BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

AFRIKA BAMBATAA April, 30, 2008

Filed under: Muziki,Watangazaji — bongocelebrity @ 9:57 AM

Anaitwa Sofia Kessy.Kipindi anachokiendesha kinaitwa Afrika Bambataa kupitia Clouds FM kuanzia jumatatu mpaka Ijumaa saa moja mpaka saa tatu usiku akishirikiana na DJ wake Mohamed Ally aka 2 Short.Afrika Bambataa ni kipindi ambacho kimejikita katika muziki wa kiafrika na mambo ya kiafrika.

Advertisements
 

DOWN THE MEMORY LANE… April, 29, 2008

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Sanaa/Maonyesho — bongocelebrity @ 9:38 PM

Umekuwa ukifuatilia maendeleo ya muziki uitwao wa kizazi kipya kwa muda sasa.Umeshuhudia wasanii mbalimbali wakiingia,wakatamba au kupotelea hewani.Lakini je umekuwa ukitunza kumbukumbu zako?Kama jibu ni ndio, unaweza kukumbuka(na kukumbusha wenzako) kuhusu kilichokuwa kinatokea katika picha hiyo hapo juu? Ni wasanii gani ambao unaweza kuwatambua katika picha hii?

 

NINI NA KWANINI? April, 28, 2008

Filed under: Mawazo/Tafakuri,Swali kwa Jamii,Uncategorized,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 8:55 PM

Yapo mambo ambayo pindi yakitokea kila binadamu hushikwa na butwaa na kutokutambua mara moja kwamba nini kimetokea,kinatokea au kinaelekea kutokea. Mojawapo ya mambo kama hayo ni kama kitendo kilichotokea hivi majuzi pale katika hospitali ya Muhimbili ambapo mtoto mwenye umri wa miaka 12 ajulikanaye kama Ramadhani Mussa(pichani) alikamatwa akiwa na kichwa cha mtoto mdogo, Salome Yohana (miaka 3) alichokuwa amekibeba kwenye mfuko wa Rambo!

Tukio hilo la aina yake,la kusikitisha na hata kuchosha akili limeandikwa na blogs mbalimbali na pia vyombo karibuni vyote vya habari nchini Tanzania.Kwa sababu habari yenyewe bado inazua mijadala mbalimbali, tumeona sio vyema kukunyima wewe msomaji na mtembeleaji wetu, fursa ya kutoa maoni yako kuhusiana na tukio hili.Nini maoni yako kuhusiana na tukio hili? Ni uchawi, imani za kishirikina, matatizo ya akili au ni nini hasa? Kwanini watoto?

Isitoshe,mtoto Ramadhani Mussa, ambaye hivi sasa anashikiliwa na Polisi Mkoa wa Ilala, Kanda Maalumu ya Dar-es-salaam akiendelea kuisaidia polisi na uchunguzi, yawezekana ndio jina au tukio lililotawala vinywa vya watu wengi hivi sasa.

Kama hujapata fursa ya kusoma habari mbalimbali kuhusu tukio hili,unaweza kufanya hivyo kwa kubonyeza hapa na hapa na hapa.

Wakati huo huo,gazeti la Uwazi(mojawapo ya magazeti ya Global Publishers), hivi leo wametoa habari ya kina ya tukio hili kama ambavyo unaweza kuiona katika ukurasa wa mbele wa gazeti hilo hapo chini.Unaweza kuisoma habari hiyo kamili kwa kubonyeza hapa.

 

BALOZI PETER KALLAGHE

Filed under: Balozi,Serikali/Uongozi,Tanzania/Zanzibar,Uncategorized — bongocelebrity @ 10:48 AM

Tunaendelea na mfululizo wetu wa mabalozi wa Tanzania nchi za nje.Pichani ni Balozi Peter Kallaghe, balozi wa Tanzania nchini Canada. Kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada, Peter Kallaghe alikuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Habari -Ikulu Tanzania.

Ukitaka kutembelea tovuti ya Ubalozi wa Tanzania nchini Canada bonyeza hapa.

 

PICHA YA WIKI # 17 April, 27, 2008

Filed under: Mambo Mseto,Photography/Picha,Uncategorized,Weekend Special — bongocelebrity @ 12:06 AM

Hiyo uionayo pichani sio boti.Ni gari tu la kawaida aina ya landrover likikatisha katika mitaa fulani ya jiji la Dar-es-salaam.In fact hilo ni gari la polisi wakiwa katika doria au wakiwajibika kwa njia moja au nyingine.

