BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

KWANINI-NURU January, 17, 2009

Filed under: Burudani,Muziki — bongocelebrity @ 1:15 PM
Tags:

nurumohdbc

Baada ya Walimwengu na Msela, mwanadada Nuru Magram (pichani) hapo jana amefyatua video ya wimbo Kwanini ambao ni miongoni mwa nyimbo 10 zinazotarajiwa kuwemo katika albamu yake aliyoipa jina Walimwengu. Albamu hiyo inatarajiwa kuingia sokoni mnano mwezi wa Machi mwaka huu.

Sikiliza mashairi yaliyomo katika wimbo huu,tazama jinsi hadithi iliyomo kwenye mashairi inavyosimuliwa katika video hiyo.Ukiiangalia kwa makini utagundua kwamba lipo jambo moja ambalo sio la kawaida linatokea katika mlolongo wa simulizi hilo.Sio la kawaida kwani katika simulizi hilo kuna mtu ambaye hafanyi kile ambacho wengi wetu tungetarajia afanye.Itazame kisha uniambie kama unaweza kuona nilichokiona mimi.Pata burudani.Kazi nzuri Nuru.


Advertisements
 

49 Responses to “KWANINI-NURU”

 1. wanakjj Says:

  So!!! where is the video,Song or ryme????

 2. T Says:

  mi nadhani ni huyu mfumaniwaji kuendelea kuwepo eneo la tukio

 3. EDDY Says:

  wimbo safi kwa 100%

 4. Chengula Says:

  Sasa mbona hutowi ngoma za kweli unaendeleza vilio mpaka lini ama ukitowa video ndio umetimiza lengo lako? kaza buti wacha mchezo nuru…kwanini lakini?

 5. Kokusima Says:

  mi sijaelewa kitu humu, sasa analalamika nini wakati yeye ndo mtendaji? nimetoka ziro humu, ngoja nisubili wengine.

 6. Diva Says:

  Have you guys seen a fly all up on her face! Look closely you’ll see it. She is cute, but the video doesn’t make sense.

 7. Dr.Majita Says:

  Huyu binti ni mzuri,meno swafi na sauti mulua kabisa.Pale kwenye chakula cha mtoto kwa kweli nimepa-pause mara kibao.Kaenda hewani kimiss miss,safi na hiyo rangi yake.

  Balaa sasa,hina imekuwa tooooo much hadi inaboa.Halafu kuna pahala matumizi ya pro active yanahitajika.Bonge la uchunusi.

  NIMEMISS HIYO AINA YA KUTUNDIKA NGUO KWENYE MISUMARI ILIYOPIGILIWA MLANGONI.Yaani nimecheke hadi basi.Itabidi na mimi niende mujini nikatundike nguo zangu manake huku kijijini nguo za kutundika zenye hakuna.

  Hii video imejitahidi kutoa hali halisi ya mazingira ya na maisha ya Mtanzania ila ujumbe wa wimbo na mantiki yake labda ngoja niicheze tena ninaweza nikaelewa zaidi lakini mhhhhhhhhhhh
  Dr.Majita (PhD)

 8. Dr.Majita Says:

  Nimerudia tena kuucheza huu wimbo naona maana yake iko “VESA VAISI”.Nahisi labda katika kushuti huyo aliyekuwa anashuti picha aligeuza kamera na sehemu alikokuwa anatakiwa kuwepo Nuru yenyewe ikawa inamuweka huyo jamaa,na sehemu ya huyo jamaa akawa anakweka Nuru.Hope waki-shoot tena kamera ikageuzwa italeta maana na kueleweka zaidi
  Dr.Majita (PhD)

 9. Kafura Says:

  Mama naona anajivunia kifua chake katika video. Uongo…umebarikiwa. Cha aina hiyo wengine hukipata kwa plastic surgery!

 10. BLACKMANNEN Says:

  Dada “Kokusima”,

  Hukuelewa nini katika video hii? Kwani unataka kuelewa kitu gani hapo? Kama hujaelewa kitu, nenda kamwulize yeye mwenyewe “Nuru” maana wewe na yeye ni majirani.

  Haya tena, mabibi na mabwana wa BC, binti yetu ndiye huyo, yupo hewani tena kwa mara nyingine. Mategemeo yangu yote ni kwenu WanaBC, katika kumwelewesha, kumwelimisha, kumsahihisha na hata kumpongeza kama amefanya kile mtu ulikitegemea akifanye.

