BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

DAWA YA MAPENZI-MBARAKA MWINSHEHE January, 15, 2009

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 9:02 PM

mbaraka3bc12Kwanza tukuombe radhi kwamba wikiendi iliyopita hatukuweza kukuletea burudani ya wikiendi kama ilivyo kawaida yetu.Maji yalizidi unga au unga ulizidi maji.Vyovyote vile haikuwezakana!

Bila shaka umeshawahi kusikia sana habari za watu kuhangaika huku na kule kutafuta “Dawa ya Mapenzi”.Ushasikia jinsi ambavyo wakati mwingine hufikia mtu akalala kwa karumanzira kisa eti,dawa ya mapenzi.Miaka nenda miaka rudi,imani kwamba dawa ya mapenzi inaweza kupatikana kwenye kibuyu kidogo kilichowekewa ugoro,unyoya wa bata mzinga na takataka nyingine imeendelea kutawala akili za baadhi zetu.

Je kuna dawa ya mapenzi?Ipo wapi?Hayati Mbaraka Mwinshehe anatusaidia kupata jibu la swali hilo hapo juu katika wimbo wake Dawa Ya Mapenzi. Tungependa pia kusikia kutoka kwako msomaji.Je kuna uwezekano wa kupatiwa kidonge cha mapenzi kushinda kile cha upendo,heshima,ushirikiano na maelewano baina ya wawili wanaoamua kupendana?Bonyeza player hapo chini upate burudani.Raha ya wimbo huu,pandisha sauti kisha nyanyuka uucheze.Kama unaweza nenda kabatini tafuta bugaloo kama unayo na kisha achia afro.Mkononi shikilia glass bila kusahau zile san gogo machoni.Wikiendi Njema.Advertisements
 

17 Responses to “DAWA YA MAPENZI-MBARAKA MWINSHEHE”

 1. Dr.Majita Says:

  Dawa ya mapenzi ipo.Kwa aliyewahi kusoma vile vitabu vya hadithi za kina PangalaShaba lazima anaijua dawa ya mapenzi.

  Kama kuna mtu anaihitaji dawa hiyo anitumie email.MASHARTI YAKE SASA weeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!
  Dr.Majita (PhD).

 2. MapigoSaba Says:

  Hiyo picha hapo juu ni ya ilikuwa ni siku ambayo Mbaraka Mwinshehe alikuwa anafunga ndoa, hii ni kwa mujibu wa maelezo ya booklet iliyomo kwenye ya CD yake ya Masimango (Moro Jazz) ambayo ipo kwenye public library hapa Alberta. Nilitaka kuonyesha tofauti kubwa iliyopo kati ya bongo celebrities wa enzi hizo na wasasa kama picha inavyojieleza.

 3. Mwanamke wa shoka (UK) Says:

  wow!…Umenikumbusha mbali!! Maana biological clock yangu imeshasonga songa na hivyo Mbaraka ndio alikuwa wetu enzi zile.
  …and that was a very simple marriage portrait…wakivishana pete….ishara ya mapenzi….

  R.I.P. We miss you.

 4. :-)Wikiendi Njema wadau wa BC!

 5. halima Says:

  Hahahah Jeff umenena yaani enzi hizo ukilipuka suruali yako ya juu ni banie chini ni achie na shati lenye picha ya ndege kwa nyuma kwa juu yake umepiga kizibao mwee hakuna mjanja kama wewe.
  Nawatakia weekend njema wana BC wote.

 6. hombiz Says:

  Asante sana BC burudani murua kabisa.

  Kwa mtazamo wangu mimi, naamini hakuna kabisa dawa ya mapenzi kwa kutumia mazingara. Watu wengi wamekuwa wakiamini kuna limbwata ambayo ukiitumia kwa umpendae, basi nae atakupenda mara dufu. Wengine wanasema oooh! Bibie akichukua nyama aliyoitengeneza kwa kuihifadhi sehemu sehemu na baadae akaichanganya na mchuzi, kisha akampakulia na kumlisha mtu anayetaka ampende, basi jamaa atampenda kupindukia. Dawa hizi za mapenzi ni uongo na upuuzi mtupu! Chonde chonde ROSS!, usijaribu kumfanyia mpenzi wako hayo mazingaombwe niliyoyataja hapo juu! Utamrusha akili bule kama si kummaliza kabisa!

  -Niaminivyo mimi ni kwamba dawa ya kweli ya mapenzi ni NENO LA MWENYEZI MUNGU. Baadhi ya vidonge vya dawa ya mapenzi vitokavyo kwenye NENO LA MWENYEZI MUNGU ni kuwa wakweli kwetu na kwa wapenzi wetu, uvumilivu, ukarimu, kutokuwa na wivu wa kijinga wala majidai, kuepuka maudhi, kutohesabu makosa, kuwa waaminifu, kumlinda umpendae, kuwa na matumaini, kujituma na kutochoka kupenda.

