BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

AFRICA AND ITS BEAUTY November, 30, 2008

migiro

Sio kila siku ni siku ya suti.Siku zingine ni lazima ziachwe kwa mavazi mengine,mavazi maalumu kama anavyoonekana pichani Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Dr.Rose-Asha Migiro wakati alipohudhuria tuzo za Glamour Women of The Year huko Carnigie Hall jijini New York mapema mwezi huu.

Advertisements
 

SEYA-NGUZA VIKING November, 27, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 9:45 PM

seyaMwaka 2008 upo mbioni kuelekea ukingoni mwake.Zimebaki wiki kadhaa tu kabla hatujaona zile fataki hewani na kusikia ving’ora vikitusindikiza kuumalizia mwaka.Kwa vyovyote vile mwaka 2008 utaenda na historia kadhaa zenyewe kuvutia kwa wengine na kutia simanzi kwa wengine.Ndio maisha.Ni mwaka ambao hakuna atakayeweza kamwe kusahau kwamba mtu mweusi wa kwanza amechaguliwa kuliongoza taifa kubwa la Marekani.

Lakini nchini kwetu pia ni mwaka ambao tunaweza kusema tumeshuhudia mengi ambayo siku za nyuma yalionekana kuwa hayawezekani.Tumeona viongozi kadhaa wakijiuzulu nyadhifa zao.Tumeshuhudia wengine wakipandishwa kwenye karandiga.Tumeona wazee wengine wakipandwa na pressure kwa sababu wanajua walishaharibu na hawana uhakika na kesho.Nadhani tunakubaliana kabisa kwamba miaka kadhaa ya nyuma,ilikuwa ni kama ndoto kusikia kiongozi akitangaza kujiuzulu.Mifano ya waliowahi kujiuzulu ilikuwa ni michache sana.

Najua kuna ambao mnasema yote hii ni “changa la macho” na kwamba kinachofanyika ni mchezo wa aina yake wenye wingu zito la kisiasa.Inawezekana kabisa(hakuna lisilowezekana katika dunia hii).Lakini pamoja na yote hayo,tofauti na siku za nyuma,hata kile kitendo tu cha kuwaona waheshimiwa wakitokwa na jasho kwa sababu hawamo ndani ya yale “mashangingi” yao na badala yake wamekalia yale yale mabenchi ambayo hawakuwahi kuona umuhimu wa kuyakarabati kwa sababu “hayakuwahusu” na huku wakiwa wameegemea zile kuta ambazo hela yake ya rangi waliipeleka kusipotakiwa,ni vitu ambavyo vinaufanya mwaka 2008 uwe na lake katika historia.Bado tunasubiri kuona jinsi “changa la macho” litakavyopelekwa.Tupo na tunatizama kwa makini.Anayedhani tumelala anajidanganya.

Ni wikiendi tena.Ni wakati wa kujikumbusha zile tulizowahi kuzipenda kama ilivyo jadi yetu hapa BC.Kwa sababu wiki hii tumeshuhudia kiasi kuhusu niliyoyaongelea hapo juu,basi sio vibaya kama tukiwakumbuka Nguza Viking na mwanae Papii Kocha ambao wapo gerezani ambako ndiko tunapotarajia “waheshimiwa” watakuwa wamehifadhiwa.Wimbo unaitwa Seya.Pata burudani,wikiendi njema.


 

ANGELIKUWA HAI ANGESEMAJE? November, 26, 2008

Filed under: Serikali/Uongozi,Siasa,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 11:40 PM

nyerere13bc

Ninapoona picha za viongozi waliokuwa wanaheshimika na pengine hata kupewa sifa za “uadilifu uliotukuka” wakiwa kizimbani kujibu shutuma za kujifanyia mambo wanavyotaka kwa manufaa ya matumbo yao na yale ya ndugu,jamaa na marafiki zao,huwa siishi kujiuliza swali lililo kwenye kichwa cha habari hapo juu;Mwalimu Nyerere angekuwa hai angesema nini kuhusu watu kama hao?Wakithibitishwa kuwa na hatia,angeshauri wapewe adhabu gani?

