BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MAXIMO AITA 27 TAIFA STARS February, 2, 2009

Filed under: Kabumbu/Soka,Michezo,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 8:38 PM

maximo1

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Mbrazil Marcio Maximo(pichani), alitangaza kikosi cha wachezaji 27 watakaoshiriki fainali za Afrika kwa nyota wa ndani, zitakazopigwa nchini Ivory Coast kuanzia Februari 22.Kwa habari zaidi bonyeza hapa.

Advertisements
 

BACK TO SCHOOL December, 2, 2008

Filed under: Blogs,Kabumbu/Soka,Michezo — bongocelebrity @ 10:13 PM

pawasabc

Mchezaji maarufu aliyewahi kuichezea Simba Sports Club, APR ya Rwanda na ambaye kwa sasa alikuwa akiichezea timu ya Azam FC Club inayoshiriki ligi ya Vodacom Boniface Pawasa (Baba Ubaya ) amejiunga na Chuo Cha Biashara (CBE) cha jijini Dar-es-salaam mwezi mmoja uliopita ili kuongeza elimu.

Akizungumza na blog ya Full Shangwe hivi karibuni,Pawasa amesema kwa sasa umri wake umeenda hivyo anahitaji kutengeneza maisha mapya na yenye malengo ya baadae na ndiyo maana ameamua kufuata nyayo za wachezaji wenzake waliopita kwa kujiendeleza kielimu.

Pawasa amesema kwa sasa anasomea mambo ya utawala wa biashara ambapo atakuwa chuoni hapo kwa mwaka mmoja akisomea cheti katika fani ya utawala wa biashara yaani Business Administration. Pawasa pia amesema akimaliza anatarajia kuendelea na elimu yake ya Diploma mpaka atakapokamata digrii yake ya kwanza hapo ndiyo ataangalia afanye nini.

Pawasa amesema kuwa pamoja na kwamba kocha wa timu yake ya Azam Santos anamuhitaji ili arejee kundini kuipigania timu yake katika mzunguko wa pili wa ligi ya Vodacom hataweza kurejea tena kwa sababu pia ana maumivu ya misuli ambayo yatamchukua muda mrefu kupona hivyo ameona asipoteze muda kusubiri apone wakati anaweza kufanya kitu kingine cha maendeleo.

Amewashukuru wachezaji wenzake kwa kumpokea chuoni hapo na anasema kwa sasa anafurahia sana maisha ya chuoni kwani rafiki zake wa karibu Ally Mayay, Aron Nyanda na Wilfred Kidilu wamempokea na wanampa sapoti ya hali ya juu na kama wao wameweza kwa nini yeye ashindwe “najua nitaweza tu na nitasoma kama nilivyojiwekea malengo yangu” anamaliza Baba Ubaya.

Pichani juu Boniface Pawasa a.k.a Baba Ubaya(kulia) akiwa na mwenyeji wake na Rais wa serikali ya wanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE) Bw. Ally Mayay ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa Yanga.

Habari na picha kwa hisani ya John Bukuku anayeendesha blog ya Full Shangwe.Mtembelee.

 

HASHEEM ATEULIWA TIMU YA TAIFA YA KIKAPU BONGO November, 24, 2008

Filed under: Michezo — bongocelebrity @ 12:31 PM
Tags: ,

hasheem

Hasheem Thabeet (pichani),mtanzania ambaye wengi wanamtarajia kuwa mtanzania wa kwanza kucheza katika ligi maarufu ya mpira wa kikapu nchini Marekani(NBA), ametajwa kuwa miongoni mwa wachezaji 21 walioteuliewa kuchezea Timu ya Taifa ya mpira wa kikapu nchini Tanzania kwa upande wa timu ya wanaume.Pia wanawake 20 wameteuliwa kuunda timu ya taifa kwa upande wa wanawake.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini Tanzania(TBF),Lawrence Cheyo, timu hiyo ya wanaume itakuwa chini ya makocha Bahati Mgunda na Evarist Mapunda wakati ile ya wanawake itakuwa chini ya makocha Salehe Zonga na Pascal Nkuba.

