BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MPOTO ASAKA NAULI YA KWENDA IKULU February, 4, 2009

Filed under: Burudani,Mahusiano/Jamii,Mawazo/Tafakuri,Sanaa/Maonyesho,Serikali/Uongozi — bongocelebrity @ 8:00 PM

mrishompotobc

UMAHIRI wa Mrisho Mpoto umekuwa ukiwakuna wengi hasa anapokuwa jukwaani akidondosha mashairi yake na mwaka jana alifanikiwa kushinda moja ya tuzo kubwa katika sanaa kwa Afrika ijulikanayo kama Slam, ambayo ilikuwa inashikiliwa na mmoja wa wasanii mahiri aitwaye, Steff H2K kutoka Mauritius.

Ushindi wa Mpoto umemfanya apate nafasi ya kushiriki fainali za tuzo za Slam za dunia, ambazo zinafanyika nchini Ufaransa Machi, mwaka huu lakini hiyo haitoshi wala haimzuii yeye kuendelea kusaka nauli ya kwenda Ikulu.

Baada ya kuwa ameshiriki katika wimbo wa ‘Salamu Zangu’ na kuweza kuchukua nafasi kubwa huku akimfunika mmliki wa wimbo huo Irene Sanga, Mpoto ameamua kuibukia upande wa pili na kutoa wimbo wa ‘Nikipata Nauli’.

[Usikilize wimbo “Nikipata Nauli” kwa kubonyeza player hapo chini kisha ndio uendelee kusoma makala hii hapo chini]JM


Kama ilivyo ada ya Mpoto ni aghalabu sana kutafsiri wimbo wake kwa wasikilizaji wake kwa kuwa anasema, kasi ya fasihi ni kuipa nafasi ifanye kazi yake. Wimbo wa ‘Nikipata Nauli’ akiwa ameshirikiana na Banana Zorro tayari umeanza kuwa kivutio kikubwa katika redio mbalimbali.

Mashairi ya wimbo huo yanazungumzia mengi lakini katika mfumo ule ule ambao Mpoto anaamini ni wa fasihi na kila msikilizaji ana nafasi ya kuamua na kukitafsiri kile ambacho anakisikiliza.

Kiitikio chake kinasema, “Bora kujenga daraja kuliko ukuta, chemchem si temi, ukitaka kunywa maji yake sharti uiname.”

Dhahiri anaonyesha kuzungumzia kwamba, Rais Jakaya Kikwete anaonekana kuwa mbali na wananchi huku akimshauri hakuna haja ya kujenga ukuta, badala yake ajenge daraja litakalomuwezesha kujua wananchi wanaishi vipi ili atatue matatizo yao badala ya ukuta ambao utazidi kumtenganisha nao.

Suala la chemchem anasema si temi, maana yake haina ubabe ila ukitaka kunywa maji yake bila kulazimishwa lazima utainama kuyanywa. Kwamba hata serikali isipowajali leo wananchi, itafika siku iltalazimika kupiga goti na kubembeleza hasa kipindi cha upigaji kura.

Lakini Mpoto anaamini kwamba suala la tafsiri kawaachia mashabiki wake ingawa anakiri kuwa lengo lake kubwa ni kufikisha ujumbe kwa serikali na viongozi wake wote akiwamo mkuu wan chi ila pia kwa wananchi ambao ndio wenye nchi kwa nia njema.

“Mapokeo ya kila mtu yako tofauti, suala kubwa hapa ni kila mtu anaelewa kwa wigo upi na kama kinachoelezwa kitakuwa kimefika basi ni bora zaidi. Napenda kufanya hivi na leo unaona kwa kuwa nia yangu ni kutaka kufikisha ujumbe naamua kushirikiana na wasanii kama Banana Zorro, Profesa Jay na Afande Sele,” anasema.

Katika video ya wimbo huo, Mpoto anaonekana akiteremka kutoka milimani kwenda inapopita barabara kuu ya kwenda jijini Dar es Salaam ambako anaamini atakutana na mjomba ‘Rais Kikwete’ na kumueza kumweleza matatizo yake ambayo ndio yanayowakabiri wengi.

