BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

NINI KILIMLIZA WAZIRI MKUU? February, 2, 2009

Filed under: Serikali/Uongozi,Siasa,Tanzania/Zanzibar,Uandishi — bongocelebrity @ 8:51 PM

pindabcWiki iliyopita kuna kitu cha nadra kidogo kilitokea nchini Tanzania.Ni kitendo cha Waziri Mkuu,Mizengo Pinda,kububujikwa na machozi bungeni.Baada ya hapo kumezuka mijadala mbalimbali likiwemo swali ambalo kimsingi sio rahisi sana kulijibu.Swali ni kama linavyoonekana katika kichwa cha habari hapo juu;Nini kilimliza Waziri Mkuu?

Sambamba na swali hilo,wapo watu lukuki,akiwemo Ansbert Ngurumo,wanaouliza msururu wa maswali ya msingi;Je Waziri Mkuu aliwalilia albino?Je aliililia serikali?Je alijililia mwenyewe?Na Ndimara Tegambwage anajadili je Waziri Mkuu akilia ndio kumaanisha kwamba serikali nzima imelia?Wewe unasemaje?

Advertisements
 

31 Responses to “NINI KILIMLIZA WAZIRI MKUU?”

 1. BLACKMANNEN Says:

  Kilichomliza Waziri Mkuu Mizengo Pinda,

  Kwanza – ni kile alichokiona kwa macho yake mwenyewe katika ziara yake kwa kukutana na Ma-Albino walionyofolewa viungo vyao. Yeye kama binadamu ameumia sana moyoni.

  Pili – kitendo cha waandishi wa habari kupindisha maneno aliyoyasema kwa nia ya kuupotosha umma ili kuleta chuki kati ya wananchi na serikali.

  Tatu – kutokana na upotoshwaji wa habari hizo, wapinzani kama ilivyokawaida yao wanatafuta mianya ya vijimakosa na kuzidi kupotosha zaidi umma kwa nia ya kuiangusha serikali iliyomo madarakani.

  Uandishi kama alivyoandika “Ndimara Tegambwage”, unaonyesha jinsi ambavyo mtu anaweza kutumia taaluma yake ya uandishi kuzidi kuuchanganya umma kwa nia anayoijua yeye mwenyewe.

  Kwanini watu tuongee zaidi kuhusu kulia kwa Pinda badala ya kuongea mengi kupeana mawazo kuhusu tatizo la kuuliwa Watanzania wenzetu Ma-Albino? Je, tatizo hilo ni la Pinda pekee yake kwa vile ni Kiongozi serikalini?

  Mizengo Pinda ameelezea namna ambavyo wananchi wanaweza kushiriki kuisaidia serikali katika tatizo hilo kwa kuwataka wananchi warudishe ulinzi wa “sungusungu” na mambo mengi mengine.

  Lakini waandishi wa habari na wapinzani, badala ya kusaidia katika kuyachambua mazuri aliyoyasema Waziri Mkuu, wamejikita kuandika kitu ambacho hakukimaanisha katika hotuba yake. Kwa mtindo wa namna hii hatutafika kule tunakokutaka katika kuboresha maisha ya kila Mtanzania.

  Watu wamejawa chuki na kila aina ya wivu na ubinafsi uliokithiri.

  It’s Great To Black=Blackmannen

 2. bombe Says:

  kwa kila mtu roho inauma huku najisifia tanzania kuna amani lakini wananipinga eti sisi ni wauwaji wa albini yani wanachafua jamii nzima ya watanzania hao wauwaji .nao huyo zito si kila kitu atafute umaarufu amejuaje kama analilia cheo anakua kama mtoto H R M bila kunyoosha kidole haridhiki.naomba wanasiasa kwa hili tisiingize siasa tushirikiane kwa moyo 1.IDUMU AMANI YA TANZANIA