Majina ya wachezaji walioteuliwa kwa upande wa wanaume ni; Frank Kusiga, Ashraph Harun, Edward Robert, Paschal Nsana, Abdallah Ramadhan Dulla, Francis Mlelwa, Frank Augustino, Sudi Abdallah Razak, Mohamed Ally Dibo, Oswald Maboko,Amon Semberya, Kafashe Abdallah, Tarimo George, Juma Kissoky, Mgindi Mkumbo, Amiri Muhidini, Batungi Gilbert, Alphonse Kusekwa, Jije Makani, Hasheem Thabeet na Alex George.

Kwa upande wa wanawake walioteuliwa kuunda timu ya taifa ni; Annosiata Anthony, Agnes Simkonda, Jabu Shabani,Grace Daud, Grace Peter, Fraja Malaki, Evodia Kazinja, Elizabeth Masenyi, Naima Boli, Mary Meshack, Nipaeli Kessy, Amina Ahmed, Neema Emmanuel, Monica Aloyce, Zakia Kondo, Dajda Ahmed, Dolita Mbunda, Hadija Kalambo,Lucy Sangu na Lucy Augustino.

Timu hizo zipo chini ya udhamini wa kampuni ya Barrick Tanzania na zinatarajiwa kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kanda ya Afrika Mashariki na Kati yatakayofanyikia nchini Rwanda.

 

BAADA YA USHINDI,MANJI AUGUA October, 28, 2008

Filed under: Michezo,Wadhamini/Sponsors — bongocelebrity @ 10:25 PM

Siku moja baada ya kuishuhudia Yanga ikiichapa Simba bao 1-0, mfadhili mkuu wa klabu hiyo, Yusuf Manji ameugua ghafla na kukimbizwa Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam kwa matibabu. SIKU moja baada ya kuishuhudia Yanga ikiichapa Simba bao 1-0, mfadhili mkuu wa klabu hiyo, Yusuf Manji ameugua ghafla na kukimbizwa Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam kwa matibabu.Kwa undani wa habari hii bonyeza hapa.

Pichani ni Mfadhili huyo,Yusuf Manji(kulia) akiwa na Rais Mstaafu wa Yanga,Francis Kifukwe(kushoto).Hii ilikuwa kwenye hafla ya kutiliana mkataba wa udhamini kati ya club za Yanga na Simba na kampuni ya bia nchini.TBL miezi michache iliyopita.

Picha na Issa Michuzi

 

HASHEEM THABEET:HISTORY IN THE MAKING September, 3, 2008

Filed under: African Pride,Michezo,Watanzania Kimataifa — bongocelebrity @ 10:59 PM

If he finally makes it to the NBA, he will become the first Tanzanian national to ever play in that league. Standing at 7″3 and weighing 272lbs, Hasheem Thabeet is the tallest player ever to play for the Huskies. He is currently on his third year at the University of Connecticut studying Psychology. He is highly projected to be among the top five overall pick in the 2009 NBA Draft! By all means, he is currently our Tanzania mostly recognizable athlete in North America if not in the world.

We recently caught up with him for a lengthy and detailed interview on his humble beginnings all the way to where he is right now as well as where he is going or wants to go. Hasheem had a lot to say. Does he believe that he will finally make his dreams to play in the NBA come true? Is he into the game for money or for the passion of the game? Who does he turn to when he needs advice? Who does he compare himself to among the big names in the NBA? Here is the full interview;

BC: For the benefit of our readers who have not yet heard or read about your life history, can you briefly tell us where were you born, which schools did you attend in Tanzania, how many brothers and sisters do you have etc?

