BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MPOTO ASAKA NAULI YA KWENDA IKULU February, 4, 2009

Filed under: Burudani,Mahusiano/Jamii,Mawazo/Tafakuri,Sanaa/Maonyesho,Serikali/Uongozi — bongocelebrity @ 8:00 PM

mrishompotobc

UMAHIRI wa Mrisho Mpoto umekuwa ukiwakuna wengi hasa anapokuwa jukwaani akidondosha mashairi yake na mwaka jana alifanikiwa kushinda moja ya tuzo kubwa katika sanaa kwa Afrika ijulikanayo kama Slam, ambayo ilikuwa inashikiliwa na mmoja wa wasanii mahiri aitwaye, Steff H2K kutoka Mauritius.

Ushindi wa Mpoto umemfanya apate nafasi ya kushiriki fainali za tuzo za Slam za dunia, ambazo zinafanyika nchini Ufaransa Machi, mwaka huu lakini hiyo haitoshi wala haimzuii yeye kuendelea kusaka nauli ya kwenda Ikulu.

Baada ya kuwa ameshiriki katika wimbo wa ‘Salamu Zangu’ na kuweza kuchukua nafasi kubwa huku akimfunika mmliki wa wimbo huo Irene Sanga, Mpoto ameamua kuibukia upande wa pili na kutoa wimbo wa ‘Nikipata Nauli’.

[Usikilize wimbo “Nikipata Nauli” kwa kubonyeza player hapo chini kisha ndio uendelee kusoma makala hii hapo chini]JM

(more…)

Advertisements
 

I AM A PROFFESSIONAL- FID Q January, 15, 2009

Filed under: Bongo Fleva,Burudani,Muziki,Sanaa/Maonyesho — bongocelebrity @ 1:17 PM

fid-qbc

Bongo,Bongo…ooh Bongo!Kila kukicha watu wanazidi kuwa wabunifu na wagunduzi. Kila siku akili zinazidi kuchemka, bongo zinazidi kutenda kinachotakiwa kutendwa.

Kama bado huamini kwamba Bongo inazidi kuja juu kwa ubunifu,basi jaribu kwanza kutizama hapo chini video mpya kutoka kwa Fareed Kubanda aka Fid Q(pichani) iitwayo I AM A PROFFESSIONAL ambayo ni single ya tatu kutoka kwenye albamu yake iitwayo Darwinz Naitmea.Kutoka kwetu hakuna la ziada bali pongezi kwa Fid Q kwa ubunifu na uchapa kazi.


 

JENNIFER MGENDI: NYOTA INAYONG’AA KATIKA MUZIKI WA INJILI January, 12, 2009

Filed under: Dini,Gospel Music,Sanaa/Maonyesho — bongocelebrity @ 11:38 AM

jenny6bc

Akiwa tayari na albamu zisizopungua tano kibindoni, Jennifer Mgendi(pichani) ni miongoni mwa wanamuziki wa muziki wa injili au kwa kiingereza Gospel nchini Tanzania ambao wamejijengea sifa na umaarufu mkubwa kutokana na kazi yake hiyo ya uimbaji na kumtukuza mola.

Lakini tofauti moja kubwa ya Jennifer na wanamuziki wengine wa muziki wa injili ni kwamba yeye pia ni mtunzi mzuri wa hadithi za filamu.Baadhi ya filamu alizowahi kutunga ni kama vile Pigo la Faraja, Joto la Roho na Teke la Mama.

Alianza rasmi kujishughulisha na kazi ya muziki wa injili mwaka 1995.Albam yake ya kwanza iliitwa ‘Nini?’. Baada ya hapo alitoka tena na albamu zake zilizokwenda kwa majina ‘Ukarimu wake’, ‘Yesu Nakupenda’,’Nikiona Fahari’ na ya hivi karibuni zaidi inayoitwa Mchimba Mashimo.

Hivi karibuni tulipata nafasi ya kufanya naye mahojiano ambayo utayasoma hivi punde. Katika mahojiano haya,Jennifer anakupa kwa undani kuhusu historia yake kimuziki na kibinafsi. Ni kweli kwamba muziki wa injili wa leo ni wa “kidunia” zaidi ya “kiroho”? Anasemaje kuhusiana na hoja hiyo? Je Jennifer anaongeleaje tofauti za muziki wa injili na ule wa Bongo Fleva?Unakubaliana naye?

Nini mipango yake kwa mwaka huu wa 2009 na ana ushauri gani kwa vijana?Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;

BC: Karibu Jennifer ndani ya BC.Sijui nikuambie mambo vipi au bwana asifiwe?