 3. mr degree Says:

  alitoa kauli kali kuhusu mauaji ya albino kuonyesha hisia zake yeye kama binadaamu lakini akaonekana ni mpuuzi! yeye kama binadamu alijisikia vibaya sana kuona watu wanamhukummu kwa kauli yake na si kile alichomaanisha . tuache siasa hawa albino wanauawa na hawana jinsi ya kujitetea tunahitaji kauli kali kama hizi la sivyo tukiendelea na siasa zetu hizi za kila siku hawa wasukuma watawamaliza albino wote! lazima tuelewe hata wewe unaesoma hapa unaweza kuzaa albino utajisikiaje unapoona watu wanamkata mapanga mtoto wako na kuondoka na mikono yake? bila shaka utatamani nawe umkamate na kumnyonga muuaji huyo na hizo ndizo hisia alizokuwa nazo waziri mkuu na si vingine!

 4. Iddah Says:

  Mimi nilibahatika kufuatilia ule utaratibu wa maswali na majibu kwa mh. waziri mkuu bungeni kwakweli yale maswali yaliyokuwa yanaulizwa na baadhi ya wabunge kuhusu mauaji ya albino na mh. waziri kuyajibu vizuri huku akioneshwa kuguswa sana na ukatili huu unaondelea kufanywa na baadhi ya watu ambao hawana roho za kibinaadamu kwa kweli mh. hili tatizo limemgusa mnoo yani tu hana jinsi ya kuelezea hisia zake hadi mtu amuelewe matokeo yake aliangusha chozi la uchungu sana.

 5. SaLaMa Says:

  NDIO WAZIRI MKUU ALIWALILIA MAALBINO KWA SABABU ALIJIONEA MASIKITIKO YAO ALIPOKUWA KATIKA ZIARA YAKE PIA ALIMUONA YULE MTOTO ALIYENUSURIKA PALE TABORA ALIVYOKATWA KATWA HATA KAMA WEWE UKIANGALIA TU KATIKA TV LAZIMA MACHOZI YA KUTOKE. KWA KWELI INASIKITISHA SANA NA HAO WATU WANAOFANYA HIVYO KAMA WAKIKAMATWA NAO WASIULIWE ILA WAKATWE MGUU AU MKONO WAFE KAMA WALIVYOUWA WAO.

 6. Edwin Ndaki Says:

  Bc nilikuwa nasubiri kwa shahuku kubwa kuona hili suala linatinga hapa bc.

  Ngoja nipite kwa Ngurumo na Ndimara alafu nami nije na nyimbo zangu nilizotaka kuziimba tangu siku ya “CHOZI”

  tupo pamojah

 7. Dr Carterman Says:

  Me nafikiri alilia kujikosha tu, naamini serikali ina uwezo wa kuyakomesha haya mauaji ila tu hawapo serious, wamefanikiwa kuzuia madawa ya kelevya kwa kiasi fulani, hali kadhalika ujambazi, sasa kwanini washindwe haya? Inawezekana hao washkaji nao(serikali na mawaziri wake) wanawatumia maalbino ili mambo yao yaende sawa! Halafu Pinda anazuga analia! Kulia kwake kutawasaidia nini hawa albino? Aaache ujinga!

 8. naimani Says:

  Mzee analilia cheo chake kwani ndio maana amelia ha dharani mbele ya wa bunge wezake

 9. naimani Says:

  MZEE ANALETA MAMBO YA ZAMANI KWANI MTU AKIUA NA AHUHAWE, BASI ATA MTU AKIBAKA NAYE ABAKWE?

 10. DUNDA GALDEN Says:

  NDUGU ZETU ALBINO LA KWANZA.PILI WATANZANIA WALIVYO NA ROHO MBAYA KULIKO HATA UNAEMZANIA INGAWA SI WOTE
  HASWA WANAOTAKA UTAJIRI KWANJIA YA MKATO

 11. any Says:

  Hamna lolote, hawa ma albino sio leo wameanza kuuwawa, na wazee wa shinyanga nao wanauwawa kwa imani za kishirikina na bado hawajafanya kitu! Ingekuwa “one of them” ndio kauwawa, ungeona moto wake. Naona Pinda hana mpya, they take too long to respond to this issue, shame on u all who didnt bother to correct the mess, na kwa awamu iliyopita pia shame on u too! .

