BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

SALAMU ZA FA KUTOKA COVENTRY February, 16, 2009

Filed under: Bongo Fleva,Burudani,Elimu na Maendeleo,Muziki — bongocelebrity @ 2:33 PM

fabc1

Hakuna ubishi kwamba kijana Hamis Mwinjuma au maarufu kama MwanaFalsafa(MwanaFA) ni miongoni mwa wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya ambao wamefanikiwa.MwanaFA amefanikiwa sio tu kufikisha ujumbe alioukusudia kwa jamii bali pia kuwa na uwezo wa kuendesha maisha yake kupitia muziki.Miziki yake imekuwa ikiimbwa na watu wa rika mbalimbali.Hayo nayo ni mafanikio.

Pamoja na mafanikio ya kimuziki au kisanii aliyonayo MwanaFA,anabakia kuwa mfano wa kuigwa linapokuja suala zima la elimu,muziki na maisha.Hivi karibuni alithibitisha hilo pale alipoamua kurejea tena shule.Safari hii ameelekea nchini Uingereza.

Nini kinamsukuma kijana huyu katika nyanja ya elimu? Na je hivi karibuni alipoachia wimbo unaokwenda kwa jina “Msiache Kuongea” alikuwa anamjibu Inspekta Haruni?Anazungumziaje maisha ya nchini Uingereza?Fuatana nasi katika mahojiano haya mafupi na MwanaFA

BC: Pamoja na mafanikio mazuri katika muziki kule Bongo bado umeamua kurudi tena shule.Nini kinakusukuma?Hapo UK umeenda kusomea nini na katika chuo gani?

FA: Kuna mengi yanafanya nifanye nnachofanya.Lakini kubwa na la msingi zaidi ni kuwa na nguzo nyingine kwa ajili ya maisha ninayoishi(Plan B).Kama unavyojua muziki pamoja na kuwa unakwenda vizuri lakini hautabiriki sana.Ni ngumu kujihakikishia nafasi ya moja kwa moja kwa angalau miaka 10 ijayo.

Na zaidi ni kuwa naona kama kuna muda mwingi kama msanii wa kibongo nakuwa naupoteza kwa kutofanya chochote baada ya kurekodi(ambayo sio kila siku),kufanya shows(mara nyingi huwa weekends),matangazo(mara chache kama una bahati) na interviews ambazo nazo sio kila siku.Kwa hiyo kwenye wiki kunakuwa na muda mwingi unaenda bure ambao nimeona ni vyema nikautumia kufanya kitu kitakachozalisha.
Hapa UK nasoma Msc Finance na nipo Coventry University.

BC: Una mpango gani na muziki kwa hivi sasa?Kama utaendeleza muziki na shule vilevile,lini labda wapenzi watarajie albamu yako mpya?

FA: Nimeacha album ikiwa tayari,inaitwa ‘mabibi na mabwana’ na naomba maswali kuhusu hiyo ayajibu Hermy B,ndio ipo mikononi mwake..sijapumzika kabisa muziki,ila nimepunguza kiwango ninachoufanya kwa sababu ya umbali.Ngoma zitaendelea kushuka kama kawa..patience kidogo inahitajika nitulize haya ya kwa Bi Eliza kwanza.

BC: Katika wimbo ulioutoa hivi karibuni kabla hujaondoka Bongo(ukishirikiana na Lady Jay Dee),inaelekea kwa namna fulani umemjibu Inspekta Haruni na wengineo wengi.Kwanini umefanya hivyo ikizingatiwa kwamba ulishasema siku za nyuma kwamba hutomjibu?

FA: Kama utakuwa umeniskiza vizuri sikumjibu..nilisema ‘…nisemeni hadharani hata bila hoja kama Inspekta’,nikimaanisha natoa ruhusa kwa kila mtu kunisema hata kama hana sababu za msingi za kufanya hivyo kama alivyofanya jamaa.Na,aina ya mziki tunayoifanya hairuhusu kabisa unyonge,ilikuwa haki yangu ya kimsingi.Watu wengi wanaongea vitu vingi vibaya siku hizi,hivyo inabidi niwaambie najisikiaje wakifanya hivyo.

Ukweli ni kuwa hawaingii kwenye lines zangu za maisha na wananipa nguvu na hasira za kufanya vyema zaidi.Na sio kwangu mwenyewe,kila mtu ana matatizo yanayofanana na yangu kwa namna moja ama nyingine kwa hiyo anaweza kuitumia kimpango wake.

BC: Umekuwa ukiingia na kutoka nchini Uingereza mara kadhaa.Ni mambo gani ambayo unadhani unayafurahia hapo UK na ambayo labda nchini kwetu tungeyaiga yangesaidia katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo?

FA: Uingereza kama nchi imejipanga.Ni dunia ya kwanza.Kuna mengi tunaweza jifunza,siwezi hata kuorodhesha.Lakini napenda namna wanavyoheshimu utawala na nguvu za sheria.Natamani kwetu kungekuwa hivi kwa kuanzia.

BC: Una mpango wowote wa kushirikiana kimuziki na wasanii wa hapo UK?Ni kina nani ambao unawazimia?

