BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

NALIVUA PENDO-MWASITI February, 1, 2009

Filed under: Bongo Fleva,Burudani,Single/Mpya — bongocelebrity @ 10:30 PM

mwasitibc

Mojawapo ya mambo mazuri ambayo yanatokea nchini Tanzania hivi leo ni kuibuliwa kwa vipaji mbalimbali miongoni mwa vijana na kitu kinachoitwa Tanzania House of Talent (THT).Kama umewahi kuhudhuria shughuli ambapo miongoni mwa watoa burudani walikuwa ni vijana wanaotokea THT bila shaka utakubaliana nasi tunaposema kwamba vipaji vipo nchini Tanzania.Kinachotakiwa ni uongozi na mikakati mizuri ya kuviboresha na kuvionyesha ulimwenguni.

Miongoni mwa vipaji vilivyowahi kuibuliwa na THT ni mwanadada Mwasiti(pichani).Msikilize hapa katika wimbo wake mpya uitwao Nalivua Pendo kwa kubonyeza hapo chini.Kazi nzuri Mwasiti!


Advertisements
 

HAINA NGWASU-INSPEKTA HARUNI January, 29, 2009

Filed under: Bongo Flava,Bongo Fleva,Burudani,Muziki,Single/Mpya — bongocelebrity @ 7:43 PM

inspektabc1

Bila ubishi Inspekta Haruni ni miongoni mwa wasanii wa Bongo Flava ambao wanastahili na wana haki kabisa ya kujiweka katika lile kundi la “wakongwe katika fani”.Pia Inspekta anadumu katika lile kundi la “wataalamu wa vina(mashairi) na tunzi ambazo baada ya kutoka hewani hugeuka zikawa misemo ya mitaani.

Kama hukubaliani name,basi jaribu kuusikiliza kwanza wimbo mpya kutoka kwa Inspekta unaokwenda kwa jina la Haina Ngwasu kwa kubonyeza player hapo chini.

Na kama jadi mpya ya wasanii wa bongo flava mashairi ya wimbo huu yanaelekea kuwa “ujumbe” kwenda kwa mtu fulani au watu fulani?Mawazo yangu.Sikiliza na wewe utuambie.Pata burudani.

Photo/Ahmad Michuzi


 

NJOO-PROF.JAY ft KLEPTOMANIACS January, 21, 2009

Filed under: Bongo Fleva,Single/Mpya — bongocelebrity @ 8:05 PM

prof-jay-bc1

Wakubwa wanapopiga kelele kuhusiana na sera za Jumuiya ya Afrika Mashariki,vijana wao wanafanya kazi.Wanashirikiana bila kusita katika kazi zao,hususani za kisanii.Sio kwamba nafananisha siasa na sanaa..hapana…nasema tu!Pengine kuna lolote wakubwa wanaweza kujifunza kutoka kwa vijana?Sina uhakika.

Ushirikiano ninaouongelea hapa ni ule wa Prof.Jay(a.k.a Red Carpert) katika single mpya iitwayo Njoo.Katika wimbo huu ambao umo katika albamu yake ya Aluta Kontinua(kama hujanunua kopi yako halali,fanya hivyo)Prof.Jay amewashirikisha wasanii kutoka Nairobi, Kenya wanaokwenda kwa jina la Depicto/D.E.P(jina kamili Collins Majale) na Nyashinski(jina kamili Nyamari Ongegu) na Munkiri(jina kamili Robert Manyasa) kutoka kundi linalojiita Kleptomaniacs.Wimbo huu umerekodiwa jijini Nairobi chini ya Producer Msyoka.

Hebu sikiliza jinsi hali inavyokuwa Kiswahili cha Dar kinapokutana na kile cha Nairobi.Patamu.Pata burudani.

Picha kwa hisani ya DJ Choka.


 

MSIACHE KUONGEA-MwanaFA ft LADY JAY DEE

Filed under: Bongo Fleva,Burudani,Single/Mpya — bongocelebrity @ 8:00 PM

mwanafabc10Ukishakuwa na umaarufu fulani ni wazi kwamba unakuwa kipenzi cha vyombo vya habari.Yaweza kuwa kwa mazuri au kwa mabaya.Watu hupenda kusikia mtu maarufu fulani kafanya nini,anapanga kufanya nini nk.

Mbali na vyombo vya habari,mitaani pia(labda kupitia walichokisoma gazetini au kukisikia redioni) maneno huwa hayaishi.Huko nako ni mwendo mdundo.Aidha kupewa “ushauri wa bure” au maneno yaliyojaa chuki binafsi na yenye nia ya kumuangamiza mtu.Ndio maisha yalivyo.

jide-komandobcLakini maneno yakizidi huwa yanaweza kuwa kero.Na hali ikifikia hapo,basi sio vibaya kukumbushana kwamba hapo sipo na mambo kama hayo.Maisha lazima yawe na uwiano.Kukumbushana tunapoteleza,kusifia inapobidi na siku zote kuwezeshana.

