Pichani ni baadhi ya wasanii watakaoshambulia jukwaa kesho.Zimepigwa na Michuzi Jr na kunakishiwa ndani ya Chapakazi Productions.
Kila mwaka wananchi wa nchi za ughaibuni wanapokuwa wanafurahia majira ya joto (summer) nchini Tanzania napo watu hujimwaga viwanjani na kwenye kumbi mbalimbali kusheherekea tamasha maarufu la kila mwaka lijukanalo kama FIESTA. Mpaka hivi sasa hili ndio tamasha maarufu kupita yote nchini Tanzania na linaendelea kujipatia umaarufu mwaka baada ya mwaka.
Mwaka huu FIESTA ya Tanzania imepewa maudhui ya Shangwe Boda 2 Boda. Kuzingatia maudhui hayo tamasha lilianzia jijini Mwanza wiki iliyopita na kesho lipo ndani ya Leaders Club Kinondoni kwa upande wa jiji la Dar-es-salaam. Baada ya Dar-es-salaam ratiba ya Fiesta inasema Zenji tarehe 19 August, tarehe 24 August Arusha(A-town), 26 August Tanga, 31 August Dodoma, tarehe 1 septemba Morogoro kabla ya kumalizia Mbeya tarehe 7 & 8 September.
Baadhi ya wasanii maarufu wanaotarajiwa kupanda jukwaani kutoa burudani ni Juma Nature na kundi zima la Wanaume Halisi, TID,Besta,Afande Sele,Wanaume TMK,Marlow,Zuhura,Alikiba,Ze Danto,Mr.Nice,Mabaga Fresh Q-Chief,Klyn,Jay Mo,MwanaFA,Black Rhino,Mangwea na wengineo.Bendi za muziki zinazotarajiwa kuwepo ni Sikinde,Twanga Chipolopolo,Akudo Sound na FM Academia. Kwa upande wa wasanii kutoka nje ya nchi wanaongozwa na Koffi Charles Olomide kutoka DRC, DNA kutoka Kenya, Ngoni Tribe kutoka Uganda na Kevin Lyttle kutoka Jamaica.
Je unatarajia kuhudhuria tamasha hili? Kama unausoma ujumbe baada ya kuhudhuria tamasha hili,je lilikuwaje?
Recent Comments