  Nuru ni mtu aliyelelewa katika malezi yenye maadili mema, ndiyo maana hata video zake zote zinakiwango cha juu, na zinakubalika kwa watu wote, watoto na wakubwa. Jinsi aonekanavyo kwenye video zake, ndivyo alivyo hata kama utabahatika kumwona “LIVE”.

  It’s Great To Be Black=Blackmannen

 11. jenga Says:

  naungana na mchangiaji wa 2,mfuniwaji hajashtuka na wala mfumaniaji hajachukua hatua yoyote? hii si kawaida ya wanaume hata kama ni ndugu! lkn naye nuru anaoengelea maneno ya watu wakati amemtenda jamaa na wala haonyeshi kujutia wala kuomba msamaha! picha na maneno ya wimbo yanachanganya,ila wimbo bila kuangalia picha umetulia!

 12. kakam Says:

  kwanza katupa walimwengu..halafu msela…mimi nimekupata bc..ni kwamba wewe ulitarajia jamaa atatia ngumi jamaa mwenzake baada ya kuwafumania i got you,,,,instead jamaa kafanya vingine,,nice song nuru na hapa umeonyesha vocal skills yako sasa yanne naomba utupe mambo ya ngwasuma tujue kama unakatika au sio….mimi nimependa kazi yake tena sanaaa hongera nuru

 13. DUNDA GALDEN Says:

  Haya kazi kweli kweli vesee vaiceee

 14. emergencypoison Says:

  that guy is a a total fake, jamaa mgoni wala hajashituka kufumaniwa,halafu at the end eti anamkumbatia mwenye mali kana kwamba anambembeleza, ujinga mtupu…aise mi ningemchapa vibao haraka sana…

 15. james Says:

  Nimependa sana blog yako pia ni mpenzi sana wa blog ya wana ccm marekani http://www.ccmmarekani.blogspot.com Napendekeza uweke link yako kwenye blog yako

 16. sweetest sin Says:

  wewe nuru mwimbo hauendani na video. halafu cha kushangaza eti wote watatu wanakumbatiana mwisho,hili ni stori la alinacha halitokei duniani haiwezekani hata siku moja.

 17. Kokusima Says:

  eheee blackman simwelewi anachokiongelea, kama atakuwa anajali kama dadetu Jennifer atajibu hapa. yani naona yeye ndo anaibisha alafu analalamika kwa nini hehehe hapo shughuli asante blackman

 18. mdau Says:

  Huyu mtoto kwa kweli kifua anacho.Lakini kama mtu unamtakia mema kwenye hiyo career yake,kwa kweli hutosita kumwambia haya ninayotaka kumweleza.

  1.Hakuna connectivity kati ya kunachozungumzwa na reactions za wahusika.Katika hali ya kawaida nilitegemea kuona jamaa anamtolea dirishani yule mwanaume aliyemfumania.

  2.Bibie inabidi aje tofauti kidogo,kwa sababu nyimbo zinaonekana zimejaa chorus zaidi kuliko vionjo vingine.Ukisiliza huu wimbo ni sasa kwaaaaaaaaaaaaaaanini,sasa kwaniniiiiiiiiiiiiiiiiiiii.Nahata ile walimwengu nayo ukiisikiliza ni walimwenguuuuuuuuuuuuuuu,walimwenguuuuuuuuuuu mpaka mwisho.Hili nalo inabidi aliangalie.

  3.La mwisho ambalo ni “lamsingi” na ndo “litakalomsaidia zaidi” inabidi mnisaidie namba yake ya simu ili niweze kuzungumza naye “faragha” ili kumsaidia zaidi kwenye kuboresha mziki wake.Naamini nikiwa nae karibu haya maoni yooote ya busara ili afanikiwe atakua anajipimia mwenyewe.
  Chonde chonde jamani Chonde,tumsaidie mtoto huyu jamani.Tafadhali namba yake jamani waungwana.

  Mdau,
  UK.

 19. Mwanamke wa shoka (UK) Says:

  naona kuna mgongano wa maneno na picha….sasa mnasemaje wana fasihi….

  ila Dr Majita, PhD umeniacha hoi….inaonekana unapenda hotel ya chukulubu sana wewe…tehe tehe tehe….
  mmehiandaaje wan BC na the around the corner “Obamalisation”…..naona Kezia ameshawahi…..(Mungu ampe nini…!!)….

 20. Mattylda Says:

  this time sijaona kitu! sorry!

 21. BLACKMANNEN Says:

  He he he he heeeee!!!! “mdau” comment # 18, umeniacha hoi kwa lile oni lako la mwisho, namba 3 lenye msisitizo mkubwa.