 12. papuu Says:

  hamna lolote uchuro tu hapa. masharti ya mganga nini?

 13. Esther N. Says:

  kila mtu ana yake michuzi ukweli halisi hakuna mtu anaeujua. ukiachana na hilo, mimi kama mwananchi wa Tanzania ningependa sana kuwaasa wanasiasa, wabunge, kila penye tatizo walitatue pasipo kuongeza tatizo. Embu angalia sasa hivi suala la umeme, mpaka leo hii kuna mgao? Mtera kuna maji mvua zinanyesha, japokuwa sio sana lakini hatuwezi kusema hakuna maji. Mikataba tuliokuwa nayo awali imevunjwa, kisa, ufisadi, hali inazidi kuwa mbaya, viongozi wafikirie upya kuhusu umeme.

 14. ANGELO Says:

  UNAFIK MTUPU + UCHURO HAMNA LOLOTE YAO YANAWAENDEA, KAZI KULA FEDHA ZA SERIKALI, WANALIA NINI,SUBIRI WAMALIZE AWAMU YAO UTAYAONA, MALIMBIKIZO YA MIMALI YA WALIPA KODI (WANANCHI)
  WAANGALIE OVYOOOOOOOO………

 15. kabwe makanika Says:

  Kisa cha kulia hadharani anakijua yeye mwenyewe, lakini si kwa sababu ya uchungu aliokuwa nao. kama ni uchungu angelia siku ya kwanza ya ziara yake aliposimuliwa jinsi mauaji yanavyofanyika.

  Pale bungeni hapakuwa mahari pake kulia. labda aliisi kiti chake kinanyemelewa ama hakuwa na jibu la kuridhisha ndio maana akatafuta huruma kwa kulia.

 16. halima Says:

  Ukiona mtu mzima mama analia mbele za watu ujue kuna jambo……… Matty na Bint mzuri mtamalizia

  Duhhh Lakini mimi hata sielewi jamani inawezekana Mh. Pinda kilimuuma sana akifikiria jins alivo waona maalbino waliokoswa koswa kuuwawa roho inamuuma sana

  Waandishi wa habari angalieni msipende kupotosha umma kwani Mh. Pinda na yeye ni binadamu na anahisia za kibinadam kwa hiyo anaona uchungu kuona viumbe wasio na hatia wanauwawa.

 17. Mwanamke wa shoka (UK) Says:

  its all mixed up, …lol.

  kwanza…bunge ndilo lenye kutunga kupitisha sheria….tatizo la ma-albino, kuchunwa ngozi watu….kukeketwa wanawake….nk…yamekuwapo….kama yapo yaliyokwisha tatuliwa….ni vipi hili la ma-albino lishindikane….???…

  BUNGE…..nimekaa sana nikafikiria kuwa huenda tunahitaji watu wenye UPEO wa ku-analyse mambo ndio wachaguliwe kuingia bungeni….nikimaanisha yawepo masharti ya kiwango cha elimu…..we need people who can really analyse issues na sio mambo holela holela…..angalia bunge lipo kwenye session baadhi ya wabunge wamepiga mbonji….lol…tutafika kweli….

  …miye siwezi elewa nini kilimliza PM Pinda….kuna majibu meeengi kwa swali kama hili…..ila….jamani naomba WABUNGE wawe makini…..kama huna hoja ya msingi kaa kimya na sio tu kujiulizia maswali ili mradi tuu unaowawakilisha wakuone kuwa upo ACTIVE bungeni….it doesnt work like that….

  ukifuatilia ISSUES zinavyoenda kiubabe ubabe….unajiuliza hivi hii ni nini????…..hivi kwa nini mtu au watu waendelee kuwageuza wenzao wajinga….(WHILE SIO WAJINGA)….wamewachagueni MFANYE KAZI……kazi rungu….chuki binafsi kibao…..wezi mmewashika lakini bado mnajiuliza muwafanyeje….mtanzania anaendela kuteseka kama vile ni maskini wa mwisho huku duniani…(we are not that much pOOR….its the people we have chosen to LEAD us who make us POOR…..)

