BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MwanaFA UNAOA LINI…? June, 30, 2008

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Muziki,Single/Mpya — bongocelebrity @ 9:37 PM

Kwa mila na taratibu za jamii nyingi,hususani zetu za kiafrika,kijana akifikia umri fulani huwa anategemewa kuoa.Ikitokea ukafikia umri ambao kila mwanajamii anakutegemea “kujipatia jiko” na ukawa hujafanya hivyo, hapo lazima ujiandae na swali;unaoa lini?Ukikutana na shangazi swali ni hilo hilo.Ukikutana na mjomba naye anasimamia hilo hilo.Jamii nzima inauliza,unaoa lini?

Sasa je ukiulizwa swali hilo huwa unajibu nini?Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya,Hamis Mwinjuma a.k.a MwanaFA a.k.a Binamu anakupa msaada wa majibu katika single yako mpya inayokwenda kwa jina Bado Nipo Nipo huku akiwa amemshirikisha Miss Universe Tanzania 2007,Flaviana Matata.

Bado Nipo Nipo imepikwa na producer Harmy B.Pia MwanaFA anapewa tough na vichwa vingine kama vile Ambwene Yesaya(AY),Alan,Jabiri,Shehe na mwanadada aitwaye Anna.

Usikilize wimbo Bado Nipo Nipo kwa kubonyeza player hapo chini.Ningependa sana kusikia majibu kutoka kwa kinadada walio single, ni kweli anayoyasema MwanaFA?

Advertisements
 

KUTOKA MISRI NA MUSTAKABALI WA ZIMBABWE

Filed under: News,Serikali/Uongozi,Siasa — bongocelebrity @ 8:49 PM

Mkutano wa 11 wa Umoja wa Afria (AU) umeanza huko nchini Misri katika mji maarufu kwa utalii wa Sharm El Sheikh. Suala la Zimbabwe ndilo linaelekea kuugubika mkutano huo.Dunia nzima inasubiri kusikia kitakachoamuliwa au kuafikiwa huko Misri.

Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU),Jakaya Mrisho Kikwete,akifungua rasmi mkutano wa 11 wa nchi wanachama wa umoja huo huko Sharm El Sheikh nchini Misri jana.

Kutoka kushoto kwenda kulia ni Rais wa Tanzania na pia Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyeji wa mkutano huo,Rais wa Misri Hosni Mubarak na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Dr.Asha Rose Migiro.

Picha zote/Freddy Maro

 

MUGABE:KIELELEZO CHA UONGOZI AFRIKA?

Filed under: Editorial,Mawazo/Tafakuri,Serikali/Uongozi,Siasa,Special Interest News — bongocelebrity @ 6:29 PM

Katika anga za siasa duniani hivi leo,lipo jina ambalo dunia nzima inaendelea kulizungumzia.Hilo si lingine bali lile la Rais wa Zimbabwe, Robert Gabriel Mugabe.Kwa wengine mtu huyu ni shujaa,kwa wengine mtu huyu ni kinyume kabisa cha neno shujaa.Kwako wewe je?Je viongozi wa Afrika wanaohudhuria kikao cha Umoja wa Afrika huko Misri(na Mugabe naye anahudhuria) wataweza kumnyoshea vidole Mugabe?Nini hatma ya siasa za Afrika?

Pichani ni Rais Mugabe akiwa na mkewe,Grace Mugabe.Wengi wanasema wakati wao wanatafuna keki,wananchi wengi wa Zimbabwe wanakufa njaa.

Photo/New York Times

 

THERE SHE GOES…OFF TO SOUTH AFRICA June, 29, 2008

Filed under: African Pride,Breaking News,Fashion,Urembo — bongocelebrity @ 12:20 PM

Mrembo wa Miss Universe Tanzania 2007, Flaviana Matata, ameondoka leo mchana nchini akielekea Johannesburg, nchini Afrika Kusini ambapo atafanya kazi na kampuni kubwa ya uanamitindo ya Ice Model Agency ya huko Afrika Kusini, kufuatia mkataba wa mwaka mmoja aliosaini kupitia kampuni yake mama Compass Communications.