  -Pia, nionavyo mimi, dawa ya mapenzi ni mawasiliano hai. Palipo na mawasiliano hai, hapana rabsha hata kidogo. Wapendanao wakiwasiliana vema, watajuana nje hadi ndani. Hii ni kuanzia nje ya nyumba, ndani ya nyumba na hadi wawapo wawili kitandani. Ni muhimu kujuana vema ili mapenzi yaweze kunoga bila kuchuja. Kalumanzila na limbwata lake, hawezi kutekeleza hata moja kati ya hayo mambo niliyobainisha hapo juu zaidi ya kutaka umletee kuku mweupe, na mbuzi ili akajiachie na familia yake “kwa raha zao”. Au kalimauganga akiona hawezi kutibu tatizo lako, basi atakupa masharti magumu ili uyashindwe na usirudi tena kwake. Kwa mfano, anaweza akakwambia ukitaka akutengenezee dawa ili fulani akupendw, basi kamletee jasho la kuku lililojaa kwenye kisoda cha Coca-cola. Sasa wewe utalipata wapi!? Na kama mganga ana roho ngumu zaidi, basi atakutaka ulete viungo vya mwili wa mtu mwenye ulemavu wa ngozi (albino) ili akupe dawa. Sasa hii ni dawa kweli au mauaji!?

  BC, mimi naamini dawa pekee ya mapenzi ni NENO LA MWENYEZI MUNGU!
  Mengine yote, kama vile, ndumba, mali cheo-ni usanii tuu!
  Keep it locked
  PENDA KWA DHATI
  HOMBIZ

 7. joe Says:

  Aksante mh. mkuu wa naniii kwa kutuendelezea lebeneke.Mimi ni mbongo hapa mamntoni ,nimepata kamera kubwa kwa kweli siku za karibuni nitakuunga mono

 8. zabibu Says:

  habari zenu wadau duniani mzima.kweli kabisa wagenga walisema kama mizizi haitafa hirizi ndiyo kabisa haifai.haya dawa ya mapenzi ipo ila siyo kwa mganga ila wawili wakipendana ndiyo kasheshe hapo unatakikana kwanzo mume au mke huu mdomo usiwe juu kwa ujeuri lazima musikilizane moja akikosa basi moja anapo kuwa hakuna hasiri basi amuwende moja wake ili apate kumuambia pale ilikuwa siyo hivi bali ni hivi unamfahamisha kwa ulaini bila makelele basi penzi lina dumu utakuta asali cungu kuliko penzi lenu.

 9. BLACKMANNEN Says:

  Mbaraka Mwinshehe, katika wikiend yake ya mwisho kabla ya kifo chake , nilikutana naye kwa bahati mbaya hapo jijini kwetu Dar es salaam akiwa katinga ile suruale yake ya draft.

  Kwa kweli naumia sana ninaposikiliza nyimbo zake hizi mnapoziwewka hapa leo ninyi BC.

  Maana zinanikumbusha mengi. Hasa hapo Mnazi mmoja alipokuja kwenye mashindano ya kupata “Bendi” ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miziki ya mtu mweusi huko – Lagosi. Ambapo Afro 70 chini ya Bingwa wetu Patrick Balisidya (R.I.P.) walishinda.

  This Is Black=Blackmannen

 10. Edwin Ndaki Says:

  Dr Majita…wasuuu umekula shule siku hizi..ila usije kutusahau huku BWAI,MAKOKO,MGANGO n.k

  Majita namkumbuka hadi mtoto wa panga la shaba nafikiri alikuwa anaitwa Ufudu…

  Nakumbuka Panga la shaba alikuwa anaminya visiga kama sijakosea maana ni jirani yangu..tee tee

  Ila tatizo mtu alikuwa akienda kutafuta dawa ya mapenzi walio wengi walibaki naye…

  Siku njema BC tupo pamoko

 11. any Says:

  mkewe mzuri sana, kama model,. look at her face, those cute lipsi, mwishehe alijua kuchagua kweli,.

 12. DUNDA GALDEN Says:

  DU MAJITA UMENIKUMBUSHA KITABU CHA PANGA LA SHABA KILE KITABU SI MCHEZO.LAKINI JAMANI DAWA KUBWA YA MAPENZI JINSI KITUMBUA UTAVYOJUA KUKISHAMBULIA IPASAVYO NA BILA KUSAHAU KONA KUU NNE MUHIMU BASI WEWE USHALOGA ZAID NDIO MAANA WANATUNGANGANIA KAMA LUBA LAKINI ONGELENI SANA NANYI MUNGU KAWAPA ……….MUHIMU SANA KWETU
  AMINI

 13. Dr.Majita Says:

  Ndaki wasu,
  Usiwe unapotea bana.Ona sasa hadi kwenye sherehe yangu ya kuukwaa udaktari hukuwepo.Yaani wewe acha tu.Mzee nilizawadiwa udaktari huo na wanakijiji wenzangu baada ya kutafasiri kizungu to kiswahili.Unacheza nini wewe???