Hofu yake kubwa ni kwamba hana nauli, ndio maana anamuahidi mjomba kwamba anataka kumfikishia ujumbe huo na tatizo lake ni nauli lakini anaahidi siku akiipata lazima atafika mjini na kumueleza kila kitu alichonacho.

Baada ya wimbo huo, safari ya Mpoto inaendelea kwa kuwashirikisha Afande Sele na Profesa Jay katika wimbo mpya ambao unaendeleza safari hiyo ya kutoka kijijini kwenda mjini hasa Ikulu ambako ni makazi ya Rais ambaye ndiye mjomba ili amueleze hali halisi ya maisha ya Mtanzania wa chini.

Ndani ya wimbo ‘Nikipata Nauli’, Mpoto anaelezea mambo kadhaa japo kwa mfumo huo wa fasihi, mfano pale anaposema kwamba anashangazwa na jinsi wanaotuhumiwa na ufisadi walivyoshikwa na ushahidi wa kutosha lakini bado suala linazungushwa japo yeye anatumia kauli hii.

“Tumbo kali jana kashika na kuku wa jirani, lakini cha ajabu inaelezwa ushahidi wa mwizi wa kuku hadi atakapokamatwa na mnofu au mchuzi wa kuku”.

Kwa ufupi, katika wimbo huo, Mpoto anajaribu kuelezea namna ambavyo serikali imekuwa ikiendesha mambo yake katika mfumo ambao anaamini si wenye mpangilio mzuri na hasa kwa Watanzania wenye maisha ya chini huku wachache wakiwa wanakula raha kupindukia.

“Muziki ninaoimba unaweza kuiita African hip hop, ninajaribu kubadilika kutokana na hali halisi ya utandawazi, lengo ni kufikisha ujumbe. Kama ninachanganya na kitu fulani na watu watapenda maana yake watapata nafasi ya kusikiliza ninachowaeleza, kitu ambacho ndio ninafanya,” anasema Mpoto ambaye alianza kuchipukia kisanaa katika kundi la Parapanda Arts linaloongozwa na Mgunga Mwa Mnyenyelwa.

Mpoto anataka kuimba tofauti na wasanii wengi, kwamba anachoimba lazima kuwe na fani na maudhui. Hiki pia kinatakiwa kueleweka zaidi, kwamba fani ni muonekano, mfano nini unachovaa na jinsi ulivyo.

“Lakini unapokuja katika suala la maudhui maana yake ni kitu gani unataka kufikisha kwa jamii. Lazima ueleze na ueleweke, uwe na kitu ambacho msikilizaji wa wimbo anafaidika. Napenda kuwa na kazi zinazodumu badala ya zile zinazovuma kwa kipindi kifupi na kupotea, tunaona kwa wasanii wengi.

“Msanii kama Bob Marley aliliona hilo, ndio maana pamoja na kufariki dunia mwaka 1981 hadi leo kazi zake zinaendelea kusikilizwa na kupendwa kwa kuwa zina fani na maudhui, anasema.

Baada ya wimbo huo, Mpoto anasema atahakikisha anakamilisha albamu yake kabla ya kufunga safari kwenda Ufaransa Machi mwaka huu kwa ajili ya mashindano ya dunia ya tuzo ya Slam.

Habari hii nzima imeandikwa na Saleh Ally wa Mwanaspoti

Advertisements
 

33 Responses to “MPOTO ASAKA NAULI YA KWENDA IKULU”

 1. Hii ndio sanaa. Nasubiri wenye utaalamu wa “muziki wa kizazi kipya” wauchambue. Sijui zitafananishwaje? Hii ni sanaa, huyu ni msanii na unaona fasihi huku ujumbe ukifika.
  Big Up Mrisho

 2. wisaka Says:

  jamaa ni mkali sana ana ujembe ambao unareflect the reality ambayo ipo .nampa big up atafanikiwa zaid

  cheers mpoto

 3. Sis Says:

  Inawezekana watu wasipende rhythm or rather midundo kwenye kazi za huyu bwana, lakini kiujumbe, huwa anagongelea msumari pale unapopaswa….Hongera bwana Mpoto…

 4. mr degree Says:

  hamna kitu hapo anaiba mashairi ya shaban robert na kuyafanya nyimbo!

