BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MH.SOFIA SIMBA;UNAMSHAURI NINI? January, 25, 2009

Filed under: Siasa,Tanzania/Zanzibar,Wanawake na Watoto — bongocelebrity @ 6:48 PM

simbabc

Pichani ni Mheshimiwa Sofia Simba,ambaye hivi karibuni alichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM nchini Tanzania.

Mheshimiwa Simba alichaguliwa katika uchaguzi ambao unasemekana ulikuwa wenye upinzani mkali katika historia ya jumuiya hiyo.Alishindana vikali na Mh.Janeti Kahama.

Kama zilivyo chaguzi nyingi kinachofuata baada ya vuta nikuvute huwa ni kazi.Je unadhani ni matatizo gani ya msingi yanayowakabili wanawake wa Tanzania?Ungependa kumpa ushauri gani Mh.Sofia Simba kuhusiana na Jumuiya anayoiongoza?


Advertisements
 

19 Responses to “MH.SOFIA SIMBA;UNAMSHAURI NINI?”

 1. any Says:

  Tunamshauri apunguze ulafi wa madaraka, kuna wengine ambao hawana cheo hata kimoja wangepewa na yeye afocus kwenye area moja, Majukumu yakizidi utendaji unapungua.

 2. Shostito Says:

  namshauri aache kuvaa ushanga mkubwa hivyo!!!!!!!!!!

 3. Gervas Says:

  wanawake wa vijijini wamesahaulika, ajikite hasa na wanawake wa vijijini kwa kuwapa elimu angalau ya kujua haki zao za msingi na elimu ya kujitegemea, wala asibague tu kwa wanawake wa ccm bali awahudumie wote maana jamii ni moja. Tatizo lao hawa viongozi wanavokuja hapa vijijini ziarani, wanasimama dakika chache tu wanapayuka kwenye vipaza sauti, kina mama wanacheza kidogo ngoma za asili afu wanawapa zawadi kama elfu tano hivi ndo imetoka hiyo. Hawa wanahitaji elimuna wala sio elfu tano!!

 4. bombe Says:

  muheshimiwa simba fanya kazi kwa bidii usisikilize maneno ya watu wanaoleta chuki zisizo na hoja.uchaguzi uliisha isha na mshindi ni wewe,sioni faida ya kuleta maoni yanaozidi kubomoa badala ya kujenga au sijui udini wameweka mbele maana kahama alikuwa anafanya kampeni kubwa makanisani.

 5. Mwanamke wa shoka (UK) Says:

  Mheshimiwa Sophia….tujiweke vipi tuinue elimu ya watoto wetu….elimu imeshuka….kulikoni…..(weye si waziri wa Elimu…lakini kama MAMA…na mwenyekiti wa Wanawake Tanzania….unalionaje hili…..??)…..nini tukifanye tukianzia hukooo majumbani mwetu kuwainua watoto wetu ambao ni taifa la kesho….??…mafao ya waalimu ni duni…hawana moyo saana na kazi yao ya kusukuma elimu juu…..malezi ya wanetu yameporomoka…..hawazingatii saana masomo ili waweze kumudu maisha yao ya usoni…..
  …tufanye nini..????

 6. Doroni Says:

  Huyu sophia simba anapashwa apige marufuku tabia moja uswahili halafu hawambie akina mama waache ushirikina, pamoja na umalaya uliokisiri katika mambo ya uchaguzi, hasa katika mikoaya Kagera,Mwanza, na Dar es Salaam, wanachaguliwa watu wasiokuwa na uwezo wakutawala. wanachaguliwa wanawake eti baba yake alikuwa mbunge, au mtu mwenyewe ajuhi kusoma wala kuhandika. Mtu anachaguliwa kwa ajili yakuhuza mwili wake pamoja na mamboya ushirikina. eti ni mwenyekiti wa UWT wa Wilaya au Mkoa.

  Naomba hilo uliangalie maana sasa utafanya kazi na watu waliofumbuka akili na wasomi,

 7. Mickey John Amos-Denmark Says:

  HONGERA MH. MAMA SIMBA.