Ukiitizama picha hii kwa makini unaweza kupata majibu au maswali (inategemea utaliangalia suala zima kwa njia gani) kuhusu hali halisi ya miundombinu(infrastructure) nchini mwetu. Kimsingi Wizara ya Miundombinu(iliyokuwa inaongozwa na Andrew Chenge mpaka alipojiuzulu hivi majuzi) ina kazi ya ziada.Hapo ni jijini Dar-es-salaam.Kule kwetu Mtangananjia je?Hii ndio picha yetu ya wiki hii na kwa hisani ya Msimbe Lukwangule.

 

MIAKA 44 YA MUUNGANO…TUSHEHEREKEE! April, 26, 2008

Leo ni siku ya kusheherekea Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanyika miaka 44 iliyopita na kutupa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania tuijuayo hivi leo. Sherehe za kitaifa za kuadhimisha kumbukumbu hiyo zinafanyikia jijini Dar-es-salaam.Watanzania tunazo kila sababu za kusheherekea. Basi na tusherekee!

Pichani anaonekana Baba wa Taifa,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, akichanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar kama ishara ya muungano rasmi.

Hapa wanaonekana Baba wa Taifa,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere(kushoto) akibadilishana na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume(kulia), nyaraka rasmi za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar miaka 44 iliyopita.

Picha zote kwa msaada wa Muhidini Issa Michuzi.

 

MARIA-HEMED MANETI & VIJANA JAZZ BAND April, 25, 2008

Filed under: Burudani,In Memory/Kumbukumbu,Muziki,Weekend Special — bongocelebrity @ 12:07 AM

Mapenzi ni dhana pana sana. Ni dhana ambayo mpaka hivi leo mwanadamu bado anahangaika kupata ufafanuzi wake. Hata hivi leo tukiuliza hapa hivi mapenzi ni nini,tunaweza kupata maoni zaidi ya hata elfu moja huku kila mmoja akiwa na maana au tafsiri yake kuhusu mapenzi. Usishangae kama tafsiri hiyo yaweza kuwa tofauti kabisa na yako au yangu!

Bahati nzuri au mbaya ni kwamba mwisho wa siku wote tutakuwa sahihi. Kila mmoja anaruhusiwa kutafsiri dhana ya mapenzi au penzi kwa kadri anavyoona yeye au kwa jinsi ambavyo “mvua inakuwa imemnyeshea”.Si unakumbuka kwamba aisifiaye mvua imemnyeshea?

Upana wa dhana ya mapenzi huenda ndio hupelekea kila kukicha wanamuziki wanazidi kutunga na kuimba nyimbo kuhusu mapenzi. Mapenzi hayajaanza jana wala leo na hayatokaa yafikie mwisho.

Pamoja na hayo, zipo nyimbo za mapenzi ambazo wenzetu wanaotumia kizungu huwa wanasema “it has stood the test of time” kumaanisha kwamba wakati sio kitu kwake kwani kitu hicho(nyimbo) bado kinapendwa na kitaendelea kupendwa kwa wakati mwingi ujao.Mfano mzuri wa nyimbo za aina hiyo ni ule uitwao Maria (Mary Maria) ulioimbwa na Vijana Jazz Band enzi hizo ikiwa chini ya uongozi wa Hayati Hemed Maneti(pichani). Katika wimbo huo utamsikia Maneti akilalama kutokana na penzi zito alilonalo kwa “mtoto” Mary. Baadhi ya maneno kwenye wimbo huo ni kama;

Kwa kweli sasa nimenaswa
Sina ujanja eeeh eeeh,
Sina ujanja eehhh
Kupenda sawa na ajali
Haina kinga eeh eeh
Haina kinga eeh

Nilivyomuhusudu mtoto Mary sijapata kupenda toka nizaliweeeee
Na wala sitapenda mpaka nife,
Mpaka nife, mama Mary oooh

Bonyeza player hapo chini upate burudani kamili ya wimbo Maria.Kama unaye umpendaye, huku naye anakupenda kwa dhati na wala sio “for convenience” basi muite mwambie mcheze kidogo wimbo huu.Nakutakia Ijumaa Njema.