BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

HONGERA MR AND MRS MALUWE. February, 16, 2009

Filed under: Familia,Watangazaji — bongocelebrity @ 6:57 PM

maluwe

Majuzi wakati ulimwengu unasheherekea sikukuu ya wapendanao,mtangazaji maarufu nchini Tanzania,Michael Maluwe alihitimisha siku hiyo kwa kufunga ndoa na kipenzi chake Diana katika Kanisa Katoliki Parokia ya Msimbazi jijini Dar-es-salaam.

Pichani ni Michael na Diana wakati wa tafrija iliyofanyika katika ukumbi wa Sunset uliopo Mbezi jijini Dar-es-salaam.BC inawatakia ndoa bora yenye Baraka na maelewano tele.

Picha hii ni kwa hisani ya Father Kidevu ambaye kama unamuhitaji kwa shughuli yako unaweza kumpata kupitia simu yake namba +255 755 373999.

Advertisements
 

MR & MRS MBUTU July, 10, 2008

Filed under: Burudani,Familia,Muziki — bongocelebrity @ 11:20 AM

Mwimbaji na mnenguaji maarufu wa Twanga Pepeta,Luiza Nyoni pamoja na mumewe Mr.Mbutu.Luiza Nyoni Mbutu ni miongoni mwa wanamuziki ambao wamekuwepo kwenye fani kwa muda mrefu nab ado anaendelea kutesa.

Picha kwa hisani kubwa ya Global Publishers.

 

HAPPY MOTHER’S DAY TO OUR SWEET MOTHERS. May, 11, 2008

Filed under: African Pride,Familia,Sikukuu,Uncategorized,Wanawake na Watoto — bongocelebrity @ 12:03 AM

Katika nchi nyingi za magharibi,leo ni Mother’s Day au kwa maneno mengine Siku ya Mama.Leo ni siku maalumu ya kumkumbuka,kuutambua na kuuthamini rasmi mchango wa mama yako katika maisha yako.Huu ni utamaduni wa kimagharibi ambao unazidi kuenea kwa kasi ulimwenguni kote zikiwemo pia nchi zetu za kiafrika.Sasa hii sio kumaanisha kwamba katika siku zingine usimkumbuke,usiutambue wala usiuheshimu rasmi mchango wa mama yako.La Hasha!Kila siku,kwa walio wengi, ni siku ya mama. Kwetu sisi waafrika ndio kabisaa.Ndio maana kuna ule usemi kwetu wa Nani Kama Mama?

Itumie siku ya leo kumkumbuka mama yako.Kama kwa bahati mbaya alishaiaga dunia,basi chukua muda maalumu kumkumbuka,kumuombea na muhimu zaidi kumuenzi.Kama upo karibu na mama yako,basi mkumbatie na umkumbushe kwamba unampenda na unamtakia kila la kheri katika maisha.

Ni muhimu pia kukumbuka kwamba, kama binadamu,huwa inatokea wakati mwingine tukakosa kuelewana.Ndio.Huwa inaweza kutokea tukakosa kuelewana hata na mama zetu! Kama hali ipo namna hiyo katika maisha yako,itumie siku hii kusameheana na kuweka mambo sawa na mzazi wako.Jinsi moja nzuri ya kuweza kusamehe ni kujiuliza swali;Je kuna ulazima au manufaa yoyote ninayoyapata kutokana na kutokuelewana huku? Usiwe mgumu wa kusamehe ili nawe upate kusamehewa.Sote tunakosea katika maisha.Kama leo basi ni kesho.Usisite kutenda lililo jema leo.

Katika kuisindikiza siku hii,tumekuchagulia wimbo maalumu kutoka kwa mwanamuziki mkongwe wa nchini Nigeria, Prince Nicco Mbagga.Wimbo unaitwa Sweet Mother. Huu ni wimbo maalumu kwa kina mama wote.Kinamama,tunawapenda na tunawathamini.Bila ninyi dunia si dunia.Bonyeza player hapo chini upate burudani,sikiliza ujumbe uliomo ndani ya wimbo.Happy Mother’s Day!