  Namuunga mkono mchangiaji # 3

  Kina mama haswa vijijini wametumika
  saana katika kujenga “Taifa” na wametumiwa
  saana kama “sura ya utamaduni wetu” lakini
  wamepata huduma haba katika mazingara
  ya maisha ya kila siku.

  kazi kubwa, inahitaji “hekima na busara” timamu kuleta
  mafanikio ya uhakika kwa kina mama mikoani na
  vijijini.

  Kina mama (wanawake) ni “moyo” wa nchi yetu ukisimama na nchi nzima itasimama,hakuna siasa ya aina yeyote itakayoikoa
  nchi yetu tukufu.

  Mickey@mail-online.dk
  Copenhagen

 8. hombiz Says:

  Hongera mheshimiwa Sofia Simba.

  -Elimu ya uzazi wa mpango na ile iliyo ufunguo wa maisha. Hii itamsaidia mwanamke kupambana na kukabiliana na mazingira yake kiufasaha bila kuwa tegemezi kwa mwanaume-hasa aliye mnyanyasaji.
  -Kinamama hasa wa vijijini (kama alivyobainisha mtaalam Gervas ktk post # 3), yafaa waelimishwe juu ya kuzijua haki zao za msingi ktk mahusiano na waume zao na jamii kwa ujumla.
  Kupambana na tatizo la vifo vya kina mama na watoto wachanga vinavyosababishwa na aidha maradhi ambayo yanaweza kuzuilika, ama kutokana na tatizo la huduma duni wakati wa ujauzito na kujifungua.
  I wish huyu mama atafuata nyayo za marehemu mheshimiwa Amina Chifupa ambaye alipigania hali ngumu za afya na maisha zinazomkabili mama mjamzito fukara, asiye na uwezo wa kununua pamba, doti za kanga, sindano na dawa za kumsaidia wakati wa kujifungua. Hayati Mh Chifupa alipigia kelele maswala kama haya ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nguvu zote.

  Ushauri wangu kwa Mh S. Simba ni kwamba matatizo ya kinamama yako mengi. Ila ningependa ukabiliane na yale ambayo ni sugu zaidi kama hayo machache niliyobainisha hapo juu. Haya mambo ya kuwa bola mwenyekiti kuliko mwenyekiti bora, yanazidi kuwa-bore wake zetu, mama zatu, dada zatu, (hasa wasio na uwezo kiuchumi)n.k.

 9. BLACKMANNEN Says:

  Mheshimiwa Simba!

  Tabasamu lako linamvuto usio wa kawaida. Ahsante kwa tabasamu lako hilo, limenipa furaha ya aina yake moyoni mwangu. Hongera sana kwa kuchaguliwa kushika wadhifa wa Uenyekiti wa wanawake Tanzania.

  Jukumu ulilopewa na wanawake wenzio kuwaongoza ni kubwa na gumu sana. Hekima na busara zako ndizo zitakazoleta mafanikio katika kuwaendeleza kina mama zetu wa Tanzania.

  Namwunga mkono “Gervas”, comment # 3. Mara nyingi wanawake wanatumiwa kama chombo cha burudani na husauliwa kutatuliwa matatizo yao.

  Wanawake wa Tanzania na Afrika kwa ujumla, wametawaliwa kifikra na wanaume. Sitaki niingie ndani zaidi katika kufafanua hiki nikisemacho hapa, lakini natoa mifano miwili.

  Kwanza, Watanzania tunapozungumzia mmonyoko wa maadili upande wa “mavazi”. Kila mtu anatizama mavazi ya wanawake na wala sio ya wanaume. Kina mama mnatakiwa kukomesha fikra za aina hiyo za wanaume na wanaume wanatakiwa kudhibiti tamaa zao zisizokuwa na mpangilio.

  Pili, Watanzania tunapoongelea kuhusu “Umalaya”, kila mtu anawaza machangudoa mitaani ambao ni wanawake. Mwanaume anayewafuata wanawake hao, hahesabiwi kama naye ni malaya. Hakutakuwa na changu yeyote mitaani, iwapo hawatachukuliwa na wanaume.