  Kama kweli unania ya kumsaidia Nuru katika shughuli zake za kisanii, mwaga contact zako hapa BC, na kama yeye ataona kuwa kuna umuhimu wa kuwasiliana na wewe atakutafuta.

  It’s Great To Be Black=Blackmannen

 22. Sam Says:

  I dont think kuna kitu chochote cha ajabu… i don’t know kama unamaanisha jamaa kulia au… kutofanya fujo… kabila letu hicho ni kitu cha kawaida kufanya but in the end mtu anajitundika.. that’s our reaction.. so may be dadaa afanye wimbo mwingine ambao ni continuation ya huu… au mnasemaje wahehe wenzangu??!!!

 23. vyne Says:

  Nilidhani mie peke yangu sijaulewa wimbo.Binafsi nimeshauri arudi shule akajifunze MAUDHUI ya hadithi yake.She isa black blonde auza wimbo kwamaungo aaaiiii aibu.

 24. sweetest sin Says:

  we blackmannen nimegundua kila sehemu unajibu wewe,kwani we meneja wake au?

 25. salma Says:

  jamani mbona siwaelewi watu humu ndani kwani dada yetu kaimba kizungu au kiswahili….sasa kwanini imekuwa hivi..yote tulopitia wangu yaani huu ndio mwisho,,hio ndio mistari from the chorus
  mwimbo unahusu kuwainvolve watu in in your relationship n wat happens when you do so…
  jaribu kusikiliza mwimbo tuu bila yakuona hiyo shooting instead of kutizama matendo yaliyomo kwenye hii shooting..

  na huyo aliyecomment nr 23..sikujua kama nasisi wasichana weusi tumeanzwa kuitwa blackblonde i suggest wewe ndio uende shule maana hii sio nyimbo yake ya kwanza na haitakuwa ya mwisho na nuru shooting zake anatumia maungo wapi nigga pliz…mbona kina beyonce na mariah carey wakikaa uchi hamlalamiki
  ivi wahehe hii nikitu ya kawaida mimi sikujua….mmmh kali hii

  ahsanteni

 26. haluu Says:

  ni kweli nimegundua hata mimi huyu black blackmen amejibu kila sehemu utafikiri yeye ndiyo promota wa huyu binti. vipi ndugu yetu,wewe ndiyo yule promota wa kubeep beep au?waachie basi na wenzio nafasi jamani

 27. BLACKMANNEN Says:

  Kwako sweetest sin, comment # 24

  Kwani hayo majibu yangu na maoni ninayotoa hapa, yanausumbua sana moyo wako? Kitu nilichomweleza Kokusima amenielewa na amekijibu (comment # 17).

  “Mdau” (comment # 18), amenichekesha hadi mbavu kuniuma kutokana na hilo oni lake la mwisho lenye msisitizo. Je, kuna kitu gani kilichokushangaza wewe hapo? Au roho yako itafurahi ukiona nikimponda Nuru?

  Hapa kila mtu anao uhuru wa kutoa maoni yake kwa kadri anavyoona. Sio lazima nielekee kule unakokutaka wewe, na wewe sio lazima uniunge mkono ninachokisema. Nuru kakubali kuja hapa BC, ili tuone kazi yake. Jukumu letu ni kumwambia kile tunachokiona katika kazi yake, ili azidi kuboresha pale atakapoambiwa kuna mapungufu katika kazi yake hiyo.

  Katika uwanja huu wa BC, kuna tofauti kubwa ya utoaji maoni. Wengine wanatumia maneno yenye mwelekeo wa chuki, kebehi na udhalilishaji. Na wengine wanatoa maoni ya kumwelimisha, kumsahihisha na kumpa moyo mtu. Kwani fani ya kisanii inaushindani mkubwa sana hapa duniani, mtu utahitaji maoni ya wengine ili kujiweka vema katika shughuli.

  Kazi yetu wote hapa ni kumsaidia aendelee na sio kumkatisha tamaa na kumdidimiza.

  This Is Black=Blackmannen

 28. vyne Says:

  Bi Salma mbona una ghubu kama nimekuibia mumeo? I have a right to my opinion and I this this song is shit so what are u going to do abt that? Au we lesbo sucking up to her?

  Hata kwa sekunde usijaribu tena mfananisha Nuru na Beyonce au Mariah, she isnothing like them

 29. anonymous Says:

  am sorry, this whole song is garbage!! seriously people if u cant sing dont do it!!

