Maisha yetu yanaboreshwa kwa pesa ambazo zinapatikana nyakati za malipo (kwa wafanyakazi, wafanyabiashara n.k).Malipo hayo huwa yanatokea kwa nyakati tofauti. Lakini uwe unalipwa mwisho wa siku, ama mwisho wa wiki, ama mwisho wa kila baada ya wiki ama mwisho wa mwezi, dalili ni kwamba siku ya leo wengi watakuwa wamelipwa maana sio tu mwisho wa siku,na wiki, bali ni Mwisho wa mwezi.Tumeingia ngwe ya lala salama ya mwaka 2008.Unaweza dhani utani vile ukiwambiwa karibuni watu tunakula Xmas.
Unakumbuka vituko vya mwisho wa mwezi?Binafsi nakumbuka kisa cha mzee mmoja ambaye ilikuwa kila mwisho wa mwezi unapofika haonekani nyumbani mpaka alizonazo zikishamuishia.Siku moja mke wake akagundua kule jamaa anapoenda akishakamata “mshiko”. Kilichotokea huko mpaka hivi leo ni simulizi lenye mafunzo.Kwa kifupi jamaa alitoka huko bila sehemu muhimu ya viungo vyake vya uzazi!
Wasikilize Vijana Jazz wakizungumzia mambo ya mwisho wa mwezi katika kibao chao kilichotamba saana cha MWISHO WA MWEZI. Wikiendi njema kwenu nyote.
Burudani ya leo imeletwa kwenu kwa hisani ya http://www.changamotoyetu.blogspot.com
NB: Kwa wasomaji na wapenzi wote wa BC ambao walimiss burudani ya kila Ijumaa kwa majuma kadhaa,tunawaomba radhi.Hiyo yote ilitokana na sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wetu.Tekinolojia ya 3G ilituangusha kwa majuma kadhaa tulipokuwa hukooo kwenye semina elekevu.
Recent Comments