  Mkulu Dunda Dalden kile kitabu wee acha tu.Yaani kilikuwa kinasisimua hadi basi,lakini si ulikuwa unaona jinsi dawa za mapenzi zilivyokuwa zinatafutwa na matokeo yake???hahahahah
  Dr.Majita (PhD)

 14. Gervas Says:

  Dawa ya mapenzi jamani ipo…. Limbwata, E-shuntama nk, research ilishafanywa hapa kijijini kwetu na wala mtu asibishe apa !! mkishaoana tu basi…ukishaikula tu na mkeo, basi hapatakuwa na Talaka wala ngumi katika maisha yenu ya ndoa hata kama mkifumaniana…..I am sorry tu inatosha.

 15. Mama wa Kichagga Says:

  Sijui nilikuwa wapi, yaani nimecheka hadi raha.

  Hicho kitabu sijui kama bado kipo? Nitakitafuta nirudie kukisoma. Jamaa mtungaji kweli aliweza kufikisha ujumbe wake sawasawa. Ufudu alikuwa ni kiboko ya njia wacha kabisa Eduwini haaaaa.

  Sasa ngoja nichangie;

  DAWA YA MAPENZI
  HATUA1: Kuwa na hitaji la moyo la kupenda na kupendwa

  HATUA2: Mshirikishe Muumba wako ili akulengeshe kwa aliyekupangia (hapa ni muhimu sana vinginevyo utachagua majibu yasiyo sahihi kibao).

  HATUA3: Mungu akishakuruhusu moyoni, anza kazi ya kushangaa shangaa yale maeneo uliyotajiwa utamkuta (mfano shuleni, kazini, kanisani, msikitini nk) kisha anza mauchunguzi ya kinagaubaga kulingana na mahitaji yako.

  HATUA4: Moyo ukidondokea (ridhika) anza mara moja bila kusita silaha ya mawasiliano ya kumjua mwenzio.

  HATUA5: Wekeni pamoja kila mmoja wenu malengo na matarajio yake katika maisha na jaribuni kuyawekea kipaumbele na ratiba ya utekelezaji kwa busara, saburi, uvumilivu, sala,upendo na kuwasiliana na Mungu wenu mara kwa mara.

  HATUA6: jimuvuzisheni kukaa pamoja ili kuweza kutimiza mikakati mliyojiwekea huku mkiendelea na sala na mawasiliano ya hali ya juu (kutoka pande zote).

  NB: Kama hukubahatika kupitia hatua hizo hapo juu, usikonde kabisa, komaa na idara ya mawasiliana na sala mambo yako yatanyooka tuu.

  Mwisho;
  Mara nyingi upendo unafifia au kupotea kabisa iwapo wahusika wa taasisi ya ndoa hawana mipango yoyote huku kila mmoja akiwa na matarajio lukuki ya kwake mwenwewe na yanayohitajika kutekelezwa na mwenzake. Matokeo yake baba akitangulia mke hamfuati, akimtanguliza mama, hafuati njia ya kuelekea mjini. Sasa hapo ndo ngoma inogile! Kila mmoja anamuona mwenzie hamnazo na mwisho wake ndio kuanza kuwatafuta kina panga la shaba wazidi kukuharibia zaidi.

  “Tembea na mwenzio kiubavu-ubavu, mkono kwa mkono huku mkishauriana, sali pamoja na kuwasiliana kwa kiwango cha juu cha taasisi yenu ili wote msaidiane kuwa na kuelekea ktk muelekeo mmoja”

 16. BLACKMANNEN Says:

  Duh!!! hiyo kali kaka “Gervas”, comment # 14. Kumbe unayajua majambo ya maana namna hii? Hata hatuambiani ndugu yangu?

  Nitupie na mimi basi hiyo E-shuntama, niitumie kwa shemeji yako “Miriam Odemba”. Maana unajua tena wengi wanamvizia kila sehemu anayopita, wasije wakanizidi kete wajanja akina Dr. Majita, wenye ndimi za “nta”.

  This Is Black=Blackmannen

 17. john Says:

  kweli nimeamini vizuri vimeshapita. mzee mzima nimemkupali kwa kila kitu, meseji zake za ukweli zenye mafundisho na ujumbe unaoishi pili nampa bigup kwa kuchagua mwenza wa maisha mwenye sifa zote anazo mpaswa kuwa nazo mwanamke wa enzi hizo, bi-mkubwa ametulia kisu cha ukweri kimeng’aa hata kwenye black and white aaah! sisemi sana nisije pata ladhi. saruti babu huko ulipo.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s