 30. Whitemannen Says:

  Jamani BC msiwe munatuwekea picha style hii huwa zina tupain!!!

 31. msumali Says:

  HATERRRRRRRRRRRSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSS STOP IT HIVI WABONGO MUNA SHIDA GANI. LET THE GIRL BE. ACHENI UJINGA WA KUHATE KILA SEKUNDE. WEWE UNAYE HATE HEBU TUONESHE UMEFANYA NINI JAMANI? KABEBE MABOX NYIE HATERS THAT’S ALL U KNOW. NA HII BARIDI INA ELEKEA WENGINE MUMEKAA KWENYE COMPUTER TUU HAMUNA LA MAANA.

 32. msumali Says:

  mhhh aisee watu munashida sana eti. haya wabeba mabox inaelekea mmebeba mpaka inawauma mkiona mtu wingine anafanya cha maana na sio kubeba box eti. HI HATERS BYE HATERS, I SEE YOU HAHHHAHHAHAHHA

 33. POPO Says:

  HAHHAHAHAHHA UWIIIIIIIIIIIIIIIIII MUSUMALI UNACHEKESHA MIMI NIMETOKA KUBEBA MABOX SASA HIVI NA BARIDI INANIUMIZA JAMANI. PLSSSSSSSSS HELP SOMEONE BOX LIMENICHOSHA

 34. chapombe Says:

  wajameni yeye anaimba bongofleva,na hii video ni ya kibongofleva kwa hiyo poa tu.sema huyu binti kifua chake kinauzika,au nyi mnasemaje?

 35. haluu Says:

  wewe popo ndio msumali..acha kujijibu mwenyewe wewe,he! wa ajabu kweli!

 36. Kweli man Says:

  dada nuru
  Great job! loved the video .But the song, not necessary
  Kweli kwangu mimi it was all but the video .the video is a sure knock off .absolutely. Kudo to the director ,producer and the the whole crew.Ofcourse ,this goes to you as well .Because if you you did not play it out well ,it would definately suck.
  If you can remember your last video here .Technically i watched them both repeatedly.Nothing compares to this video especially if you look at the technical cinematic attributes of it
  The combination of MOT story and you performing live is really owsome .Looks really professional. Looking at the kind of songs you like performing i guess this kind of technique fits perfectly with the pace and your kinda stories

  I checked your substance,different shots/angles,your performance and the flow,if i have to compare with the last video i saw here,dada.there is no comparison .period .this video is waaaaay over the top. At least that’s my opinion

  A few things obviously it seems to me that your director and producers have got work on.
  Make shots more dynamic
  Video’s pixels are so obviously visible
  Video is too videosh (bring on that filmic look)
  But other than that .i must confess , this time together with you they made a great accomplishment.to me this video is a real deal,relatively speaking
  Tena naona this time dada ,kuna kiwango cha ukomavu fulani ktk acting yako .inaokena ukomavu .ile ya wakati ule ilionekana so “staging” it was a crap , if you ever ask me
  Energy niliyoiona kwenye video hii kwa kweli it was exceptional .it fits so perfectly with your emotions,the overall pace of the the song and ofcourse the substance of your song

  Nuru dada,hongera .kazi nzuri japo mziki wenyewe siupendi .kazi ni nzuri.pia hongera sana kwa kuzingatia ushauri nilioutoa last time hapa kuhusu video qualities
  my opinion to you. usisikilize sifa za kinafiki za kitanzania soma criticism na ujifunze ktk hizo criticism you can always pick a thing or two Nuru una potential kubwa sana nionavyo mimi ya kuvuka daraja na kuenda kwenye ulimwengu wa pop wa kimataifa ,you’ve got the looks ,sauti unayo japokuwa hujui kama unayo au labda haifit aina ya muziki yaani bongo flava sijui lakini you got it all (great vocals) isipokuwa matumizi yake … if anything i would say ..it’s OK ,pili bado ni kijana mdogo yaani umri wako unaruhusu .chukua vocal au singing lessons usually kwa mtu kama wewe my guess tells me it will be about six months .hakika utaweza kuandika nyimbo vema,kuimba aina yoyote ile ya mziki kiutaalamu kabisa,bahati mbaya huko ulipo sweden si hasa sehemu nzuri lakini with all the ammunitions you’ve got ,dada only sky is your limit
  KIla la heri
  Kweliman
  Edmonton Canada

 37. Kokusima Says:

  Hapa hatupondani, hatutukanani wapenzi, lazima ukweli tuuweke wazi. Video haikwendana na mwimbo, bila kumwambia hivyo atajuaje kosa?? Dear Nuru mimi nilishindwa kuelewa wimbo coz, wewe umeibisha, alafu unasema hivi kwa nini, kwa nini sasa wakati wewe ndo umeibisha na ukafumaniwa?? Ungekuwa unasema hivi kwa nini nawakati bwana kakuibishia hapo sawa, video haiendani na wimbooooo.