 5. Christabell Says:

  Ujumbe mkali na una ukweli mwingi mwingi tu. Mungu atuwezeshe kukabiliana na haya majanga

 6. Edwin Ndaki Says:

  ni miongoni mwa wasanii wazuri ninao wakubali wa tz.

  ni kweli jamani..kuanza upya sio ujinga..

  mjomba msalimie MASHA waziri wa mambo ya ndani muulize vipi vitambulisho lini?

 7. Nautiakasi Says:

  Huyu nae mwizi wa mashairi, hana lolote..! Kelele nyingiiiii kwa mashairi ya wizi. Kutunga mashairi kunahitaji kipaji, elimu na uwezo wa kutafakari mambo, sio kukurupuka tu, utaishia kuiba mashairi. Tatizo hawataki kwenda shule, yaani wakifika chuo cha utamaduni bwagamoyo wanaona ndo washamaliza elimu katika sanaaa.!

  1. Hana uwezo wakutunga mashairi yenye akili
  2. Hawezi hata kuweka vina vikaendana
  3.Hana personalety ya kughani mashairi
  3.Nimwizi wa mashairi, then anasema ni yakwake
  4. Hana uwezo wakujifunza kwa haraka na kubadilika
  5. Mchafu, hata rasta zake kuhudumia hawezi (si sifa ya msanii ambaye ni kioo cha jamii)

  NB: Ajaribu kusoma mashairi ya akina shaban robert, Andanenga na Chozi. Ili angalau ajuwe ushairi unahitaji nini!

  • bongocelebrity Says:

   Nautiakasi,
   Unaonaje kama ungetusaidia sote hapa kwa kuweka wazi kwamba Mrisho Mpoto amemuibia nani mashairi?Asante

 8. MapigoSaba Says:

  japo tenzi zimetulia, lakini unahitaji kutengeneza muziki wenye mpangilio mzuri ukitumia waimbaji wazuri zaidi. Au achana kabisa na miziki; kuwa kama malenga wengine kwa kuimba/kusema mashairi au ngonjera zako ‘kavukavu’.

 9. DUNDA GALDEN Says:

  HUU NDIO MZIKI KATI YA MIZIKI SIO KUBANA SAUTI UTENZI BABU KUBWA BIG UP MRISHO
  NA FUNGA SAFÄRI UKAONANE NA MJOMBA NAJUA HATUKUSIKILIZA

 10. jj Says:

  Mjomba imetulia sana nimekukuba

 11. binti-mzuri Says:

  nautikasi rafkiangu donge la nini,panda juu uende ukazibe… UPO HAPO!?!?

 12. Edwin Ndaki Says:

  USHAURI KWA MRISHO MPOTO..

  Mimi naona haina umuhimu wa wewe kuharibu nauli kwenda kwa Mjomba.Maana ulipomtumia salaam nakuhakikishi alizipata sema kujibu ndio hataki.

  Tatizo mjomba wako sijui ndio majukumu mengi labda mwaka huu ila miaka iliyotangulia alikuwa anamisele mingi sana.Nahofia unaweza kwenda alafu usimkute hilo nalo kumbuka.

  Alafu unaweza kwenda ukamkuta kajifungua ndani si unajua tena akiacha mlango wazi kuna kelele nyigi sana mara EPA,KIWIRA,UDSM,East Africa COMMUNITY,TRL..

