Tofauti moja kubwa kati ya watangazaji wa kwenye luninga na wale wa redioni ni kwamba wale wa luninga huwa tunapata bahati ya kuwaona mara kwa mara,wengine hata kila siku kupitia kwenye luninga. Wale wa redioni mara nyingi huwa tunaishia kuzisikia tu sauti zao na hivyo kubaki tukihisia tu juu ya muonekano wao.Ikitokea tukawaona ana kwa ana au kupitia picha basi huwa ni jambo jema.Mfano mzuri ni huu katika picha hii.
Kutoka kushoto kwenda kulia ni Violet Mzindakaya maarufu kama Sister V, mtangazaji wa kipindi cha taarabu kutoka Radio Uhuru ambacho kinarushwa kuanzia saa sita mpaka saa nane mchana kila siku.
Anayemfuatia ni Sauda Mwilima mtangazaji wa kipindi cha Bongo Beats ambacho hurushwa kuanzia saa moja na nusu mpaka saa mbili usiku na pia kipindi cha mcheza kwao kinachorushwa kila jumapili. Vipindi vyote hivi ni kupitia kituo cha televisheni cha Star TV chenye makao yake makuu jijini Mwanza.
Wa tatu ni Maimatha Jesse mtangazaji wa kipindi cha Afro Beat akishirikiana na Ben Kinyaiya (hayupo pichani) ambacho hurushwa kila siku ya Jumamosi kuanzia saa moja mpaka tatu usiku kupitia televisheni ya East Africa TV maarufu kama Chanel 5.
Wa mwisho kulia ni Mussa Hussein, mtangazaji wa radio ya East Africa FM ambaye kipindi chake kinarushwa kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa saba mchana.
Picha kwa hisani ya Ahmad Michuzi.
Recent Comments