BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

KUHUSU BongoCelebrity May, 21, 2007

Karibu ndani ya BongoCelebrity. Shukrani kwa kututembelea.Hii ni tovuti/blog ambayo inaandika kuhusu watu mashuhuri au maarufu wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Tunaandika na kukupa wewe msomaji nafasi ya kujadili habari za watu mashuhuri wa zamani na wa sasa hivi. Nia ya msingi ni kujenga na sio kubomoa.

Tupende tusipende, maisha ya watu maarufu (celebrities) yana mvuto mkubwa kwa jamii.Iwe ni mwanasiasa, mwanamuziki,msakata kabumbu,mchekeshaji,mcheza sinema,mpiga simu maarufu redioni,msanii wa ngoma za asili,za kisasa,mtangazaji maarufu wa tv au redio,mtu mwenye umbo la aina yake,balozi nk wote kwa pamoja huwa ni wenye mvuto achilia mbali ushawishi fulani katika jamii. Inasemekana jamii isiyo na watu wake mashuhuri, maarufu,alwatani nk ni kama jamii isiyo hai.Tukisikia habari zao huwa mara nyingi tunataka kujua zaidi.Haina maana kwamba hatuna mambo mengine muhimu zaidi ya kufanya,la hasha.Ni hulka ya ubinadamu tu. Isitoshe, jamii inaweza kujifunza mengi sana kupitia mwangaza wa maisha na mienendo ya watu maarufu/ mashuhuri/celebrities.

Kwa kuzingatia sababu tulizozitaja hapo juu ndio maana tumejikita katika kuandika habari za watu hao maarufu. Hapa ndio chanzo cha habari motomoto, mahojiano, habari za kina, matoleo mapya ya albamu za muziki, picha kutoka kwa wapiga picha wetu maarufu za matukio, mikasa nk, habari za chochote kile kipya au cha zamani ambacho tusingependa kisahaulike ndani ya jamii yetu nk.

Isitoshe hapa ndipo vipaji vipya vinapotambulishwa, celebrities wapya wanapoanzia. Kwa maana hiyo ukikuta amewekwa mtu ambaye unadhani bado hana hadhi ya ki-celebrity usishangae,ndio anaanza safari yake.

Kwa kuzingatia ukweli kwamba lugha maarufu zaidi ulimwenguni inabakia kuwa kiingereza, BongoCelebrity inatumia kiingereza na kiswahili kama lugha zake maalumu.Tunaamini ni muhimu na pia ni jukumu letu, kuienzi, kuiendeleza na kuikuza lugha yetu ya Kiswahili. Lakini kwa namna yoyote ile Kiswahili ndicho kinapewa kipaumbele zaidi.

Kama una habari za mtu maarufu au wewe mwenyewe ni mtu maarufu na unalo jambo ambalo ungependa liwafikie watanzania na wa-Afrika Mashariki kwa ujumla kupitia tovuti/blog hii,usisite kuwasiliana nasi kwa kupitia; bongocelebrity at gmail.com au kwa kutumia fomu iliyopo hapo chini.

Maoni ya aina zote yanakaribishwa ingawa matumizi ya lugha chafu hatuyavumilii. Yawezekana kabisa kutoa mchango wako au maoni yako bila kutumia lugha zenye matusi.

Pia tunakaribisha matangazo.Kwa maulizo ya bei au gharama za kutangaza biashara au matukio wasiliana nasi pia kwa kutumia fomu hiyo hiyo hapo chini.Mnakaribishwa!

Karibuni sana.

BongoCelebrity Team.