BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

“KARIBUNI RAINBOW CLUB”-BONNY LUV January, 19, 2009

Filed under: Burudani,Muziki,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 8:37 PM

bonnybc1Endapo kila ifikapo mwisho wa wiki umekuwa miongoni mwa watu ambao wamekuwa wakijiuliza waende wapi wawapo jijini Dar-es-salaam,BC leo inakuletea habari nzuri.Sasa una mahali pa kwenda. Sehemu hiyo inaitwa Rainbow na ipo maeneo ya Mbezi Beach ukiwa unatokea Michocheni(Kwa Nyerere).

Yapo mambo mawili ya msingi ambayo yanaifanya Rainbow kuwa kimbilio la wapenda burudani jijini Dar-es-salaam.Kwanza klabu hii ndio itakuwa “kijiwe” maalumu kwa wale wenzangu na mie ambao wanapendelea miziki ya “Old School”.

Pili burudani nzima itakuwa ikiporomoshwa na kusimamiwa na DJ mzoefu na ambaye katika watu kumi,tisa wanakubaliana kwamba ni moto wa kuotea mbali na anajua anachokifanya linapokuja suala zima la kukata kiu ya burudani. Huyu si mwingine bali ni DJ Bonny Luv(pichani)

bluvbc

Tulipopata habari kuhusu ufunguzi rasmi wa klabu hii,tulimtafuta Bonny Luv ili tujue machache kuhusiana na klabu hiyo maalumu kwa Old School na burudani zingine.Fuatana nasi katika mahojiano haya mafupi;

BC: Kwanza hongera sana kwa kuanzisha joint mpya na karibu tena ndani ya BC.Mambo yanakwendaje?

BONNY LUV: Shukrani sana kaka.Namshukuru Mungu

BC: Tumekutafuta ili tuongelee kidogo kuhusu hii sehemu mpya ya maraha uliyoianzisha.Kwanza ilikuwaje ukaamua kuanzisha disco hili.Uliona mapungufu yoyote kwenye medani ya burudani hususani upande wa disco? (more…)

Advertisements
 

SECOND CHANCE! January, 13, 2009

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Muziki,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 8:17 PM

tid-chokoraabc

Everybody deserves a second chance!Bila shaka ushawahi kusikia msemo huo.Ni kweli kabisa na ni haki.Hali hiyo ndiyo iliyothibitika hivi karibuni kwa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Khalid Mohamed ‘TID’ (kulia katika picha)pale alipopanda jukwaani kuungana na wana Twanga Pepeta wakati wa onyesho maalumu la usiku wa Zain ndani ya ukumbi wa Mango Garden jijini Dar-es-salaam.Ilionekana wazi kwamba watu walikuwa wamemmiss TID na pia kwamba wapo tayari kumpokea na kumpa tena nafasi kama mwanajamii.

Noti uionayo kwenye paji la uso la TID alituzwa na rapa wa Twanga Pepeta Saulo John “Ferguson”.

Photo/Michuzi.

 

TUNAWATAKIA KHERI YA SIKUKUU December, 23, 2008

Filed under: Sikukuu,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 1:46 PM

happy-holidays-glitter

Sikukuu imewadia.Ni wakati mwingine wa kusheherekea Sikukuu ya Xmas na wakati huo huo kuanza makaribisho ya mwaka mpya,2009.Kama ilivyo jadi ya enzi na enzi,huu ni wakati wa kukumbukana,kutembeleana,kujuliana hali,kutakiana kheri,kujumuika pamoja,kula na kunywa kwa furaha,amani na upendo.Kwa wengine ni wakati muhimu wa kupeana zawadi.Kwa ujumla ni wakati wa kufurahi!

Ni kwa kuzingatia hayo yote yaliyotajwa hapo juu ambapo tunakukaribisha wewe msomaji,mchangiaji au mtembeleaji wa BC,kutumia nafasi hii kuwatumia ndugu,jamaa na marafiki zako,popote pale walipo,Kheri ya Sikukuu ya Xmas kwa mwaka huu wa 2008.Unaweza kufanya hivyo kwa kuandika salamu na majina yao hapo kwenye sehemu ya maoni au kututumia picha au chochote kile ambacho ungependa ili kusindikiza salamu zako.Tumia anuani pepe (bongocelebrity at gmail dot com)Ukituma picha tutaiweka kwenye post hii hii.Jisikie huru.

Kutoka kwetu: Tunatoa shukrani nyingi na za dhati kwa jinsi ambavyo umekuwa nasi kwa wakati wote huu.Tunapenda kuchukua nafasi hii kukutakia wewe,ndugu,jamaa na marafiki zako KHERI YA SIKUUKUU YA XMAS na maandalizi mema ya MWAKA MPYA 2009.Tunatumaini itakuwa sikukuu ya kukumbukwa na iliyojaa furaha na mafanikio tele.Amani itawale.

Kwa niaba ya timu nzima ya BC-Jeff Msangi

 

DR.JAKAYA MRISHO KIKWETE December, 19, 2008

Filed under: Serikali/Uongozi,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 3:48 PM

jk

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kenyatta nchini Kenya, Dk.Harris Mule akimtunuku Phd ya Heshima Rais Jakaya Kikwete wakati wa mahafali ya 25 ya chuo hicho yaliyofanyika mjini Nairobi,Kenya leo. Phd hiyo inatokana na jitihada zake za utatuzi wa migogoro kwa nchi za Afrika hasa mgogoro wa Kenya uliozuka baada ya uchaguzi mapema mwaka huu.

Photo/Freddy Maro

 

FRIDAY WITH JOE THOMAS,DEVONTE AND TANTO METRO December, 4, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 12:40 PM

joebc

Hapo zamani ilikuwa ni nadra sana kusikia wanamuziki wenye majina makubwa kutoka nchini Marekani au sehemu zingine za dunia kuitembelea Tanzania na kufanya maonyesho.Siku hizi mambo yamebadilika.Kila kukicha wanazidi kumiminika.

Kuthibitisha hilo,kesho pale ndani ya viwanja vya Leaders Club,mwanamuziki Joe Lewis Thomas au maarufu kama Joe,akishirikiana na wenzake Devonte na Tanto Metro wanatarajiwa kufanya onyesho la kukata na shoka.

Pichani juu ni wanamuziki hao (toka kushoto ni Devonte,Joe Lewis Thomas na Tanto Metro) wakizungumza na waandishi wa habari leo jioni ndani ya Hotel ya Kilimanjaro Kempisk jijini Dar-es-salaam kuhusiana na onyesho lao.Wasanii hao wameingia jijini Dar jana.

joebc2

Picha na Ahmad Michuzi.

 

KLIMAX

Filed under: Burudani,Muziki,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 11:45 AM

bcc1

 

AFRICA AND ITS BEAUTY November, 30, 2008

migiro

Sio kila siku ni siku ya suti.Siku zingine ni lazima ziachwe kwa mavazi mengine,mavazi maalumu kama anavyoonekana pichani Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Dr.Rose-Asha Migiro wakati alipohudhuria tuzo za Glamour Women of The Year huko Carnigie Hall jijini New York mapema mwezi huu.