BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

RAGE AREJEE TFF? March, 31, 2008

Filed under: Mahusiano/Jamii,Michezo,News,Soka,Swali kwa Jamii — bongocelebrity @ 12:05 AM

Kwa mpenzi yeyote wa soka nchini Tanzania,jina Ismail Aden Rage (pichani) sio geni.Jina hili ni miongoni mwa yale majina ambayo yamekuwa yakisikika katika medani za ulimwengu wa soka nchini Tanzania kwa muda sasa hususani tangu enzi akiwa Katibu Mkuu wa wa kilichokuwa Chama Cha Soka Tanzania(FAT),sasa TFF na baadaye Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Jina la Rage lilizidi kutawala vinywa vya wapenzi wa michezo nchini Tanzania, hususani soka, baada ya kushitakiwa kwa kosa la wizi wa mali na fedha za FAT kesi ambayo ilipelekea kupewa kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na hatia za makosa hayo.Hata hivyo, alikata rufaa kupinga kifungo hicho na kabla ya rufaa hiyo kusikilizwa, Desemba 2005, alitoka kwa msamaha wa Rais.

Kufuatia hali hiyo Rage alibaki nje ya TFF kupigania rufaa yake na Alhamisi wiki iliyopita, jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa wakiongozwa na Damian Lubuva, walimfutia makosa yaliyokuwa yamemtia hatiani Rage.Hivi sasa Rage ni Mkurugenzi wa timu ya Moro United.

Sasa hivi majuzi klabu 12 kati ya 14 za Ligi Kuu Tanzania Bara zimetaka aliyekuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ismail Aden Rage, kurejea katika wadhifa wake.Unaweza kuisoma habari hiyo kwa kubonyeza hapa.Nini maoni yako?Je Rage arejee TFF?

Advertisements
 

PICHA YA WIKI # 13 March, 30, 2008

Filed under: Editorial,Photography/Picha,Wanawake na Watoto,Weekend Special — bongocelebrity @ 11:04 AM
Picha moja ni sawa na maneno elfu moja.Wakati mwingine huwa ni zaidi ya hata ya maneno elfu moja.Ukiisoma picha hii vizuri utaweza kuona mengi.Hatuhitaji kuandika maneno mengi ili kukuwezesha wewe msomaji na mtazamaji kupata ujumbe.Picha hii ambayo ni ya kina mama huku wengine wakiwa na watoto wao migongoni(sijui kina baba wako wapi hapa) ni kutoka katika kijiji cha Bermi huko Babati,kaskazini mwa Tanzania. Picha ni kwa hisani ya peacecorpsonline.org.Hii ndio picha yetu ya wiki hii.
 

75 WAHOFIWA KUFARIKI MERERANI- ARUSHA March, 29, 2008

Filed under: Breaking News,Developing News,News — bongocelebrity @ 5:23 PM

Zaidi ya watu 75 wanahofiwa kuwa wamefariki dunia huko katika machimbo ya Mererani mkoani Arusha kutokana na mafuriko yaliyolikumba eneo hilo maarufu kwa uchimbaji wa madini.Kwa undani zaidi wa habari hii bonyeza hapa na hapa na hapa.

BC inaungana na watanzania wote ulimwenguni kuwapa pole ndugu,jamaa na marafiki waliopoteza ndugu zao au walio katika jitihada za kupata habari zozote kuwahusu ndugu,jamaa na marafiki zao.Jitihada za uokozi bado zinaendelea huko mkoani Arusha.Tunaendelea kufuatilia na tutaendelea kupashana habari kadri zinavyozidi kupatikana

Pichani ni wachimbaji wa madini Mererani wakiwa katika jitihada zao za kutafuta riziki.

 

MSHINDI WA BSS APATIKANA

Filed under: Bongo Reality TV,Muziki,New Artist,Television,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 12:40 PM

 

Shindano la kumtafuta star mpya wa Tanzania(Bongo Star Search) kwa upande wa muziki lilifikia ukingoni jana kwa mwanadada aitwaye Misoji Mkwabi kuibuka mshindi.Fainali za shindano hilo zilifanyika hapo jana ndani ya ukumbi wa Ubungo Plaza.

Misoji alijinyakulia kiasi cha Tshs. milioni 15,Furniture,TV ya LG pamoja na masomo ya kompyuta katika chuo cha Desktop Computer na masomo ya uandishi wa habari kwenye chuo cha DSJ (Dar es salaam School of Journalism.

Pichani juu ni Mc Jimmy Kabwe akiwa na Misoji Mkwabi jukwaani.

 

Misoji akiperform jukwaani.

Kwa picha na habari zaidi za tukio hili mtembelee MichuziJR.Kwa mahojiano tuliyowahi kufanya na mwanzilishi na mmojawapo wa majaji wa shindano hili,Rita Paulsen, bonyeza hapa.

 

BOSS WA NGWASUMA

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special — bongocelebrity @ 9:25 AM
Anaitwa Nyoshi El-Sadaat.Ndiye kiongozi wa bendi inayotamba nchini Tanzania ya FM Academia au maarufu kama “Wana Ngwasuma“.
 

MESENJA KALETA BALAA! March, 28, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 12:05 AM

Ni Ijumaa tena.Baada ya mapumziko ya sikukuu ni wakati mwingine tena wa kutafakari na kupanga mikakati.Maisha ndivyo yalivyo,hakuna kusimama wala kungoja.Kila siku ni mchakamchaka.Raha na karaha ndio mtindo.

 

Zipo nyimbo ambazo zikipigwa,kwa njia moja au nyingine,ni lazima zikukumbushe jambo au mambo fulani.Kama hukumbuki enzi zile za mchana mwema chini ya utawala wa RTD peke yake basi unaweza kukumbuka kuyaruka majoka huku noti nyekundu zikiwa na thamani.Ili mradi tu,kwamba hivi leo kila kukicha kheri ya jana!Yaani kwamba dunia ile ilikuwa nzuri kuliko tuliyonayo hivi sasa.Najua kwamba hoja hii inaweza kuwa pana.Lakini leo sio wakati wake.Ijumaa ni wakati wa kubwaga manyanga chini na kupumzisha akili.Majirani zetu(kule ulipo Mlima mrefu!!!) wao siku hizi wanasema ni wakati wa “kubanjuka”.

 

Leo tunao Bima Lee Orchestra.Wimbo ni Mesenja.Naam,mesenja yule yule aliyeleta balaa.Za nyumbani akapeleka ofisini na za ofisini akapeleka nyumbani.Nyumba unaweza kuiona ndogo ukifanya masihara.Bonyeza player hapo chini upate burudani.Ijumaa Njema.

 

PROF.ANNA TIBAIJUKA NA MWENGE WA OLIMPIKI March, 27, 2008

Filed under: African Pride,News,Wanawake na Watoto,Watanzania Kimataifa — bongocelebrity @ 1:12 PM

 

MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa (UN Habitat), Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka(pichani), ni miongoni mwa watu sita mashuhuri barani Afrika walioteuliwa kukimbiza Mwenge wa Olimpiki utakaokimbizwa jijini Dar es Salaam, Aprili 13, mwaka huu.Kwa undani zaidi wa habari hii bonyeza hapa.