BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

ANSBERT NGURUMO ANAPOJADILI BLOGS January, 18, 2009

Filed under: Blogging,Blogs,Mtandao,Uandishi — bongocelebrity @ 1:50 PM

ansbert-ngurumobcJina la Ansbert Ngurumo sio geni hata kidogo miongoni mwa wapenda habari na mawasiliano na hususani wapenzi wa habari za magazetini. Ansbert ni miongoni mwa waandishi wa habari mahiri nchini Tanzania ambao wamejijengea sifa na heshima kutokana na kazi zao za uandishi wa habari.

Safu yake ya Maswali Magumu,inayochapishwa katika gazeti la Tanzania Daima kila jumapili inabakia kuwa safu yenye wasomaji lukuki huku kila mara ikizua mijadala ya aina yake jambo ambalo ni uthibitisho kwamba sio tu inapendwa bali pia hujibu na pia kuuliza Maswali Magumu.

Ansbert ni blogger mzoefu pia.Blog yake ambayo inaongozwa na kichwa cha habari, Utakapojua Hujui Ndipo Utakapojua, ni sehemu mojawapo nzuri ambapo unaweza kukuta kazi zake za uandishi,mitizamo na pia mikingamo.

Hivi karibuni,jamaa wa mtandao wa Rap21,walifanya naye mahojiano ambayo kwa kila hali ni “must read” kwa mtu yeyote ambaye yupo kwenye fani ya ku-blog au ni mfuatiliaji wa maendeleo ya tekinolojia hii ambayo mimi naiita mapinduzi ya karne katika ulimwengu wa habari na mawasiliano.

Katika mahojiano hayo,Ansbert ameongelea kwa mapana jinsi ambavyo blogs,ikiwemo ya kwake, zinazidi kuboresha mapinduzi hayo na pia jinsi gani blogs zinaweza kutumika katika kuboresha maisha ya wanajamii,kutunza historia zetu,kufichua maovu nk.Bonyeza hapa ili kusoma mahojiano hayo.

Advertisements
 

HONGERA TK! January, 14, 2009

Filed under: Blogging,Blogs,Bongo Reality TV — bongocelebrity @ 7:16 PM

tk-bannerbc

Kwa mujibu wa jamaa wa Technorati,inakadiriwa kwamba blog mpya zaidi ya mbili huanzishwa katika kila sekunde,kila siku.Mpaka tarehe 31 Julai mwaka 2006 kulikuwa tayari na blog zaidi ya milioni 50!

Pamoja na mafanikio hayo ya uandishi huu unaoitwa uandishi wa kiraia (Citizen Journalism) ,bado hakuna takwimu za uhakika zinazoonyesha ni blogs ngapi “zinakufa” kila siku au kutelekezwa.Lakini ni wazi kwamba ni nyingi pengine kupita kiasi.Mtu anaanza kublog kwa kasi ya aina yake.Baada ya siku chache haonekani tena hewani.Amekosa muda au amekosa hamasa.Lengo alilokuwa nalo limempotea. Hawezi tena.Kila mtu ana majibu yake.

Ndio maana inapotokea mtu akadumisha blog yake kwa angalau mwaka mmoja inasemekana hawezi kuacha tena ku-blog.Kimsingi mtu huyo anastahili sio tu pongezi bali heshima.

Mmojawapo miongoni mwa watu hao ni mwanadada anayeonekana pichani hapo juu.Kwa wengi anajulikana kama TK lakini jina lake halisi ni Teddy Kalonga.TK ni miongoni mwa watu wanaotambulika kirahisi nchini kwetu ambao hawajabaki nyuma kunako tekinolojia hii ya blog.Hivi majuzi alisheherekea mwaka mzima tangu aanzishe blog yake inayopatikana kwa kubonyeza hapa.