  …we poorly MANAGE OUR RESOURCES thats WHY WE ARE POOR

  ….mtu anapewa tax-holidays kwa kuchimba madini….WHY…??????????????….kwa nini TUNAPENDA KUJIKOMBA kwao….ama ndio ile “kitu kidogo…”…..WHY…???…..hayo mabilions huendi nayo popote…nOW kwa nini UWAIBIE watanzania PESA ZAO…UWASABABISHIE MAISHA YA KIMASKINI…..(wakati wao sio MASIKINI…..)…WHY……?????????

  incompetences every where……kama huwezi shughuli pull out…kaa kando…..kuna DAMU changa zinaweza KULETA MABADILIKO…..

  …issue ya MASHA nayo inani-BORE nasikia kama kutapika….anataka nini hasa…au ndio ameshapokea “kitu kidogo”…..

  …..Jamani JK ana kazi…..

  …anyways…..KAZA BUTI……konda angalia vichwa…..tutafika….ILA SIO KWA MTINDO HUO……we need to change…..WORK HARD with determination at all levels,……TUACHE UROHO WA MALI…..tuangalie MASLAHI ya nchi yetu….watu wetu……WATOTO WETU…….

  ta….

 18. kyara joseph Says:

  nadhani kilichomliza ni kitendo cha watanzania kutoliona swala hilo ni la pamoja kwa kuishirikisha jamii mkuu anaomba tulione kuwa ni tatizo la kitaifa na linahitaji ufumbuli wa haraka ili kila mtu na kula mtanzania apate haki yake kimsingi.

 19. Gervas Says:

  No, Mh. Pinda alipinda tu kidogo…hamna aliyesafiri kwenye mind yake akaona kilichomsibu….may be alikuwa anasikia njaa!! kila mtu anazuka na lake hapa.

 20. Kekue Says:

  Wizi mtupu!!!!!!!!!!!!

 21. any Says:

  jeff ivi ki FLITER CHAKO hakiharibikagi! nataka sikumoja kigome ku filter watu twende freestyle apa ndio ingekuwa noma. Nina uchungu sana na hawa jamaa! basi tu!

 22. papuu Says:

  wewe esther N aliekwambia hapa kwa michuzi nani? we nawe ndio wale wale! acheni uchuro waswahili jamani,aah,mnaudhi

 23. ramona Says:

  we pinda unalia lia nini sasa! acha upuuzi.leta solutions sio kilio. nakubaliana na wanaosema ni uchuro na unafiki!

 24. watubwana Says:

  watu bwana,siri ya mtungi aijuaye ngata,anafahamu yeye mwenyewe kilichomliza.
  naona TANZANIA hamna jipya,kila siku matatizo ni yale yale,umeme,maji,albino,ulimbizaji wa mali,wizi wa mali za uma,matumizi mabaya ya fedha za serikali,RUSHWA,migomo,uchumi kuporomoka na pesa yetu kushuka kwa thamani na mambo mengine kadha wa kadha.
  hivi KAGAME ametumia njaia gani kuweza kuuinua uchumi wa nchi yake na kutushinda nchi yetu TANZANIA? wakati nchi yake ilikuwa katika vita kwa muda mrefu??embu tujifunze jamani,kwani wenzetu waweze wana nini na sisi tushindwe tunanini??

