BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

TAHADHARI: MICHUZI YUPO DAR SIO NIGERIA! July, 28, 2007

Filed under: Alert-Tahadhari,Blogging,Blogs,Breaking News,Photography/Picha — bongocelebrity @ 1:14 PM

 

Yawezekana umeshapata ujumbe uliosambazwa na Issa Michuzi mwenyewe au ule ambao Da’Chemi wa Swahili Times blog ameusambaza ikiwa ni tahadhari kuhusu e-mail ya kitapeli ambayo ilisambaa jana na bado inaendelea kusambaa hivi sasa ikidai Issa Michuzi amekwama hotelini huko nchini Nigeria na hivyo anaomba msaada wa kifedha.

Tungeweza kuipuuzia tu e-mail kama hiyo.Tatizo ni kwamba sio tu ni ya kitapeli,bali hivi sasa imemfanya Issa Michuzi ashindwe hata ku-update blog yake maarufu. Kimsingi e-mail ya issamichuzi at gmail ambayo ndio aliyokuwa akiitumia kuingia ndani ya blog yake haipo mikononi mwake tena! Ndio maana kama mnavyoweza kuona ukiitembelea blog yake tangu jana hajaweza kuweka picha mpya,jambo ambalo sio kawaida yake kabisa.

BongoCelebrity imewasiliana na Michuzi na kufanya naye mahojiano yafuatayo. Yasome na kisha mkumbushe na mwenzio kuhusu kwamba aipuuzie tu e-mail kama hiyo. Hapa Michuzi anaelezea nini kilitokea,lini ataweza tena kuendelea ku-update blog yake(archives zote bado zipo na zinapatikana online),vipi unaweza kuepuka yasikukute yaliyomkuta na anapatikana kwa njia gani hivi sasa? Majibu haya hapa chini;

BC:Nini hasa kimetokea? Ilikuwaje? (more…)

 

UNAMKUMBUKA LAWRENCE MWALUSAKO? July, 27, 2007

Filed under: Kabumbu/Soka,Michezo,Soka,Wachezaji — bongocelebrity @ 11:55 AM

Kwa mpenda soka ya Tanzania yeyote yule, hususani mnamo miaka ya themanini,jina Lawrence Mwalusako sio geni hata kidogo. Alikuwa sio tu kipenzi cha wapenda soka bali beki wa kutumainiwa wa timu zote alizowahi kuchezea, zikiwemo Waziri Mkuu Dodoma, Pan African, Yanga na timu ya taifa,Taifa Stars. Ndio maana yanapotajwa majina ya wachezaji soka nchini Tanzania waliowahi kuwika na jina la Mwalusako likakosekana,wadau wa soka,wanaoijua vyema historia ya soka la Tanzania,watakuambia wazi,something is missing.

 

Lawrence Mwalusako ni wa sita kutoka kushoto waliosimama.

Waliosimama kutoka kushoto: Marehemu Daktari wa timu Peter Manyika,Meneja John Manongi,Abeid Mziba “Tekero”,Athumani China,Yusuf Ismail Bana,Lawrence Mwalusako,Said Mrisho,Edgar Fongo,Isihaka Hasan,Golikipa Joseph Fungo,Kocha Mwinda Ramadhan.

Waliochuchumaa kutoka kushoto: Marehemu Lucias Mwanga,Rashid Idd Chama,Moshi Majungu,Allan Shomari,Ali Mchumila,Freddy Ferix Minziro,Abubakar Salum “Sure Boy”

Picha hii ilipigwa Mwaka 1987 uwanja wa taifa wakati wa mechi ya premier kati ya Yanga na Maji Maji.

Safari ya Mwalusako katika medani ya soka inaanzia kule Kyela mkoani Mbeya alipozaliwa mnamo mwaka 1960.Tulipofanya naye mahojiano hivi karibuni,Mwalusako ameongelea mambo mengi yakiwemo mtazamo wake wa soka la bongo hivi sasa,washambuliaji aliokuwa anawaheshimu,ushauri kwa wanasoka chipukizi nk.Pia anagusia jinsi “juju” ilivyo katika timu kubwa na pengine hata zile ndogo. Fuatana nasi katika mahojiano haya ambayo hata yeye mwenyewe anakiri,hajawahi kufanya na chombo chochote cha habari duniani akiwa kama mchezaji na hata baada ya kustaafu. Hivi sasa yeye ni Corporate Affairs Manager wa kampuni ya Sumaia Group Tanzania.Anaishi Dar-es-salaam.