 

NDOA YA JUMA NATURE YAJIBU April, 9, 2008

Filed under: Bongo Flava,Familia,News — bongocelebrity @ 12:05 AM

Pichani ni Mr and Mrs Juma Nature. Hivi karibuni blog ya Abdallah Mrisho imeripoti kwamba Sir Juma Nature na mkewe aitwaye Bi.Pili, wamebarikiwa kupata mtoto wa kike aliyazaliwa katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke.BC inaungana na wengine wote katika kuwapongeza.

Pichani ni Juma Nature na mkewe Pili siku ya harusi yao mwaka jana.Picha kwa hisani ya Global Publishers.

 

BI.TUNU PINDA March, 3, 2008

Filed under: Familia,Serikali/Uongozi,Siasa,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 12:05 AM

 

Bila shaka ushawahi kuusikia ule msemo wa “kulala masikini kuamka tajiri”.Nia au kiini cha msemo ule huwa ni kuzungumzia jinsi ambavyo maisha huweza kubadilika ghafla,bila hodi wala karibu.Hii ndio hali halisi kwa mke wa Waziri Mkuu(Mizengo Pinda),Tunu Pinda(pichani) ambaye miezi michache tu iliyopita sio watu wengi sana walikuwa wakimjua.Leo hii mambo sio hivyo tena.Bi Tunu keshaanza kulikwea jukwaa la wananchi maarufu.Wanapoketi wake wa “vigogo” wa nchi,huwezi kumkosa au kumuacha pembeni.That’s life!

 

HERE COMES MR. AND MRS. BANANA December, 31, 2007

Filed under: Bongo Flava,Familia,Mahusiano/Jamii,Maisha,Muziki,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 8:41 AM

 

Jana ndio ilikuwa jana.Kama ambavyo imekuwa ikiripotiwa,Banana Zorro na Suzy Walele jana walifunga pingu za maisha.Pichani ni Banana Zorro akimlisha keki mkewe Suzy Walele.Sherehe hiyo iliyofana ilifanyika katika ukumbi wa Msasani Beach Club jijini Dar-es-salaam.Banana na Suzy wamefungua ukurasa mpya.BC inawatakia kila la kheri.Kwa picha zaidi endelea hapa (more…)

 

LEO NI XMAS, NI KUBANJUKA TU. December, 25, 2007

Filed under: Burudani,Familia,Maisha,Sikukuu,Watu na Matukio,Weekend Special — bongocelebrity @ 12:05 AM

Sehemu nyingi sana ulimwenguni hivi leo ni shamrashamra za sikukuu ya Christmas. Mitaani leo kuna kila aina ya shamrashamra.Leo ndio ile siku ya kuvalia zile mpya ulizonunuliwa na mzazi,mke,mume,rafiki,mjomba,shangazi,binamu nk. Harufu iliyotanda mitaani ni ile ya pilau(uh uh uh uh). Fukwe za jiji la Dar-es-salaam kwa mfano,leo zinapata habari yake. Simu za viganjani zinaita kuliko mfano, ni mwendo wa miadi ya kukutana na kufurahia siku hii ambayo hutokea mara moja tu mwaka. Hii ni tofauti na mitaa ya Ulaya au Marekani ya kaskazini. Mitaani hamna mtu, mall na maduka yote leo yamefungwa. Ni siku ya familia.Kila mtu kwao au kwake.Kimya kimya hivi.Usipojua style hizi za wazungu katika kusheherekea Xmas unaweza dhani kuna msiba fulani. Subiri kesho sasa,Boxing Day.Kila mtu mtaani,madukani.Kazi kweli kweli.

Kama anavyoimba mwanamuziki Dennis Kagia aka DNA(pichani) kutoka kwa majirani zetu Kenya, leo ni mwendo wa kubanjuka tu. Ni siku unayotakiwa kusahau matatizo yote,japo kwa muda. Toka nje,ingia mitaani.Jichanganye na wenzako. Usijitie upweke hivi leo. Ni sikukuu.

Mtizame DNA hapo chini kwenye wimbo wake Banjuka. Msikilize akisema “Weka shida chini,tupa mikono juu, Banjuka tu.Life ni fupi na mimi sijivungi” Kama vile haitoshi anasema ‘Sisi tuna shida zetu,tusikilize zako kwanini”? Xmas Njema.Furahia kwa sana lakini kuwa makini,hata kama maisha ni mafupi. Amani na upendo vitawale.