 25. KT Says:

  We ndaki, siku 3 bado unasoma tu Ndimara na mwenzake, sijaona comment zako na ulisema unarudi! usituzingue.
  Maoni yangu Wazir Mkuu Pinda aliguswa sana na suala la mauaji ya albino ndo maana akalia, Pinda hana unafiki ndo mana hata ktk suala la Zanzibar ni ncji au sio nchi hakuwa na unafiki; alisema kile anachokijua kwa mujibu wa katiba bila kuweka siasa; so aliongea hisia zake kama binadamu na alitoa chozi sababu hiyo hiyo; nia yake ilikuwa njema kuwasaidia maailbino na vikongwe; lakini approach ilikuwa sio sahihi ya kuruhusu wananchi wajichukulie sheria mkononi; ni hatari sana. Lakini naye hilo aliliona ndo mana akaomba radhi WaTZ.

 26. kindo Says:

  kama mawaziri na watendaji wengine serikalini wangekuwa wanawajibika mh. waziri mkuu asingetoa kauli kama aliyotoa kwasababu issue ingekuwa imeshadhibitiwa zamani…lakini kwasababu watu hawako committed na kazi zao ndio maana kaka mkuu anapata matatizo….sasa hivi IGP kaunda “kikosi kazi” kushughulikia issue hii ya albino, kwanini hili halikufanyika mapema,? Kama kikosi maalum cha polisi kinaweza kusimamia uchaguzi Tarime, kwanini kikosi hicho hicho kisifanye hii kazi muhimu ambao Vicky Mtetema wa BBC alishawatengenezea njia? Mimi nakwazika sana na watendaji wa serikali yetu…..loh!

 27. Dr. Rogers Says:

  WIZI MTUPU………..! TUMESHAGUNDUA MBINU ZAO SIKU HIZI. KAMA KULIA ANGELILIA KULEKULE KWENYE ZIARA YAKE. HAPO ANAJIKOSHA TU NA KUTAFUTA HURUMA YA WANANCHI…. TUMEMSTUKIA.
  KWA KIFUPI ANALILIA CHEO CHAKE CHA UWAZIRI MKUU…
  HATUFAI HUYU!!!!!!!!!!!!!!!!!

 28. Mattylda Says:

  Ancora uno~!

 29. Kwakweli hatua ya kulia Mh Pinda sidhani ni kama inatokana na hisia nyingine nje ya swala la mauji ya albino! Kweli wapo wanaosema labda ugumu wa swali ukizingatia tayari alishateleza kimaelezo kukiuka katiba. Lakini mbona Mh Pinda ni kiongozi mwenye uwezo mkubwa wa kutoa majibu ya haraka haraka tena yalio sahihi ambayo kwa viongozi wetu waliotangulia na hawa tulionao si rahisi kwao! Ni mara nyingi tu Mh amepigwa maswali magumu mengine mengine alilazimika kukiri udhaifu wanaoufanya akisema ni makosa ya kibinadamu kutokana na mazingira! Naamini kama swali lingekuwa gumu kutokana na maelezo yake ya awali hilo si lakumfanya alie isipokuwa ni swala lenyewe ni lamasikitiko makubwa then alisikitishwa zaidi kuona VIONGOZI wenzake walichaguliwa na wananchi kwa lengo la kutatua matatizo yao hawalipi uzito swala la mauji na badala yake wanajenga hoja si zenye nia ya kuleta ufumbumbuzi bali ni za kutaka kumtia udhaifu! Nadhani haukuwa muda muafaka na ndio maana akalia.

 30. Aunt D Says:

  Ni vizuri kulia kwani unaondoa uchungu moyoni,Mh Pinda wamemuweka hapo kumnyanyasa tu hawezi hiyo nafasi…..sasa yeye akilia sisi tutafanyaje?kiongozi unatakiwa kukabiliana na magumu yote………………..ndio maana waziri mkubwa aliyepita alikuwa mbabe(hivi yuko wapi mbona hatumsikiii??)
  Sipati picha siku anatakiwa kujiuzulu itakuwaje ATAZIMIA HAPO HAPO.
  Ukiwa kiongozi ukilia tu kwisha habari
  PINDA pole baba ndio ukubwa huo…..jalala kila baya na zuri lako kaza buti Mzee


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s