Tunaungana na wengine wote kumpongeza TK na kumtakia kila la kheri katika kuendeleza “libeneke” kama anavyopenda kusema mwanablogu mwingine maarufu,Muhidini Issa Michuzi.Bonyeza hapa uone jinsi Teddy alivyosheherekea mwaka wake mmoja wa ku-blog.Hongera.

NB: Kama na wewe una blog yako na unasheherekea mwaka au miaka,usisite kuujulisha umma kupitia hapa hapa ndani ya BC.

 

MICHUZI YUPO,ATAREJEA PUNDE August, 11, 2008

Filed under: Blogging,Blogs — bongocelebrity @ 2:03 PM

Kama kawaida,e-mails na ujumbe kupitia sehemu ya maoni zimetufikia kutoka kwa “wadau’ mbalimbali wakitaka kujua ni kwanini hawaipati blog ya Muhidin Issa Michuzi.Tumewasiliana naye na ametujulisha kwamba blog yake imekumbwa na tatizo la kiufundi ambalo hivi sasa anahangaika kulirekebisha.Tatizo lipo kwa upande wa host wa blog yake(blogger=google).Tatizo wanalijua na wanalishughulikia.Anaangalia pia uwezekano wa kubadilisha host ili mambo yaendelee kuwa mazuri kama ilivyokuwa.

Pia ameomba kuwatoa shaka baadhi ya wasomaji au waulizaji ambao walikuwa wanahisi labda kuna “ufisadi” umefanyika kuiondoa hewani blog yake.Anasema hakuna kitu kama hicho.Wakati huo huo,huku akisubiri mambo yarejee,hivi sasa anaendeleza libeneke kupitia pale kwenye uwanja mpana wa Daily News.Bonyeza hapa ili uone pamoja na mambo mengine,jinsi Watoto wa Jangwani,Yanga, walivyoepushwa na kifungo cha miaka miwili.Haki imetendeka sasa,taratibu zilipindishwa!

 

MICHUZI BLOG YA MUDA July, 12, 2008

Filed under: Blogging,Blogs,Tangazo/Matangazo — bongocelebrity @ 3:45 PM
Ufuatao ni ujumbe kutoka kwa Michuzi.

Wadau kunradhi,

Kutokana na matatizo ya kiufundi aliyonayo host wa globu ya jamii, tutaendeleza libeneke kwa muda kama kawa kupitia michuziblog.blogspot.com hadi hapo mambo yatapokuwa mswano.

Wadau nawaomba msikonde wala nini haya ni mambo ya kawaida ikiwa ni katika kuboresha huduma maana sasa www.michuzi-blog.com ni website kamili na itafanya vitu maradufu ya awali.Asanteni kwa uvumilivu na kunradhi kwa usumbufu ulio nje ya uwezo wetu.

 

MAGAZETI YA UDAKU:YANAJENGA AU KUBOMOA JAMII? July, 8, 2008

Filed under: Blogging,Magazeti,Mahusiano/Jamii,Uandishi — bongocelebrity @ 9:58 PM

Mjadala kuhusu mchango wa magazeti ya “Udaku” katika kujenga au kubomoa jamii una historia ndefu sana. Ni mjadala ambao ulikuwepo,upo na utaendelea kuwepo labda mpaka hapo itakapotokea kwamba maisha na watu watapotea katika sura ya ulimwengu.

Binadamu anabakia kuwa kiumbe mdadisi anayependa kupata habari,kujua kinachoendelea na pia hata kujua alichokifanya jirani yake jana usiku kama sio alichokifanya au anachokifanya mkuu wa nchi awapo mapumzikoni.

Nchini Tanzania, baada ya mapinduzi ya habari na mawasiliano,yaani baada ya kuvuka kile kipindi ambacho kulikuwa na magazeti matatu na kituo kimoja cha redio, paliibuka magazeti ambayo baadaye tumekuja kuyaita “magazeti ya udaku”. Hapo ndipo nasi tulipoingia rasmi kwenye mjadala wa; Je magazeti haya yana mchango gani katika jamii? Yanajenga au yanabomoa?