  Ugumu wa maisha ya mwanamke, unachangiwa kwa kiasi kikubwa na wanaume, ambao kila sehemu mwanamke anawindwa na wanaume ili atafunwe kama simba anavyomuwinda swala kwenye Mbuga za wanyama. Mtoto wa kike akiwa shule, anakodolewa macho na walimu wake wa kiume. Akizubaa kidogo tu anatafunwa kweli. Mh. Sofia Simba, kazi unayo!!!

  Mengi ya kusema hapa nawaachia wanawake wenyewe, kina Mattylda, any, binti-mzuri, Mwanamke wa shoka (uk), halima, Lalola, Dinah, Mama wa Kichagga na wengine.

  This Is Black=Blackmannen

 10. halima Says:

  kwanza napenda kukupongeza kwa kuchaguliwa kwako kuwa kiongozi wa jumuiya ya wanawake wa UVCCM.

  Mama Sophia simba kazi uliyokuwa nayo ni kubwa sana kutokana na jins wanawake wa tanzania tulivyo nyuma kimaendeleo hasa vijijini.

  Elimu ya Uzazi wa mpango inatakiwa iwafikie kule sitimbi kinyume cha hapo unaweza umalize miaka yako ya uongozii na bado hujawasaidia chochote wanawake wenzako.

  Utoaji wa mimba kwa wanafunzi unatakiwa ukomeshwe mara moja ilikunusuru maisha ya wanafunzi hao. haya machache niliyoyazungumzia yanahitaji msaada mkubwa kutoka kwako. Nakutakia mafanikio mema katika kazi yako.

 11. Mama wa Kichagga Says:

  Doroni, “simba anapashwa apige marufuku tabia moja uswahili halafu hawambie akina mama waache ushirikina”

  Is totally incorrect phrase to describe how you feels about women in political positions. Are all women use prostitution to get their post? I think you should take your political agenda elsewhere.

  Say want you want but no one can point a finger to women in political positions basin on your poor research.

  Sophia Simba exemplifies all that a decent woman should be and she deserves that position. So back off, lady!

  Simba intends to do her best to put Tanzanian women on the map and to prepare a better place where women and children can live to the fullest. Appreciate that.

  People always try to bring others down especially when they excell in their life. Shame on them all.

  Blackmen, very well said, you took the words out of my mouth & thnkx.

 12. kindo Says:

  Blackmannen, Gervas na wachangiaji wengine mmesema kweli kabisa nawaunga mkono asilimia mia moja. Napenda kuongeza tu kuwa wanawake wanatakiwa kuondoa fikra za kutegemea wanaume. Hii tabia ndio inadhoofisha wanawake katika kila kada kwamba mwanamke bila msaada wa mwanaume hawezi kufanya lolote. Hii dhana ya utegemezi inatokana na mfumo dume uliopo. Lakini katika zana hizi za utandawazi mwanamke yeyote anaweza kujitegemea ili mradi tu awe na confidence na uwezo wa kusimamia kitu anachokitaka. Kwa hiyo challenge kubwa ni kwa Mh. Simba kuhamasisha awareness on self-confidence among women, self-reliance na uwezeshaji kiuchumi. Kama mtu hana confidence, awe mwanamke au mwanaume, hata ukimuwezesha ni makidamakida tu. Na ndio maana wanaume wengi wenye mawazo finyu mara tu akioa anamuachisha kazi mkewe ili kuondoa kabisa confidence yake. Ndio sababu pia wanawake wengine hupigwa sana na waume/partners wao lakini hawathubutu kuwashtaki kwasababu anaona huyo mume/partner akifungwa basi survival yake ipo mashakani. Ni challenge kubwa alionayo Mh. Simba ila mapinduzi yanatakiwa yaanzie kwenye akili za wanawake wenyewe. Wale ambao wana upeo tayari wahamasishe wenzao kwa vitendo kuwa “mwanamke anaweza”. Zipo gender NGOs nyingi, lakini zipo mijini, na mjini kwenyewe ni wanawake wachache sana wanafikiwa. Tungependa kipindi cha uongozi wa Mh. Simba kiwe kipindi cha mageuzi ya vitendo…hata akimaliza muda wae wa uongozi awe na kitu cha kuonyesha. Sasa hivi ukiniuliza vision au mission ya UWT sina cha kukuambia…… wapo wapo tu!

