BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

HONGERA TK! January, 14, 2009

Filed under: Blogging,Blogs,Bongo Reality TV — bongocelebrity @ 7:16 PM

tk-bannerbc

Kwa mujibu wa jamaa wa Technorati,inakadiriwa kwamba blog mpya zaidi ya mbili huanzishwa katika kila sekunde,kila siku.Mpaka tarehe 31 Julai mwaka 2006 kulikuwa tayari na blog zaidi ya milioni 50!

Pamoja na mafanikio hayo ya uandishi huu unaoitwa uandishi wa kiraia (Citizen Journalism) ,bado hakuna takwimu za uhakika zinazoonyesha ni blogs ngapi “zinakufa” kila siku au kutelekezwa.Lakini ni wazi kwamba ni nyingi pengine kupita kiasi.Mtu anaanza kublog kwa kasi ya aina yake.Baada ya siku chache haonekani tena hewani.Amekosa muda au amekosa hamasa.Lengo alilokuwa nalo limempotea. Hawezi tena.Kila mtu ana majibu yake.

Ndio maana inapotokea mtu akadumisha blog yake kwa angalau mwaka mmoja inasemekana hawezi kuacha tena ku-blog.Kimsingi mtu huyo anastahili sio tu pongezi bali heshima.

Mmojawapo miongoni mwa watu hao ni mwanadada anayeonekana pichani hapo juu.Kwa wengi anajulikana kama TK lakini jina lake halisi ni Teddy Kalonga.TK ni miongoni mwa watu wanaotambulika kirahisi nchini kwetu ambao hawajabaki nyuma kunako tekinolojia hii ya blog.Hivi majuzi alisheherekea mwaka mzima tangu aanzishe blog yake inayopatikana kwa kubonyeza hapa.

Tunaungana na wengine wote kumpongeza TK na kumtakia kila la kheri katika kuendeleza “libeneke” kama anavyopenda kusema mwanablogu mwingine maarufu,Muhidini Issa Michuzi.Bonyeza hapa uone jinsi Teddy alivyosheherekea mwaka wake mmoja wa ku-blog.Hongera.

NB: Kama na wewe una blog yako na unasheherekea mwaka au miaka,usisite kuujulisha umma kupitia hapa hapa ndani ya BC.

Advertisements
 

7 Responses to “HONGERA TK!”

 1. Mitchez Says:

  Big up TK project imetulia hongera sana wadau tupo wengi wa project unayaofanya nasamini kazi yako i wish u more the best gal….www.bongoyetu.com

 2. hombiz Says:

  keep it locked!

 3. Dinah Says:

  Hongera sana Tk, kukip ze blog u need 2 be commited. Kila la kheri.

  Hey Mitch (comment #1) umepona Bro. Nice 2 c u back…..back 2 c u nice!

 4. BLACKMANNEN Says:

  Ni furaha kubwa sana kwetu sisi wanaume wa Kitanzania tunapoona dada zetu wakijitahidi kuinua maisha yao kwa njia njema kama hii ambayo dada yetu “TK” anaifanya na imeweza kuishi mwaka mmoja sasa. Hongera sana dada yetu “TK”.

  Blogi nyingi za Kitanzania zinaishi muda mrefu kama mtu mwenye blogi yake atajitahidi kuwajua Watanzania wakitakacho. Kikubwa kuliko yote, ni lugha inayotumiwa katika blogi (Kiswahili) na miziki ya kiswahili. Kenya wanatumia kiingereza zaidi katika blogi zao, na matokeo yake wanapigwa mabao na blogi za kitanzania. Hawapati watu wengi. Ahsante sana Mwl. Nyerere (R.I.P.). Bongo tambarareeeee!!!

  Tembeleeni pia, …www.jambonetwork.com. Ni kijiwe cha nguvu cha Wabongo, masaa 24 utawakuta hapo wakichat.

  This Is Black=Blackmannen

 5. Edwin Ndaki Says:

  Hongeera TK kwa kuendeleza kublog..

  nasubiri “anivesari ya Dinah” NAJUA ipo karibuni..

  kwa wale ambao bado wanaendelea kublog na sometimes wanapatwa na tujimafua wajitahidi kunywa maji kwa wingi wasikate tamaa na kuendeleza mazoezi hakika blog zao zitazidi kupumua…

  aaaa..aaaaa….kama mmmmmmmmmmmmmm nda.aa…………aaa….

 6. MARIAM Says:

  well done , keep it up! and GOD BLEES U.CONTACT ME PLEASE .THANKX UR PRIMARY TEACHER NIKO HAPA UK.

 7. hot baby Says:

  keept ma sis


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s