BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

HERE COMES MR. AND MRS. BANANA December, 31, 2007

Filed under: Bongo Flava,Familia,Mahusiano/Jamii,Maisha,Muziki,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 8:41 AM

 

Jana ndio ilikuwa jana.Kama ambavyo imekuwa ikiripotiwa,Banana Zorro na Suzy Walele jana walifunga pingu za maisha.Pichani ni Banana Zorro akimlisha keki mkewe Suzy Walele.Sherehe hiyo iliyofana ilifanyika katika ukumbi wa Msasani Beach Club jijini Dar-es-salaam.Banana na Suzy wamefungua ukurasa mpya.BC inawatakia kila la kheri.Kwa picha zaidi endelea hapa (more…)

 

CAROLA KINASHA,TAFSIRI YA “MWANAMUZIKI”

Filed under: Burudani,Mawazo/Tafakuri,Muziki,Sanaa/Maonyesho — bongocelebrity @ 12:10 AM

 

Sio jambo rahisi na wanamuziki wasio wengi duniani wanaweza kufanya.Tunazungumzia kuimba na kutumia kifaa chochote cha kimuziki (kama gitaa,piano,ngoma nk) wakati huo huo.

Carola Kinasha(pichani) ni mmojawapo miongoni mwa wanamuziki tulionao nchini Tanzania ambao wanaweza kufanya hivyo.Carola anaweza kuimba na wakati huo huo kucharaza gitaa kama anavyoonekana pichani hapo juu.Habari za undani za Carola Kinasha unaweza kuzipata kwa kutembelea tovuti yake kwa kubonyeza hapa.

Halafu bado kuna ule ubishi/mjadala kwamba mtu anayejua kuimba tu huku akiwa hawezi kutumia kifaa chochote cha kimuziki, hastahili kuitwa mwanamuziki bali mwimbaji tu peke yake.Ni kweli? Wewe unasemaje?

Picha kwa hisani ya Bob Sankofa.

 

UCHAGUZI KENYA…KASHESHE TUPU! December, 30, 2007

Filed under: Breaking News,Developing News,Siasa — bongocelebrity @ 2:56 PM

 

Majirani zetu Kenya hivi majuzi walipiga kura za kuchagua Raisi na wabunge wa nchi yao. Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo (ECK) imemtangaza Mwai Kibaki(pichani) kuwa mshindi wa uchaguzi huo.

Hata hivyo utata mkubwa bado umegubika kuhusiana na uchaguzi huo,matokeo yake na mengineyo. Ushindi huo unapingwa vikali na aliyekuwa mgombea wa chama cha upinzani (ODM), Raila Odinga. Tayari Mwai Kibaki ameshaapishwa.

Habari hizi unaweza kuzipata kwa undani zaidi kwa kubonyeza hapa na hapa. Ukitaka kuona video mbalimbali kuhusiana na mchakato mzima wa uchaguzi huo bonyeza hapa.Kenya itaendelea kuwa salama? Tusubiri tuone.

Habari hii bado inaendelea.

 

PICHA YA WIKI # 16

Filed under: Photography/Picha,Serikali/Uongozi,Weekend Special — bongocelebrity @ 12:20 AM

 

Kila mwaka hutokea picha moja ikatokea kupendwa,kuzusha gumzo,kusababisha tafakari mbalimbali nk. Kwa mwaka huu,picha unayoiona hapo juu inaweza kabisa kuwa miongoni mwa picha za namna hiyo.

Picha hii ambayo inawaonyesha baadhi ya viongozi wakiwa ‘off guard” ilipigwa na Mroki Mroki wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Mapinduzi Zanzibar tarehe 12 Januari mwaka huu. Hii ndio picha yetu ya wiki hii.

Picha kwa hisani ya Mroki

 

OFF SHE GOES… December, 29, 2007

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Muziki,Utamaduni,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 12:20 AM

 

Kama tulivyoripoti siku chache zilizopita, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Banana Zahir Ally Zorro anatarajia kufunga pingu za maisha kesho ndani ya Msasani Beach Club.Anamuoa mchumba wake aitwaye Suzy Walele.

Pichani ni Banana Zorro(kushoto) akiwa na mchumba wake Suzy wakati wa send-off iliyofanyika katika ukumbi wa Sababa uliopo Kilwa Road jijini Dar-es-salaam jioni ya jana. Kila la kheri Banana na Suzy.

Picha na Michuzi

 

JOHN POMBE MAGUFULI

Filed under: Serikali/Uongozi,Siasa,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 12:10 AM

Ukiongelea viongozi wa kiserikali nchini Tanzania,hususani kutoka kwenye Baraza la Mawaziri, ambao wamewahi kutokea kupendwa sana na wananchi,huwezi kumuacha nje Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Pombe Magufuli(pichani). Unajua kwanini anapendwa?

Picha ya UN-HABITAT/World Urban Forum

 

NAPENDA NIPATE LAU NAFASI December, 28, 2007

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 12:06 AM

Leo ni ijumaa ya mwisho kwa mwaka 2007! Mwaka mpya wa 2008 ndio huo unawadia. Majuzi ilikuwa Xmas. Tungependa kusikia kutoka kwako msomaji kwamba ilikuwaje Xmas ya mwaka huu.Ulifanya nini? Wapi uliisheherekea nk.