Flaviana alipata umaarufu mkubwa wa kimataifa katika mashindano ya Miss Universe mwaka jana ambapo alishika nafasi ya sita katika mashindano haya makubwa ya urembo, na alisaini mkataba wake na Ice Models jijini Dar-es-Salaam hivi karibuni baada ya majadiliano kati ya Compass Communications na Ice Models kukamilika. “Hii ni mara ya kwanza kwa mrembo anayeshikilia taji la kimataifa hapa nchini kupata nafasi kama hii,” alieleza mkurugenzi wa Compass Communications Maria Sarungi Tsehai ambaye alisimamia majadiliano na mkataba wa mrembo huyu. (more…)

 

PICHA YA WIKI # 22 -Nini Kinaendelea?

Filed under: Photography/Picha,Weekend Special — bongocelebrity @ 11:15 AM

Wikiendi inakwendaje au ilikuwaje? Hapo juu ni picha yetu ya wiki hii.Badala ya kutoa maelezo tumeona tumpe kila mtu fursa ya kutoa maelezo yake.Unadhani nini kinaendelea katika picha hii?Unaweza kutoa maelezo yapi kwa kuiangalia picha hii?

Hii ndio picha ya wiki na imepigwa na Ahmad Michuzi.Kama una picha ambayo ungependa tuiweke kama picha ya wiki,tafadhali tutumie,pamoja na maelezo yake kwa kutumia anuani pepe ya bongocelebrity at gmail dot com.

 

SOLO THANG ATETA NA SPOTI STAREHE June, 28, 2008

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Muziki — bongocelebrity @ 10:34 AM

Muziki ni safari.Kwa wanaokumbuka enzi hizo ukilitaja jina Solo Thang kila mtu mpenda Muziki anasisimuka, kwani ni mmoja wa wanamuziki wa Kizazi kipya ambao kwa kiasi kikubwa “walipigana vita ya msituni” kufanya muziki huu ukubalike kwa jamii. Kwa sasa Solo Thang AKA Traveller AKA Msafiri anaishi Uingereza akiwa ameoa na mtoto mmoja anayeitwa YASSIR na Mama yake anaitwa YASMIN(Pichani juu ni Solo Thang na mwanae Yassir)

Kwa muda sasa mwanamuziki Solo Thang amekuwa kimya.Ili kutaka kujua yuko wapi hivi karibuni blog ya Spoti Starehe ilifanya naye kutaka kujua machache toka kwake na maisha yake hasa ya kisanii kwenye sanaa nzima ya Muziki.Bonyeza hapa usome mahojiano hayo.

 

NARUDI NYUMBANI-DR.REMMY ONGALA June, 26, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special — bongocelebrity @ 10:05 PM

Nyumbani ni nyumbani.Ooh nyumbani.Hata pawe pabaya namna gani,nyumbani ni nyumbani.Hilo ndilo nililoliona baada ya post ya Mambo Ninayoyamiss Kuhusu Tanzania.Lazima niseme kwamba kuona jinsi ambavyo watu wengi wanapakumbuka nyumbani ni jambo la kutia moyo.Nina imani kwamba wote wanaopamiss nyumbani,siku moja watarejea kwa minajili ya kujenga nchi.Inawezekana.Unachotakiwa ni kucheza karata zako vizuri na pia kuhimiza kwamba “ufisadi” ufikie mahali panapoitwa “kikomo”.

Kwa upande wa burudani,sidhani kama kuna ambaye anaweza kukidhi mada ya wiki zaidi ya Dr.Remmy Ongala & Matimila Band na wimbo wao uitwao Narudi Nyumbani.Pata burudani na enjoy your weekend!