BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

WILL AND JADA IN TANZANIA August, 26, 2008

Filed under: Filamu/Movie,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 3:24 PM

Siku hizi inaelekea Tanzania inakuwa ndio chaguo la superstars wengi kutoka Marekani linapokuja suala la kupumzika au kutoa misaada mbalimbali ya kijamii ingawa wengi bado wanapenda kuingia na kutoka kimya kimya pengine kwa kuogopa “paparazzi wa kibongo”

Kuthibitisha hayo hivi leo waigizaji mashuhuri kutoka nchini Marekani,Will Smith na mkewe Jada Pinkett(si unawaona pichani?), leo hii wameonekana jijini Dar-es-salaam wakiwa wanatoka ndani ya The Kilimanjaro Hotel Kempinski tayari kuelekea visiwani Zanzibar.Kabla ya hapo Willy na Jada walikuwa wametoka Bagamayo mkoani Pwani ambapo walitoa msaada wa vyandarua katika Hospitali ya Wilaya Bagamoyo.

Shukrani Jiachie kwa picha hii.

Advertisements
 

SALAMU ZA BOBBY KUTOKA SOUTH AFRICA August, 6, 2008

Filed under: Elimu na Maendeleo,Filamu/Movie,Maisha,Television,Watangazaji — bongocelebrity @ 10:26 PM

Jina lake kamili ni Robert Gathecha Mongi.Wengi hivi leo tunamtambua kama Bobby.Bila shaka kabisa,Bobby ni miongoni mwa wasimamizi mahiri wa shughuli(MC),watangazaji wa radio na televisheni ambao Tanzania ya leo inaweza kujivunia.Awe anasimamia shughuli,radioni au kwenye televisheni ukimsikiliza utagundua jambo moja;anaipenda kazi yake na anaifanya kwa umakini na utulivu wa hali ya juu.Pengine utulivu huo ndio uliomfanya awe ni mtangazaji wa kutegemewa katika vituo mbalimbali vya radio nchini Tanzania na pia msimamizi wa shughuli zenye hadhi za kimataifa.

Pamoja na mafanikio na “soko” ambalo tayari alikuwa ameshajitengenezea,hivi karibuni alifanya uamuzi mgumu wa kuamua kurudi shuleni ili kunoa zaidi kipaji alichonacho.Hivi sasa anasoma katika Chuo Kikuu cha Cape Town nchini Afrika Kusini.Mbali na kuamua kurudi shule,Bobby ndio kwanza alikuwa “amepata jiko” kabla ya kuwa baba mapema baadaye.Mchanganyiko huo wa mambo ndio unaotufanya tuuite uamuzi wake wa kurudi shule kuwa mgumu!How is he handling all these?

Hivi karibuni tulipata nafasi ya kuzungumza naye machache kuhusiana na maisha yake,shule,ndoto zake na mengineyo mengi.Je anasemaje kuhusu Afrika Kusini anaposomea hivi sasa?Anasomea nini?Nini ushauri wake kwa vijana wanaoota kila siku kwenda “bondeni”?Anazungumziaje maendeleo ya muziki na filamu ya Tanzania akilinganisha na Afrika Kusini? Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo; (more…)

 

MONALISA July, 21, 2008

Filed under: Filamu/Movie — bongocelebrity @ 9:41 PM

Jina lake halisi ni Yvonne Cherry.Ila ukitaka watu watambue haraka kwamba unamuongelea nani basi huna budi kumuita “Monalisa” kwani ndio jina ambalo wengi wamelizoea kutokana na fani yake ya uigizaji filamu kitu ambacho binti huyu amebobea.Monalisa aliwahi kuwa mke wa prodyuza maarufu wa filamu aitwaye George Otieno almaarufu kama Tyson kabla mambo hayajakwenda ndivyo visivyo.

 

ILIVYOFANA ZIFF

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Filamu/Movie,Muziki,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 2:17 PM

Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar au kwa lugha ya wenzetu Zanzibar International Film Festival limemalizika hivi karibuni huko Zanzibar.Tamasha lilifana na pia lilipambwa na wasanii mbalimbali mahiri wa kitanzania.Ngoja picha ziongee. Picha zote na Peter Bennett.

Prof.Jay alikuwepo kuwapa raha kamili mashabiki wake.

Bingwa wa mashairi au mistari, MwanaFA alikuwa gado jukwaani kujibu swali MwanaFA unaoa lini?

AY hakuachwa nyuma.Hapa kwa kushirikiana na MwanaFA(unayemuona kwa mbali) walikuwa wanasema Habari Ndio Hiyo

 

B ZORRO NA MAMBO YA FILAMU July, 7, 2008

Filed under: Burudani,Filamu/Movie,Muziki — bongocelebrity @ 7:08 PM

Banana Zorro,mwanamuziki mahiri wa kizazi kipya ambaye hivi karibuni ameamua kujiingiza katika mambo ya uigizaji filamu.Filamu yake ya kwanza ambayo anatarajia kutoka nayo inaitwa Handsome ambayo imetengenezwa chini ya usimamizi wa kampuni ya New Solution ya jijini Dar-es-salaam.

 

JOHARI June, 9, 2008

Filed under: Filamu/Movie,Television — bongocelebrity @ 7:41 PM

Amezaliwa mkoani Shinyanga nchini Tanzania tarehe 27 Julai 1983.Ni miongoni mwa waigizaji wa kike nchini Tanzania ambao wanafanya vizuri.Safari yake katika uigizaji ilipata spidi alipojiunga na kundi la sanaa lijulikanalo kama Kaole Sanaa Group.Waigizaji wengi nchini Tanzania wamepitia katika kundi hilo. Jina lake halisi ni Blandina Chagula.Lakini kwa wengi anajulikana kama Johari.

Photo/GP

 

UNAMKUMBUKA NORA? June, 7, 2008

Filed under: Filamu/Movie,Television,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 12:53 PM

Bila shaka hujamsahau Nuru Nassoro ambaye kwa wengi hujulikana kama Nora.Kama umemsahau basi kumbukumbu rahisi ni kwamba ni msanii wa maigizo na filamu nchini Tanzania ambaye miaka ya nyuma kidogo aliwahi kujipatia umaarufu na mashabiki kibao.Lakini pia alikuwa kipenzi cha vyombo vya habari.Katika siku za hivi karibuni amekuwa kimya sana kiasi ambacho wengine wamefikia kusema keshastaafu fani.

Hivi majuzi,baada ya kupotea katika macho ya watu kwa muda mrefu, alijitokeza tena wakati wa utoaji wa tuzo za Vinara wikiendi iliyopita pale Diamond Jubilee kama anavyoonekana pichani.Pamoja na kujitokeza,Nora aliwapa watu something to talk about. Bonyeza hapa uone kwanini.

Photo/Ahmad Michuzi.