JM:Asante sana ndugu yangu. Yote mema tu kwani mambo ni safi na Bwana anaendelea kusifiwa…

BC:Kwa kifupi tu unaweza kutueleza historia ya maisha yako?

JM:Nilizaliwa miaka karibu 37 iliyopita hapa hapa jijini Dar es Salaam katika familia ya watoto watatu nikiwa nimetanguliwa na kaka wawili. Nimepata elimu yangu katika mikoa ya Dar es salaam na Tanga. Nilianza uimbaji rasmi mwaka 1995 na hapo katikati nilifanya kazi kadhaa za kuajiriwa kama Ualimu na Ukutubi lakini tangu mwaka 2007 niliacha kazi za kuajiriwa na mpaka hivi leo ninafanya shughuli zangu binafsi. (more…)

 

KILA LA KHERI PROF! November, 19, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Sanaa/Maonyesho,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 10:35 PM
Tags: ,

jaybc

MWANAMUZIKI maarufu wa Hip Hop nchini, Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay, anaondoka nchini kesho (Novemba 20, 2008) kwenda Abuja, Nigeria kutumbuiza kwenye tuzo za muziki za MTV Africa Music Awards with Zain (MAMA).Kwa undani zaidi wa habari hii bonyeza hapa.BC inamtakia kila la kheri Prof.Jay.

 

NURU KUFUNGUA SHOW YA ALI KIBA NCHINI SWEDEN November, 16, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Sanaa/Maonyesho,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 8:54 PM
Tags:

nurubc1Anaitwa Nuru Magram.Makazi yake ni ndani ya jiji la Stockholm nchini Sweden. Bila shaka unamkumbuka kwa vibao vyake kama vile Walimwengu na Msela ambavyo ndivyo vilimtoa katika ulimwengu wa muziki.

Hivi karibuni amekuwa studio akikamilisha project yake mpya ya muziki ambayo itakamilika hivi karibuni.Lakini kuonyesha jinsi ambavyo bado hajajiweka kando na mambo ya muziki, hivi karibuni mnamo tarehe 22 Novemba anatarajiwa kufungua show ya mwanamuziki mwingine wa Bongo Flava, Ali Kiba.Show hiyo itafanyikia jijini Stockholm.

Ali Kiba inasemekana ameweka rekodi ya kuwa mwanamuziki wa kwanza wa muziki wa kizazi kipya kufanya tour ndefu kushinda zote zilizowahi kufanywa na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya.Nuru ameahidi kufanya vitu visivyo vya kawaida hiyo tarehe 22 Novemba.Kazi kwenu wakazi wa Sweden na nchi zilizo jirani.Unaweza kumcheki Nuru hapo chini katika wimbo wake Walimwengu.Ni zouk iliyokuwa imetulia na yenye ujumbe mzuri.


 

FIESTA MWANZA:Full Kujiramba! November, 4, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Sanaa/Maonyesho,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 9:48 AM
Tags: , ,

img_7642

Ilikuwa ni full kujiramba Rock City

img_7833Kundi la TMK Wanaume linaloongozwa na mheshimiwa Temba wakilishambulia jukwaa la fiesta ndani ya img_7902Mwanamuziki kutoka Mombasa-Kenya aitwaye Nyota Ndogo akiwa na mcheza shoo wake zawadi wakilipagawisha dume la Mwanza mbele ya umati wa watu waliofika kwenye tamasha la fiesta jirambe ndani ya uwanja wa mpira wa ccm Kirumba jijini Mwanza.Kwa picha zaidi ya tamasha hilo ingia michuzijr.blogspot.com

 

NYOTA NJEMA YAANZA KUMUANGAZIA MIRIAM ODEMBA October, 28, 2008

Filed under: African Pride,Sanaa/Maonyesho,Urembo — bongocelebrity @ 9:39 AM

Mrembo Miriam Odemba(pichani) ambaye yuko nchini Philippines akiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Earth amefanikiwa kuingia katika tano bora katika shindano la kutafuta mrembo aliyependeza katika vazi la ufukweni katika kundi lake.

Mashindano haya yalijumuisha baadi tu ya warembo 90 ambao wanashiriki katika mashindano ya Miss Earth 2008 kwani fainali ya mashindano ya vazi la ufukweni yatafanyika tarehe 1 Novemba. Katika kundi lake, Miriam aliweza kuwapiku warembo wenzake takriban 30 kwa kupita jukwaani kwa kujiamini katika vazi hili la ufukweni.

Washindi wengine ni Columbia, France, Greece na Canada. Mshindi wa kwanza alikuwa Canada ambaye alijinyakulia zawadi ya dola 1,500.