BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

JK AKIAGA SHINYANGA February, 8, 2009

Filed under: Serikali/Uongozi,Siasa — bongocelebrity @ 2:11 PM

jk-shybcKwa heri kaka…uje tena!

jkshy2bc

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na baadhi ya wakazi wa mji wa shinyanga muda mfupi baada ya kuwahutubia katika mkutano wa hadhara katika uwanja wa michezo wa Kambarage mjini humo jana.Rais Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete tayari wamerejea jijini Dar es Salaam(picha na Freddy Maro)

Advertisements
 

MPOTO ASAKA NAULI YA KWENDA IKULU February, 4, 2009

Filed under: Burudani,Mahusiano/Jamii,Mawazo/Tafakuri,Sanaa/Maonyesho,Serikali/Uongozi — bongocelebrity @ 8:00 PM

mrishompotobc

UMAHIRI wa Mrisho Mpoto umekuwa ukiwakuna wengi hasa anapokuwa jukwaani akidondosha mashairi yake na mwaka jana alifanikiwa kushinda moja ya tuzo kubwa katika sanaa kwa Afrika ijulikanayo kama Slam, ambayo ilikuwa inashikiliwa na mmoja wa wasanii mahiri aitwaye, Steff H2K kutoka Mauritius.

Ushindi wa Mpoto umemfanya apate nafasi ya kushiriki fainali za tuzo za Slam za dunia, ambazo zinafanyika nchini Ufaransa Machi, mwaka huu lakini hiyo haitoshi wala haimzuii yeye kuendelea kusaka nauli ya kwenda Ikulu.

Baada ya kuwa ameshiriki katika wimbo wa ‘Salamu Zangu’ na kuweza kuchukua nafasi kubwa huku akimfunika mmliki wa wimbo huo Irene Sanga, Mpoto ameamua kuibukia upande wa pili na kutoa wimbo wa ‘Nikipata Nauli’.

[Usikilize wimbo “Nikipata Nauli” kwa kubonyeza player hapo chini kisha ndio uendelee kusoma makala hii hapo chini]JM

(more…)

 

NINI KILIMLIZA WAZIRI MKUU? February, 2, 2009

Filed under: Serikali/Uongozi,Siasa,Tanzania/Zanzibar,Uandishi — bongocelebrity @ 8:51 PM

pindabcWiki iliyopita kuna kitu cha nadra kidogo kilitokea nchini Tanzania.Ni kitendo cha Waziri Mkuu,Mizengo Pinda,kububujikwa na machozi bungeni.Baada ya hapo kumezuka mijadala mbalimbali likiwemo swali ambalo kimsingi sio rahisi sana kulijibu.Swali ni kama linavyoonekana katika kichwa cha habari hapo juu;Nini kilimliza Waziri Mkuu?

Sambamba na swali hilo,wapo watu lukuki,akiwemo Ansbert Ngurumo,wanaouliza msururu wa maswali ya msingi;Je Waziri Mkuu aliwalilia albino?Je aliililia serikali?Je alijililia mwenyewe?Na Ndimara Tegambwage anajadili je Waziri Mkuu akilia ndio kumaanisha kwamba serikali nzima imelia?Wewe unasemaje?

 

KAZI BADO INAENDELEA… January, 27, 2009

Filed under: Serikali/Uongozi,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 7:41 PM

amatus-bliyumba

Kazi bado inaendelea…Zaidi bonyeza hapa.

 

PROF.JUMANNE MAGHEMBE January, 7, 2009

Filed under: Elimu na Maendeleo,Serikali/Uongozi,Swali kwa Jamii — bongocelebrity @ 9:36 PM

maghembe

Pichani ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Profesa Jumanne Maghembe.Huyu ni miongoni mwa mawaziri ambao wizara zao zimekuwa zikikumbwa na vimbwanga mbalimbali.Utakumbuka mwaka huu jinsi mitihani ya kidato cha nne ilivyovuja.Kwa upande mwingine kumekuwepo na kuongezeka kwa lawama kwamba kiwango cha elimu nchini kinazidi kushuka.Profesa Jumanne Maghembe ni Mbunge wa CCM akiwakilisha Wilaya ya Mwanga iliyopo mkoani Kilimanjaro. Unakubaliana na mtazamo kwamba kiwango cha elimu nchini kinazidi kuporomoka siku baada ya siku?Kama jibu ni ndio,nani unadhani anatakiwa kubebeshwa lawama?Nini kifanyike?


 

DR.JAKAYA MRISHO KIKWETE December, 19, 2008

Filed under: Serikali/Uongozi,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 3:48 PM

jk

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kenyatta nchini Kenya, Dk.Harris Mule akimtunuku Phd ya Heshima Rais Jakaya Kikwete wakati wa mahafali ya 25 ya chuo hicho yaliyofanyika mjini Nairobi,Kenya leo. Phd hiyo inatokana na jitihada zake za utatuzi wa migogoro kwa nchi za Afrika hasa mgogoro wa Kenya uliozuka baada ya uchaguzi mapema mwaka huu.

Photo/Freddy Maro

 

NI ZAMU YA GRAY MGONJA! December, 15, 2008

Filed under: Breaking News,Developing News,Serikali/Uongozi,Sinema — bongocelebrity @ 10:13 AM

mgonjabc1

Kama ulidhani ya mwaka 2008 ndio yashaisha basi ulikosea.Mambo yangali yakiendelea.Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha na Mipango,Bw.Gray Mgonja leo ametinga kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Henzron Mwankenja, akikabiliwa na mashtaka mbalimbali.Mojawapo ya mashtaka anayokabiliwa nayo ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka kama ilivyokuwa kwa mawaziri wa zamani wa wizara hiyo nyeti, Daniel Yona na Basil Mramba waliofikishwa kizimbani wiki mbili zilizopita.

Habari hii inaendelea…stay tuned.