 13. said komba Says:

  HONGERA MAMA ACHANA NA WAOSHA VINYWA
  PIA NINGEPENDA KUWAFUNDISHA WASIO JUA NINI MAANA YA MSWAHILI MAANA INAONESHA WA TU HAWAJUI NINI MAANA YA MSWAHILI
  MAANA MOJAWAPO YA MSWAHILI NI MTU ANAEZUNGUMZA KISWAHILI NA PILI NI MTU AMBAYE AMESTAARABIKA MTU AMBAYE ANAUJUA USTAARABU NINI
  PIA NIMTU AMBAYE ANAKONTACT NA WATU WENGINE HASA PWANI KUTOKANA NA KUFANYA BIASHARA AMA VYENGINE
  WAKATI SISI TULIOTOKA POLINI KIPINDI HICHO TUNAJENGA NYUMBA ZETU KWA MAVI YA NG’OMBE MSWAHILI ANAJENGA NYUMBA YAKE KWA CHOKAA AMA CEMENT
  KWA KIFUPI HUYO NDIO MSWAHILI NA SIVYO KAMA HII LEO TUNAVYOJARIBU KUJISHUSHA SISI WASWAHILI WATUMIAJI WA LUGHA YA KISWA1HILI MACHONI MWA WATU WENGINE NA KUWATUKUZA WAZUNGUY

 14. zabibu Says:

  ninamshauri apunguze kula mafuta mengi kabla haja shikwa na maradhi ya moyo na sukari kisha azibe pua kaifungua sana.

 15. Mwanamke wa shoka (UK) Says:

  tunapenda tuone UWT wana dira…..tunaelewa fika wapi wametoka….ni wapi wanaenda….???…kuna kichwa Mwenyekiti….

 16. BLACKMANNEN Says:

  WanaBC wenzangu,

  Kila mara tunaomba kupeana maoni ya kimaendeleo kwa mtu yeyote anayeletwa hapa BC. Je, ni kweli tunafanya hayo? Leo hii tunaye Mheshimiwa Bi. Sofia Simba, aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa “Umoja wa Wanawake Tanzania”, tunampa maoni gani ya maendeleo?

  Hebu tuangalie baadhi ya maoni. Je, maoni nr. # 1, # 2, # 6 na # 14, ni kweli yatamfaa? Mimi nilitoa maoni yangu hapa # 9, na nilitegemea ukurasa huu ungejazwa na maoni ya wanawake waliokuwa na shauku ya kutoa maoni yao wanapopata nafasi kama hizi, lakini, sasa kumbe sivyo. Sasa tunaelekea kulifunga pazia hili bila hata kusikia kilio kikubwa kutoka kwa dada zetu, mama zetu, shangazi zetu na pengine hata Binti zetu tuliowazaa na wale tunaotegemea kuwazaa, mama zao watawasimulia nini?.

  Dada halima umechemsha na wewe ki%nzi hapo, kwa kusema Mheshimiwa Sofia Simba ni Kiongozi wa UVCMM – Ni “Mwenyekiti Wa Umoja wa Wanawake Tanzania – UWT” ,sio UVCCM kama ulivyosema wewe comment # 10, upo hapo dadaangu????

  It’s Great To Be Black……I mean Blackmannen

 17. papuu Says:

  wewe blackmanenn acha sifa basi mzee,wewe si umeshatoa comment yako kama ulivyosema,sasa usilazimishe wengine kufikiri kama wewe. mzee ulitaka usifiwe nini,aah bwana,mambo gani haya

 18. kabwe makanika Says:

  Vyeo vingi sana utaweza kuvimudu kweli? wewe mbunge, wewe waziri katika serikali, mjumbe wa nec mama mkuu wa akina mama wa ccm. kweli utamudu kutumikia nafasi zote kwa ufanisi?
  Punguzeni tamaa ya madaraka.

 19. naila Says:

  ngoma iko hovyo1 halafu swaziiiiiiiiii!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s