HT: First of all thank you very much for inviting me for this interview. My Name Is Hasheem Thabeet.I was born on February 16, 1987. I was raised in Dar-es-salaam, Tanzania. I have a 22 years old sister called Sham and a 17 years old brother called Akbar. As for school, I first went to Mlimani Primary School and then Makongo High School (both in Dar-es-salaam Tanzania) before transferring to Laser Hill Academy in Kenya. (more…)

 

ANA KWA ANA NA “MWENYEKITI” MAGGID MJENGWA. August, 17, 2008

Kama wewe ni msomaji mzuri wa magazeti na majarida mbalimbali kutoka Tanzania,basi sina shaka kabisa kwamba jina Maggid Mjengwa (pichani) litakuwa sio geni kwako! Makala zake za kusisimua,kuchokoza hisia na kujenga hoja za nguvu ni miongoni mwa vivutio muhimu vya wasomaji wa magazeti ndani na nje ya Tanzania. Leo hii tunaweza kabisa kuthubutu kusema kwamba Maggid ni miongoni mwa wanahabari bora tulionao kwani hana uoga wowote pale anapokuwa anaandika au kuongelea jambo ambalo analiamini kwa dhati.

Lakini Maggid,kama ambavyo pengine unafahamu tayari, haishii magazetini tu bali pia ni blogger maarufu hivi sasa. Blog yake ya picha ambayo mwenyewe anaiita “kijiji” na hivyo wasomaji wake na watembeleaji wake “wanakijiji”, imejipatia umaarufu sana kwa kuonyesha au kwenda kule ambapo ndiko kunahesabika kuwa kwenye hali halisi ya maisha ya mtanzania. Ukiitembelea na kuisoma blog yake vizuri kwa kutizama picha lukuki zinazoipamba blog yake,utaweza kuwa jaji mzuri kama “bongo ni tambarare” au bado zile ahadi za uchaguzi uliopita ni mbwembwe za kisiasa tu.Mwenyewe anasema blog yake ni kimbilio na sauti kwa wale ambao kila mara huwa wanasahauliwa!

Maggid pia ni mjasiriamali.Yeye ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ijulikanayo kama Ikolo Investment Co ambao ndio wachapishaji wa Gozi Spoti; jarida la michezo, sanaa, maisha na burudani linalotoka kila Jumatano. Maggid pia ni mwanamichezo,mpenda michezo na shabiki mkubwa wa soka.

Hivi karibuni,baada ya kumsaka kwa muda mrefu kutokana na ratiba zake za kazi kumbana,tulifanikiwa kupata fursa ya kufanya naye mahojiano utakayoyasoma hivi punde.Kama ambavyo ungetegemea,Maggid anatoa “darasa” katika mahojiano haya.Mbali ya kukupa historia ya maisha yake kwa undani,Maggid anakumbusha vipengele fulani fulani vya historia ya nchi yetu ambavyo ni muhimu. Lakini kwa mapana, anaongelea kuhusu suala la uandishi na pia blog yake bila kusahau changamoto ambazo nchi yetu inakabiliwa nazo hivi leo katika nyanja mbalimbali. Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo; (more…)

 

TBL NA UDHAMINI WAO KWA YANGA NA SIMBA

Filed under: Michezo,Wadhamini/Sponsors,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 6:10 PM

Usiku wa leo,pale katika Hotel ya Movenpick jijini Dar-es-salaam palifanyika uzinduzi rasmi wa udhamini kutoka kampuni ya bia nchini(Tanzania Breweries Limited ) kwa timu mbili maarufu za soka nchini Tanzania,Yanga na Simba.

Ufadhili huo wa miaka mitatu una thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja kwa mwaka.Kila timu inatarajiwa kupata zaidi ya milioni 654. Pesa hizo zitatumika kwa gharama za uendeshaji, mishahara ya wachezaji na viongozi wanaoongozana na timu,vifaa vya mazoezi,jezi,usafiri wa timu,matangazo nk.Hapo chini ni baadhi ya picha za tukio zima.Picha zote na Issa Michuzi.

Viongozi wa TBL,Yanga na Simba wakitia saini makubaliano ya udhamini huo

Makabidhiano ya mkataba.

Mara tu baada ya kutiliana sahihi makubaliano ya udhamini kilichofuata ni makabidhiano ya “mkwanja”.Pichani kiongozi wa Yanga,Imani Madega(kulia) akipokea mfano wa hundi ya milioni 25 ikiwa kama kianzio tu cha udhamini huo.

Kiongozi wa Simba,Hassan Dalali(kushoto) naye akipokea alichokabidhiwa mwenzake wa Yanga hapo juu.