BC: Unaweza kukumbuka wakati ulipokuwa mdogo ni nani alikuvutia katika mchezo wa soka? Kulikuwa na mtu yeyote maalumu ambaye ulimuona kama role model wako katika soka? (more…)

 

“MENGI YASEMWAYO NI UONGO”-RAY C July, 23, 2007

Filed under: Bongo Flava,Muziki — bongocelebrity @ 11:53 PM

Inasemekana ndiye msanii wa kike mwenye mvuto kushinda wote Afrika Mashariki. Jina lake halisi ni Rehema Chalamila. Wapenzi wa muziki wake wanamtambua zaidi kwa jina Ray C. Ndio kwanza una umri wa miaka 25. Jina lake lilianza kuvuma alipokuwa mtangazaji redioni kabla hajaamua kuingia rasmi kwenye ulimwengu wa muziki,sio tena kama DJ bali muimbaji/mwanamuziki. Ingawa anasema angependa watu wausikilize na kuucheza muziki wake zaidi ya kuongelea uchezaji wake awapo jukwaani(viuno), ukweli unabakia kwamba Ray C ni mmojawapo wa entertainers wazuri jukwaani.Hivi karibuni BongoCelebrity ilifanya naye mahojiano yafuatayo. Katika mahojiano haya Ray C anazungumzia historia yake kimuziki toka utotoni mpaka alipo hivi sasa,mipango yake ya baadaye na kama lengo la BongoCelebrity anatoa ushauri kwa vijana wanaotaka kuingia kwenye fani ya muziki.Pia anaweka wazi swali je alishawahi kuolewa? Na nani? (more…)

 

USIPIME July, 17, 2007

Filed under: Bongo Flava,Muziki — bongocelebrity @ 7:29 AM

 

Miaka sita iliyopita wapenzi wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania walianza kuisikia sauti yake redioni na baadaye kumuona kwenye luninga. Single yake ya kwanza iliyomuingiza kwenye ulimwengu wa muziki iliitwa “Sogea Karibu”. Hivi sasa anatambulika kama Black Rhino aka The Dan Dada.

Black Rhino ambaye pia ni mwanafunzi katika chuo kikuu cha Sokoine mjini Morogoro akisomea shahada ya kwanza katika masomo ya biashara ni mdogo wa kuzaliwa wa msanii mwingine maarufu wa bongo flava, Professor Jay ambaye tovuti hii ilifanya naye mahojiano hivi karibuni.

Ndani ya mwezi huu wa saba, anatarajia kuingiza sokoni albamu yake ya kwanza itakayokwenda kwa jina USIPIME. Itasheheni nyimbo si chini ya kumi.Wasanii aliowashirikisha ni kama Dully Sykes, Noorah,Hard Mad,Fatma,Q Chief,Chidi Benz,Producer Lucci,Enika,na wengine wakali kibao. Albamu imetayarishwa kwenye studio za Mandugu Digital chini ya producer Ambrose kwa kiasi kikubwa. Baadhi ya miziki imepikwa katika studio za Bongo Records.

Hizi hapa baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye albamu hii mpya;Wa kwanza ni Usipime wa pili Mistari.

 

I AM PROUDLY TANZANIAN-MISS KINONDONI 07 July, 12, 2007

Filed under: Urembo — bongocelebrity @ 2:26 PM

Alipotangazwa kuwa ndio mshindi wa taji la urembo la wilaya ya Kinondoni 2007 (Miss Kinondoni 2007) hivi karibuni, mashabiki wake walipiga vigelegele.Lakini punde suala la “Utanzania” likaibuka. Suala la rangi ya ngozi, asili ya wazazi wake na yeye mwenyewe kuwa au kuonekana “mhindi” kuliko mtanzania likashika hatamu. Hata hivi sasa anapojiandaa kwa kinyang’anyiro cha kuwania taji la Miss Tanzania hapo baadaye,bado wapo watu wanaohoji ilikuwaje,kwanini,itakuwaje na mambo kama hayo. Tunamzungumzia RICHA ADHIA,Miss Kinondoni 2007,binti mdogo wa miaka 19 tu.