 

YONA NA MRAMBA KIZIMBANI! November, 25, 2008

Filed under: Breaking News,Developing News,Serikali/Uongozi — bongocelebrity @ 8:11 AM

yona-na-mrambabc

Mawaziri wa zamani (wote wamewahi kuwa mawaziri wa Fedha), Mheshimiwa Daniel Aggrey Ndhira Yona(pichani kushoto) na Mheshimiwa Basil Pesambili Mramba(pichani kulia) leo hii wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi ya Kisutu jijini Dar-es-salaam wakikabiliwa na mashtaka 13 ikiwa ni pamoja na kutumia vibaya madaraka yao walipokuwa mawaziri, kuingia mikataba tata ya madini nk

Pichani ni waheshimiwa hao muda mfupi baada ya kusomewa mashtaka yao.Wote wamewekewa masharti ya dhamana kwamba kila mmoja atoe fedha taslimu bilioni 3.9,wasalimishe hati zao za kusafiria,wasitoke nje ya Dar-es-salaam na kila mmoja wao awe na wadhamini wawili ambao mahakama itaridhika nao kuwa ni wa kuaminika.

basil-yona

“Pana joto sana hapa au”?

yona

Masharti ya dhamana magumu,siyawezi.

Picha kwa hisani ya Bongo Pix 

HASHEEM ATEULIWA TIMU YA TAIFA YA KIKAPU BONGO November, 24, 2008

Filed under: Michezo — bongocelebrity @ 12:31 PM
Tags: ,

hasheem

Hasheem Thabeet (pichani),mtanzania ambaye wengi wanamtarajia kuwa mtanzania wa kwanza kucheza katika ligi maarufu ya mpira wa kikapu nchini Marekani(NBA), ametajwa kuwa miongoni mwa wachezaji 21 walioteuliewa kuchezea Timu ya Taifa ya mpira wa kikapu nchini Tanzania kwa upande wa timu ya wanaume.Pia wanawake 20 wameteuliwa kuunda timu ya taifa kwa upande wa wanawake.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini Tanzania(TBF),Lawrence Cheyo, timu hiyo ya wanaume itakuwa chini ya makocha Bahati Mgunda na Evarist Mapunda wakati ile ya wanawake itakuwa chini ya makocha Salehe Zonga na Pascal Nkuba.

Majina ya wachezaji walioteuliwa kwa upande wa wanaume ni; Frank Kusiga, Ashraph Harun, Edward Robert, Paschal Nsana, Abdallah Ramadhan Dulla, Francis Mlelwa, Frank Augustino, Sudi Abdallah Razak, Mohamed Ally Dibo, Oswald Maboko,Amon Semberya, Kafashe Abdallah, Tarimo George, Juma Kissoky, Mgindi Mkumbo, Amiri Muhidini, Batungi Gilbert, Alphonse Kusekwa, Jije Makani, Hasheem Thabeet na Alex George.

Kwa upande wa wanawake walioteuliwa kuunda timu ya taifa ni; Annosiata Anthony, Agnes Simkonda, Jabu Shabani,Grace Daud, Grace Peter, Fraja Malaki, Evodia Kazinja, Elizabeth Masenyi, Naima Boli, Mary Meshack, Nipaeli Kessy, Amina Ahmed, Neema Emmanuel, Monica Aloyce, Zakia Kondo, Dajda Ahmed, Dolita Mbunda, Hadija Kalambo,Lucy Sangu na Lucy Augustino.

Timu hizo zipo chini ya udhamini wa kampuni ya Barrick Tanzania na zinatarajiwa kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kanda ya Afrika Mashariki na Kati yatakayofanyikia nchini Rwanda.

 

MU-ANGOLA ASHINDA BIG BROTHER AFRICA November, 23, 2008

Filed under: Television,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 7:04 PM
Tags: , ,

riccoangola

Shindano la tatu la Big Brother Africa limemalizika leo huko Afrika Kusini ambapo kijana kutoka Angola, Ricardo David Ferreira Venancio a.k.a Ricco (21) kama alivyojulikana ndani ya Big Brother House ndio mshindi wa shindano la mwaka huu.

Tofauti na mashindano mengine,shindano la mwaka huu lilibidi liamuliwe kwa mbinde ya kutafuta asilimia ya jumla ya kura zote zilizopigwa mwaka huu baada ya Ricco kufungana na binti kutoka Malawi, Hazel(25)

Hongera kwa Angola kwa kuibuka washindi.


 

FATUMA MWANANGU-MAGEREZA JAZZ BAND November, 22, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 9:18 AM
Tags:

fatumabcLeo sina maneno mengi.Ninachokuomba ni kuisikiliza burudani ya leo(hususani ujumbe wake) kisha uniambie je ushauri anaopewa Fatuma ni mzuri au mbaya? Burudani inatoka kwa Magereza Jazz Band.Wimbo unaitwa Fatuma Mwanangu.Weekend Njema.