Hivi karibuni tulipata fursa adimu ya kufanya mahojiano na Abdallah Mrisho Salawi (pichani) Meneja Mkuu wa kampuni inayoongoza kwa uchapishaji wa magazeti ya “udaku” nchini Tanzania ya Global Publishers.Pamoja na mambo kadha wa kadha kumhusu yeye binafsi, Abdallah Mrisho anajaribu kueleza kuhusu kazi zao kama wanahabari na mchango wao au ubomoaji wao wa jamii.Hiyo itatokana na unavyoona wewe hasa baada ya kusoma alichotuambia Abdallah Mrisho.Pia anatoa ushauri muhimu kwa jamii hususani vijana kuhusiana na majanga kama umasikini,ukosefu wa ajira,ukimwi nk.Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo; (more…)

 

BC IS ONE YEAR TODAY! May, 21, 2008

Filed under: Blogging,Blogs,Special Interest News,Uncategorized — bongocelebrity @ 12:04 AM

Tarehe kama ya leo,mwaka mmoja uliopita,BongoCelebrity au BC ilianzishwa. Kwa maana hiyo, leo BC inasheherekea mwaka mmoja!. Tangu kuanzishwa kwake,BC imepost zaidi ya Posts(mitundiko) 440 na kupata zaidi ya maoni 15,613 kutoka kwa wasomaji,watembeleaji na wachangiaji kama wewe. Kwa uhakika kabisa tunaweza kusema kwamba imekuwa ni faraja kubwa. Tuna kila sababu ya kusheherekea siku hii.

Kama ilivyo ada,unaposheherekea kitu kama mwaka mzima uliosheheni mijadala motomoto,mahojiano mbalimbali, habari motomoto nk, unakuwa ni wakati mzuri wa kutafakari ulipotoka na kujenga picha ya unapokwenda.

Tangu kuanzishwa kwake, BC imebakia kuwa na nia ya kukupasha habari mbalimbali kuhusu au zinazowahusu watu mbalimbali ambao aidha tayari ni maarufu au wako mbioni kuelekea kuwa maarufu wakiwa ndani au nje ya Tanzania.Pia burudani,elimu na mahusiano mazuri ya kijamii ni mambo ambayo tunaendelea kuyapa kipaumbele.

Ndani ya mwaka mmoja uliopita,tumefanikiwa kufanya mahojiano na kuandika habari mbalimbali za watu wetu maarufu. Ukitembelea ukurasa wa “Umezisoma Hizi” hapo juu kulia, utaweza kuona orodha nzima ya watu mashuhuri ambao aidha tumeandika habari zao kwa kina au kufanya nao mahojiano ya moja kwa moja. Tunapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru sana celebrities ambao wameturuhusu kutumia picha zao,habari zao nk.Isitoshe, bila kinyongo, wengi wamesikiliza,wamesoma maoni yenu wasomaji kwa heshima na utulivu wa hali ya juu. Walioona wanapaswa kujifunza wamejifunza, tabia zimebadilika, mawasiliano yameongezeka, tija zimezidishwa na kwa ujumla mahusiano ya kijamii yameimarishwa. Haya ni mambo ambayo,kama jamii, tunaweza kujivunia nayo. (more…)

 

SPOTI NA STAREHE April, 23, 2008

Filed under: Blogging,Kabumbu/Soka,Mambo Mseto,Michezo,Soka,Tangazo/Matangazo — bongocelebrity @ 12:54 PM

Kwa wale wapenzi wa habari za michezo na burudani zikiwemo habari motomoto kuhusiana na ligi maarufu ulimwenguni kama vile Premier League, La Liga, Serie A na nyinginezo kijiji kipya kiitwacho Spoti na Starehe kimeanzishwa ili kukupa uhondo wa aina yake. Unaweza kukitembelea kwa kubonyeza hapa.Kazi kwenu.