FA: Muziki wa UK hauendani sana na wa kwetu.Wana muziki tofauti na sisi.Pamoja na umbali wa kimaendeleo waliotuacha nao sijui hata wanamuziki 10 wa hapa.Hata rap/hiphop ya hapa siamini kama inapendwa mahala pengine popote zaidi ya UK.Haina mafanikio makubwa nje ya hapa.

Hata hivyo napenda mziki wa Lemar na Jay Sean na natamani nifanye nao kitu kama ninavyotamani kuifanya hii shughuli na 2face.

Nimekutana na Amit(Mentor) ambaye apparently ndio amemtoa Jay Sean(japo sasa Jay amepata record deal Cash Money),na tunajaribu kuona nawezaje kufanya mawili matatu toka nyumba yake ya muziki.Huwezi jua..nasubiri nione kitakachotokea!


 

30 Responses to “SALAMU ZA FA KUTOKA COVENTRY”

  1. Sophie Says:

    Safi sana FA…naona umeamua sasa kweli music na shule…vipi sasa ndoa lini na yule demu wako wa SInza……mshikaji ulifanya certificate how come sasa unafanya masters??

  2. any Says:

    Sophie, thats too personal. leave him alone, wee kwani una mangapi zaidi ya hayo yake hiyo siri yako, na kwa vile wewe sio celebrity, ndio maana hatuyasikii, otherwise, this guy is just like any other human being, same needs, like shelter, food, mavazi and of course SEX!

  3. bantu Says:

    Mh,we sophie.Si alifanya advance diploma ya insurance ifm?

  4. Gwantwa Says:

    kanajibu vizuri maswali.kana akili akili kumbe

  5. Mkali kwanza Says:

    Si hatuachi kuongea FA, Vipi hapo kwenye CERTIFICATE hadi MASTERS how come.

    tunataka kujua kama inawezekana tutamrusha Mr blue toka fom 2 hadi 6 na yeye asome.

  6. mjanja Says:

    hongera sana man inapendeza shule ni jambo la msingi sana keep it up

  7. Foster Says:

    In the UK, but in some universities and colleges, you may register for a masters level and opt for an early exit whilst having to follow from a certificate, diploma and finally to a master degree. So, is no wonder that this fellow-MwanaFA has opted to follow such a route, and that means if you ask him what level he is aiming to achieve, yes, he will definitely say a masters level. It does sound POA yeah?

    Is it right to say so? On the one hand, it is right to say so if he is really determined to achieve the finals but, on the other hand, he may be deceiting if he will not be able to finish to masters level. Many people who enroll in this kind of program have tended to opt to leave their course at a diploma level. They say “Too many years and too much work to do buddy” Sort your self up.

    By the way I saw this guy in one of the place where I usually visit on Friday midnights for disco. He was with another feller and got into this music hall quietly but later I noted repeatedly some guys mentioning of Tanzania for many times and it shove me to have a look to see who these guys are on the stage. You know what they were throwing their trucks like no one else in the hall and every TZmania in the house/ hall was already crazy. I too was, but already had 6000 mls of alcohol intake, which made a complete night for me. Not bad for once a month!, it is permitted. This was London, E13. Club Afrique on the 30th,January 2009.

    KEEP IT UP FA

  8. nice2 Says:

    Sophie… hiyo certificate unayoongelea ni kama miaka mitano iliyopita, inaelekea uko nyuma ya wakati sana, tembelea japo website yake for more info. Na zaidi, kama vile una wivu na huyo demu wa sinza hivi ( ni mtazamo tu)
    Keep it real B, you’re the DON you know……

  9. jaysan Says:

    Kwa taarifa tu FA alifanya Advance Diploma pale THE IFM. Hivyo ni sahihi kufanya masters provided advanced diploma ya IFM ni equivalent kabisa na degree.actually sasa hivi inaitwa degree.haa haa habari ndo iyo.

  10. asa Says:

    we sophie nae kujifanya unamjua sana mwana fa kumbe hamna kitu sasa mwana f.a kwataarifa yako kasoma certificate na advance diploma pale i.f.m incase udidnt know

  11. kaka mkubwa Says:

    nana kakwambia alifanya certficate wewee? ndiyo ninyi mnaoongea hovyo. Mbona mm nilikuwa naye darasani sasa wewe hizo habari za cert. umezitoa wapi? huo ndiyo udaku bora uende kule kwenu utamu ikifufuka

  12. mr degree Says:

    Mh! mbona coventry hakuna MSc finance? au ndo changa la macho? manake huyo jamaa ni Mr misifa jamani. nakumbuka alipofanikiwa kupata admission ya kusoma certificate pale IFM akaanza kujiita majina kibao ya kujifagilia. mara ‘college boy’ mara ‘the don’ na kila kitu anapenda kujipa sifa sana huyo.sasa anatuambia anasoma Msc finance isije ikawa ndo yaleyale yo solo thang!

  13. Kafura Says:

    Issue ni kutoka ATECH 1 kwenda MSc FINANCE. hapo ndo hujatueleza huo ujanja.

