kutoa changamoto kwa serikali yetu tukufu ya kuvifufua vyombo vya umma nilivyovitaja hapo juu pamoja na vingine vyenye mitizamo ya kizalendo na kitaifa. Vyombo hivyo vijiendeshe kwa njia ya “KIUWAKALA – AGENCY” zinazojitegemea na vifanyekazi chini ya uangalizi wa Wizara mama kama zilivyo TIC, TAA na mawakala wengine wa serikali kwa njia ya kibiashara na kiufanisi zaidi nk. Kwa mahesabu ya harakaharaka, SUKITA ikifufuliwa na kuwa na matawi nchi nzima , yaweza kuzalisha ajira zaidi ya 1,000 kwa kila mkoa x mikoa 25 (gawa DSM mara 3) = 25,000!!!!!!

  KAZI ILIYOBAKIA KWETU SASA HIVI NI KUFUFUA MIUNDO MBINU ILIYOKUWA MUHIMU NA KUANZIA MIPYA NA KUWAFUNGA WAHALIFU WOTE WALIOTURUDISHA NYUMA.

 28. Renee Says:

  I agree with you Kindo: Refresher course! Kama tunataka wanafunzi wapate elimu bora ni lazima walimu wapigwe msasa kila mara. Mwalimu ndiye mtu wa kwanza anayemfundisha mtoto herufi na baadaye mtoto anazitumia herufi hizo kuwa mtaalamu, ni vipi mwalimu asahaulike na kudharauliwa?

  Mimi hadi leo nakumbuka mwalimu wangu aliyenifundisha darasa la kwanza hadi la tatu, alikuwa anaitwa Mwl. Amani; juma ambalo yuko zamu ulikuwa huwezi kuona wanafunzi wakizurura nje saa za masomo. Somehow, I will never forget how committed that guy was!

  Walimu wataipenda kazi yao kama tu watapata heshima wanayostahili.

 29. Dave Says:

  Elimu inaporomoka ni matokeo ya sera za CCM. Uongozi wa CCM wameweka mbele maslahi yao km kununua mashangingi mapya kila baada ya mwaka(?), Watoto wao wote wanasoma nje. Sielewi kwa nini mpaka leo kusiwe na shule ya watoto wa madiplomati wetu hapo hapo Tanzania badala yake hata walio ubalozi Rwanda wanasomesha watoto London kwa kodi zetu. Matokeo yanke viongozi wa CCM hawalazimiki ama kuwajibika kuinua hali ya elimu Tanzania. Ukikutana nao utona tu nyuso zao zilivyo na furaha kama wao hawatoki TANZANIA tunayoiongelea, kwao mambo shwaaari.

 30. Dinah Says:

  Walimu ni watu muhimu sana kuliko hata Wabunge (nionavyo mimi) lakini hawathaminiwi, hawaheshimiwi na hawalipwi kwa wakati.

  Walimu wakiridhishwa hakika watafanya kazi zao kwa kujituma na hakutakuwa na “masomo ya ziada” nje ya masaa yao ya kazi wala kununua na kuuza mitihani kabla haijatoka rasmi.

  Kutokana na ugumu wa maisha Walimu kuiba mitihani na kuiuza ni bonge la biashara…..karatasi moja inaweza kufikia hata laki 5Tsh.

  Watoto wa mafisadi wengi ndio wateja wakuu……which sio fair kwa walalahoi ambao wanajituma kusoma na hawana uwezo wa kununua hiyo mitihani kabla ya mtihani wenyewe.

 31. hombiz Says:

  Watanzania wenzangu, samahani kwa kutoka nje ya mada. Nimesoma habari inayoripotiwa na Lulu George toka Tanga aliyoichapisha januari 12, 2009, saa 10:36 ktk gazeti la Nipashe. Habari hii inahusu ajali mbaya ya basi iliyotokea likiwa safarini tanga na kuua raia wema 27. MWENYEZI MUNGU AWAREHEMU, WAPUMZIKE KWA AMANI.
  Lulu George anabainisha kuwa mwaka huu 2009 umeanza vibaya kutokana na ajali za barabarani zilizosababisha vifo vya watu 41 na kuwajeruhi 57, ndani ya siku 10.