  Labda ungesubiri 2010 LAZIMA atakuja kukutembelea ..hapo kijijini na kukuletea zawadi ya kanga,fulana ila VIATU anaweza kusahau maana yupo BIZE ila itabidi umpatie MUDA tena ili aende kukunulia..ila usisahu kumwambia unavaa number ngapi…

  Sikufundishi MPOTO …hiyo ni sms yangu pokea…

  Tutafika tu

 13. watubwana Says:

  kwikwikwikwi,watu bwana,mrisho wimbo wako unamaana sana ukikaa kuusikiliza na kuutafakari.usijali wasemayo,ishi upendavyo na si wapendavyo,binadamu haturidhiki.
  haijalishi mashairi umeyatoa kwenye vitabu gani cha msingi ujumbe umetufikia walengwa.bora utukumbushie methali,misemo yetu ya zamani maana toka tulivyoiacha kuitumia tulivyokua shule ya msingi ndio basi,sikuhizi ze ze na kiswanglish kingi,tukumbushie bwana mrisho,na madongo yetu tupage.inchi haijengwi kwa nyundo na misumari,uwepo tu wa watu kama wewe unatosha kutuambia ukweli.kanyaga twende kaka

 14. GUNZI Says:

  poa sana

 15. ramona Says:

  no no no sijapenda kabisaaaa

 16. mimina Says:

  mpoto unaweza kuanza safari taratibu kwa miguu na uhakika mjomba atakuwa njiani anakuja kukutembelea kwa hiyo mtakutana pale njia panda si unajua mwakani anakuja kuongeza mke mwingine maana yule aliyemchukua amekaa nae miaka mitano sasa anataka mwingine tena akae nae miaka mitano.atakuja na zawadi kibao viatu pia vitakuwepo usijali tabasamu lake litakuwa zaidi utapata chochote ila akikupa ahadi kataa

 17. kindo Says:

  Swali zuri sana kutoka kwa Bongocelebrity….Mpoto kamuibia nani mashairi? Tukishajua hilo tutajua tuendelee vipi…otherwise allegations without proof ni kelele tu…..

 18. Pandu Says:

  Nyie mnaosema kaiba mashairi ya Shaban Robert mmeishiwa.
  Mbona nyie hamuigi mkaimba? mnatamani muwe kama mpoto lkn mmechelewa, wanamuziki wangapi wamejaribu kucopy nyimbo za Marijani? wakowapi?
  Watu huiga kilicho bora, wangapi wamesoma mashairi ya shaban robert? kuna ubaya gani Mrisho akawaimbia wale ambao hawakupa fursa ya kusoma mashairi ya shaban robert?
  Hata Obama alikuwa anasikiliza na kusoma kuhusu maandiko ya Lincoln, naye hanajui?
  Kama huna la kuchangia fungua zeutamu au globapublisher, huko ndio kunawafaa.

 19. Kazi nzuri Mpoto!Kama asemavyo Edwin Ndaki, TUTAFIKA!

 20. mkaku Says:

  Nautiakasi una matatizo makubwa sana na wewe ndio wale watanzania ambao mtabakia hapo hapo hamuendelei kwa kujaribu. Wasanii wote wakubwa duniani wameanza kwa kuiga sanaa za watu wengine ndio wakaweza kusimama, Huwezi kumbwambia mtoto asitembee kwasababu anakuiga. Una roho mbaya tena ya kimasikini huna msaada wowote kwa jamii kazi yako ni kuponda tu sanaa za wenzako. Hakuna pointi yoyote uliyosema zaidi ya chuki binfsi roho yako imetengenezwa kwa damu na nyama kweli?