Lakini wakati huo huo tungependa kutosahau jadi yetu mpya ya ijumaa.Jadi ya midundo kidogo huku tukitafakari mawili matatu.

Hivi ishawahi kukutokea ukawa na hamu sana ya kuongea japo machache tu na mpenzi wako lakini asikupe kabisa nafasi hiyo kwa sababu “umeshalikoroga” na yeye kakukasirikia na hataki kabisa kusikia hata sauti yako? Unafanya nini kitu kama hicho kikikutokea?

Kama huna jibu basi wasikilize Kilwa Jazz Band katika wimbo Napenda Nipate Lau Nafasi. Pata burudani.Ijumaa Njema.

 

 

Picha hii haina uhusiano wa moja kwa moja na post hii.Ni ya magofu ya Kilwa.

 

UHALIFU UNALIPA? December, 27, 2007

Filed under: Mahusiano/Jamii,Maisha,Ulimwengu,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 12:05 AM

 

Wakati wengine wakifikia hatua ya kuitwa bongo celebrity kwa michango yao mbalimbali ya kijamii,wapo ambao wanaukwaa umaarufu kwa mambo ambayo kimsingi yana sura ya upande mwingine wa shilingi. Ule upande ambao kila mtu anatamani usingekuwepo.Yaani mtu anafanya uhalifu kisha ndio jina lake linavuma kila kona ya nchi. Mmojawapo wa watu hao ni Justine Kasusura(pichani anayepanda karandinga).

Justine Kasusura hivi sasa anatumikia kifungo cha miaka 30 jela na viboko 12 baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa dola za kimarekani milioni mbili (2 million USD) mali ya benki ya Citibank mwaka 2001. Kesi hiyo ndio ilitufanya sote tulijue na kulisikia jina la Kasusura usiku na mchana.Swali ni je uhalifu unalipa? Wazungu wanasema Does Crime Pay? Unasemaje? Ukitaka kujikumbusha kuhusu kesi hiyo na hukumu yake bonyeza hapa.

Picha na Mroki.

 

SUMU YA TEJA,HAPPY BOXING DAY December, 26, 2007

Filed under: Burudani,Muziki,Sanaa/Maonyesho — bongocelebrity @ 12:05 AM

 

Kama wewe ni mpenzi wa muziki wenye ujumbe mkali huku ukisindikizwa na mirindimo yenye kuleta burudani muafaka,basi kwa Vitali Maembe(pichani) utakuwa umefika. Wengi tunamfahamu kama Sumu ya Teja jina ambalo sio lake bali la wimbo wake maarufu uliompa umaarufu. Vitali ambaye pia ni mchoraji mzuri ni matunda ya Chuo Cha Sanaa Bagamoyo. Unaweza kusikia nyimbo zake ukiwemo Sumu ya Teja kwa kubonyeza hapa.

Wakati huo huo BC inawatakia Happy Boxing Day.

Picha kwa hisani ya Mroki

 

LEO NI XMAS, NI KUBANJUKA TU. December, 25, 2007

Filed under: Burudani,Familia,Maisha,Sikukuu,Watu na Matukio,Weekend Special — bongocelebrity @ 12:05 AM

Sehemu nyingi sana ulimwenguni hivi leo ni shamrashamra za sikukuu ya Christmas. Mitaani leo kuna kila aina ya shamrashamra.Leo ndio ile siku ya kuvalia zile mpya ulizonunuliwa na mzazi,mke,mume,rafiki,mjomba,shangazi,binamu nk. Harufu iliyotanda mitaani ni ile ya pilau(uh uh uh uh). Fukwe za jiji la Dar-es-salaam kwa mfano,leo zinapata habari yake. Simu za viganjani zinaita kuliko mfano, ni mwendo wa miadi ya kukutana na kufurahia siku hii ambayo hutokea mara moja tu mwaka. Hii ni tofauti na mitaa ya Ulaya au Marekani ya kaskazini. Mitaani hamna mtu, mall na maduka yote leo yamefungwa. Ni siku ya familia.Kila mtu kwao au kwake.Kimya kimya hivi.Usipojua style hizi za wazungu katika kusheherekea Xmas unaweza dhani kuna msiba fulani. Subiri kesho sasa,Boxing Day.Kila mtu mtaani,madukani.Kazi kweli kweli.

Kama anavyoimba mwanamuziki Dennis Kagia aka DNA(pichani) kutoka kwa majirani zetu Kenya, leo ni mwendo wa kubanjuka tu. Ni siku unayotakiwa kusahau matatizo yote,japo kwa muda. Toka nje,ingia mitaani.Jichanganye na wenzako. Usijitie upweke hivi leo. Ni sikukuu.

Mtizame DNA hapo chini kwenye wimbo wake Banjuka. Msikilize akisema “Weka shida chini,tupa mikono juu, Banjuka tu.Life ni fupi na mimi sijivungi” Kama vile haitoshi anasema ‘Sisi tuna shida zetu,tusikilize zako kwanini”? Xmas Njema.Furahia kwa sana lakini kuwa makini,hata kama maisha ni mafupi. Amani na upendo vitawale.