 

Yeye mwenyewe anasemaje kuhusu haya yote? Anajisikiaje suala la “ubaguzi” linapoingia? Nini anatarajia kuifanyia Tanzania? Hivi karibuni, BongoCelebrity ilifanya naye mahojiano ili kuweka sawa baadhi ya mambo. Soma mahojiano yetu naye hapa chini.

BC: What is your full name and who are you??(Brief life history).

RICHA: My name is Richa Adhia, I am 19yrs old and I come from a family of five, I being the eldest. I have one brother and two younger sisters and we all live with our mother in Kariakoo. I grew up in Mwanza where I spent more than 10 years before moving to Dar. I just completed my O’Levels at Shabaan Robert Secondary School in 2005 and at the moment I work as a personal Assistant to the managing Director of Berger Paints Ltd. (Robbialac).

BC: Did you expect to win the Miss Kinondoni Title? (more…)

 

RUMMY NANJI July, 11, 2007

Filed under: Muziki — bongocelebrity @ 10:39 AM

Kama wewe ni mtanzania, unaishi au umeshawahi kutembelea Ulaya ya Kaskazini(Northern Europe) sio ajabu ushawahi kusikia jina la kundi la muziki linaloitwa Mighty 44. Jambo ambalo inawezekana hulijui ni kwamba kiongozi wa kundi hilo ni Rummy Nanji, kijana wa kitanzania ambaye amekuwa akiwakilisha huko Ulaya Kaskazini kwa miaka chungu mbovu sasa na kujizolea sio tu umaarufu (celebrity status) bali kuthibitisha kwamba watanzania wana vipaji vya kila aina na nafasi ikijitokeza wanafanya vitu visivyo vya kawaida. Tizama mojawapo ya kazi zake hapa chini.Muziki anaouipiga hapa ndio haswa unaozimiwa huko Ulaya. BongoCelebrity hivi karibuni inatarajia kufanya mahojiano rasmi na Rummy Nanji.

 

THE NGOMA AFRICA BAND July, 6, 2007

Filed under: Muziki — bongocelebrity @ 7:32 PM

 

Kila wanapotokea jukwaani katika maonyesho yao mbalimbali, mashabiki hulipuka kwa mayowe, miruzi, makofi na vigelegele. Wanapoibuka huwa wamevalia mavazi ya kiafrika bila kusahau bling bling kibao za kutoka Afrika. Wamekuwepo kwenye medani ya burudani kwa zaidi ya miaka 14 sasa. Wanasema wawapo jukwaani kazi yao huwa ni moja tu; kuwapa wapenzi wa muziki burudani isiyo na mfano jambo ambalo huwatia kiwewe wahudhuriaji wa kila onyesho lao.

Hawa si wengine bali watanzania, The Ngoma Africa Band,bendi maarufu barani Ulaya yenye makazi yake huko Oldenburg nchini Ujerumani. Wamekuwepo kwenye medani ya muziki huku wakitingisha katika majukwaa ya kimataifa kwa zaidi ya miaka 14 sasa.

Kiongozi wa bendi hii ni mwanamuziki nyota Ebrahim Makunja a.k.a Ras Ebby Makunja au kwa jina lingine maarufu Bwana Kichwa Ngumu mwimbaji na mtunzi mchokozi.

 

Hivi karibuni walifanikiwa vilivyo kuzikonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa dansi waliposhiriki na kufanya onyesho la kufa mtu huko Hamburg, Ujerumani katika tamasha maarufu lijulikanalo kama Africa Market.

 

Wakati maonyesho ya Saba Saba (7-7-2007)yatakapokuwa yanafikia kilele nchini Tanzania, The Ngoma Africa Band wao watakuwa wakifanya vitu vyao katika sehemu maarufu ya mabwanyenye “WOYTON” .Baada ya hapo tarehe 11th August 2007 watakuwa jijini Frankfurt ambako wamealikwa katika tamasha maarufu la “African and Carribean Music Festival”.

Katika picha mwenye rasta ndiye kiongozi mkuu na muasisi wa The Ngoma Africa Band, Ebrahim Makunja a.k.a Ras Ebby Makunja au Bw.Kichwa Ngumu (mtunzi na lead vocalist). Mwenye kilemba cha njano ni Said Vuai a.k.a Prince Jazbo Vuai.(mpiga bass guitar). Mwenye shati jeupe la maua ni Christian Bakotessa a.k.a Chris-B (mcharaza solo guitar). Mwenye shati la njano, mnene kidogo ni Musa Boujang a.k.a Al-Hajj Musa (mpiga tumba {drum}.