  Blackmannen husiwajali, wasiopenda ukosoe, au ujibu hii nikuonyesha unajali, wanaosema uwaachie wengine, wengine kinanani? mbona tokea mada ianze sijaona mtu akijibu?? SABABU Unaijua?? Wanaogopa kuitwa wambea. Haya wabongo tutasongaje mbele kwa kuwaogopa watu?? Kazi tunayo

 38. Sikujui Says:

  sijaelewa chochote yaani hata sijui kilichoendelea zaidi ya kuona kifua tu. maudhui na shooting kizungu zungu

 39. halima Says:

  Mhhhhh!!!!!!!! kazi kweli kweli

 40. POPO Says:

  HALUU UNASHIDA NA MIMI AU ETI NIMEJIBU MWENYEWE, ACHA KUFATILIA WATU WEWE KITU ZIMA. MBONA UNAPENDA KUHATE SANA,SASA SHIDA YAKO NINI. U WISH YOU WERE ME MBUZI WA KIZARAMOOOOOOOO WEWE.

  HALUU inaelekea wewe ndio hao wabeba mabox wasio na mbele wala nyuma hapa kisa cha kutaka kuanzisha ungovi ni nini?

 41. Dr.Majita Says:

  Haya tena kazi imeanza.Msumali ndo huyo huyo popo.Sasa wewe popo mwenye kazi mbona unajijibu mwenyewe???

 42. BLACKMANNEN Says:

  Kweli man, comment # 36,

  Maoni ENDELEVU na yaliyoenda shule kama hayo, ndiyo tunayoyataka hapa BC. Maoni yako ni shule kamili si kwa Nuru pekee yake, bali ni kwa kila mtu anayependa maendeleo.

  Tanzania kama tungekuwa na watu kumi wa aina yako (Kweli man), uwanja huu wa BC, ungegeuka kuwa chuo cha kujifunza mambo mengi mapya ya kimaisha kwa Watanzania, badala ya watu kuja hapa kuonyesha chuki zao za wazi, na wivu usiokuwa na maendeleo kwa Watanzania wenzao.

  Comments # 28 na # 29, zinatuonyesha ni jinsi gani Watanzania wengine tulivyo nyuma kimaendeleo, na tupo tayari kuwasifia wasanii wa Kimarekani (Beyonce na Mariah) ambao wala hawatayaona maoni yetu na wala upendo wetu kwao. Lakini NURU wetu anayasoma maoni yetu hapa, na kuyatafakari na pia kuyafanyia kazi.

  Dada Kokusima, comment # 37, nakubaliana na wewe kuwa ni kweli Wabongo “Kazi Tunayo”, tena si ndogo katika kulisukuma gurudumu letu la Maendeleo kwa Watanzania.

  It’s Great To Be Black=Blackmannen

 43. binti-mzuri Says:

  hahahahahahhahahahhahaha ujue wewe majita unanichekesha sana..lol..huyu popo bawa mi kanichekesha si kis*ng* .. na nuru anaitaji proactive,ila hina hilo babake ndilo la kisawasawa,inaelekea hujakolezwa mambo ya pwani..hio iko fresh

  naona kuna blackmannen na whitemannen! … humu bc ni vituko vya hali ya juu.

  nuru sista doo,naona mambo yako si kitoto.. u look whoa,ila kama wengi walivyosema we ndio umeibisha halafu wewe ndio unauliza kwanini HEEEE!toba yairabi!hizi video huzikagui kabla ya kuzisambaza..kwenye mfumanio hapo umechemsha na kuunguza..ila sio siri umetoka ki beyonce beyonce vile..ur cute..sema im not 100% sure if i would buy your records..so far zote zipo too slow..try mixing different stuff kama rayc na jide..a little bit of everything..other than that,bravo! 😉

 44. Mattylda Says:

  Job tru true hapa duuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu yote tisa kumi KWELI MAN, U SAID IT ALL WELL DONE BRO!!!!!!

  Kingine Chapombe umenivunja mbavu mie hhahahhaaa!

  Abt this song, Nuru sio kama tunaponda but the reality is that the video doesnt match with the song ma dear,mbona last time ulifanya vizuri na tulikusifu?pls work on it!