 21. halima Says:

  Sijui Nautiakasi wewe kila msanii anae kuwa hapa wewe unaponda tu unamatatizo sana wewe, kwanza sauti yako sijui hata ni ya ngapi unaonaje ukitoa wimbo wako kuliko kuendelea kuwavunja moyo wasanii wa nyumbani. HOVYOOOOOOOOOOO

 22. papuu Says:

  ala! sasa watu bwana kwakweli nimeamini siri ya mtungi aijuaye ngata (copyrighted from ‘watubwana’ to avoid risks of plagarism), wewe sasa unasema haupendi yeye kakuomba upende. watanzania tuache uchuro na kasumba za ajabu ajabu,mnasifia visivyosifiwa mambo ya maana mnakandia

 23. eve Says:

  wadau mnaotoa maoni huyo nautikasi anayekosoa anataka watu wajibu jazba huku kwa ushauri wangu ni kutokujibu alichoandika isitoshe hafai kuelimisha jamii kwa kifupi ni mwendawazimu !!!!!!!! na pia inaonyesha akili zake zilivyo punguani! tuendelee kuwatia moyo wasanii wenzetu big up!

 24. watubwana Says:

  papuu ndugu yangu soma vizuri comments,
  sio PLAGARISM ni PLAGIARISM hapa tunaeleweshana tuu ndugu.
  na nilivyomwambia MRISHO aishi apendavyo na si wapendavyo, binadamu haturidhiki ni sababu ya NAUTIAKASI alivyomsema na KUMUITA MCHAFU na maneno mengine kede wa kede.kumtoa mtu kasoro inaruhusiwa ila tumia basi maneno yasio na ukali na chuki,pia uhuru wa mtu usiuingilie yeye kama anapenda kande mwache ale kande zake.
  ushauri wangu,ukisoma vitu vilivyoandikwa humu soma kwa makini ndugu yangu umwelewe mtu huyo anamaanisha nini.sio wote wanachokiandika ndio wanachokimaanisha inabidi utafakari kidogo kuelewa comments za watu mbali mbali.asante

 25. pius Says:

  kawaida yetu wabongo,hata tulipoletewa magari ya automatic tuliponda ooh gari za wanawake! wangapi wanasoma mashairi ya Shaaban Robert?.Afadhali yake anasoma(kama ni kweli) na kutupatia sisi tusiopata bahati ya kuyasoma.Tupeane moyo na kukosoana kwa hoja safari yetu ndio kwanza inaanza.Hongera brother endelea kutupa vitu adimu.

 26. SaLaMa Says:

  HONGERA SANA BWANA MRISHO MPOTO
  TUTAKUCHANGIA TU NAULI UKAMUONE MJOMBA WAKO

 27. mwana Says:

  Achana na hao watu wenye roho za kwanini kaka, songa mbele.

 28. Mattylda Says:

  mashairi mazuri ila wasiwasi wangu huo mwili na hizo rasta mhhh nahisi jasho kali!

 29. Nikisikiliza hotuba za Raisi jakaya nacheka sana,huwa najiuliza anawahutubia wananchi wake au kuna kundi fulani anaongea nalo?

  Mpoto kazi nzuri.

 30. che Says:

  …Tutoe sifa pale inapostahili na tuache kukatishana tamaa.
  Mashairi ya wimbo huu yametulia,
  Mpoto ameyaghani vizuri,
  Yana Ujumbe Mzito sana kwa jamii na Mjomba,
  Banana ameitikia kwa sauti nzuri,
  Mdundo wa wimbo wenyewe umetulia,

  …mnataka nini tena????

 31. pongezi Says:

  Watu wachache wameponda lakini ni kawaida ya Watanzania kazi zetu mpaka zionwe na watu wa nje wanaojua muziki na mashairi ndugu zangu mimi pia ni mwana mashairi na mashairi sio vina peke yake poleni kwa uelewa mdogo huyu bwana mrisho anahitaji pongezi na support kubwa kutoka kwetu la sivyo tutaishia kusema anaiga shaabani robert, shaaban robert katoka wapi 2008? sijasikia lolote hapo poleni na someni msivunje wasanii moyo poleni wapondaji na Hongera sana Mr mpoto

 32. I.Q Says:

  nimefurahishwa na mashairi kwani ni ukweli mtupu mrisho anaongea ikifikia wakati wa kuuza albam yake plz me ninimkubali sana mrisho endelea na moyo huohuo ni matumaini yangu uwaamsha waliolala hongera sana m2 wangu nimekukubali


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s