Unaweza kusikiliza baadhi ya nyimbo zao katika www.myspace.com/thengomaafrica

Una swali ungependa kuwauliza The Ngoma Africa Band? Tuandikie bongocelebrity@gmail.com

Shukrani Msema Kweli wa pale Bremen kwa taarifa hizi.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

ALUTA CONTINUA-PROFESSOR JAY July, 2, 2007

Filed under: Bongo Flava — bongocelebrity @ 1:22 PM

 

 

“Jina langu limevuma, Kwenye mitaa.Jina langu lina hadhi ya ki-superstar.Jina langu…..” Hayo ni maneno kutoka kwenye wimbo Jina Langu wa msanii mahiri wa Bongo Flava, PROFESSOR JAY au Prof Jiizeh. Hakuna ubishi, jina lake limevuma na ni kweli ana hadhi ya ki-superstar.

Alizaliwa jijini Dar-es-salaam tarehe 29 December 1975. Ni mtoto wa sita kati ya watoto tisa wa Mzee Leonard Steven Haule na Mama Rose Majanjara. Baadaye akasoma Ukonga Primary School kabla hajaelekea mji kasoro bahari(Morogoro) kusoma Kigurunyembe Secondary na baadaye Mbeya Lutengano High School.

Ana tuzo za muziki zisizopungua 25 ambazo amezikusanya ndani ya miaka 15 ambayo amekuwa kwenye game. Hivi karibuni BongoCelebrity iliketi chini na msanii huyu ambapo alifungua milango ambayo hajawahi kuifungua kabla. Katika mahojiano haya nadra, Professor Jay anazungumzia kwa undani shughuli zake za muziki, siasa za nchi,ushauri kwa vijana, role models, vilio vya wasanii kuhusu kazi zao na mzunguko mzima wa muziki. Pia anatoa ushauri makini kwa Raisi Kikwete, anabainisha mtizamo wake wa kisiasa na mengi mengineyo. Yafuatayo ni mahojiano kamili;

BC: Karibu sana katika BongoCelebrity na shukrani nyingi kwa kukubali kufanya mahojiano nasi.

PROF.JAY: Asante Sana na najisikia faraja sana kupata fursa hii ya kufanya mahojiano nanyi kwani itakuwa ni nafasi nzuri ya kuwajulisha mashabiki wangu kuhusu mustakabali wa shughuli zangu za kimuziki

BC: Unaweza kukukumbuka ni lini ilikuwa ndio mara yako ya kwanza kupanda jukwaani kama mwanamuziki huku umati wa watu ukisubiri uwape burudani. Ilikuwa wapi?

PROF.JAY: Yeah nakumbuka ilikuwa ni mwanzoni mwa mwaka 1992 nikiwa pamoja na mshkaji wangu KILLA B pale Chuo Kikuu cha Dar es salaam ukumbi wa UDASA. Nakumbuka watu walikuwa kibao nanilikonga sana nyoyo za mashabiki wa muziki huu kwa style yangu ya enzi hizo ya TONGUE TWIST.

BC: Mara nyingi wanamuziki wengi huwa wameanza muziki kutokana na kupata ushawishi (influence) fulani hivi. Unaweza kutuambia nini au nani alikushawishi kuingia katika masuala ya muziki?

PROF.JAY: Nilikuwa napenda sana kusikiliza nyimbo za akina RUN DMC na PUBLIC ENEMY kwa kuwa walikuwa wanaimba nyimbo za kupigania na kutetea haki za mtu mweusi. Kwa hiyo nikawa nazikariri na kuziimba shuleni na pia nikawa najaribu kuongeza maneno yangu na mwisho nikawa taratibu na mimi natunga mashairi yenye ujumbe tofauti tofauti kwenye jamii yangu iliyonizunguka.

BC: Ulipojitokeza rasmi katika ulimwengu wa muziki ulijulikana kama Nigga Jay, kisha yakafuata majina kama Jay wa Mtulinga, Mti Mkavu nk.Baada ya hapo majina kama HeavyWeight MC, Professa Jay na hivi sasa Daddy yakaibuka.Nini chanzo cha majina yote haya? (more…)