BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

SHUKRANI WADHAMINI December, 2, 2008

Filed under: Tangazo/Matangazo,Wadhamini/Sponsors — bongocelebrity @ 9:45 PM
Tags: ,

zara-tours-logoLeo tunapenda kuwashukuru wadhamini wetu kampuni ya Zara Tours ambao wanaongoza kwa huduma zote zinazohusiana na utalii nchini Tanzania.Zara Tours ndio inayoongoza pia kwa kuandaa safari za kupanda Mlima Kilimanjaro.Shukrani nyingi kwa udhamini wenu.

Kwa habari zaidi kuhusu huduma za utalii zitolewazo na Zara Tours,bonyeza hapa ili kutembelea tovuti yao.

NB: Kama na wewe una biashara au kampuni na ungependa kuwa mmoja wa wadhamini wa BC,usisite kuwasiliana nasi kupitia bongocelebrity at gmail dot com au kupitia kwenye fomu inayopatikana katika ukurasa wa “Kuhusu BongoCelebrity” hapo juu.

Advertisements
 

BAADA YA USHINDI,MANJI AUGUA October, 28, 2008

Filed under: Michezo,Wadhamini/Sponsors — bongocelebrity @ 10:25 PM

Siku moja baada ya kuishuhudia Yanga ikiichapa Simba bao 1-0, mfadhili mkuu wa klabu hiyo, Yusuf Manji ameugua ghafla na kukimbizwa Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam kwa matibabu. SIKU moja baada ya kuishuhudia Yanga ikiichapa Simba bao 1-0, mfadhili mkuu wa klabu hiyo, Yusuf Manji ameugua ghafla na kukimbizwa Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam kwa matibabu.Kwa undani wa habari hii bonyeza hapa.

Pichani ni Mfadhili huyo,Yusuf Manji(kulia) akiwa na Rais Mstaafu wa Yanga,Francis Kifukwe(kushoto).Hii ilikuwa kwenye hafla ya kutiliana mkataba wa udhamini kati ya club za Yanga na Simba na kampuni ya bia nchini.TBL miezi michache iliyopita.

Picha na Issa Michuzi

 

TBL NA UDHAMINI WAO KWA YANGA NA SIMBA August, 17, 2008

Filed under: Michezo,Wadhamini/Sponsors,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 6:10 PM

Usiku wa leo,pale katika Hotel ya Movenpick jijini Dar-es-salaam palifanyika uzinduzi rasmi wa udhamini kutoka kampuni ya bia nchini(Tanzania Breweries Limited ) kwa timu mbili maarufu za soka nchini Tanzania,Yanga na Simba.

Ufadhili huo wa miaka mitatu una thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja kwa mwaka.Kila timu inatarajiwa kupata zaidi ya milioni 654. Pesa hizo zitatumika kwa gharama za uendeshaji, mishahara ya wachezaji na viongozi wanaoongozana na timu,vifaa vya mazoezi,jezi,usafiri wa timu,matangazo nk.Hapo chini ni baadhi ya picha za tukio zima.Picha zote na Issa Michuzi.

Viongozi wa TBL,Yanga na Simba wakitia saini makubaliano ya udhamini huo

Makabidhiano ya mkataba.

Mara tu baada ya kutiliana sahihi makubaliano ya udhamini kilichofuata ni makabidhiano ya “mkwanja”.Pichani kiongozi wa Yanga,Imani Madega(kulia) akipokea mfano wa hundi ya milioni 25 ikiwa kama kianzio tu cha udhamini huo.

Kiongozi wa Simba,Hassan Dalali(kushoto) naye akipokea alichokabidhiwa mwenzake wa Yanga hapo juu.

 

UJUMBE KUTOKA KWA WADHAMINI July, 1, 2008

Filed under: Safari,Tangazo/Matangazo,Wadhamini/Sponsors — bongocelebrity @ 12:02 PM

Kwa habari zaidi bonyeza hapa.