BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

ANSBERT NGURUMO ANAPOJADILI BLOGS January, 18, 2009

Filed under: Blogging,Blogs,Mtandao,Uandishi — bongocelebrity @ 1:50 PM

ansbert-ngurumobcJina la Ansbert Ngurumo sio geni hata kidogo miongoni mwa wapenda habari na mawasiliano na hususani wapenzi wa habari za magazetini. Ansbert ni miongoni mwa waandishi wa habari mahiri nchini Tanzania ambao wamejijengea sifa na heshima kutokana na kazi zao za uandishi wa habari.

Safu yake ya Maswali Magumu,inayochapishwa katika gazeti la Tanzania Daima kila jumapili inabakia kuwa safu yenye wasomaji lukuki huku kila mara ikizua mijadala ya aina yake jambo ambalo ni uthibitisho kwamba sio tu inapendwa bali pia hujibu na pia kuuliza Maswali Magumu.

Ansbert ni blogger mzoefu pia.Blog yake ambayo inaongozwa na kichwa cha habari, Utakapojua Hujui Ndipo Utakapojua, ni sehemu mojawapo nzuri ambapo unaweza kukuta kazi zake za uandishi,mitizamo na pia mikingamo.

Hivi karibuni,jamaa wa mtandao wa Rap21,walifanya naye mahojiano ambayo kwa kila hali ni “must read” kwa mtu yeyote ambaye yupo kwenye fani ya ku-blog au ni mfuatiliaji wa maendeleo ya tekinolojia hii ambayo mimi naiita mapinduzi ya karne katika ulimwengu wa habari na mawasiliano.

Katika mahojiano hayo,Ansbert ameongelea kwa mapana jinsi ambavyo blogs,ikiwemo ya kwake, zinazidi kuboresha mapinduzi hayo na pia jinsi gani blogs zinaweza kutumika katika kuboresha maisha ya wanajamii,kutunza historia zetu,kufichua maovu nk.Bonyeza hapa ili kusoma mahojiano hayo.

Advertisements
 

7 Responses to “ANSBERT NGURUMO ANAPOJADILI BLOGS”

 1. Hamisi Says:

  Ngurumo,
  Nimekubali kaka.Mahojiano mazuri sana hayo.Naamini kila mwenye kutaka kublog proffessionally anahitaji kusoma haya mahojiano.Hongera

 2. BLACKMANNEN Says:

  Mimi huyu jamaa simjui kabisa. Lakini kwakuwa kumbe ana “Blogi” yake, nitaanza kuitembelea ili nimfahamu. Nawashukuru BC kwa kutufahamisha na kumleta hapa ndugu yetu huyu ili tumjadili.

  This Is Black=Blackmannen

 3. Mattylda Says:

  mhhh simjui, ila kazi nzuri kaka!all the best!

 4. Dinah Says:

  Si wa Kitururu naomba unitafasirie tafadhali.

  Asante Ngurumo kwa kuweka wazi maelezo fulani ambayo ni jana tu nilijikuta nina hasira za ajabu mpaka nikatamani kulia baada ya mtu mmoja kudai kuwa Uandishi wa habari ni Umbea/Udaku (kufuatilia maisha binafsi ya watu) na wote wenye kublog hawana tofauti na Waandishi wa habari 😦

  Nadhani sehemu ya mahojiano yako imesaidia baadhi ya watu kutambua tofauti kati ya Uandishi wa Habari (Journalism) na Uandishi (Writer).

 5. @Di a.k. Dinah: ngojea nimuachie Jeff na timu ya BC katika tafsiri:-(Asikulize mtu DI, watu hawataacha kusema hata iweje na kisiwe kitu cha kukukatisha tamaa.

 6. CityBoy Says:

  Dinah usilie bana, ukilia nami utaniliza!!!!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s