  Kwakweli hizi ajali za barabarani zinaniudhi sana. I am so sick and tired of hearing terrible news regarding road accidents in Tanzania all the time! Hivi kuna ugumu gani wa kuboresha na kuzitekeleza kikamilifu hizi sheria za usalama barabarani!? Kwa nini serikali haiweki sheria kali za usalama barabarani ili kulinda usalama wa raia wake wanaoteketea kila kukicha kutokana na majanga haya makubwa ambayo yanaweza kabisa kuepukika!?.
  Madereva wazembe wako wengi sana nyumbani Tanzania tena wanapewa dhamana kubwa ya kubeba roho za watu mikononi mwao. Watu hawa ambao hawathamini maisha ya binaadamu, huendesha magari kwa mwendo wa kasi, bila kujali kuwa wamebeba roho za watu. I think, linapokuja swala la usalama wa raia, serikali inabidi iwe kali sana ktk kuhakikisha uhai wa watu haupotei kizembe kiasi hiki. Hivi haiwaudhi hawa viongozi kutuma salamu za rambirambi kila siku!?
  Kwakweli hapa nilipo, nina-type message hii huku nimejawa na hasira mithili ya koboko!. Natamani ningekuwa na uwezo, japo niwalambe bakola wafanyakazi wa wizara husika, ili wawajibike zaidi.
  Ndio maana mimi ninaposafiri kwenye basi, huwa siwachekei hawa madereva wazembe hata kidogo, pale wanapoendesha mabasi kwa mwendo wa kasi huku wakifanya mbwembwe za kijinga utafikili wamepandwa na maruhani fulani!
  Maoni yangu ni kama ifuatavyo:
  – Ni lazima barabara zote ziwe na speed limit, na askari wa usalama barabarani, wachukue hatua kali kwa madereva wanaovuka kiwango cha mwendo kilichopangwa kwenye barabara husika. Fine kali iwe ni kwa kosa la kwanza, na dereva akirudia tena anyanganywe leseni na asiruhusiwe kuendesha gari kwa miaka 5 na rekodi zao zihifadhiwe vizuri.
  – Askari wa usalama balabalani waache kufanya urafiki na madereva wa mabasi na kufanya kazi yao kama inavyopaswa. Mtindo wa hawa askari (traffics) kukamata madereva wazembe na kisha kuwaachia baada ya kupewa rushwa, inafaa ukemewe kwa nguvu zote kwani tabia hii hivi sasa imekuwa ni kama utamaduni. Ni vema hawa askari wasio waadilifu, wachukuliwe hatua kali, “ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi na kifungo”, kwani tabia zao zinachangia kuteketeza nguvu kazi ya taifa.
  – Leseni za udeleva zisitolewe kiholela. Kwa mfano utakuta, utingo kajifunza kurudisha gari nyumba na kulisogeza mbele tu, lakini kwakuwa anavijisenti vya kuhonga, basi anapewa leseni ya kuendesha gari, tena la abilia. Wahusika wanaobainika kuuza leseni za kuendesha magari kwa madereva wabovu, ni lazima wachukuliwe hatua kali za kisheria. Nchi za wenzetu zilizoendelea, sheria za usalama barabarani hawachezi nazo hata kidogo. Kwa mfano, gavana wa 39 wa Illinois, U.S.A. aitwaye George Ryan, mwenye umri wa miaka 74, anatumikia kifungo cha miaka 6 1/2 kwa kosa la ubadhilifu wa mali ya umma na tabia yake ya kula rushwa. Moja ya rushwa alizokula huyu mzee, ilitokana na uuzaji wa leseni kwa dereva wa lori ambaye alikuwa hajafuzu kufanya kazi hiyo. Matokeo yake, huyo dereva alisababisha ajali mbaya sana ya barabarani kwa kugonga gari dogo na kuua watoto 6 wa familia ya Scott na Janet Willis. Adhabu ya gavana Ryan, haikuishia kwenye kifungo tu. Huyu mzee pia kanyan`ganywa haki zake zote za kustaafu ikiwa ni pamoja na kiinua mgongo. Baadhi ya wanasiasa wenzake walijaribu kumuombea msamaha kwa raisi wakidai afya yake nay a mkewe zimedhoofu, lakini wananchi walio wengi wamepinga uamuzi huo. Hivyo basi hadi hivi sasa anaendelea kutumikia kifungo chake.
  – Badala ya kununua mashangingi ya waheshimiwa, na kumwaga mahela kibao kwenye kampeni za chaguzi mbalimbali, serikali itumie pesa hizo kukipatia kitengo cha usalama wa raia computer za kisasa zitakazotumika kuhifidhi kumbukumbu ya kila mtu aliye na leseni ya kuendesha gari nchini Tanzania na jinsi alivyoipata leseni yake. Pia serikali inunue magari ya usalama barabarani ambayo yana compyuta zitakazoweza kusoma rekodi ya dereva, pale anapokamatwa na kosa lolote la usalama barabarani, hasa la uendeshaji (moving violation). Computer zote za recodi za usalama barabalani, ziingiliane na zile za kwenye gari za traffic ili kurahisisha kazi. Na watumiaji wapewe mafunzo ya kutumia nyenzo hizo muhimu, ili kuleta ufanisi unaotakiwa.
  Ningependa kuendelea kuizungumzia mada hii, lakini naomba niishie hapa kwa leo.
  POLE KWA WAFIWA. MOLA AWAREHEMU MAREHEMU WOTE WAPUMZIKE KWA AMANI.
  NAWAOMBEA MAJERUHI WOTE WAPATE NAFUU NA KUPONA MAPEMA.
  AMINA

 32. any Says:

  ELIMU INASHUKA KWA SABABU WALIMU WANAUZA VISHETI SAA ZA MADARASA, NA LAMBA LAMBA! SASA MUUZAJI NI MWANAFUNZI NA ANAUZA SAA ZA VIPINDI, UKO APO? HIZI NJAA ZINALETA YOTE HAYA.
  MAJITA NTAKUPIGIA KURA MWANAWANE!
  KWELI MWANAMKE WA SHOKA UK, WAKOLONI WAMEKUJA KWA SURA MPYA. DUUH KAZI TUNAYO DEAR.

 33. halima Says:

  Any umenikumbusha mbali sana mwanawane, tabu inakuja pale unapokopa kisheti cha mwalimu halafu huna hela ya kulipa uwiiii utakoma kila swali linaanza kwako usipojibu haha viboko vinakuhusu.

  Matty nimekumiss shost Bint mzuri upo wapi?

 34. any Says:

  BC TEAM INABIDI MUAJIRI MTU/AU MTU AJITOLEE KUFANYA SUMMARY YA HIZI POST! MI NAINGIA CAFE YA KIMANZICHANA HAZIFUNGUKI SHALA, SASA UKISOMA POSTS NDEFU IVI HATA HUJAMALIZIA MOJA MIA TANO YAKO IMEENDA. SIJUI WENGINE MNASEMAJE? MATTY JITOLEE SHORT HAND BASI RAFIKI.

 35. any Says:

  haa, alima,. kila swali linakuhusu apo ukute ni math na wewe hesabu hazipandi, kama vile ugali wa maziwa na mlevi! haaaaa, utakoma.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s