Sikiliza wimbo huu mpya kutoka kwa MwanaFA akiwa ameshirikiana na Lady Jay Dee.Wimbo unaitwa Msiache Kuongea. Katika chorus sikiliza kwa makini kwanini Jide na FA wanasema Msiache Kuongea.Kisha sikiliza kwa makini mashairi yaliyomo.Kazi nzuri FA na Jide. 

BABA WA KAMBO-THE NGOMA AFRICA BAND November, 16, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Single/Mpya — bongocelebrity @ 8:09 PM
Tags: , ,

ngoma-africabc1

The Ngoma Africa Band(pichani),bendi ya muziki wa dansi yenye makao yake nchini Ujerumani bado wanaendelea kuwa mabalozi wetu wazuri katika anga za muziki na burudani hususani katika nchi za Ulaya.

Hivi karibuni wamekuja na wimbo unaokwenda kwa jina la Baba wa Kambo ukiwa ni utunzi wake kiongozi wa bendi hiyo Ebrahim Makunja aka Ras Makunja. Wimbo umeimbwa na yeye mwenyewe Ras Makunja akishirikiana na mpiga solo guitar wa bendi hiyo Chris B.

Unaweza kuusikiliza wimbo huo kwa kubonyeza player hapo chini.Sikiliza jinsi The Ngoma Africa walivyopeleka kesi kwa Mkuu wa Wilaya ya Tegeta,Issa Michuzi. Salamu kwa wote huko Ujerumani wana The Ngoma Africa Band.


 

NI WAKATI WA “FREEZE” KUTOKA KWA AY October, 29, 2008

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Muziki,Single/Mpya — bongocelebrity @ 1:52 PM

Anaitwa Ambwene Yessayah.Kwa wengi anafahamika kama AY huku wengine wakiendelea kumuita “Mzee wa Commercial”.Kwake muziki ni burudani na pia ni kazi.Mafanikio yake katika game ni mfano wa kuigwa na wengi hususani wasanii wanaochipukia.Ni miongoni mwa “mabalozi” wazuri wa Tanzania nje ya nchi kupitia sanaa ya muziki.Kwa mara nyingine tena mwaka huu anawania tuzo maarufu za Kisima za nchini Kenya.

BC ina furaha kuutambulisha kwako wimbo mpya kutoka kwa AY.Wimbo unaitwa FREEZE.Amewashirikisha P.SQUARE kutoka nchini Nigeria. Wimbo umetayarishwa na kurekodiwa na Producer Hermy B kutoka Tanzania.Tayari wimbo huu unakamata chart katika vituo mbalimbali vya radio.Unaweza kuusikiliza kwa kubonyeza player hapo chini.
 

“WASANII WAJIELIMISHE,WAPENDANE NA WASIDANGANYANE”-KBC September, 14, 2008

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Muziki,Single/Mpya,Tanzania/Zanzibar,Watangazaji — bongocelebrity @ 7:47 PM

Kabla ya makundi ya muziki kama vile Wanaume TMK,Das Nundaz,Nako2Nako,East Coast na mengineyo kuibuka au hata kutambulika kwenye anga za muziki nchini Tanzania yalikuwepo makundi ambayo hivi leo wengi tunakubaliana kwamba hao ndio waanzilishi wa kinachoonekana hivi leo kuwa kama vuguvugu la vijana katika kupigania haki yao ya msingi ya kujielezea(freedom of expression) katika jamii kupitia sanaa ya muziki.

Miongoni mwa makundi hayo ni lile lililotamba sana na kujulikana kama Kwanza Unit.Miongoni mwa wasanii waliokuwa wanaunda kundi hilo ni KBC au KSingo(pichani) kama alivyojulikana wakati ule na hata hivi sasa.Mbali na Kwanza Unit,wengi bado mtakuwa mnamkumbuka kama mpigania haki za Wana Hip Hop na pia miongoni mwa wanamuziki waliojitolea sana katika kuhakikisha kwamba Hip Hop ya Tanzania inaeleweka na kukubalika.Pia wengine mtamkumbuka kama DJ pale Clouds FM katika Dr.Beat.

Tukiwa bado katika kuhakikisha kwamba historia ya vuguvugu hilo na kwa ujumla historia nzima ya muziki tunaouita “wa kizazi kipya” hivi leo,haipotei na inawekwa vyema mtandaoni,hivi karibuni tulifanya mahojiano na KBC kama utakavyoyasoma hivi punde.

Je unakumbuka Kwanza Unit ilianzishwa mwaka gani?Nini yalikuwa malengo ya mwanzoni?Leo hii KBC akiangalia nyuma anaona tofauti gani au maendeleo ya aina gani katika muziki wa kizazi kipya?Nini ushauri wake kuhusu masuala ya haki miliki na utawala wa biashara ya muziki?Kwa maoni yake,nani anachangia kudidimiza muziki?Ni producer au Radio DJ?

Ili kupata majibu ya maswali hayo na mengineyo mengi,fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo ambayo pia yana Swanglish ya aina yake katika kuleta au kuchanganya ladha kiaina; (more…)