 45. Kokusima Says:

  ahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! mbavu zangu leo jamani, kumbe m2 unaweza ukaandika kisha ukajijibu ahahahaaaaaa,hii inatia aibu kidogo yani nacheka hapa ahahaa, nilikuwa nimeshajiuliza mmemgunduaje popo a.k.a msumali ahahaa kweli nilipogundua nimecheka hadi basi, afu hata majibu yalivyofuatana lazima ugundue kuna kitu kabla hujakamatwa na mtego wa bc, unajua ukiandika post zinachukua muda mpaka ziruhusiwe na bc kuonekena hapa, ila za msumali a.k.a popo zimefuatana km dk nyingi ni mbili tatu.

  Pole kakangu popo msumali ila husirudie tena kujijibu unajidhalilisha.

 46. haluu Says:

  we popo hacha kutukanana sio utamu hapa,unabisha nini na ushapatikana. you are busted, the least you can do is KULA KONA

 47. salsa Says:

  Nuru Magram kuwezesha kazi yako ionekane hata kama watu hawakujui, video yako ungeipachika jina kubwa zaidi ya kwanini- nuru na kuweka jina kubwa Tanzania – kwanini -nuru.

  Pia TAGS: Tanzania music – kwanini -nuru. Nasema hivyo kwa kuwa nikifanza search kwa jina :Nuru magram jina lako hali pop-up bali zinakuja kazi za watu wengine duniani.

  Pia nikiweka ‘kwa nini’ zinkuja kazi za jirani zetu Kenya. Si wewe tu bali wasanii wengi wa Tanzania wanafanya kosa hilo la msingi na kazi zao kutazamwa na watu wa ‘ mtaani’ kwao tu walio bahatika kuwajua vyema.

  Wasanii mkumbuke kuwa YOUTUBE ina ‘archive’ ya mamilioni ya kazi za wasanii duniani na ina ‘biase’ ya kutanguliza kazi za nchi/mabara mengine yaliyotawala youtube kwa ‘tags’ zilizopangiliwa vizuri au kwa vile ni wasanii maarafu kama vile wa Amerika, Ulaya na Arabuni.

  Ni hayo ila nimependa sana mdundo na quality ya sound, na ukifuata hayo mapendekezo hapo juu kazi zitaonekana na hata watu walio mbali na wewe, kwa ku-search:’Tanzania music’ na kazi yako na za wabongo wengine zitaibuka na kutambua, kumbe yupo Nuru au FidQ au Dulla Sykes au AY au Tanzanite band au Kilimanjaro band au Msondo au RayC au Kinasha au Mchiriku au Segere au ZeComedy au Mzee Small au Bi Chau, au Sedekia au Mtoni lutheran au Kijito n.k

 48. watubwana Says:

  kwikwikwikwikwi…hehehehehe…tehetehetehe ..
  siri ya mtungi aijuaye ngata.
  watanzania wote jamani huu ni mwaka wa KIMAENDELEO,huu ni mwaka wa WAAFRICA,
  OBAMA 1st BLACK PRESIDENT,
  LEWIS HAMILTON1 1st BLACK F1 WORLD CHAMPION,
  WILL SMITH WORLD’S HIGHEST PAID ACTOR,
  TIGER WOODS WORLD’S BEST GOLFER, haijalishi hata kama ni mchanganyiko ila bado wanauafrika ndani yake so iwe changamoto kwetu sote kuwa na sisis TUNAWEZA.
  tuwe na mawazo ya kimaendeleo ya kumsaidia mtu na si kumkandia tu,mkandie mpe mawazo mazuri ya kumuelimisha na sio ya chuki,wivu,ubinafsi,VYOTE HIVYO havijengi.
  kuijenga nchi yetu TANZANIA sio mpaka kila mtu ashike nyundo na misumari,ni kwa mawazo ya kimaendeleo.mpeni mawazo nmazuri Nuru na kumsaidia aendelee vizuri na fani yake.na sio kumkatisha tamaa.asanteni

 49. anonymous Says:

  wewe sijui “popo” watu wakiongea ukweli doesnt mean that they r hatin dummy…she might be gud but judging from this song and the video….AM SORRY KACHEMSHA!! WHY WUD ANYONE HATE ON A GAL LIKE HER? SO WAT KAMA WATU WANABEBA BOX, BORA WAO KULIKO WEWE MPANGUSA MAVI YA VIZEE VYA KIZUNGU! GTFOH


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s