  14. PUZZO Frm Dodom University Says:

    sophie una uhakika na unachokisema? Ingawa mi sio msemaji mkuu wk…Bt Am talkin as his biggest fun!!!!Jamaa alipiga Advance Diploma pale IFM….Big up Bro FA Unajua unachofanya!!

  15. till Says:

    let him leave his life jamani kuwa msanii cio kwamba hawezi fanya mambo personal evryone gotta live thr life big up FA mi nakufil vibaya mno i wish u ol the best.

  16. Riziki Says:

    we sophie unajifanya unamjua binamu kumbe la u r just those haters..amesoma certificate then advance diploma pale IFM na above all amepata work experience NBC ndo maana yuko zake masters…stop hating alikupiga kibuti nn maana unaulizia anaoa lini? big up binamu ni jambo la muhimu uliloamua they say education is the best succeful key in life…tuko pamoja tunakutakia kila la kheri..God Bless uuuuu!!!

  17. mr degree Says:

    jaysan unamaanisha nini unaposema advance diploma ya IFM ni equivalent kabisa na degree? unaijua degree wewe? na unajua tofauti ya institute na university? au hujui maana ya IFM? hata kama sasa wanatoa degree lakini yeye hana degree. na hiyo Certificate yake na advance diploma yake ya kudesa sio sawa na degree. kwa kuwa waingereza wapo kibiashara inawezekana wakampa admission ili mradi alipe tuition fee tu.any way hiyo sio ishu, swali langu ni kwamba hicho chuo hakina MSc finance anayodai anasoma. niambieni anasoma chuo gani hasa maana nyinyi mmezoea kudanganywa na kushangilia tu!

  18. Jazzy Says:

    Haya mi simo…

  19. Mwanamke wa shoka (UK) Says:

    teh teh teh…inachekesha…..
    take it easy pals….lol

    …HE knows what he’s doing….

  20. Kweliman Says:

    mwana fa hongera sana kwa kazi nzuri za sanaa(urban music) nimefurahia sana kazi zako.

  21. sabrina Says:

    huyu aliyekasirika kabisa tunadanganywa na tunachekelea tu utasema kuna kitu anaweza fanya kuzuia jamaa asisome.tehtehteh,ovyo

  22. asa Says:

    WE MR DEGREE YAKUDESA ME NIMESOMA ADV DIPLOMA I.F.M NA SASAHIVI NNA MASTERS FALA WE WHY NOT MWANA F.A? WE BAKI NA DEGREE YAKO HUNA HATA LOLOTE WENZIO TUNAPAA TU HALOOOO

  23. clarasita Says:

    fa i just wish you luck in every ting u do.. do ur thing. no one has to decide for you.. sawa.. i hate idea crashers.. why do people have to discourage you… SUCESS. you have my love clarah

  24. carin Says:

    Ni kweli wabongo wanashangaza kwa kufananisha Advanced diploma na Degree! kama ingekuwa sawa si ingeitwa degree nayo hiyo advanced diploma!? Ebo? danganyaneni huko huko! Hizo daraja za elimu zina uzito wake jamani oho!
    Kwani mnaongoza pia kwa kupeana vyeti ovyo ovyo! aangalie mwana FA UK mjini jamani asijeliwa vipesa vyake vya mziki bila kupewa Masters! haya!
    Mimi sio hater wala nini Mwana FA namkubali lakini sikubali elimu kubakwa!

  25. EDO Says:

    mwana FA WE CONCETRATE NA SHULE YAKO ,HAPA COVENTRY KUNA WABONGO WENGI WANA WIVU WAMEMBEA NA MAJORITY KISOMO ZIRO,USIJIIUMIZE NAO WEWE KAMA NI BOX BEBA ,ISHI VIZURI UPASI SHULE YAKO BASI ACHANA NA WAJINGA.

  26. babie Says:

    hivi mr degree ule mwaka mwanafa alipoanza kusoma ifm we ndio ulidisco pale ama ilikuwa mwaka kabla ya huo?heheheeeee..

  27. anita Says:

    jamani fa sa kwanini uliniacha karibu unaondoka jamani c ungenivumilia kidogo at least ningekuwa na chat na wewe ona sasa cingii hata kwenye net, now a dayz….
    n wayz mafanikio mema wangu….

  28. msongo Says:

    mr degree anasema ukweli hakuna hiyo programme hapa conventry university and oh yeah adv.diploma IS NOT EQUAL TO a degree infact ni kichekesho eti mtu kafanya Adv.Diploma in Insurance aruke to Masters in Finance very doggy 🙂

  29. watu bwana Says:

    siri ya mtungi aijuaye ngata.hongera mtanzania mwenzangu kwa kujituma,kama kweli umekuja kusoma soma kaka.watu hawajui muziki ni bahati,akili kichwani.chochote ukikipata kutokana na muziki,kiinvest. sababu muziki hautabiriki,na hauna future kwa bongo.usipo fanya cha maana mapema,utakuja ishia nilikuwa,nilikuwa,nilikuwa,kipindi hicho huna hata dala mfukoni.

  30. SPC zoo Says:

    Wish to be like U


Leave a comment